Mbunge Cherehani: Kata 11 Jimbo la Ushetu Kunufaika na Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE CHEREHANI - KATA 11 JIMBO LA USHETU KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA ZIWA VICTORIA

Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa Fedha nyingi kwaajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Cherehani ameyasema hayo leo katika Hafla ya Utiaji saini wa Miradi ya Maji uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo amesema,katika kipindi cha Miaka Mitatu Rais ametoa fedha nyingi kwenye miradi ya Maendeleo ikiwemo maji Afya Elimu na barabara huku katika eneo la maji ameridhia mradi wa maji ya ziwa victoria kutoka Manspaa ya Kahama kwenda Kata 11 za Jimbo la Ushetu.

"Nashukuru sana Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa yale anayoyafanya , katika kipindi cha miaka mitatu ametupa fedha nyingi sana kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wetu,Miradi ni mingi ya maji imekamilishwa katika kata za Ushetu, Na sasa tupo katika kusubri mkataba wa mradi mkubwa wa maji ya ziwa Victoria kutoka Manspaa ya Kahama kwenda Ushetu .Nifedha nyingi Mh Rais Ametupa ambapo ni kama Bilion 46 kwaajili ya mradi huo"

"Lakini leo kata tatu za jimbo langu Bukomela,Ubagwe na Chona Zipo katika bajeti ya mikataba hii tuliyosaini leo,hakika Mh Rais anatupenda sana,sasa sisi wana Ushetu tutamlipa haya kupitia Masanduku ya Kura, Kuanzia Serikali za Mitaa Na Mwaka 2025 naamini Ushetu tutaongoza kwa kura nyingi za Mh Rais"Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.40.jpeg
    37.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.40(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.40(1).jpeg
    50.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.41.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.41.jpeg
    51.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.41(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.41(1).jpeg
    50.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.42.jpeg
    51.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.42(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-10 at 13.31.42(1).jpeg
    43.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom