JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari katika Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World.

Soma hapa hotuba nzima

=======

Dkt. Slaa: Hadi kufikia hatua ya azimio hili kuridhiwa na Bunge, ikumbukwe makubaliano ya awali yalifanyika tarehe 28 February, kampuni ya DP World na bandari waliingia kwenye makubaliano yalitokana na shughuli iliyofanyika Dubai expo 2022, hatujaambiwa ni tathmini gani au utafiti gani ulifanyika

Kwenye expo, kwenye maonesho kama yale ya sabasaba Dar es Salaam watu wanaingia kwenye mkataba mkubwa wa kulifunga Taifa, nadhani mnaelewa hiyo maana yake ni nini!

Hadi wakati huu Taifa na watanzania walikuwa hawajapewa taarifa yoyote ile inayohusu mkataba mkubwa wa aina hiyo.

Naomba kuwakumbusha pia kuwa pamoja na mkataba huu, katika Dubai 2020 Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Rais mwenyewe kulisainiwa mikataba 17, nani kati yenu hadi leo hii anaifahamu mikataba 17 inahusu nini, ni usiri mtupu, ni nchi inaingizwa kwenye giza, Rais wa Nchi amehudhuria lakini mambo hayo yote yako ndani ya giza.

Waliohudhuria maonesho ni viongozi wa Serikali, wamesafiri, wamelala hoteli, wamekula chakula kwa kodi ya watanzania, ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa wananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii, jambo ambalo linalazimisha kuwakumbusha uhitaji wa haraka wa katiba mpya na bora.

Hii taarifa tunayozungumzia hatukuipata Serikalini, tumepata taarifa iliyovuja. Ni nchi gani duniani tunasubiri taarifa ivuje tuanze kuizungumzia. Siku siku 30 zilizotajwa kwenye mkataba na Bunge, kwa maneno mengine umeridhiwa ndani ya siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takribani 8, kwa hali hiyo tuna uhakika gani Tanzania ina uwezo wa kutimiza mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza uchelewashaji huo unatokana na nini.

Dkt. Slaa ametoa hoja zifuatazo
  1. Dkt. Slaa: Nchi inayojulikana kisheria ni United Arab Emirates, Je Dubai ni Serikali? Dubai ni mji unaojiongoza, sisi ni nchi ya Jamhuri ambayo maamuzi yetu yanafanyika kwa kutumia Bunge. Bunge lilitangaza wanataka maoni ya wananchi tarehe 5 Juni wanaotoka maeneo mbalimbali wawe wamefika bungeni tarehe 6. Kwa saa 24 mtanzania gani anafika Dodoma na kutoa maoni yake. Ni dhahiri kuliwa na hila na Serikali haikuwa na nia ya kushirikisha wananchi wake. Hatukushirikishwa na imepelekwa bungeni na mjadala ulivyokuwa bungeni ulikuwa ni mjadala wa ki-mangimushi
  2. Aidha ikumbukwe Serikali iliyopo ina legitimacy ya wasiwasi kutokana na uchaguzi wa 2019 na 2020. Simung'unyi maneno, uchaguzi wa 2019 na 2020 inaweza kuwa na legitimacy lakini sina hakika kama uchaguzi huo ulikuwa sahihi, najua ulivurugwa kwa makusudi na chama cha mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye macho haitaji kuambiwa kuhusu hilo na wananchi wote ni mashahidi.
  3. Kwa mujibu wa kifungu cha nne cha IGA kinatamka wazi rasilimali zote zilizotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya kigeni. Rasilimali hizo ni bandari zote za nchi nzima(bahari, maziwa, mito, zitakazokuwepo hata kwenye mabwawa) yale yote yaliyokuwepo leo na hata yatakayokuja. Huu ni uuzaji wa nchi, hakuna mtanzania mwenye akili atakaekubali jambo hilo bila uhakika wa rasilimali zake hizo.
  4. Serikali ya awamu ya nne wakati inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari, aliyetupa taarifa alifukuzwa kazi. Alitupa taarifa ya kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa.
    Dkt. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia hivyo. Slaa amedai kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwasababu ya mafuta wakati nchi inaendelea kupigwa.
  5. Slaa pia ametoa mfano wa 'Entebbe Raid' ambapo amesema ndege ya Air France ilitekwa nyara na wapiganaji wa Palastine wakishinikiza mambo yao ya kisiasa ndani ikiwa na waisraiel ilitua uwanja wa Entebbe. Slaa amedai Waisrael iliwachukua chini ya dakika 90 kuwakomboa watu wao na amedai iliwezekana kwasababu wao ndio waliojenga uwanja na ramani zote walikuwa nazo ikiwepo sehemu ya kuingilia na kutokea.
  6. Slaa amesema sababu hapo juu pia ilisababisha Serikali ya awamu ya tano itumie wajenzi wa ndani kujenga Ikulu lakini sasa bandari zote zinakabidhiwa kwa mgeni.
  7. Dkt. Slaa: Mkataba unaotoa 'exclusive rights' daima uogope, inatoa pia kifungu baadae yatakayojadiliwa kwenye mikataba midogo midogo, unatoa kwanza mali yako, unajuaje wakifika kwenye hiyo mikataba midogo midogo wakikutalia! Una nguvu gani, ulishasain 'exclusive rights'
  8. Utekelezaji wa DP World sio kwamba unaanza Tanzania, katika Afrika peke yake tuna migogoro mingi. Nenda nchi za Ulaya, Brussels ni ya Ulaya lakini wako mahakamani, karibu kote kunakogombaniwa ni rushwa, kuna wabungwe walipelekwa, wakalishwa, wakapewa posho ya dola 2000 yote hiyo ni rushwa. Kama ingekuwa nchi nyingine, hizo zinatosha kufuta mkataba huu na kapeleka hata hiyo kampuni mahakamani.
  9. Sijawahi kuona mkataba(IGA) Marekani na Ulaya ambao una lugha kama hii ya kwetu, waathirika tumewaandaaje mfano ujenzi wa reli bandarini mpaka airport. Tumeona barabara ya Kibaha watu walivyolia Kimara. Mikataba hii lazima iwe ya tahadhari sana.
  10. Tunayasema haya kwa nia njema lakini tunashangazwa na kutishwa na propaganda ambayo Serikali inafanya, jambo jema huwa haliendeshwi kwa propaganda, ukiona mtu anafanya propaganda ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye madhehebu ya dini anza kuweka mashaka, kuna maslahi gani nyuma ya makubaliano hayo!
Dkt. Slaa: Niseme yafatayo
  1. Kwa lugha rahisi, taarifa hii haina lengo la kupinga. Hoja ya msingi ni kukosekana kwa uwazi katika namna ya kushughulia rasimali ya nchi yetu

  2. Vifungu vingi vinavyotia mashaka vinahitaji kuangaliwa upya hata kama mkataba ni mzuri au mbaya, unaweza kuboreshwa kwa kushauriana na wananchi wake. Mkataba wowote hata kama ni mbaya, mzuri unaweza kuboreshwa. Mkataba huu utazamwe upya ili vipengele vyote vyenye utata viondolewe.

    Mfano tunaona mkataba huu wanasema ni nchi nzima, bandari zote. Kwanini tusiseme bandari ya Dar es Salaam, mengine yote tutaingia wakati tumeridhika.

    Mkataba hauweki muda maalum, kwanini tusiseme tutakuwa na mkataba wa bandari kwa miaka 10, tena kuna kifungu kinazungumza hatutaweza kuondoa. Halafu kuna masharti kama tunataka kuondoa tufanye nini, unaweka masharti. Haya masharti yote wanajua ni ya kutupiga, hata mkienda kwenye mahakama ya malalamiko tumeshapigwa tayari. Hata Serikali ikibadilika hatuwezi kuondoa mkataba huu.

  3. Bandari inazungumzia upande mmoja wa Tanzania, nimeshangaa na watu hawakosei. Wanasema Rais ni kutoka upande mmoja wa muungano, waziri wake ni kutoka upande huo huo wa muungano. Tafsiri za watu huwezi kuzifungia kwenye sanduku, huwezi kuzuia watanzania wasifikiri kwasababu Rais anatoka upande huu, waziri wake ndio maana wameuza bandari zetu, mbona zile hazikuuzwa.

    Slaa amesema suala la bandari ni la muungano lakini ameshangazwa kwa Zanzibar kuwa na sheria ya bandari yao. Slaa ameshangazwa na nchi moja kuwa na bandari mbili ilhali sheria ni moja.

    Dkt: Slaa: Mbona hawalielezi hata bungeni hilo, kumbe kuna mambo mengi hata bunge limefichwa na bunge letu jinsi lilivyo la hovyo, naomba radhi sana na waniite kwa hilo, kilichofanyika juzi ni uhuni.
Dkt. Slaa: Natoa wito kwa watanzania wote kwa pamoja tusikubali kupokea upotoshwaji aina yoyote katika mambo yanayotuhusu sisi wenyewe na vizazi vyetu vijavyo. Mkataba huu ujadiliwe upya, uangaliwe upya tuweze kukubaliana vitu gani vifanyike.

Zaidi soma: Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Naam Dr.slaa mzalendo kabisa

Huyu Samia kwa mara ya kwanza nadiriki kusema ni kiongozi asiyefaa hata kidogo

Kwenye picha kubwa ni asilimia mia moja hajali chochote kuhusu Tanganyika mbaya zaidi wale waliomleta kwenye siasa za Tanganyika wanamuunga mkono kwasababu wanafaidika na maamuzi yake yanayohusisha ufisadi mkubwa ikiwemo kuuza nchi! Ukiuza bandari,ukiuza loliondo ukiruhusu madini yatoroshwe wewe umepiga mnada Tanganyika huna tofauti na muhujumu uchumi yule seth

Yaani huyu Rais anaona kwasababu anafanana utamaduni na waarabu basi wanafaa kuuziwa nchi!
Waarabu ni waharibifu, majangili, ukiwapa bandari tarajia kila aina ya uchafu! Ni wazi nchi yetu imezikwa rasmi

Samia ni mwepesi kuzungumizia mambo ya hovyo km simba na Yanga ila kwenye mambo muhimu km kuuzwa loliondo na bandari anakaa kimya kwasababu amehusika

Ukiangalia sura ya samia anawachukia sana watanganyika hana namna kwasababu anavuna kutoka kwao


Jana aliuza loliondo leo ameuza bandari! Bado baadhi ya watanganyika wanamchekea kwasababu wanahongwa mipesa

Mungu atakuadhibu Samia kwa ubaya wa kuiangamiza Tanganyika! Hautadumu apo

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Back
Top Bottom