Misafara ya JK Kuandamana na Private Ambulance: Picha gani kwa Huduma za Serikali?

Elifasi

Senior Member
Nov 1, 2010
180
5
Ni mtazamo wangu, labda na Watanzania wengi kwamba serikali ina imani na mifumo na mipango yake ya huduma za kijamii mfano Afya, elimu nk. kwa watu wake. Hii ambulance ya Ultimate Security inayoambatana na misafara ya JK kila siku inaashiria hata yeye hana imani na mifumo yake mwenyewe au ndo mkubwa anafaidi PAJA siku zote, Km ilivo kwa wao kupeleka watoto wao ulaya kusoma?

Mifumo ya serkali imekufa hata ya kumsave Mkuu? Bili yake tunaijua? Au intelijensia applies?

Kwa njia hii, ata
yajuaje machungu ya mama mjamzto wa Chongoleani anaefia njian kwa kushindwa fika hospital kwa kukosa referral support?
 
Anayajua sana ndio sababu ya kukimbilia private service
 
Tatizo la Rais wetu linafahamika na walio karibu nae wanasema limeongezeka zaidi sasa. Niliiona ambulance hiyo juzi wakati anakwenda kutembelea shule ya mkewe kule Rufiji.
 
Bajaji hazijafika mkuu, zikifika ataachana na hiyo ambulence ya u. security usihofu!!!!! :clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:

" Rais Kikwete kuweka pikipiki za matairi matatu (Bajaji) kama moja ya vipaumbele vyake ili zitumike kubeba wajawazito wakati wabunge wanalipwa mamilioni.

Katika hotuba yake ya kulizindua bunge Kikwete alieleza mpango wa serikali yake kununua pikipiki hizo 400 zitakazosambazwa maeneo mbalimbali hasa vijijini kwa ajili ya kuwabebea wajawazito kama njia ya kupunguza matatizo ya usafiri kwenye maeneo hayo
"
 
Tatizo la Rais wetu linafahamika na walio karibu nae wanasema limeongezeka zaidi sasa. Niliiona ambulance hiyo juzi wakati anakwenda kutembelea shule ya mkewe kule Rufiji.
Sasa jamani tumuombe APUMZIKE na shughuli hizo nzito za upresida!
tunamtesa mzee wetu!
 
Ni mtazamo wangu, labda na Watanzania wengi kwamba serikali ina imani na mifumo na mipango yake ya huduma za kijamii mfano Afya, elimu nk. kwa watu wake. Hii ambulance ya Ultimate Security inayoambatana na misafara ya JK kila siku inaashiria hata yeye hana imani na mifumo yake mwenyewe au ndo mkubwa anafaidi PAJA siku zote, Km ilivo kwa wao kupeleka watoto wao ulaya kusoma?

Mifumo ya serkali imekufa hata ya kumsave Mkuu? Bili yake tunaijua? Au intelijensia applies?

Kwa njia hii, ata
yajuaje machungu ya mama mjamzto wa Chongoleani anaefia njian kwa kushindwa fika hospital kwa kukosa referral support?
Kazi za Bongo technical know who, ujue hapo kuna ndugu yake anahisa Ultimate security. Hospitali zetu hazina huduma hiyo nguvu zote zimeelekezwa ultimate.
 
Jamani afya ya rais wetu inafahamika kuwa ni mgogoro, si mnakumbuka ile mieleka ya hapa na pale? Ni lazima tahadhari zichukuliwe kwani siku hizi hali imekuwa mbaya kuliko wakati wa kampeni.Ndiyo maana wakati fulani niliwahi kupendekeza akiwa kwenye majukwaa awe anavaa steel helment ili wale wadakaji wakichelewa kumdaka asije akapata brain damage.
 
Mmh! kweli bajaji ziende mahenge kwenye makorongo wakati wabunge wanafaidi pesa ya nchi ameshindwa vp kuwashawish awapunguzie ulavi ili awape unafuu wakula walioko vijijini?
au aliyeshiba hamuoni mwnye njaa?
Siku moja atachukua mwenye uchungu na nchi watu watapumnzika, naamini daudi wa Tz au Samweli wetu atazaliwa tutapona waache wajione Mungu mijitu tutawafukuza kimisri
 
Suala moja tu ninaloweza kusema hapa ni kuwa INAUMA.
Inauma kuona walalanjaa wanakufa kwa magonjwa wakati wakubwa wetu wanatibiwa bure, huduma nzuri na pengine nje ya nchi.
Inauma kuona vijana wetu wanashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa karo, wanakalia viroba kwenye vumbi na chini ya miti, wakati wakubwa wetu wanasomesha watoto wao katika ""Internationals" na pengine nje ya nchi.
Inauma kuona nchi imo katika giza wakati bado tunataka kuwalipa Dowans ambao wamo humu humu nchini.
Inauma kuona nchi inautajiri wa malighafi na rasilimali wakati wananchi ni masikini wa kutupwa.
Inauma kuona kila siku tunapigwa date kwa ahadi hizi na zile wakati kila uchao shida zinaongezeka.
Inauma kuona bado tunatia saini mikataba ya kiujanjaujanja wakati tukijua kuwa na mabomu ambayo yanasubiri kuturipukia mikononi.
INAUMA, INAUMA, INAUMA.
 
jiulize nani mmiliki wa Ultimate security na ana uhusiano gani naye - in the back door
 
...lakini kwa speed ile misafara inaondoka nayo, kuna haja ya kutumia ambulance huku mitaa ya jiji wakati anawahishwa mara moja tu kwenye eneo la huduma? nadhani Inaweza kuchukua muda zaidi kumuhamisha kutoka kwenye gari lake kuingia kwa ambulance zaidi ya kuongeza speed, kuwahi pale.... (sore, jina tunahifadha-intelijensia).
 
jiulize nani mmiliki wa Ultimate security na ana uhusiano gani naye - in the back door

Turuchie hapa mzee, inaweza kutusaidia katika hoja zetu mjengoni! Maana kweli haiingii kichwani ati katika serikali yote, hakuna kitengo chochote kinaweza kuaminika kutoa huduma hiyo, mpaka twende private.. Inanipa picha mbaya sana kwa nchi yangu. inaniondolea matumaini ya KUONA MAISHA BORA KWANGU KAMA MMOJA WA WALE WATANZANIA WASUBIRIO AHADI YA MAZIWA NA ASALI YA UONGOZI HUU!

Alafu mtu anakwambia eti serikali ipunguze matumizi..kwa kuacha kununua mashangingi....wakati juzi juzi nimeona maPRADO MAPYA YAMEANDIKWA OFISI YA WAZIRI MKUU...... haya MACHANGA YA MACHO mpaka lini!!!!???? aaaaaaaaaaaaaaaaaggggggggghhhhhhhhhhh... siasa za madaraka!!!!!
 
Hii ambulance ya Ultimate Security inayoambatana na misafara ya JK kila siku inaashiria hata yeye hana imani na mifumo yake mwenyewe au ndo mkubwa anafaidi PAJA siku zote, Km ilivo kwa wao kupeleka watoto wao ulaya kusoma?

Public Private Partnership
 
Sasa jamani tumuombe APUMZIKE na shughuli hizo nzito za upresida!
tunamtesa mzee wetu!
kwani ana matatizo gani makubwa? tunazo dawa nzuri tu za mitishamba kutoka China na Brazili zinatibu magonjwa makubwa kama cancer, tujulisheni tutatoa ushauri kumsaidia Mheshimiwa Raisi wetu.
 
Kweli lile ambulance linakimbia kwa kati ya msafara kwa kasi sana...nimeliona pande za mwenge lilikuwa kasi sana..lile mashine kwa mkasi wake kiwandani ni zaidi ya 150m tsh..nafikiri yako kama matatu tanzania...Moja wapo liko mgodi wa North Mara...Uko kwenye mapanga shaa...

Linaweza kuhudumia wangojwa watatu mpaka wanne kwa wakati mmoja vifaaa vingine vingi ya kuokoa uhai.Huyu bwana ana expect kupata tatizo au ajali wakati wowote?au kuwa attacked?Gharama ya kulikimbiza barabarani bila kutumia ipasavyo..ni kiasi gani..kwani kama kulinunua ni zaidi ya 150m tsh...kulitunza itakuwa juu sana....

Gari anazotembelea mkuu mie kwa mtizamo wangu nafikri ziko well protect na wheel balance na kwa ajiri ya barabara za tz..kupata ajali tz ni kidogo ..mwendo anao tumia kwa kuwa anakuwa kaachiwa njia mwenyewe na dereva proffesional sio rahisi kupata ajari labda awe kategwa..na kuna gari tangulizi..mbile yake....hii tu inanishawishi kuwa kwa gari alizo nazo kwenye msafara hahitaji ambulance..mind you ile gari yake kwenye back seat ukichana kuna first aid zote unazo hitaji...kwa mfani kama una bleed,mkoni umefunjia kichwa kina matatizo ni jinsi ya kuzitumia...na kuna watu naamini wamepelekwa training kwa hili...
 
Tatizo sio Kikwete bali wapiga kura. Ni sawa kuna watu watasema hakushinda uchaguzi, lakini hakutakiwa kupigiwa hata kura moja. Na maana ya kuwa kati ya wagombea sijui watano waliokuwepo alitakiwa ashike namba ya tatu kwenda chini.
 
Kwa njia hii, ata
yajuaje machungu
ya mama mjamzto wa Chongoleani anaefia njian kwa kushindwa fika hospital kwa kukosa referral support?

Kwani yeye ana interest za kuyajua machungu? Nadhani anafuata ule msemo ..'If you want to live happy, don't be concerned about others'...
 
Ni mtazamo wangu, labda na Watanzania wengi kwamba serikali ina imani na mifumo na mipango yake ya huduma za kijamii mfano Afya, elimu nk. kwa watu wake. Hii ambulance ya Ultimate Security inayoambatana na misafara ya JK kila siku inaashiria hata yeye hana imani na mifumo yake mwenyewe au ndo mkubwa anafaidi PAJA siku zote, Km ilivo kwa wao kupeleka watoto wao ulaya kusoma?

Mifumo ya serkali imekufa hata ya kumsave Mkuu? Bili yake tunaijua? Au intelijensia applies?

Kwa njia hii, ata
yajuaje machungu ya mama mjamzto wa Chongoleani anaefia njian kwa kushindwa fika hospital kwa kukosa referral support?

Hivi ni ya AAR ama ya Ultimate? kama ni Ultimate jamani si ni mali ya mshikaji Tanil?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom