Waziri Mchengerwa: Muda umefika kwa DART kuwa na mtoa huduma zaidi ya mmoja wa Mabasi ya Mwendokasi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa ameelekeza Uongozi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuongeza watoa huduma ili kuboresha huduma ya usafiri wa haraka kwa wananchi wa Dar es salaam.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Oktoba 24, 2023 kwenye ziara yake kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ili kupata taarifa ya utendaji kazi wa Wakala huo.

Amesema huduma ya mabasi yaendayo haraka ni muhimu sana kwa maisha ya wakazi wa Dar es salaam na inatakiwa kusaidia kupunguza adha ya usafiri, hivyo uwapo wa mtoa huduma mmoja anazidiwa na kusababisha changamoto kwenye baadhi ya maeneo.

Amesisitiza kuwa suala la kuongeza watoa huduma kwa sasa haliepukiki na linatakiwa kuwa kipaumbele kwanza kwa kuwa kuna njia mpya zitakazoanza hivi karibuni.

“Mtoa huduma mliyenaye kwa sasa ni UDART pekee muda umefika sasa kuwa na mtoa huduma zaidi ya mmoja ili kuleta ushindani kwenye kutoa huduma za Usafiri kwa ili wananchi wapate huduma bora," amesema Mchengerwa.

Pia Waziri Mchengerwa amewataka uongozi wa DART kuimarisha mifumo ya kutoa Taarifa mara tu panapoteka changamoto yeyote ya usafiri.

"Sijapenda kuendelea kuona vurugu kwenye Vituo vya kusubiria mabasi, ni vyema panapotokea hitilafu kuwe na mifumo ya kutoa taarifa ili kupunguza manung’uniko kwa wananchi ambao huenda wamekaa pale muda mrefu kusubiria basi,"amesema.

Awali, akitoa taarifa za utendaji kazi wa Wakala huo, Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Edwin Mhede amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya sita, uwezo wa kusafirisha abiria kwa siku umeongezeka kutoka abiria 90,000 mpaka 210,000 na umetokana na maboresho makubwa yaliyofanyika kwa Wakala huo.

Pia, soma: Dar: Abiria wateseka kwenye foleni kusubiri mabasi ya mwendokasi Kituo cha Mbezi Mwisho
FB_IMG_1698180041389.jpg
FB_IMG_1698180044564.jpg
FB_IMG_1698180047908.jpg
FB_IMG_1698180050847.jpg
FB_IMG_1698180054038.jpg
FB_IMG_1698180056829.jpg
 
Hao jamaa wana ofisi nzuri kuliko huduma wanazotoa na si ajabu wanalipana mishahara mikubwa na posho huku jambo dogo tu la kupanga ruti za mabasi linawashinda.
 
Hili Mimi nilishaliona siku nyingi..mfano pakawa na watoa huduma wawili mfano udart ikawa na rangi blue na mtoa huduma na mbili Azam..akawa na mabasi rangi nyekundu...


Huduma utapendeza,a malalamiko yataisha
 
Hao jamaa wana ofisi nzuri kuliko huduma wanazotoa na si ajabu wanalipana mishahara mikubwa na posho huku jambo dogo tu la kupanga ruti za mabasi linawashinda.
I say wanaudhi mpaka unataka uende kuwatukana pale wanapopaki magari na kuenda kutongozana au kuongea ya Simba na yanga!
Ndorobo kabisa hao UDART 😡☹️👺
 
Ili kupunguza wafanyakazi UDART ingekuwa inatumia malipo kupitia N-Card.

Hivyo wafanyakazi wenge wangekuwa Walinzi na Madereva.

Kampuni lazima ianze na wafanyakazi wachache, ikichanganya inaongeza idadi ya wafanyakazi.

Wakatisha tiketi wangesubiri wakati huo.
 
Ili kupunguza wafanyakazi UDART ingekuwa inatumia malipo kupitia N-Card.

Hivyo wafanyakazi wenge wangekuwa Walinzi na Madereva.

Kampuni lazima ianze na wafanyakazi wachache, ikichanganya inaongeza idadi ya wafanyakazi.

Wakatisha tiketi wangesubiri wakati huo.
Waweke mfumo wa N-card wao watapiga wapi? Ndio maana wamejaza wakata tiketi wakusanye cash ili zipigwe mkuu.

Wanashindwa hata na vivukoni kwa sasa wanatumia mfumo hakuna haja ya kukusanya cash.
 
Ndio kifuatacho ITV ,itakuwa tayari kila kitu
Mbona ni sual zuri
Technically kuw na mtoa huduma mmoja anakua anajisahau pengine
Akipatikana na mwingine ushindan utaongezeka. Si ni kilio chenu kila siku
Iweje muanze kutia inda na hila? Au tatizo nini?
 
Back
Top Bottom