Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

Naona Bunge linakosa demokrasia. Spika anapitisha maamuzi kwa nguvu bila kusikiliza wabunge!
 
Hii ya Mnyika ya kupunguza msamaha wa kodi kwa wawekezaji inayotozwa na Halmashauri kutoka miaka 10 hadi mitano isipopita basi nitapata jibu
 
Wabunge wa ccm Ole Sendeka na Zambi wameigeuka kambi ya ccm juu ya namna wawekezaji wanavyoinyonya Tanzania kupitia kodi (msamaha wa kodi kwa wawekezaji utachukua miaka 10), wapinzania . Wamesema tunadanganywa kwamba uchumi unakua huku hali inazidi kuwa mbaya kwa wananchi. Je hawa wanakubaliana na wapinzani?
 
Hivi Nyarandu alifaulu darasani kweli??? kichwa kigumu!!! Yaani mpaka Simbachawene kamwamsha lakini bado haelewi kabisa kitu kinaitwa maslahi ya watanzania, haelewi kabisaaaa. Yeye na siasa za peremende tu, kweli mawaziri tunao!!!!
 
Haya Nyarandu, wewe unaelezewa juu ya 'internal tariff', wewe unalipotosha Bunge kwa kuzungumzia 'external tariff' ambayo hata Kenya wameikataa, ameelimishwa na Mnyika, bado anaendelea na kichwa ngumu oooh nilikuwa natoa mfano, ooh fursa kwa wa wekezaji, upuuzi mtupu. Hivi anatuthibitishia kuwa serikali inataka kuwalamba miguu wawekezaji kuwanyonya watanzania kwa mitaji ya kimachinga ya SHs 150 milioni ambayo haifikii vijisenti vya Andrew Chenge!!!! HATUNA MAWAZIRI.
 
Wabunge makini kama Tundu Lissu wanatoa hoja makini za kuzuia ubakaji wa haki za watanzania, lakini huyu spika wa kupandikizwa anaburuza bunge kwa kusaidiana na wabunge (wa kichina) wa CCM. Nyalandu anaelezewa juu ya misamaha haramu katika EPZ kwa watanzania yeye anaelezea maendeleo ya china(kama alivyo wa China), yaaani kuburuzwa buruzwa tu. Natazama hapa Live natamani kupasua TV.

Hivi hili Bunge ni Bunge ama Bungo?

Lile ni jumba la soga, ndio maana wengine utawaona wamelala wanawaza mashimo na vizibo tu.
 
Wabunge wa ccm Ole Sendeka na Zambi wameigeuka kambi ya ccm juu ya namna wawekezaji wanavyoinyonya Tanzania kupitia kodi (msamaha wa kodi kwa wawekezaji utachukua miaka 10), wapinzania . Wamesema tunadanganywa kwamba uchumi unakua huku hali inazidi kuwa mbaya kwa wananchi. Je hawa wanakubaliana na wapinzani?

Hii thread sijui imekaaje.Hivi kama hamjui kuandika si muache.
 
Tatizo wanaweka ushabiki wa kichama mbele, ibara wanayoipigania ya serikali kutotoa msamaha wa kodi kwa miaka 10 kwa EPZ inafanana na hoja aliyoitoa Mnyika kabla, kwa kuwa walimzima Mnyika kiushabiki wa kichama sasa hoja ya kada mwenzao wanashindwa kuitetea because maudhui ni yaleyale. Halaf wabunge wa ccm ni wapuuzi kweli, wamepitisha kwa ndiyo kubwa yale yale waliyoyapinga Sendeka, Selukamba na Zambi.
 
Hao sijui Dhambi au Zambi, Simba, na Ole si unaona majina yao yalivyo? Unafikiri wapo kumtetea Mtanzania?
 
Hivi mnajua Makinda hakuchaguliwa na wananchi wake? Labda ndiyo maana anawabana wawakilishi wa kweli wa wananchi. LEO KINDA AMEFANYA UAMUZI ''KIDOMOKRASIA''
 
Kweli ngoma nzito leo Bungeni kwa chama changu ccm. Mh Nkono ameshindwa hoja kuhusu madiwani. amejichanganya kihojaWaziri Lukuvi. ngoma nayo kidogo nzito. kama mpira basi leo chadema ni baka na CCM ni man u FINAL kombe la ulaya.Mh Lissu kweli leo kiboko. hasa kuhusu kodi.hongera chadema. Tunataka hoja hizi na bajeti yenu kwenye magazeti yanakupigieni zumari kama mwanahalisi
Nimeipenda hii.....
 
Bunge likiwa na akina Lissu watatu na wawe kwenye kambi ya upinzani nami niambiwe nateuliwa kuwa waziri nitakataa. Jasho linamtoka Nyalandu ambaye anajitahidi kuiokoa serikali dhidi ya hoja za Lissu. Tundu Lissu anasema huyu waziri mdogo hatuammbii kitu.
 
Wanaanza kufurukuta baada ya kuhakikisha kuwa wameshapiga kura ya pamoja ya kuidhinisha huo ukoloni mambo leo. Wakafie mbali hao. Ni wasaliti wa jitihada za ukombozi wa mtanzania.

.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom