Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!Willie @ NYC, USA.
Dear Willie,The the point that aanze Slaa wengine wafuate is way too low for you to make for the following reasons:1.The rulling party and government-responsible for the revenues and expenditures has very awkwardly rejected the move in parliment, contradicting their own promise for additional revenues and reduced expenditures. Sasa nani amkate Slaa kodi, na nani atakayeiga? PM, AG, na wabunge wa CCM ndipo watakapoelewa umhimu wa hili suala?It sounds like u are making awkward ridicule of an important topic!2.Hoja yako ya Taifa kwanza iko wapi? Kama kweli unaimaanisha, rejea my first bullet na urevisit coment yako. Pili, mtetea maslahi ya Taifa yeyote atatambua living champions wakuu wa kutetea maslahi ya taifa hili-akiwemo Slaa-na atawaheshimu. Unapochomeka vijembe juu yake ktk serious topic unajitia madoa na unafanya tu watu wakushangae/wakutilie shaka zaidi!
 
Nimekerwa sana na misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini. Mawaziri kila wanapoulizwa maswali kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo, wanajibu tatizo ni fedha. Wakati wanawasamehe wageni mabilioni ya fedha. Ni ujinga mtupu.
 
- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!Willie @ NYC, USA.
Dear Willie,Your point that aanze Slaa wengine wafuate is way too low for you to make for the following reasons:1.The rulling party and government-responsible for the revenues and expenditures has very awkwardly rejected the move in parliment, contradicting their own promise for additional revenues and reduced expenditures. Sasa nani amkate Slaa kodi, na nani atakayeiga? PM, AG, na wabunge wa CCM ndipo watakapoelewa umhimu wa hili suala?It sounds like u are making awkward ridicule of an important topic!2.Hoja yako ya Taifa kwanza iko wapi? Kama kweli unaimaanisha, rejea my first bullet na urevisit coment yako. Pili, mtetea maslahi ya Taifa yeyote atatambua living champions wakuu wa kutetea maslahi ya taifa hili-akiwemo Slaa-na atawaheshimu. Unapochomeka vijembe juu yake ktk serious topic unajitia madoa na unafanya tu watu wakushangae/wakutilie shaka zaidi!
 
Dear Willie,The the point that aanze Slaa wengine wafuate is way too low for you to make for the following reasons:1.The rulling party and government-responsible for the revenues and expenditures has very awkwardly rejected the move in parliment, contradicting their own promise for additional revenues and reduced expenditures. Sasa nani amkate Slaa kodi, na nani atakayeiga? PM, AG, na wabunge wa CCM ndipo watakapoelewa umhimu wa hili suala?It sounds like u are making awkward ridicule of an important topic!2.Hoja yako ya Taifa kwanza iko wapi? Kama kweli unaimaanisha, rejea my first bullet na urevisit coment yako. Pili, mtetea maslahi ya Taifa yeyote atatambua living champions wakuu wa kutetea maslahi ya taifa hili-akiwemo Slaa-na atawaheshimu. Unapochomeka vijembe juu yake ktk serious topic unajitia madoa na unafanya tu watu wakushangae/wakutilie shaka zaidi!

Good..!!
 
siyo rahisi ccm kujipinga wao wenyewe kwa kisingizio kuwa eti ni maamuzi ya chama.
 
mimi napendekeza kuwekwe mfumo wa kubonyeza button. Na matokea kuonyesha kwenye screen ya spika. Kama ndiyo press green, kama siyo press the red button. Hii itapunguza wabunge wanaofuata mkumbo wa ushabiki. Hakuna haja ya kupaisha mayoe yao.
Hata mimi nilikuwa nafikiria hiki kitu, it is a very simple system haihitaji hata kununua nje, ni project ya vijana wa mwaka wa tatu wa computer/telecom Engineering pale chuo kikuu. System hii inatakiwa iwe inakuwa verified kila siku na kikundi cha wabunge wa vyama vyote kabla ya kuanza kuitumia siku hiyo.Jana nilikasilika sana pale Bi mkora alipopeta kwenye hoja ya mnyika ilihali waliomuunga mkono walikuwa ni wengi zaidi ila huyu bibi akapoteza akajifanya hakusikia kelele za zitto.Huyu bi mkora ni wa kudili naye asirudi kabisa bungeni 2015 iwe adhabu yake.
 
nasikia obama atakuja Tz sasa cjui anakuja Wekeza nini,mana Barick mining Bush anahisa pale,ndo mana haki kupatikana ni ngumu.
Bi Hilary Clinton tayari naye ameshachukua chake kwani Amerika huwa hawafungi safari za bure ama za misaada.
 
Viboko alivyochapa Mh Mbowe mbona katumia mabua ya mtama tu. Angetumia vya ngozi halisi ya kiboko vifuatavyo:
-RUZUKU kwa vyama vya SIASA ifutwe.
-VITI MAALUM bungeni vifutwe.
-Idadi ya MAJIMBO ya UCHAGUZI ipunguzwe. Kila Halmashauri/ Manispaa/Mji iwe na Mbunge mmoja tu.
-Idadi ya Mawaziri na wizara itajwe ndani ya KATIBA ya JMT.
-Tume ya Utumishi ya Bunge ifutwe kabisa.
 
Inaonekana Wabunge wa CCm wapo kutetea Posho sio maslahi ya nchi hii inasikitisha sana,badala wapitie mikataba mibovu ya madini ili Serekali ipate mapato ya kutosha na wananchi wafaidike wanaishia Bla bla bla Posho zisifutwe
 
CDM wakitoka bunngeni waje kwa wananchi ili ujumbe ufike mbali zaidi,bado kuna kazi ya kufanya. Wabunge wa CCM inaonekana wameambiwa wakiingia mjengoni akili za kufikiria waache mlangoni!
 
- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!

Willie @ NYC, USA.

Kwa nini unaamini ikianza kwa Slaa na sio kwa Mukama ndo wengine watafuata? Kwani utekelezaji wa sheria huanza kwa baadhi ya watu na kidogo kidogo kusambazwa kwa wengine, na sio kwa watu wote kwa mara moja?
 
Hata kama wanapitisha hoja zisizo na tija kwa kigezo cha wingi wao ,historia itakuja kuwahukumu,ccm haina wabunge wazawa ,wanazidi kujichimbia kaburi la kisiasa,watanzania wa leo wana ufahamu mkubwa,watu maisha magumu,eti mwekezaji asitozwe kodi miaka 10,nashauri tucta waitishe maandamano ili watumishi wa umma nao wasilipe kodi walau kwa miezi mitano tuone posho wanazogombania wabunge wa ccm zitatoka wapi.hii si haki
 
Napenda kumpongeza sana kumpongeza Mh.Tanguu Lwisuuu kwa Hoja yake kuhusu Wizi unaofanywa na wawekezaji kwenye Madini yetu!Huu ndio mjadala wa maana kabisa kwa sasa kuufanya sisi Watanzania,hatuwezi kuwa Wapumbavu kiasi hiki kukaa kujadili mambo ya Posho na krudisha mashangingi wakti tunasahau WIZI MKUBWA unaofanywa na wawekezaji Matapeli kwenye kwenye Sekta ya Madini.

Ni sawa na kumfukuza kwa nguvu zote sisimizi aliyebeba Punje ya Mchele huku ukiwasahau Wezi wanaobeba Magunia ya mchele ndani ya nyumba yako.Nielweke wazi kwamba siukatai mjadala wa posho,ila naona sio wa Msingi kwakuwa tunaadhimisha Miaka 50 ya uhuru wetu na hatuwezi kusema kwamba POSHO sababu inayofanya Taifa letu liendelee kuwa Maskini mpaka sasa hivi.Mtu makini kama LISWUU Hawezi kusimama kujadili mambo madogo madogo kama hayo!


Inasikitisha sana kuona kwamba mjadala wa Posho za Wabunge na Watumishi wa Serikali umechukua muda mwingi sana katika Bunge la bajeti na hii na vyombo vya Habari Tanzania,mimi nasikitika sana,naona Taifa letu linaelekea pabaya,na Wanasiasa wetu wamfilisika sana Mawazo

Hivi ni kweli Posho za Wabunge na Watumishi wa Serikali ndio sababu ya msingi ya Umaskini wa Taifa letu la Tanzania?
Mbona wanasiasa mumefilisika mawazo kabisa,kabisa kabisa ,kabisa,mnasahau kujadili mambo muhimu na kero za wananchi mnajadili Posho usiku na Mchana?Posho ni Pesa,ni kweli kwamba Posho ndio sababu la Umaskini wetu?kwelli ninyi Wabunge,wasomi na Ma Dr wengine ma Prof. Mnatuambia kwamba POSHO,POSHO,POSHO,POSHO ndio tatizo la Umaskini wa Watanzani? Mimi nasmea,mumefiliska mawazo! Tatizo la Tanzania ni:-

1.Katiba ya kizamani na Sheria mbovu zilizopitwa na Wakati.

2.Elimu Duni
Hatujawekeza kwenye Elimu vya kutosha na tumekimbilia kwenye Kilimo kwanza!Je Watu wasio na Elimu wanaweza kulima,kufuga na kufanya Uvuvi wa Kisasa?Je '' Si Elimu Kabla na Kilimo Kwanza''? au ''KILIMO KWANZA''!!!!

3.Uzalishaji Duni
Nchi yetu haizalishi,Viwanda vimeuzwa kwa wawekezaji wezi,Sekta ya Kilimo haijapewa kipaumbele na uzalishaji ni Duni

4.Rushwa na ufisadi

4.Wizi wa Rasilimali za Taifa Letu
Wawekezaji matepeli wanachimba madini yetu,dhahabu na kupora Mabilioni ya Utajiri wa Taifa letu na tuawasamehe Kodi juu,nadhani Posho ni kama tone la maji katika bahari ya wizi unaofanywa wa wawekezaji kwenye Sekta ya Madini na zinginezo

5.Ukosefu wa Ajira kwa Vijana
Kutokana na sababu nilizotaja hapo (1 hadi 4) imepelekea ukosefu mkubwa wa Ajira kwa mamilioni ya Vijana wa Kitanzania,Viwanda vimekufa,Kilimo Duni,Sekta Binafsi haikui,Ajira zitatoka wapi?Maelfu ya Vijana hawana Ajira!

6.Huduma za jamii zilizo Duni,kama maji,miundombinu ya usafiri,Makazi,Hospitali na Madawa na nk
Mamia ya akina mama wanafariki kwa kukosa Huduma bora za Afya hasa vijijini,Hospitali hazina Dawa,Foleni,Usafiri usio wa Uhakika( mfano wa Reli umekufa)

7.Mfumuko wa Bei na kupanda kwa Gharama za Maisha amabako si kwa kawaida

Wabunge,jadilini Wezi wa Madini yetu,je Madini tunaibiwa Shs. Ngapi?What is Posho za Wabunge Bwana!!!!!! Tuambieni nani anachimba Chuma Chetu,tuambie Dhahabu inapatikana kwenye Migodi yetu?Tuambieni mliowasamehe Kodi wamemsaidiaje mama Swema wa Kijiji cha Tujitegemee kule masasi Mtwara au kwigineko?Mnajadili Hoja za Posho?Posho?This is non-sense!
 
BAJETI ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2011/12 ilipitishwa bungeni mjini Dodoma jana jioni katika mazingira yaliyoibua upinzani mkali kati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi na wale wa upinzani wakiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akisoma majumuisho ya bajeti hiyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo aliwataka wabunge kupima wenyewe kuhusu hoja za ama kuendelea kulipwa posho wanazostahili au la.

Mkulo ambaye wakati akisoma majumuisho hayo alikiri kwamba suala la posho liliibua mjadala alisema serikali ilikuwa imeshachukua maamuzi mapema kabisa kuhusu haja ya kupunguzwa kwa posho zisizo na tija kwa watumishi wote wa umma.

Akifafanua alisema serikali katika uamuzi huo ilishatangaza kuzipunguza posho zinazojumuisha safari za viongozi nje na ndani ya nchi na zile zinazogusa maeneo ya uendeshaji wa warsha na semina.

Waziri Mkulo alisema uamuzi huo wa kupunguza kodi zisizo na tija alishautangaza wakati alipowasilisha bajeti yake Juni 8 mwaka huu na kwamba kipengele hicho kipo katika aya ya 63 ukurasa wa 50 hadi 54.

Akifafanua kuhusu kiwango cha posho, Mkulo alisema posho zote kwa ujumla ni sh bilioni 312.74 kati ya hizo fedha hizo bilioni 25.68 ni posho za vikao (Sitting Allowance).

Alisema iwapo wabunge watatafakari na kuridhia kufutwa kwa posho zao, serikali itaokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.92.

Mbali ya hilo, mkulo alitangaza uamuzi wa serikali kukubali kufanya marekebisho katika bajeti ikizingatia hoja mbalimbali za wabunge ikiwamo ile ya kukubali kushusha viwango vya ushuru wa mafuta ya diseli.

Waziri Mkulo alisema serikali imekubali kurekebisha ushuru katika diseli kutoka sh 314.5 kwa lita hadi sh 256.

Kwa upande wa tozo katika mafuta ya diseli, Mkulo alisema imepunguzwa kwa sh 224.5 kwa lita wakati ushuru wa kodi ukipunguzwa kwa sh 100 kwa lita, ili kuondoa ushawishi wa uchakachuaji mafuta na kukwepa kodi.

Kuhusu mafuta ya taa, alisema ushuru wake utarekebishwa baada ya Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kupitia wataalamu wake kufanya hesabu, ili kuona namna ambavyo suala hilo litaweza kusaidia uchakachuaji na kwepaji kodi.

“Pamoja na hatua mbalimbali serikali itachukua kwa tahadhari hatua za urekebishwaji wa bei ya mafuta,” alisema Waziri Mkulo.

Hata hivyo, wakati wa kupiga kura ili kuamua hatima ya bajeti hiyo, wabunge wote wa vyama vya upinzani walikataa kuunga mkono bajeti hiyo.

Akitangaza matokeo ya kuungwa mkono au kutoungwa mkono kwa bajeti hiyo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alitangaza kuwa wabunge waliopiga kura walikuwa 315 kati ya wabunge 350.

Alisema kati ya hao wabunge 81 walipiga kura ya hapana wakati 234 waliiunga mkono hali ambayo ilimfanya Spika kutangaza waliosema ndiyo kushinda hivyo bajeti hiyo kupitishwa.

Hatua hiyo ya Bajeti kupita katika mazingira hayo, ilisababisha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kuitisha kikao na waandishi wa habari na kutangaza uamuzi wake wa kupinga kupitishwa kwa bajeti hiyo.

Mbowe, alisema chama chake hakitochukua posho sambamba na yeye binafsi kurudisha gari aliyopewa kama mkuu wa kambi hiyo.

Alisema Waziri Mkulo amewadanganya wananchi na Bunge kwa kutaka kuwachonganisha kutokana na kuacha hoja ya maana ya posho (Sitting allowance) na kuwazungumzia wanajeshi wastaafu pamoja na jeshi la polisi.

“Mkulo anawadanganya wananchi anaacha mjadala wa maana anakuja kutaka kutuchonganisha na wazee wetu wastaafu. Sisi hatukusema huko tumesema tunahitaji posho za wabunge zifutwe na sisi ndio tulioanza; hatuchukui posho hizo kuanzia kesho na hata hatutasaini karatasi za kuchukua posho,” alisema Mbowe.

Hata hivyo, alisema leo atarudisha gari la kambi ya upinzani, mafuta na dereva wao na kurudi kuendesha magari kama ya wabunge wenzake na kuongeza kuwa hakuna haja ya kuwa na magari ya anasa wakati Watanzania wakifa kwa njaa.

Alisema pamoja na serikali kukubali baadhi ya vipengele vyao vya bajeti kama vile kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petroli na dizeli, kupunguza kiwango cha faini ya makosa barabarani kutoka sh 300,000 hadi 50,000 hadi kufikia ukomo wa sh 30,000.

Alisema mambo mengine waliyochukua ushauri kutoka kwao ni pamoja na kufuta leseni za biashara kwenye majiji, halmashauri za wilaya na vijiji, kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi nchini.

Alieleza kuwa serikali imekubaliana na chadema katika kuongeza pesa kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya mikopo.

Katika bajeti hiyo pia alitaja mambo ambayo serikali haikukubaliana na hoja ya kufuta au kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo makampuni makubwa ya madini yanapata, ili kuhakikisha serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Serikali pia imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee.

Hata hivyo, alisema serikali haijakubaliana na hoja yao ya kuhakikisha kuwa wanapunguza gharama za safari na hasa kuhakikisha kuwa wanapunguza gharama za safari hasa kwa kutumia daraja la kwanza ambao ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu.

Alisema mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili na viongozi wengine wote wa umma na utumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafari kwa kutumia daraja la kawaida.

“Hata hivyo, misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya nchi, kwa maana hiyo sisi CHADEMA tumeamua kumwandikia barua Katibu wa Bunge, ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho,” alisema Mbowe.
 
Back
Top Bottom