TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

IMG_20170114_134620.jpg
Fundi akiwa katika kazi ya kapau bweni la wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari Bulunde nzega,

Huu ni moja ya mpango kazi wa mradi wa Tushirikishane uliopo katika jimbo la nzega mjini.
 
1484469598981.jpg
IMG_20170115_111841.jpg
PICHA NI CHUJIO LA MAJI JIPYA KATIKA KITUO CHA MAJI BWAWA LA UCHAMA NZEGA LIKIWA KATIKA MAJARIBIO

Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300 ni moja ya mpango kazi wa mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini

MAENDELEO YA MPANGO KAZI KUU KWA SASA
Ujenzi wa chujio la maji la tatu katika kituo cha maji Uchama umekamilika na hivi sasa chujio lipo katika majaribio, ukamilishaji wa chujio hili ulianza baada ya ukamilishaji wa machujio mawili ya maji mwezi wa tisa mwaka 2016, machujio hayo mawili kwa sasa yanafanya kazi

Kwaiyo ukamilishaji wa ujenzi wa chujio hili la tatu unapelekea uwepo wa machujio manne ya maji katika bwawa la Uchama

Ikumbukwe kipindi mradi wa Tushirikishane unaanza katika jimbo la nzega mjini, kulikuwepo na chujio moja tu la maji katika kituo cha maji bwawani Uchama
 
(11).jpg
IMG-20170115-WA0016.jpg
IMG_20170115_173631.jpg
Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde kazi ya upauaji wa mabweni ilivyokuwa inaendelea imekamilika Siku ya leo tarehe 15 /01 /2017
 
Napongeza kwa jitihata zote za MBUNGE. Nilikuwepo nzega last week kwa kweli kuna jitihada kubwa zimefanyika. Lakini nimeona jengo lla abiria pale stand ni dogo sijui kama litakidhi matakwa
 
mazungumzo mafupi na mwenyekiti wa kijiji cha Nhobola akielezea maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola.
 
Tunaona maendeleo ya maji, shule, na stand vipi kuhusu nyumba ya Daktari mbona tarifa za maendeleo hatuzioni
Tarifa za maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Daktari zipo kiongozi endelea kufuatulia mijadala yetu utaziona asante kwa kuwa pamoja basi katika mjadala huu wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini
 
IMG_20170119_120020.jpg
uujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora

MAENDELEO YA MPANGO KAZI HUU KWA SASA

Kazi ya upauaji nyumba ya Daktari imeanza siku ya tarehe 18/01/2017, kazi hii inategemea kukamilika mwishoni mwa wiki hii
 
1484826277354.jpg
Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega


MAENDELEO YA MPANGO KAZI HUU KWA SASA

Siku ya leo tarehe 19/01/207 ilikuwa ndio Siku ya mwisho ya upokeaji wa maombi ya zabuni ya ujenzi wa mabanda ya biashara katika eneo la kituo kipya cha mabasi Nzega Zoezi hili la utoaji wa zabuni linafanyika hii ikiwa ni awamu ya pili baada ya utoaji zabuni wa awamu ya kwanza kukamilika mwezi wa tisa mwaka 2016

Zoezi hili limekamilika Siku ya leo saa sita mchana, maombi yote yaliopokelewa katika awamu hii ya pili yameanza kufanyiwa kazi Siku si nyingi tutakuja na tarifa ya idadi kamili ya watu waliomba.


SASABU ZILIZOPELEKEA ZABUNI KUTANGWAZWA AWAMU YA PILI

sababu ambayo ilipelekea halmashauri ya mji wa nzega kutangaza zabuni kwa awamu ya pili ni kwa sababu awamu ya kwanza kulikuwa na mwitikio mdogo wa watu waliomba zabuni ulinganisha na eneo ambalo limetegwa ajiri ya ujenzi wa vibanda hivyo ambalo ni kubwa.

Katika awamu ya kwanza idadi ya watu waliomba zabuni ilikuwa ni watu sitini na moja tu (61), waombaji wote sitini na moja (61)wamekizi vigezo katika awamu hiyo ya kwanza na mda wowote kuanzia sasa majina yao yatatangazwa kuwa ni washindi wa zabuni ya ujenzi wa mabanda ya biashara katika kituo kipya cha mabasi Nzega.
 
Maendeleo ni mazuri tunashukuru leo kupata majibu kwanini zabuni ilitanganzwa Mala ya pili, kitu kingine suala la maji tatizo nini maana mashine zipo tunaona machujio tunayaona kama tatizo ni miundombinu ya mitaani kwetu uku ibalisheni basi maana mabadiliko kwenye vyanzo vya maji tunayaona tuwape hongera kwa hilo lakini mtaani uku maji baadhi ya maeneo maji bado tatizo
 
Maendeleo ni mazuri tunashukuru leo kupata majibu kwanini zabuni ilitanganzwa Mala ya pili, kitu kingine suala la maji tatizo nini maana mashine zipo tunaona machujio tunayaona kama tatizo ni miundombinu ya mitaani kwetu uku ibalisheni basi maana mabadiliko kwenye vyanzo vya maji tunayaona tuwape hongera kwa hilo lakini mtaani uku maji baadhi ya maeneo maji bado tatizo
Suala usemalo kuhusu maji ni kweli kiongozi Kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa Maji bado ni tatizo

Suala hili katika ufuatiliaji majibu yake ni kwamba maeneo mengi ya nzega miundombinu yake ya maji kuelekea katika makazi ya watumiaji ni ya kizamani yani maeneo mengi nzega zipo bomba za chuma ambazo Watalamu wanasema bomba hizo kwakua zipo kwa miaka mingi basi zishaweka kutu nk kwaiyo hata yakifunguliwa basi Kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa Maji bado utakuwa ni tatizo

Hivyo basi Kuna ulazima wa kubadilisha miundombinu ya mabomba yaliyopo mtaani kutoa ya chuma yaliyopo sasa na kuweka mabomba ya prastiki
 
Habari ya asubuhi, niwape pongezi sana kwa maendeleo ya kazi hizi. Pili huko nyuma nilizungumzia suala la kupanda miti hasa na sasa tunaona maji yameanza kupatikana. Je kuna plan yeyote ya kupanda miti hapo stendi mpya au katika shule na zahanati zinazoboreshwa. Hiyo stendi inaonekana kama jangwani kabisa na jua linachoma sawa sawa vipi idara ya misitu na mji wanajishughulisha kufanya mji uonekane green. Nafikiri kipindi hiki cha mvua ni kipindi kizuri cha kupanda miti na gharama ya mche mmoja wa mti haizidi shs 2000/=. Dar inabadilika kwa sababu wanapanda miti huko msiwe watazamaji tu, jaribuni kuiga mambo mazuri pia.
 
Habari ya asubuhi, niwape pongezi sana kwa maendeleo ya kazi hizi. Pili huko nyuma nilizungumzia suala la kupanda miti hasa na sasa tunaona maji yameanza kupatikana. Je kuna plan yeyote ya kupanda miti hapo stendi mpya au katika shule na zahanati zinazoboreshwa. Hiyo stendi inaonekana kama jangwani kabisa na jua linachoma sawa sawa vipi idara ya misitu na mji wanajishughulisha kufanya mji uonekane green. Nafikiri kipindi hiki cha mvua ni kipindi kizuri cha kupanda miti na gharama ya mche mmoja wa mti haizidi shs 2000/=. Dar inabadilika kwa sababu wanapanda miti huko msiwe watazamaji tu, jaribuni kuiga mambo mazuri pia.
Tunashukuru kwa mawazo yako kiongozi tutalifanyia kazi suala hili
 
Nahukuru kwa kuliona hilo afisa habari. Ninafahamu viongozi wote (Mbunge, katibu, halmashauri na maafisa wake) wanasoma uzi huu, kwani una michango mizuri sana. Kwa kuwa technolojia ya habari imekuwa sana. Ninawashauri sasa muweke facebook page ya mji ili taarifa zisambae kwa kasi zaidi, ni rahisi pia hata kama mnataka kumobilize funds kwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo kutoka kwa wadau na wananzega ndani na nje ya nchi kwani taarifa inasambaa kwa kasi sana.
 
1485164473580.jpg
IMG_20170123_121317.jpg
kazi ya upauaji nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola imekamilika Siku ya leo tarehe 22/01/2017 kama inavyoonekana katika picha


Ujenzi wa nyumba hii ni moja ya mpango kazi wa mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini.
 
IMG_20170123_121036.jpg
IMG_20170123_121209.jpg
hiki ndio kituo cha afya Nhobola ambacho ujenzi wake ulikwisha kamilika zaidi ya miaka miwili lakini hakifanyi kazi kutokana na ukosefu wa nyumba ya Daktari

Hivyo basi wadau wa maendeleo katika jimbo la nzega katika kachagua vipaumbele vya miradi ambayo walihitaji mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini usimamie ilikuwa ni ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo hiki cha afya Nhobola , nyumba hiyo ujenzi wake unaendelea vizuri, kama unavyoonekana katika tarifa mbali mbali za maendeleo ya mipango kazi minne ya mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini.
 
Safi sana kazi ni nzuri ombi langu Mbunge ajaribu kututafuta watu wa nzega tushio nzega na nje ya mji wa nzega tufanye harambee pesa zitakazopatikana ziende saidia ukamilishaji wa hiyo nyumba ya Daktari pamoja na hayo mabweni ya shule ya bulunde tukisema kila kitu kifanye serikali tutachelewa sana Mbunge
 
TARIFA YA MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE KWENYE JIMBO LA NZEGA MJINI KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OCTOBA 2016 MPAKA JANUARY 207


MAENDELEO YA MRADI

1. Kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega

Katika tarifa iliyopita ya mwezi September mpaka Octoba, ilielezwa kuwa Kuanzia tarehe 17/10/2016 Halmashauri ya Mji wa Nzega ilianza kutoa fomu kwa ajili ya maombi ya zabuni ya ujenzi wa vibanda vya biashara katika kituo kipya cha mabasi Sagara, Nzega. Zoezi hilo lilikamilika tarehe 19/10/2016, na hatua nyingine za ukamilishaji wa upataji wa zabuni unaendelea.


MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OCTOBA 2016 MPAKA JANUARY 2017


Zoezi la kupata wazabuni katika awamu ya kwanza umekamilika na wazabuni sitini na moja (61) wamekidhi vigezo vya kupewa zabuni kama washindi. Hivyo muda wowote kuanzia sasa majina yao yatatanganzwa ili waweze kuanza ujenzi


Kutokana na ukubwa wa eneo lililotengwa kwa jili ya ujenzi wa vibanda kuwa kubwa, Halmashauri iliamua litegwe mara mbili na kila moja liwe na mchakato wake wa zabuni. Kukamilika kwa zabuni ya kwanza kumetoa fursa kwa zabuni ya eneo jingine kutangazwa tarehe 19/01/2017. Mchakato wa tathmini ya kuwapata washindi wa zabuni wa awamu hii bado unaendelea


Vile vile, mwezi huu wa kwanza, kumefanyika jaribio la kupima kiwango cha maji kinachotoka kwa saa kutoka katika kisima kilichochibwa hapo kituoni ili kutambua mashine za aina gani zinaweza kufungwa kwa ajiri ya kusukuma maji katika mantaki ambayo yatatumika kusambaza maji kwa watumiaji hapo kituo cha mabasi.


2. Kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora unakamilika


MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017

Kazi ya upauaji wa nyumba ya Daktari kwa kiwango kikubwa imekamilika kama habari-picha mbali mbali zinavyooneka katika tarifa zetu za kila wiki. Hatua iliyobaki ambayo ndiyo inayofuata ni kupiga lipu.


3. Kusimamia ukamilishaji wa mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa maji safi na salama –Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300


MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI– OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017.

Kazi ya ujenzi wa machujio ya maji matatu umekamilika. Machujio yote kwa sasa yanafanya kazi. Vile vile mashine za kusukuma maji zote tatu zimefungwa na zinafanya kazi. Lakini kutokana na ukarabati wa miundombinu ya maji kwa watumiaji, mashine moja imesimamishwa kwa sasa.


Vile vile idara ya maji bado inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya maji katika mitaa mbali mbali ya Nzega Mjini. Mfano tanki lililopo Pakingi lililokuwa halimfanyi kazi kwa muda mrefu sasa limeanza kufanya kazi. Pia magati ambayo yalikuwa hayatoi maji, likiwemo gati la Pakingi sasa yanafanyakazi. Hii imewezesha upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi kuwa ya uhakika kulinga na ratiba. Haya ni maendeleo na ni tofauti na siku za nyuma ambapo baadhi ya maeneo yalikuwa yanakosa maji katika siku yao ya kuwa kwenye ratiba ya mgao.


Tarifa ya mwezi wa pili, mwaka huu kuhusu maendeleo ya mradi huu itakuja na majibu ni kiwango kipi cha ujazo wa Maji umeongezeka kwa sasa tangu ukarabati huu miundombinu ya maji uanze kwani hivi sasa bado miundombinu ajakamilika vizuri


4. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondaro Bulunde.


MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI – OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017

Ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Bulunde, ujenzi huo mwezi huu wa kwanza 2017 umendelea kwa mabweni hayo mawili kueezekwa kwa bati, hivyo hatua hii inafanya kuwepo na madarasa mawili ya kusomea ambayo yamekamilika pamoja na mabweni ya wanafunzi mawili ambayo yamepauliwa hivyo basi hatua inayofuatia baada ya upauaji wa mabweni haya bado ofisi husika inayohusika na usimamizi wa ujenzi huu ambayo ni ofisi ya serikali ya mtaa wa nzega mashariki hawajaitoa Siku wakitoa mtaipata kupitia tarifa zetu za kila wiki.




Imeandaliwa:


Joseph Sanga


Afisa mawasiliano wa mradi-Nzega
 
Back
Top Bottom