Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

Huyu jamaa ni mbishi sana,eti anajua kila kitu,yaani anafanya bunge liwe la ajabu,ndio maana mhe.rais aliwaomba wananch wa singida wasimpigie kura..anapenda sifa hadi anapitiliza..
Werema anamjua Lisu ,ni nani ,hadi anaugua akiwaza moto wa lisu,Wanaopenda sifa wako Magogoni jumba jeupe.magamba nini!
 
Kweli ngoma nzito leo Bungeni kwa chama changu ccm.
Mh Nkono ameshindwa hoja kuhusu madiwani. amejichanganya kihoja
Waziri Lukuvi. ngoma nayo kidogo nzito. kama mpira basi leo chadema ni baka na CCM ni man u FINAL kombe la ulaya.
Mh Lissu kweli leo kiboko. hasa kuhusu kodi.
hongera chadema. Tunataka hoja hizi na bajeti yenu kwenye magazeti yanakupigieni zumari kama mwanahalisi

Bado hujaacha unafiki tu? Tangu lini ukawa CCM wewe wakati unajulikana kuwa ni CUF
 
Huyu Mh Lisu mi namkubali sana katika bunge hili mpaka nashindwa kuona pengo slaa, is a serious man . Nadhani amedhutu,ameweza na atasongo mbele ktk bunge hili.
Duuuuuuh,Mkuu,Tundu Antiphas Mughwai Lissu ni Mashine Kubwa mno,ameviva kabisa viatu vya mzee wetu mpendwa Wilbroad!!! Lissu is one hell of a Man,a patriotic man with a very fine Mind,I revere him!!
 
Tundu Lisu na wapinzani wote wa kweli wanalitendea haki taifa letu kwa misimamo yao, wasiogope...bandu bandu humaliza gogo la mti. CCM waetikisika, hawajahi kukutana na bunge la namna hii. Ni moto wa kuotea mbali.
 
Kweli ngoma nzito leo Bungeni kwa chama changu ccm.
Mh Nkono ameshindwa hoja kuhusu madiwani. amejichanganya kihoja
Waziri Lukuvi. ngoma nayo kidogo nzito. kama mpira basi leo chadema ni baka na CCM ni man u FINAL kombe la ulaya.
Mh Lissu kweli leo kiboko. hasa kuhusu kodi.
hongera chadema. Tunataka hoja hizi na bajeti yenu kwenye magazeti yanakupigieni zumari kama mwanahalisi

Maleria Sugu, Je Mh. Membe ni Mkristo au Mwislamu? Au kwa sasa hilo la dini ya mtu kwako siyo la msingi tena? Kama ni hivyo umepona, umekuwa mtoto mzuri!
 
Twende mbele turudi nyuma Tundu Lissu ana hoja zilizopangiliwa hasa kuhusu misamaha ya kodi ila tu anashindwa kwa kuwa CCM wanaweza kupiga Kelele kubwa ya ndiyooooooo!!
 
Nahisi kuchefuka kila ninapoangalia kikao cha bunge la Jamhuri ya Muungano! Yaani hawa jamaa hawabadiliki kabisa! Hii "ndiyoooo.....!" kwa kila jambo linalopendekezwa na serikali inazingatia tafakari na utafiti yakinifu au "chetu" lazima kiwe sahihi hata kwa wasiokuwa na hoja?
Halafu kumbe hata wanasiasa wanajua unapofanya jambo bila hoja unakuwa unafanya siasa? Nyarandu anasema swala la misamaha ya kodi si la kupingwa kwa siasa......
 
Malaria futa hiyo siganture yako inatia aibu sana, wewe ni mtu makini husione aibu kujiunga na watu makini wenzako hapo CDM!
 
Duh Lissu amemshika pabaya Dr. Kigwangala. Kwa hoja nadhani CHADEMA na Bungeni kwa ujumla hakuna kama Lissu. Lissu anasema miezi miwili iliyopita Dr. Kigwangala aliandamana kupinga unyonyaji wa kampuni za madini lakini leo anasema wawekezaji wapewe msamaha wa kodi!! Naona Dr. Kigwangala amenyewa na mvua ya mawe.
 
Wakulaumiwa ni wananchi walio wachagua,wabunge wana reflect akili za wapiga kura
zao,utake usitake ndio ukweli wenyewe,...sijui wakazi wa bunda wana akili gani
 
Nyalandu naye amejitutumua. Sijui watu wa Singida wanakula samaki toka wapi
 
Wabunge makini kama Tundu Lissu wanatoa hoja makini za kuzuia ubakaji wa haki za watanzania, lakini huyu spika wa kupandikizwa anaburuza bunge kwa kusaidiana na wabunge (wa kichina) wa CCM. Nyalandu anaelezewa juu ya misamaha haramu katika EPZ kwa watanzania yeye anaelezea maendeleo ya china(kama alivyo wa China), yaaani kuburuzwa buruzwa tu. Natazama hapa Live natamani kupasua TV.

Hivi hili Bunge ni Bunge ama Bungo?
 
Back
Top Bottom