TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

TARIFA FUPI YA MWEZI MACHI 2017 KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE KATIKA JIMBO LA NZEGA MJINI

Mradi unaendelea vizuri kama tarifa ya awali ilivyotoka kuwa katika ahadi nne ambazo zilikubalika ziwe sehemu ya mradi huu katika Jimbo la Nzega ahadi moja tayali utekekezaji wake umekamilika kwa asiliamia mia ahadi hiyo ilikuwa hii hapa


= Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

Utekelezaji wake ahadi hiyo umekamika mwezi uliopita mwezi wa tatu mwaka 2017 ikiwa ni miezi saba tu tangu mradi uanze



Ahadi nyingine tatu ambazo bado azijakamilika ila na utekelezwaji wake bado unaendelea chini ya mradi wa Tushirikishane katika jimbo la Nzega mjini ni hizi zifuatazo


A) Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

Kazi inayoendelea katika ahadi hii ni kukamilisha mchakato wa kutangaza wazabuni walioshinda zabuni ya ujenzi wa vibanda vya Biashara katika eneo la kituo cha mabasi

B) Ujenzi wa Nyumba ya Daktari-Kituo cha Afya Nhobora

Ujenzi wa nyumba ya mganga jengo limeshakamilika na bati tayali limepigwa hatua inayofuata kwa sasa ni upigaji ripu pamoja na uwekaji wa mirango na madirisha

C) . Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde

Ujenzi wa mabweni tayali umekamilika na katika hatua ya kusimamisha mabweni na kuyapaua hatua iliyobakia ni upigaji wa plasta pamoja na uwekaji wa milango na madirisha, vile vile hatua nyingine inayofuata ni kuanzisha ujenzi wa ukumbi wa wanafunzi zoezi la ujenzi huu wa ukumbi unaweza kuaza mda wowote kuanzia sasa.
 
Great, usichoke kutujuza. Natumaini matokeo ya zabuni za walioshinda vibanda stendi yatatangazwa mapema kipindi hiki maji yanapatikana ili ujenzi uwe rahisi.
 
Bwana Sanga hiyo tenda ya ujenzi wa stendi mbona imekawia sana kutolewa majibu, matumaini watu walioomba wamejipanga kwa muda mrefu msiwakatishe tamaa hebu tangazeni watu waanze kujenga wakati huu maji hata ya mvua yanapatikana....
 
Kumbe hata humu jf uongo ruksa, maji ni tatizo kubwa hapa NZEGA mjini.
 
Kumbe hata humu jf uongo ruksa, maji ni tatizo kubwa hapa NZEGA mjini.
Kiongozi ndio maana mjadala upo wazi ili kama unaona kilichosemwa hapa ni uongo njoo na ukweli

Kitu kingine soma malengo ya mradi huu katika Jimbo la Nzega upo nzega ipi na katika suala la maji mradi ulijikita katika eneo lipi kwaiyo tarifa unazoziona hapa ndio zilizofanyiwa kazi suala la shida ya maji katika mji wa nzega haliwezi kuisha lote kwa wakati mmoja kwa sababu

Mji wa nzega unakuwa kuna maeneo yana wakazi ya watu ni mapya hakuna kabisa miundombinu ya maji, watu hao ukiwambia nzega tatizo la maji limetatuliwa katika mpango wa mda mfupi hahawezi kukuelewa

Lakini ukienda maeneo ambayo miundo mbinu ya maji ya bomba ipo tangu zamani ukiwambia wakazi wanzega sasa hivi wana uhakika wa kupata maji kila siku ya mgao maji yanatoka, pia baadhi ya magati ya maji yanatoa maji masaa 24, maji yamekuwa masafi zaidi na zamani hawawezi kukataa maana ndio uhalisia uliopo

Hivyo basi tunaposema changamoto ya maji imetatuliwa tambua tunaongelea Nzega mjini, hususani maeneo ambayo miundombinu ya maji ilikuwepo ila upatikanaji wa maji ulikuwa si wauhakika sana mfano

Mgao ambao ulikuwa haufuati utaratibu
Magati ya maji baadhi kupata maji mara mbili kwa Wiki lakini sasa suala hilo hakuna kwani magati zaidi ya matano yanatoa maji masaa 24, vile vile mgao wa Maji sasa unafuata ratiba nzuri na maji yanatoka

Pia ukumbuke huu ni mpango wa mda mfupi katika kuondoa tatizo la maji katika mji wa nzega kipindi wakisubilia mradi wa maji kutoka ziwa victoria

Karibu tena kwa mchango wako mdau
 
Bwana Sanga hiyo tenda ya ujenzi wa stendi mbona imekawia sana kutolewa majibu, matumaini watu walioomba wamejipanga kwa muda mrefu msiwakatishe tamaa hebu tangazeni watu waanze kujenga wakati huu maji hata ya mvua yanapatikana....
Tunashukuru kwa mawazo yako mdau tutayafanyia kazi
 
Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde

Baada ya ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa mawili na pamoja na ujenzi wa mabweni kufikia hatua ya kuyainua na kuyapaua mabweni hayo ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Bulunde unaendelea tena baada ya serikali kutoa pesa kiasi cha shilingi milioni mia mbili hamsini na tisa , ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema, ili mwaka huu 2017 shule ya sekondari Bulunde iweze kuanza kutoa elimu ya kidato cha tano na cha sita hili ni tangazo la zabuni za ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Bulunde lilotolewa siku ya tarehe 10/04/2017
IMG_20170419_101037.jpg
ikumbukwe hatua ya kwanza kabisa ya ujenzi wa madarasa mawili ya kidato cha tano na cha sita katika shule hii ya sekondari Bulunde ajiri ya kuifanya shule ya Bulunde iwe na kidato cha tano na cha sita ilianzishwa na mh mbunge wa jimbo la nzega mjini mh Hussein Bashe binafsi, badae ofisi ya mbunge ilishirikiana na halmashauri ya mji katika ujenzi wa mabweni mawili kupitia pesa za mfuko wa jimbo.
 
Pongezi kwa serikali kuona jitihada za mbunge wa nzega kuamua peleka pesa zimalizie ujenzi huo wa mabweni madarasa mabara hongereni wana nzega kwa hatua hiyo
 
Bwana josephat sanga vipi kuhusu stand ya mabasi mbona kimya hatuoni tarifa yoyote kuhusu maendeleo yake
 
Miye na swali kuhusu hiyo shule ta Bulunde kuanzisha kidato chi tano Na cha sita nataka kujua hao wanafunzi watakao chaguliwa kwenda kusoma hapo je ni wanafunzi watakao toka katika jimbo la Nzega mjini kwa mbunge Hussen Bashe au ni wanafunzi kutoka sehemu tofauti tofauti inchi nzima watachaguliwa kwenda kusoma hapo
 
Miye na swali kuhusu hiyo shule ta Bulunde kuanzisha kidato chi tano Na cha sita nataka kujua hao wanafunzi watakao chaguliwa kwenda kusoma hapo je ni wanafunzi watakao toka katika jimbo la Nzega mjini kwa mbunge Hussen Bashe au ni wanafunzi kutoka sehemu tofauti tofauti inchi nzima watachaguliwa kwenda kusoma hapo
Kiongozi shule hii itafanya shughuli zake kama shule nyingine za umma nchini kwa kudahili wanafunzi wenye sifa za kujiunga kidato cha tano kutoka sehemu tofauti tofauti inchini kutokana Na mchepuo wake wa kimasomo ambao shule utakuwa ukiendesha
 
IMG-20170422-WA0004.jpg
IMG-20170422-WA0003.jpg
Sherehe za utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi Wa maji kutoka ziwa victoria kuja nzega, kwenda tabora mjini na wilaya nyingine za mkoa wa Tabora, zoezi hili limefanyika Leo siku ya tarehe 22/04/207.
 
Back
Top Bottom