Misafara ya JK Kuandamana na Private Ambulance: Picha gani kwa Huduma za Serikali?

Kwa kuangalia Serikali yetu...oops yake...oops yao, ya kukurupuka na kutokuwa na mipango, kutokuwa na wanaoweza kuweka mipango bila ubinafsi na roho mbaya. Wamejikuta wanahitaji ambulance, kuangalia zinazopelekwa hospitali za manispaa na jeshini kiutapeli na cmc na toyota wakaona sio ambulance ikabidi mbadala utafutwe... lingepatikana la ikulu hata kwa haraka, ila kwanini lipatikane....kodisha la tanil tule hela ya wananchi...yote haya yana mwisho.
 
Jamani afya ya rais wetu inafahamika kuwa ni mgogoro, si mnakumbuka ile mieleka ya hapa na pale? Ni lazima tahadhari zichukuliwe kwani siku hizi hali imekuwa mbaya kuliko wakati wa kampeni.Ndiyo maana wakati fulani niliwahi kupendekeza akiwa kwenye majukwaa awe anavaa steel helment ili wale wadakaji wakichelewa kumdaka asije akapata brain damage.
Ndio atumie private ambulance?? Ina maana haamini huduma za afya zinazotolewa na serikali yake?
 
Najua ambulances za serikali ni vimeo but mjue rais wa wanaccm ni mgonjwa na anahitaji sana intesive care ndo maana anatembea na gari ambalo kidogo liko safi!
 
MWENYE USHAHIDI ALETE........SI MANENO MATUPU.....rangi ya gari kufanana na ya ultimate tayari imeshakuwa ni ya ultimate...? TUWE TUNAFIKIRI KWANZA NA KUWA NA UHAKIKA KABLA YA KUJA NA KUANDIKA
 
Ultimate Security Tanzania Ltd ni ya fisadi papa Tanil Somaiya.
Hawa watu (washkaji wa JK) wanapewa tenda ili wazidi kunyonya watanzania. Ni makusudi tu ya serikali hii ya Kikwete isiyo na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha za umma.
Serikali haishindwi hata kidogo kununua ambulance ya kuambatana na Kikwete kila mahali (kama afya yake inahitaji hilo) ila ndio wanaendelea kukamua hata na hicho kidogo.

Tahrir Square ni muhimu kwa Ukombozi...
 
ultimate security ni mali ya toni somaiya yule mtuhumiwa wa rada na mbia na rostam aziz, wanatumbua nchi inayongozwa na mafala kama makamba kwa kuwahuwarushia makombo

...lakin afadhal hata wao wanaambulia makombo, sis tunaongeza magonjwa tu-presha kbao za hasira za haya-na mtanzania wa kijijin ndo kabsaa, alime sis twabeba malumbesa-mwanakijiji anayajua zaid. mnyonge na mnyonge wake bwana!

Ila on a more serious note, hawa jamaa wametawala kwny kila tenda kubwa ya nchi hii inayohusu serkal! Tufanyeje hawa jamaa jamani wajue hata sis ni nchi yetu hii? Au ndo tatizo la kisiasa litafutiwe suluhisho la kisiasa, therefo twaachie CDM?
 
huyu mkulu engine yake imefungwa turbo ya kichina...lazima spana mkononi kila dakika
 
MWENYE USHAHIDI ALETE........SI MANENO MATUPU.....rangi ya gari kufanana na ya ultimate tayari imeshakuwa ni ya ultimate...? TUWE TUNAFIKIRI KWANZA NA KUWA NA UHAKIKA KABLA YA KUJA NA KUANDIKA

Ushaidi ni kweli gari ambulance ipo na inaonekana kwenye misafara yake na kwamba mmiliki ni somaiaya halina ubishi kwani ni jambo linalofahamika pale ultmate kindondoni au unataka ushaidi gani?
 
MWENYE USHAHIDI ALETE........SI MANENO MATUPU.....rangi ya gari kufanana na ya ultimate tayari imeshakuwa ni ya ultimate...? TUWE TUNAFIKIRI KWANZA NA KUWA NA UHAKIKA KABLA YA KUJA NA KUANDIKA

Kama unaona huu ni uzushi, kuna post zngine za kuisapoti serikali yako tukufu, unaonaje ukafanya km umepita tu, ukaendelea uko kupakana mafuta kwa mgongo?

Just so u remember/know, ktk scientific methods za reseach, Observation inform the findings...therefore analysis-ambayo ndo twafanya, then hitmisho na mapendkezo, ambayo JF members wanatoa hapa pia.. Then utekelezaji-then the choice is ours- thru political parties (CDM), free thinkin n mobilize 4action au kwa People's Power (mapinduziiiii)
 
TUNATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TUME HURU
YA UCHAGUZI BUNGENI SASA HIVI!!!


Enyi Ndugu Waheshimiwa viongozi wetu

akina Kikwete, Dr Slaa, Prof Lipumba, Mbowe, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Mbatia, Dr Mvungi, Prof Baregu, Prof Mukandala, Dr Bana, Dr Azaveli, Mama Nkya, Ndg Mgaya, Makwaia wa Kuhenga, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mengi, Pius Msekwa, Fredrick Sumaye Fredrick Msuya, John Malecela, Mama Anna Makinda, Sheik Issa Bin Simba, Mhe Iddi Simba, Maaskofu na Wachungaji wote nchini, Denis Mwamnyange, Said Mwema, The Othma's, Tundu Lissu, Sitta, Mwakyembe, Mzee Mkapa, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Prof Sarungi, Selasini, Ole Sendeka, Tido Mhando, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Selelii, Prof Bangu, Dr Matumaini, Bashe, Celina Kombani, Kafulila, Hamad Rashid, Regia, Lukuvi, Mama Maghimbi,Mama Anna Abdala, Pombe Magufuli, Mstaarabu wa Siasa Tanzania - Dr Mohammed Shein, Salmin Amour, Godbless Lema, Mzee Mwanakijiji, Maxence Melo, Candid Scope, Fareed, Mwakalebela, Mnyika, Halima Mdee, viongozi wote wa serikali za wanafunzi vyuoni ... na wengine wengi wengi wengi tu, sisi kama vijana wa nchi hii sasa hivi tunawaulizeni nyote kwa pamoja kwamba ...

... suala letu la michakato wa kujiandikia KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ZINAANZA LINI BUNGENI???
 
Ultimate Security Tanzania Ltd ni ya fisadi papa Tanil Somaiya.
Hawa watu (washkaji wa JK) wanapewa tenda ili wazidi kunyonya watanzania. Ni makusudi tu ya serikali hii ya Kikwete isiyo na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha za umma.
Serikali haishindwi hata kidogo kununua ambulance ya kuambatana na Kikwete kila mahali (kama afya yake inahitaji hilo) ila ndio wanaendelea kukamua hata na hicho kidogo.

Tahrir Square ni muhimu kwa Ukombozi...

Sijajua, afya inawezaje kuhitaji Ambulance!! mi navyofahamu siku zote toka nimezaliwa kuna mtu anaitwa Daktari wa Rais, ndio uandamana na msafara yeye na tools zake basi, sasa hii imekaaje au hatuna rais tena kama ni hivyo kwanini hasipumzishwe!! maana hata marehemu Jackson alikuwa anaishi kwa madawa kibao lakini halikuwa atembei na Ambulance au Yahya ametabiri hajali mbaya!!

Maswali ni mengi sana shida vingozi wa Afrika hawana nidhamu kwa waajiri wao (Wananchni) ndio maana hawaoni umuhimu wa kutoa taarifa kwa umma.
 
Hilo la kuwa na ambulance ni la kawaida kabisa, kwani marais wengi sana duniani huwa na escot hiyo inategemea tu kama litakuwa gari maalum la President lina facilities hizo, tizama msafara wa Obama , ambulance ipo pia

Kwa nini private ambulance? kama msafara ukipata ajali na ikatokea member of the public ameumia, atahudumiwa na hiyo private ambulance au itabidi ije ambulance nyingine ya umma kumhudumia? Kama atahudumiwa na hiyo private ambulance, nani atakuwa reponsible for the costs? Pili ndio kusema kuwa hata our own president doesnt trust our own ambulances that he decided to go for the a private one?
 
Turuchie hapa mzee, inaweza kutusaidia katika hoja zetu mjengoni! Maana kweli haiingii kichwani ati katika serikali yote, hakuna kitengo chochote kinaweza kuaminika kutoa huduma hiyo, mpaka twende private.. Inanipa picha mbaya sana kwa nchi yangu. inaniondolea matumaini ya KUONA MAISHA BORA KWANGU KAMA MMOJA WA WALE WATANZANIA WASUBIRIO AHADI YA MAZIWA NA ASALI YA UONGOZI HUU!

Alafu mtu anakwambia eti serikali ipunguze matumizi..kwa kuacha kununua mashangingi....wakati juzi juzi nimeona maPRADO MAPYA YAMEANDIKWA OFISI YA WAZIRI MKUU...... haya MACHANGA YA MACHO mpaka lini!!!!???? aaaaaaaaaaaaaaaaaggggggggghhhhhhhhhhh... siasa za madaraka!!!!!

shivacom group of companies, and who owns shivacom....? find out
 
Public Private Partnership

Kwenye private (ndio dowans, ultimate sec, nk) mikataba inakua ya ulaji, hata hivyo ambulance ikiwa mali ya serikali ya CCM dereva atauza mataili ya gari ama mafuta ama atabebea nyasi za ng'ombe. Yaani hapana pa kukimbilia ili mradi CCM walishabomoa misingi bora ya uongozi TZ na kutuachia UFISADI.

Dawa iliyobakia kwa serikali ya CCM sisi wote tunaijua.
 
Ni mtazamo wangu, labda na Watanzania wengi kwamba serikali ina imani na mifumo na mipango yake ya huduma za kijamii mfano Afya, elimu nk. kwa watu wake. Hii ambulance ya Ultimate Security inayoambatana na misafara ya JK kila siku inaashiria hata yeye hana imani na mifumo yake mwenyewe au ndo mkubwa anafaidi PAJA siku zote, Km ilivo kwa wao kupeleka watoto wao ulaya kusoma?

Mifumo ya serkali imekufa hata ya kumsave Mkuu? Bili yake tunaijua? Au intelijensia applies?

Kwa njia hii, ata
yajuaje machungu ya mama mjamzto wa Chongoleani anaefia njian kwa kushindwa fika hospital kwa kukosa referral support?

huduma za serikali mbovu kwa walala hoi,,,,ila kwa vigogo ni swaafi!!! Ni kweli kuwa hatuwezi kuishi bila matabaka ila hii ya Tanzania imezidi mno!!!!
 
Kuna 10% za kukodi ambulance hiyo na kuiweka kwenye msafara wa Rais. Ama kweli nchi inaliwa na wenye Meno.
 
Hilo la kuwa na ambulance ni la kawaida kabisa, kwani marais wengi sana duniani huwa na escot hiyo inategemea tu kama litakuwa gari maalum la President lina facilities hizo, tizama msafara wa Obama , ambulance ipo pia

Kweli ni haki kumlinganisha rais wa marekani na wa Tz?
 
Back
Top Bottom