Unamzungumzia Spika Anne Makinda??Huyu jamaa ni mbishi sana,eti anajua kila kitu,yaani anafanya bunge liwe la ajabu,..
Wabunge makini kama Tundu Lissu wanatoa hoja makini za kuzuia ubakaji wa haki za watanzania, lakini huyu spika wa kupandikizwa anaburuza bunge kwa kusaidiana na wabunge (wa kichina) wa CCM. Nyalandu anaelezewa juu ya misamaha haramu katika EPZ kwa watanzania yeye anaelezea maendeleo ya china(kama alivyo wa China), yaaani kuburuzwa buruzwa tu. Natazama hapa Live natamani kupasua TV.
Hivi hili Bunge ni Bunge ama Bungo?
Wabunge wa ccm Ole Sendeka na Zambi wameigeuka kambi ya ccm juu ya namna wawekezaji wanavyoinyonya Tanzania kupitia kodi (msamaha wa kodi kwa wawekezaji utachukua miaka 10), wapinzania . Wamesema tunadanganywa kwamba uchumi unakua huku hali inazidi kuwa mbaya kwa wananchi. Je hawa wanakubaliana na wapinzani?
Hii thread sijui imekaaje.Hivi kama hamjui kuandika si muache.
Nimeipenda hii.....Kweli ngoma nzito leo Bungeni kwa chama changu ccm. Mh Nkono ameshindwa hoja kuhusu madiwani. amejichanganya kihojaWaziri Lukuvi. ngoma nayo kidogo nzito. kama mpira basi leo chadema ni baka na CCM ni man u FINAL kombe la ulaya.Mh Lissu kweli leo kiboko. hasa kuhusu kodi.hongera chadema. Tunataka hoja hizi na bajeti yenu kwenye magazeti yanakupigieni zumari kama mwanahalisi
Hao sijui Dhambi au Zambi, Simba, na Ole si unaona majina yao yalivyo? Unafikiri wapo kumtetea Mtanzania?
Kwa hoja waliyoitoa leo lengo lilikuwa ni kwa manufaa ya wananchi. Ila wenzao wamewageuka.Hao sijui Dhambi au Zambi, Simba, na Ole si unaona majina yao yalivyo? Unafikiri wapo kumtetea Mtanzania?