Afisa mawasiliano vip mbona umepowa sana umekula mrungura nini si kawaida yako hii habari za maendeleo ya kazi zakozimepungua vipi afisa habari wetu unajua wewe ni jembe basi tu ebu leta mambo hapa bwana
Habari zenu wadau, nazi embe na wadau wengine, ukimya wa kutopata habari za maendeleo ya miradi yetu katika jimbo la nzega mjini inatokana na miradi kukamilika katika hatua moja, kwaiyo kipindi hatua nyingine inasubulia kuanza ndio ukimya unatawa hapa katika mijadala yetu na ndio maaana kuna kipindi habari zinakuja kwa wingi sana kipindi ambacho mradi unaanza awamu nyingine
Pengine wadau mtajiuliza Kwanini sasa hatua moja ikikamilika, kunakuwepo na uchelewaji wa kuanza hatua nyingine
Jibu ni kwamba miradi hii inategemea pesa za umma na wahisani kwaiyo upatikanaji wa pesa ajiri ya kuendeleza mradi huwa zina mchakato yake , hivyo basi kipindi hiyo michakato inafanyika ndio ukimya utawala kama huu
Muda si mrefu miradi yetu inaendelea, vile vile wananzega msisite kutumia mjadala huu kuelezea changamoto nyingine za kimaendeleo zilizopo katika halmashauri ya mji wa nzega
Kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega
MAENDELEO YA MPANGO HUU
Kisima cha maji ambacho ujenzi wake ulikuwa unaendelea katika kituo kipya cha mabasi Nzega sagara, umekamilika na kisima kipo tayali ajiri ya matumizi kama picha inavyoonekana.
Haya ni mantaki ambayo yamewekwa katika magati ya maji ambayo upatikanaji wa Maji katika maeneo hayo bado ni wa mgao hivyo basi Siku maji yanatoka, maji huifadhiwa katika matanki hayo, Siku ambayo maeneo hayo wana mgao wa Maji basi wananchi huweza kupata maji katika mantaki hayo hivyo basi kufanya upatikanaji wa Maji uwe kila siku upo, mantaki haya yamewekwa katika Gati la maji maeneo ya maporomoko, Gati la maji eneo la ipilili, na tanki la mwisho limewekwa eneo la uswilu
Hatua hii ni moja ya mpango kazi wa mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega ambao ni
Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300
Great, well planned. Kiu ya wadau hapa ni ya muda mrefu ila mnakwenda na ratiba japokuwa changamoto za hapa na pale zipo. Mipango ya muda mrefu ya maendeleo ianze kujadiliwa na iwekewe utaratibu wa implementation hata vizazi vinavyokua hivi sasa wakue na matarajio hayo.
Gati la maji eneo la hospitali ya wilaya nzega mjini.
Gati la maji eneo la kachoma sokoni nzega mjini, Gati hili La kachoma sokoni, Gati la eneo la parking, na Gati la maji eneo la hospitali ya wilaya ni magati ya maji ambayo kwa sasa maji ya napatikana masaa ishirini na nne 24,
Tofauti na awali kabla miundombinu haijafanyiwa marekebisho, magati haya yalikuwa yanatoa maji Mala mbili kwa siku ina maana katika kipindi cha mwezi mmoja maji katika magati haya yalikuwa yanatoka Mala nane tu 8, lakini hivi sasa maji yanatoka kila siku
Upatikanaji wa huduma ya maji kwa uhakika katika mpango wa mda mfupi kwa kurekebisha miundombinu ya maji katika mji wa nzega ni mpango moja kazi mmoja wapo ambao utekelezaji wake unasimamiwa na mradi wa tushirikiane katika jimbo la nzega mjini.
Kwa hili suala la kupunguza kero ya maji kiukweli niwape pongezi, sasa hivi ingawa majumbani ni maji ya mgao ila sasa hivi uhakika tena maji yanatoka masafi, mengi haya kwenye magati hayo uhakika wa Maji upo kiukweli kwa hili tuwape pongezi sema muawambie tu idara ya maji wajaribu kuwa wanapita mitaa uko kwani mabomba mengi sasa yamepasuka kwaiyo maji yanavuja na hii nadhani kwa sababu maji yamekuwa mengi hivyo basi miji mingi mabomba yanafungwa kwaiyo maji yanabaki katika mabomba kwaiyo mabomba yaliyokuwa na tatizo ndio haya yanapasuka ila hongera Sana kazi nzuri
Yani hali isipobadilika basi hata bustani za mboga mboga japo matuta mawili msimu wa kiangazi tutalima hongereni sana kuhusu hili la maji kiukweli maji kwa sasa yanapatikana
Tunashukuru timu nzima ya halmashauri ikishirikiana kwa karibu na mbunge na timu yake, haya ni mambo ya kuendelezwa. you have been a good team big up guys..
vipaumbele ambavyo watu wa nzega walichagua vifanyiwe kazi katika mradi wa tushirikiane katika jimbo la nzega mjini ni miongoni mwa vipaumbele ambavyo vinapatikana katika ilani ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe Hussein bashe, katika kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Wadau wa maendeleo katika jimbo la nzega mjini walipitia vipaumbele mbali mbali vinavyopatikana katika ilani hiyo ya Mbunge na kuamua kuchagua vipaumbele vinne ambavyo ndio vinafanyia kazi kwa sasa na mradi wa Tushirikishane katika jimbo la nzega mjini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.