Mke wa Mbunge Lema ashtakiwa kwa kumtumia ujumbe Mkuu wa Mkoa wenye neno 'Shoga'

Sasa ndio anajitetea, imekula kwake. Huyu lazima aende ndani na yeye akapewe anacho kifata mume wake.
 
Kumbe siku zote tunazosikia HARAKATI ZA KUPINGA USHOGA ni juhudi za kuzuia watu wasiwe marafiki!!!! Kweli Kiswahili lugha ngumu sana.
 
Kwahiyo sisi tumekaa huku tunafikiri ugonvi ni kiwanja, hospitali, na wahisani kumbe ni mkeo kuwa na ushoga na mkuu wa mkoa. Mm kazi kweli kweli
 
Maana ya shoga ni hii.
shoga

  1. Mtu ambaye hana hisia za kike
  2. Rafiki uliyeshibana naye kiurafiki (hasa hutumiwa na wanawake.
 
Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini, Neema Tarimo amefikishwa mahakamani jijini Arusha na kusomewa shtaka la kumtukana Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo baada ya kumtumia ujumbe kwenye simu yake wenye neno 'shoga'.

Mke wa Mbunge huyo amekana kumtusi Mkuu huyo wa Mkoa baada ya kudai kuwa neno shoga sio tusi bali ni neno ambalo hulitumia kuwaita marafiki zake.

Amesema neno shoga kwenye mazingira ya Tanzania humaanisha rafiki.

Hapa kuna tatizo kwamba amemuita shoga RC kwasababu ni rafiki yake, sidhani kama makamanda huwa mnaitana shoga kwasababu ya urafiki nahisi kuna tatizo hapo.
Hana wakili wa kumshauri kwamba yeye na Gambo ni marafiki
 
Mpe mkeo uone asiporudi na dabo dabo.
Kuna " mashoga" wameoa wake na wana watoto." Ushoga" si ubaradhuli, kama jongoo hapandi mtungi,lakini mchezo tu huwa anaufurahia!
Yaani mwanamke anamwita mwanaume tena mkuu wa mkoa shoga huyu mke wa lema kiboko
Sasa kama ana uthibitisho na tabia zao zinalingana basi ni stahili yake; kwa nini asiwite " mkufu kuwa mkufu na kuwa hausimiki hausimami?"
 
Shoga ni marafiki wa kike kwa kike. Ukimuita mwanaume shoga tayari ushatukana.
Shoga maana yake rafiki.Hayo mengine yamekuja baada ya kutafuta jina mbadala.Lakini kW auhakika shoga maana ni rafiki wa karibu
 
Shoga ni marafiki wa kike kwa kike. Ukimuita mwanaume shoga tayari ushatukana.
Siyo kweli...jivunze ku associate fikra zako mkuu...kwa wanawake neno shoga humaanisha 'rafiki' na unapoitwa shoga na mwanamke inamaanisha 'rafiki'. Mchezo huu hauhitaji hasira..nadhani ingekuwa vema serikali ikajikita katika kutatua kero za wananchi kuliko kupoteza raslimali za walipa kodi....Hivi Gambo alivyomtusi mwanasheria wa korogwe alichukuliwa hatua gani...hapa Rais wangu mpenzi ukichunguza kwa umakini, Gambo hana sifa kuwa kiongozi au mteule wako. Hapa Kenya tunatamba mitaani kwasababu ya kasi yako ya kupambana na ufisadi na kurudisha heshima ya nchi katika mstari baada ya kupotea last 10 yrs. Sasa ni ushauri tuu..huyo Bwana Gambo muda mwingi anautumia kupiga madili pale Kibo palace Hotel...sijui anakuwaga na vikao vya nini kila mara...tupia jicho lako huko mkuu..kuna mengi yamejificha ...jaribu kuwawekea perfromance agreements utagundua kuwa hana uwezo na hivyo amejificha nyuma ya kivuli cha lema...
 
Utetezi wake hauna msingi, tangu lini mwnamke amwite mwanamme shoga tena kiongozi mkuu wa mkoa. Nitashangaa hakimu kuliona kivingine swala hili.
 
Kwa hiyo kama siyo hiyo maana ya pili basi ana maana mlalamikaji ni rafikiye wa kike
 
Attachments

  • 1478005139052.jpg
    1478005139052.jpg
    51 KB · Views: 35
Aina ya siasa anazofanya Lema sio Nzuri siasa sio ubabe Bali na hekima na maridhiano sio nguvu na maneno ya kuudhi.

Wabadilike.
 
Siyo kweli...jivunze ku associate fikra zako mkuu...kwa wanawake neno shoga humaanisha 'rafiki' na unapoitwa shoga na mwanamke inamaanisha 'rafiki'. Mchezo huu hauhitaji hasira..nadhani ingekuwa vema serikali ikajikita katika kutatua kero za wananchi kuliko kupoteza raslimali za walipa kodi....Hivi Gambo alivyomtusi mwanasheria wa korogwe alichukuliwa hatua gani...hapa Rais wangu mpenzi ukichunguza kwa umakini, Gambo hana sifa kuwa kiongozi au mteule wako. Hapa Kenya tunatamba mitaani kwasababu ya kasi yako ya kupambana na ufisadi na kurudisha heshima ya nchi katika mstari baada ya kupotea last 10 yrs. Sasa ni ushauri tuu..huyo Bwana Gambo muda mwingi anautumia kupiga madili pale Kibo palace Hotel...sijui anakuwaga na vikao vya nini kila mara...tupia jicho lako huko mkuu..kuna mengi yamejificha ...jaribu kuwawekea perfromance agreements utagundua kuwa hana uwezo na hivyo amejificha nyuma ya kivuli cha lema...
Hujanielewa wapi mkuu? Mbona nimesema shoga ni marafiki wa kike?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom