FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,212
Binafsi ni mwana CCM kindakindaki tokea ilipobuniwa 1977, kabla ya hapo nilikuwa TANU Youth League.
Ingawa ni mwana CCM lakini si kila jambo la serikali linaniridhisha, kuna ambayo tukipata nafasi tunayafikisha vikaoni lakini hivi sasa imekuwa ngumu sana kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi, sifahamu kwanini wakati sasa hivi tunaishi kwenye dunia inayopitia kwenye miongo ya mawasiliano habari (IT).
Kwanza naishauri CCM iboreshe namna ya kuwasiliana na ngazi za uongozi; pili naishauri serikali kuu, mawaziri wote mpaka Rais wa Tanzania waige mfumo wa Zanzibar wa "sema na Rais".
Kwa kukosa njia za kufikisha ujumbe kwa haraka nimeona bora ushauri wangu niutoe hapa JF, nafahamu utawafikia walengwa wote.
1) Nashauri huduma zinazotelewa bure na serikali ziwe za kulipia rasmi, kwa zote namaanisha zote. Kuanzia huduma zinazotolewa Polisi, iwe mtu ukitaka huduma yoyote ya kipolisi ulipie, kama siyo siku hiyo hiyo basi uandikiwe una deni kwa kupewa huduma hiyo na utailipa kupitia control numbers.
Rushwa imezidi serikalini, kama haujaombwa waziwazi basi utazungushwa kupatiwa huduma mpaka utie akili utowe rushwa au atokee "kishoka" wa hapo akusomeshe utowe rushwa, ndipo huduma yako ishughulikiwe.
Kwa mambo kama hayo, iwekwe wazi tu, kuwa ukienda kushitaki Polisi unapewa control number unalipia unapewa huduma, na afisa ataekuhudumia atalipwa mgao wake hukohuko official kabisa.
Ili kupigana na rushwa, kama tumeshindwa kuweka sheria kali ni vyema tukaihalalisha tu malipo kwa kila huduma.
Au kama ilivyofanywa kwenye matibabu, iwekwe bima ya lazima kwa kila raia awe analipia hizo huduma, na pesa zitazotokana na hiyo bima waongezewe mishahara na posho watoa huduma badala ya kuzungusha watu ili wale rushwa serikalini. Hii ni kwa wizara na idara zote zinazotoa huduma za bure kwa jamii, ambako ndiko kunakonuka uozo wa rushwa.
Kauli za viongozi kama zile za "za polish ya viatu", "kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" zimekuwa zikihalalisha rushwa kiaina, sasa iwe ni wazi kabisa ihalalishwe kwa kuzilipia hizo huduma.
Polisi, mahakama, uhamiaji, ardhi, huduma zote za bure za manispaa. Ongezea na wewe kwengine.
Tunataka tuwe ni wateja rasmi wenye kuweza kudai haki zetu tunaponyimwa huduma kwa wakati.