TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Wana Nzega vp katibu wa mbunge na afisa habari kimya shwari lakini....Niwatakie Sikukuu njema na heri na baraka nyingi ktk 2017. Natumai 2017 utakuwa wa mafanikio zaidi
 
(2).jpg
ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola

MAENDELEO YA MPANGO HUU
Jengo limekamilika takribani mwezi mmoja na nusu tangu jengo likamilike kama tarifa ya awali ilivyoelezea hatua iliyokuwa imebakia ni upauaji

Hatua hiyo ya upauaji haikwenda kwa wakati kutokana na sababu zile zile za awali za ukosefu wa pesa ambazo zipo benki kwani awali uongozi wa kijiji uliweza kuchukua pesa benki kwa kupitia mtia saini wa mda mfupi ambaye ndani ya kipindi kifupi ilitajika huyo mtia saini awe amethibitishwa kuwa mtia saini wakudumu kwakua mtendaji wa kijiji hayupo ilipaswa uongozi wa kijiji ukaimishe huo utendaji wa kijiji kwa mtumishi yoyote wa umma ambaye anafanya kazi katika kata hiyo ya Mbogwe

Zoezi hilo la ukaimishwaji wa mtendaji wa kijiji kwa mtumishi yoyote wa umma halikwenda kwa wakati mpaka ujenzi wa boma umekamilika, hivyo basi uongozi wa kijiji ulipoenda kuchukua pesa benki hawakukubaliwa kutokana na kaimu waliyemuweka katika nafasi ya utendaji hakuwa mtumishi wa umma hivyo wakaobwa wabadilishe wa muweke kaimu ambaye ni mtumishi wa umma

Hatua zimefanyika kaimu mtendaji wa kijiji ambaye ni mtumishi wa umma amekwisha patikana, vile vile uongozi wa kijiji ambao unahusika na masuala ya ujenzi imekwisha Kaa Siku ya ijumaa ya tarehe 23/12/2016 kuandaa makadilio ya pesa inayoitajika ajiri ya upauaji wa jengo hilo hivyo mda wowote kuanzia sasa ujenzi wa nyumba hii ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola unaendelea.
 
Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

MAENDELEO YA MPANGO KAZI KUU KWA SASA
Halmashauri ya mji wa nzega imetangaza tena zabuni za ujenzi wa vibanda vya biashara katika kituo kipya cha mabasi Nzega, mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19/01/2017


Kwa maelezo zaidi ya wahitaji wa zabuni hii wanaweza kutembelea ofisi ya halmashauri ya mji wa nzega Siku za kazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi mpaka saa tisa na nusu mchana
IMG-20170102-WA0003.jpg
 
Tunashukuru Afisa habari kwa mrejesho, mi nashauri mngeweza pia kuweka kwenye magroup aina za biashara au vibanda , kama vile vibanda vya maduka ya mahitaji ya kawaida , maduka ya dawa , huduma ya chakula , huduma ya benki i.e ATM , ofisi, na nyingine ambazo ujenzi wake wa mabanda una special features , naamini vibanda haviwezi fanana kwa huduma mbalimbali . hata hivyo niwapongeze kwa hatua hii tutazidi boresha kadri muda utakavyo tufaa .
 
Kwa wale waliopata nafasi kutembelea mji wa Moshi pale kuna sehemu inaitwa Uhuru park Ukiingia ndani utaona mpangilio mzuri wa vibanda vya huduma ya chakula hii inaweza pia kutumika kwa stendi ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma hii
 
IMG_20170106_163102.jpg
Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega, hii ni hatua moja wapo ya maendeleo ya mradi huu pichani ni kibanda cha mlinda geti pamoja na geti la kutokea na kuingilia magari katika kituo kipya cha mabasi Sagara, Nzega.
 
Kwaiyo hiyo stand itakuwa ni vumbi siyo rami au maana mpaka geti na kibanda kinajengwa ina maana mda si mrefu itaanza kazi, na katika magari yana simama ni moram tu je ndio itakuwa hivyo tupeni tarifa tujue
 
Kwaiyo hiyo stand itakuwa ni vumbi siyo rami au maana mpaka geti na kibanda kinajengwa ina maana mda si mrefu itaanza kazi, na katika magari yana simama ni moram tu je ndio itakuwa hivyo tupeni tarifa tujue
Majembe majembe nikuondoe hofu kuhusu swali lako mda si mrefu ndani ya wiki hii utapatiwa majibu kuhusu swali lako
 
Kulikuwa na wazo la kuongeza sekondari zaidi za serikali kutoka kwa wadau hapa, najua suala hili ni la muda mrefu na linahitaji pesa, vipi viongozi hapo mmejipangaje hata tu majadiliano ya ku identify/kutafuta eneo au uwanja yanafanyika au suala hili halijapewa kipaumbele...Naomba mtujuze
 
1484230667458.jpg
d. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde

Picha za juu ni muonekano wa awali tangu mradi wa tushirikiane nzega unaanza katika mpango kazi huu


MAENDELEO YA MPANGO KAZI KUU KWA SASA

kazi ya upauaji wa mabweni umeanza rasmi Siku ya leo tarehe 12/01/207 kama picha inavyoonekana hapo chini
1484234477487.jpg
1484234477487.jpg
 
1484309612923.jpg
Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

MAENDELEO YA MPANGO HUU KWA SASA

Kazi ya ukamilishaji wa kisima cha maji katika kituo kipya cha mabasi Nzega umendelea leo tarehe 13 /01 /2017

Zoezi likuwa linafanyika leo ni kupima kiwango cha maji kinachotoka baada ya kisima kuchimbwa lengo ni kuweza kujua ujazo wa Maji unaotoka kwa saa endapo watafunga pampu ambayo itakuwa inasukuma maji katika mantaki ambayo yatakuwa yanatumika kusambaza maji katika kituoni hapo


Zoezi limekamilika na kubaini kuwa, kiwango cha maji ambacho kinatoka kwa saa moja ni lita za ujazo elfu sita (6,000
 
Safi sana afisa habari wetu ndio maaana ulipopotea tulikuulizia maana tulikosa kujua mambo kama haya safi sana tupo pamoja ila majibu yetu ujajibu hiyo stand itakuwa vumbi au wanaweza rami au nini tuulizie bwana ila Mbunge akija katika mkutano yake tuweze mhoji vizuri
 
Back
Top Bottom