Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

Je, ni halali viongozi wanaotarajiwa kuzijua sheria kama Mwanasheria MKUU WA Serikali kutumia maneno ya kejeli na ya tharau kwa Wabunge wenzake hasa wale wa CHADEMA ?
Hebu fikiria imefikia hata Spika Makina pamoya na upendeleo wake wa wazi kwa CCM ameamua kukemea kitendo cha Warema

Swali : Nini hatua anayopaswa kuchukuliwa huyu Warema kwa Ubabe wake ?
Si huyu huyu alikuwa na kiburi cha kusema ati Tanzania haihitaji katiba Mpya ?

Taarifa kamili soma hapa :
Jaji Werema achafua hali ya hewa bungeni
 
- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!

Willie @ NYC, USA.

Ninachoshangaa viongozi na watumishi wa serikali wanaopata posho ziada ya mishahara pindi wabunge wa upinzani wanapojenga hoja ya kupunguza matumizi ya serikali kwa kukata kodi na kuondoa posho zisizo za lazima kama posho za vikao, kwa nini waambiwe wanafanya hivyo kwa kutafuta umaarufu? Ye yote mwenye mwelekeo wa kutetea maslahi ya umma basi ni mtafuta umaarufu, nani sasa atapokeleka kama mteteza wa haki za raia?
 
Je, Serikali ya CCM itaendelea kuwadanganya Watanzania hadi lini ? Mtakumbuka walikuja na bajeti inayosema ati ni ya kukata matumizi yasiyo na ulazima na kwamba vyazo vyote vinavyopoteza mapato vingeondolewa. Hawakujua kwamba CHADEMA ni watendaji na sio wapiga domo. Wameanza kuumbuka na kuonyesha wazi unafiki wao pale CHADEMA walipoamua kwa vitendo kuondoa matumizi ya posho ya viongozi wa serikali pamoja na wabunge, kufuta safari zisizo na lazima, kuacha matumizi ya mashangini (magari) ili yauzwe, ili fetha zitakazo patikana ziende kwenye hosipitali zisizo na dawa na pia kuwaajiri walimu nk, nk.

Cha kushangaza ni pale, ambapo badala ya kuunga mkono juhudi hizi za thati za CHADEMA zilizoonyesha kuunga mkono kile kilichoitwa na CCM kupunguza matumizi, wao CCM wakiongozwa na waziri wa Fetha - Mkulo, Waziri Mkuu - Pinda, Makinda, Warema, nk, nk wakaamua kupinga mapendekezo rasimi ya CDM !

Je, hili linaingia akilini kweli ?
Je, kama CCM ilikuwa na nia thati ya kupunguza matumizi, mbona sasa hawakubaliani wala hawatoi mapendekezo yoyote ya msingi kuzuia upotofu wa fetha na kodi za wananchi ?
Wakuu, Naomba msaada wenu kwa hili ili nielewe nini kinachoendelea hapa !
 
Spika ANNA MAKINDA! damu ya watanzania tena maskini itakuwa juu yako!Yaani unapitisha swala nyeti la msamaha wa kodi kwa wawekezaji kimzaa hivyo kisa ni wazo la mpinzani?.Hama kweli bunge limekuwa km uwanja wa wa maigizo na sehemu ya kuendelea kutuumiza watanzania badala ya kutukomboa. Mi nasikia uchungu sana. 00
 
- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!Willie @ NYC, USA.
William,Unachosema ni sawa mkuu haiwezekani wengine walipe kodi wengine wasamehewe....tatizo wale jamaa wa chama chako walipinga hii hoja ya Lisu, Lissu anataka kusiwepo na sheria ya kusamehe kodi kwenye posho, wenzako chamani wanataka huo msamaha ili waendelee kupeta
 
T.K. magamba vichwa vigumu sana kuelewa, kinachoongelewa ni mfumo si kufukuza mbuzi moja tu ndani ya shambani na kuwaacha wengi waendelee kumaliza mazao.
 
Je, Serikali ya CCM itaendelea kuwadanganya Watanzania hadi lini ? Mtakumbuka walikuja na bajeti inayosema ati ni ya kukata matumizi yasiyo na ulazima na kwamba vyazo vyote vinavyopoteza mapato vingeondolewa. Hawakujua kwamba CHADEMA ni watendaji na sio wapiga domo. Wameanza kuumbuka na kuonyesha wazi unafiki wao pale CHADEMA walipoamua kwa vitendo kuondoa matumizi ya posho ya viongozi wa serikali pamoja na wabunge, kufuta safari zisizo na lazima, kuacha matumizi ya mashangini (magari) ili yauzwe, ili fetha zitakazo patikana ziende kwenye hosipitali zisizo na dawa na pia kuwaajiri walimu nk, nk.

Cha kushangaza ni pale, ambapo badala ya kuunga mkono juhudi hizi za thati za CHADEMA zilizoonyesha kuunga mkono kile kilichoitwa na CCM kupunguza matumizi, wao CCM wakiongozwa na waziri wa Fetha - Mkulo, Waziri Mkuu - Pinda, Makinda, Warema, nk, nk wakaamua kupinga mapendekezo rasimi ya CDM !

Je, hili linaingia akilini kweli ?
Je, kama CCM ilikuwa na nia thati ya kupunguza matumizi, mbona sasa hawakubaliani wala hawatoi mapendekezo yoyote ya msingi kuzuia upotofu wa fetha na kodi za wananchi ?
Wakuu, Naomba msaada wenu kwa hili ili nielewe nini kinachoendelea hapa !

Bado hujajua kwamba sikio la kufa halisikii dawa?
Kwa sasa serikali imeongeza utamu wa maandamano ya mikutano ya Chadema kuongeza idadi ya watu na wanachama.
 
Wabunge wengi wako kwa maslahi yao hili linahihirika inapokuja suala la kukata kodi kwa mishahara na posho. Kenya waliliweka kwenye katiba mpya lakini utekelezaji wabunge hao hao ndiyo wamekuwa wa kwanza kuvunja katiba yao mpya kwa kukataa kulipa kodi eti wanakazi nyingi halafu mshahara na marupurupu ni midogo,
Hapa kwetu bongo ndo hayo tunasikia bungeni, wabunge wa ccm wanataka wananchi tuumie kwa kodi lakini wao waendelee kuneemeka na posho lukuki
 
Huu mtindo wa kura za sauti za 'ndiyo' au 'sio' kuna wakati naona spika anahukumu kwa kujiangalia ye binafsi anapendelea nini, nadhani bora wangekuwa wanasimama pale ambapo utata unajitokeza wa sauti kuwa 50/50 na inapoonekana bado utata ni bora kura zitumike tu.
 
Kila kitu kina mwisho watanzania wanasikia,wanasoma,pia wanaona,Maisha ya sasa yanamgusa mtanzania wa chini,na wengi wao wapo vijijini,Pia wao wanayaona haya.Hivi kwanini watu wa Nje ya DAR wameamasika mno ya kuunga harakati za maadamano ya CDM.Jua kuwa sasa ali ni mbaya tena sasa.Aliyekuwa anapa sh 5,000/= miaka 2 iliyopita sasa anatakiwa kupata sh 15,000/= na njia hilehile,imekuwa ngumu tena sasa kuipata,Bunge lilitegemewa kuibana serikali lakini imekuwa ngumu,Je Mchezaji kama MESSI anapata umaarufu kwa kuingia tu uwanjani au vitu anavyovionyesha uwanjani,au uwa anataka kuonekana kwenye luninga.?
 
Maskini wabunge wa CCM hawajui wanachokifanya mjengoni. Si mmemwona yule Kigwangala, H jana alisimama mishipa imemwiva kupinga hoja ya Tundu Lissu kutaka muda wa misamaha ya kodi kupunguzwa? Kumbe ni hivi juzi tu aliongoza maandamano ya wananchi wake jimboni kupinga utaratibu wa serikali ya chama chake kuruhusu wawekezaji kuvuna bila kulipa kodi kwa manufaa ya wananchi! Hawa ndio wabunge wetu Tanzania bana! Eti tupate maendeleo, thubutu! Tusubiri tu ngwe ya CHADEMA 2015 kuanza mikakati ya maendeleo.
 
kawaziri kadoogoooo kwanza yeye ni msaidizi wa waziri kiwizara hana nguvu yoyote huyu
anatakiwa akabebe mafail ya waziri wake dr chami huyu ni kama house boy mbele ya tindu lissu
 
Tanzania Bana, mimi nilipoajiliwa wiki moja baada ya kumaliza chuo hawakunipa msamaha wa kodi kwani nilikuwa sina kitu. mwezi huo huo nikaanza kulipa kodi PAYE, mwaka mmoja baadae bodi ya mikopo ikaniletea barua nao wanadai niwalipe zile fedha walizonikopesha. Ningewaona wa maana kama wangekuwa wanatoa msamaa wa kodi kwa watumishi wanaoanza kazi.
 
hizi si dharau jamani? kwa nini spika awe na nguvu hivi?
mimi napendekeza kuwekwe mfumo wa kubonyeza button. Na matokea kuonyesha kwenye screen ya spika. Kama ndiyo press green, kama siyo press the red button. Hii itapunguza wabunge wanaofuata mkumbo wa ushabiki. Hakuna haja ya kupaisha mayoe yao.
 
Mbowe anaingiaje hapo!!au ilimradi umeandika tu.Inaonekana Mbowe anakunyima sana usingizi na bado hadi mchambie mchanga mwaka huu.
Duuh! Hii kali kuchambia mchanga!! Huyu nafkiri atawafunika wanaochambia rungu au wanaochamba wima
 
Back
Top Bottom