Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.
Picha linaanza kuingia kwa daktari, mama wa mtoto anaeleza mwanaye kaumia baada ya kuaguka wakati anacheza, dk bila hata kumgusa wala kumwangalia mtoto akatoa jibu, NENDA KAMCHUE NA UMPE NA DAWA YA MAUMIVU!
Mama wa mtoto akamwambia dk nishampa dawa ya maumivu na kumchua ila hakuna matokeo mazuri, dk akasisitiza aende, ikabidi mama wa mtoto alazimishe kuomba dk aandike akapigwe X-ray, cha ajabu dk. anakubali ila anamuuliza mama wa mtoto unataka apigwe picha wapi, mama akamwambia mkague ili uone ni eneo gani hasa maana alipoumia mguu ulivimba na hataki kuguswa, dk akarudia tena we sema apigwe wapi mama wa mtoto ikabidi ajibu apigwe picha mguu mzima.
Daktari akaandika kwenda kwenye picha(X-ray), kufika huko mama wa mtoto akiwa na kadi ya kliniki akijua huduma ni bure, anaambiwa anatakiwa kulipia 15000 kwa ajili ya kupata huduma hiyo na hakuwa na hela hapo maana Serikali kutwa inaimba huduma ya matibabu chini ya miaka 5 ni bure, huku wananchi wanatozwa pesa.
Nikaenda nikapewa namba nikalipia japo mwanzo hawakutaka nilipie kwa namba ya malipo walitaka niwape pesa taslimu nikakataa, ili kuonesha ni malipo halali ya serikali hivyo sina shaka kuwa serikali inawadanganya wananchi kuwa huduma za matibabu chini ya miaka 5 ni bure na huku wanalipa na hii ni risiti halali ya malipo.
Baada kupiga picha kurudisha majibu kwa Dk, akasema kavujika mguu kwenye paja, na apewe 50000 ili mtoto afungwe PoP, nikasema hiyo hela ni ya nini? akajibu ni ya kununua vifaa na gharama ya kufungia, nikasema nipewe namba ya malipo nilipe, dk akakunja sura mara mbili zaidi maana tangu mwanzo alishaonesha chuki.
Dk akasema hapa hakuna vifaa ni vya kununua na gharama yake ni 32,000 nikamwambia niandikie nikanunue mwenyewe, akaandika huku anasema kwa hiyo umeamua kwenda kununua mwenyewe sawa kanunue.
Nikafika duka la dawa nikapata vifaa kwa gharama ya 11500, nikapata hisia huenda alikuwa kashapiga hesabu zake juu ya hela ya kunuua vifaa ndio maana sura ilibadilika na kuuliza kama nimeamua kwenda kununua mwenyewe.
Niliporudi kwa Dk. akasema nikalipie gharama ya huduma ya kufunga, nikaenda mapokezi kulipia nao vilevile wakataka niwape pesa taslimu nikagoma ndipo wakanipa namba ya kulipia nikalipa sh, 20,000.
Je, Serikali kwa nini mnadanganya matibu bure kwa watoto chini ya miaka 5? Kama si kweli hamdanganyi ni kwa nini kituo cha Kimara watoze pesa ambazo zinakuja Serikalini?
Wafatilieni watoa huduma wa Kimara, wana lugha mbaya na wanatoa huduma mbovu, na hawako makini kabisa maana wakati nipo pale kuna mama mmoja alikuwa karudia kupiga picha mara ya pili baada ya mwanzo kupigwa uti wa mgongo na wakati yeye anasumbuliwa na kichwa!
Pia wanataka walipwe pesa wao na si kwenye mfumo wa malipo.