Mkurugenzi wa LATRA anapata wapi nguvu ya kupingana na Rais? Serikali inakataza kufunga biashara, yeye anafungia mabasi 35 yasitoe huduma

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Watumishi wa umma wanapaswa kuwa watu wanaotumia akili na busara kubwa sana. Wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi , wanalipwa kwa sababu kuna watu waliamua kufanya biashara. Lakini wao ni kama wanalipwa kwenda kuua biashara nchini.

Nasema haya baada ya kuona LATRA ikitoa tangazo kwa umma lakufungia mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro yasitoe huduma. Ukisoma tangazo lao hakuna Sehemu popote walipoeleza kwa ushahidi kampuni husika imetenda kosa gani, wameandika general statement ambayo inaonyesha wao wana mamlaka yakutuhumu na kutoa hukumu bila kusikiliza.

Hakuna Sehemu kwenye barua wanaonyesha wamechukua juhudi gani kushauriana na Kampuni ya Kilimanjaro. Hakuna Sehemu wanasema lini wahusika walikiuka haya masharti. Hakuna Sehemu wanasema mfumo wa kampuni hiyo unawaathiri vipi wananchi? Hii ingesaidia wananchi kutambua mapungufu na kuripoti endapo yapo kwa makampuni mengine.

Nirudi kwenye hoja, mhe. Rais anapotoa tamko ni amri na ndio mtizamo wa Utawala wake. Mhe Rais wakati anakataza kufungwa biashara alikuwa anaeleWa madhara yatokanayo na kufungia biashara na namna yalivyotishia uhai wa uchumi wetu.

Unapotafakari mtizamo wa Mhe. Rais ambao umekuwa unasisitizwa sana na Mh. Waziri wa fedha unajiuliza hawa wakurugenzi huwa wanawasikiliza mabosi zao?

Kupitia tangozi hili wapo watu wanakwenda kuathirika moja kwa moja

1. Kuendesha magari 35 maana yake madereva na makondakta wote hawana kazi ya kufanya na hivyo awatalipwa mishahara kwa kipindi chote.

2. Wahudumu wa kampuni hii wote wanakwenda kubaki nyumbani wakisubiri LATRA wakubali kufungulia au wakatae

3. Kodi ya serikali haitakusanywa kwa magari haya 35 ambayo yamefungiwa

4. Wasafiri waliokata tiketi kwa tarehe hizi maana yake watalazimika kutafuta utaratibu mwingine na may hakuna refund itakayofanyika. Kumbuka hiki ni kipindi ambacho watoto wanarudi shule.

Huu ni uchambuzi mdogo tu kuhusu athari za tamko hili. Lakini tujiulize makampuni mangapi mifumo ya tiketi inasumbua? Leo tujiulize mifumo ya serikali ikiwa na kasoro tunafunga hizo ofisi za umma? Ofisi gani ya umma imewahi kufungwa kupisha matengenezo ya mfumo?

Inawezekana Mh. Rais anawaza vingine na watendaji wanawaza kivingine.

Nilitegemea kwenye tangazo hili iwepo kauli kwamba LATRA wamefanya ukaguzi wa mfumo wa Kilimanjaro nakubaini kasoro 1,2,3.....wamewaelekeza kuzitatua na kufikia tarehe .......zisipotatuliwa kampuni itafungiwa kutoa huduma........kupitia tangazo la aina hi means kampuni inajua, wasafiri wanajua na hivyo unawaandaa kisaikolojia kuzikwepa hizi athari.

Sory to say, NI TANZANIA PEKEE NDIPO MAMLAKA ZINAKAZANA KUUA BIASHARA BADALA YA KUSIMAMIA UFANISI. NA HII INATOKANA NA MAMLAKA HIZI NYINGI KUPEWA JUKUMU LA KUDHIBITI. MDHIBITI SIKU ZOTE NI MTU WAKUKWAMISHA.
 
Watumishi wa umma wanapaswa kuwa watu wanaotumia akili na busara kubwa sana. Wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi , wanalipwa kwa sababu kuna watu waliamua kufanya biashara. Lakini wao ni kama wanalipwa kwenda kuua biashara nchini.

KUUA BIASHARA BADALA YA KUSIMAMIA UFANISI. NA HII INATOKANA NA MAMLAKA HIZI NYINGI KUPEWA JUKUMU LA KUDHIBITI. MDHIBITI SIKU ZOTE NI MTU WAKUKWAMISHA.
Fuateni sheria
 
Wengi hatupendi kufuata sheria, wala kupinga sheria mbovu, tunapiga kelele zinapogusa maslahi yetu.

Mtoa maelezo utetezi wake ni kutaka kuonyesha LATRA wako kinyume na boss wao na kwamba Kilimanjaro wameonewa bila kusema Kilimanjaro wamefanya makosa gani.
 
Watumishi wa umma wanapaswa kuwa watu wanaotumia akili na busara kubwa sana. Wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi , wanalipwa kwa sababu kuna watu waliamua kufanya biashara. Lakini wao ni kama wanalipwa kwenda kuua biashara nchini.

Nasema haya baada ya kuona LATRA ikitoa tangazo kwa umma lakufungia mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro yasitoe kia tarehe .......zisipotatuliwa kampuni itafungiwa kutoa huduma........kupitia tangazo la aina hi means kampuni inajua, wasafiri wanajua na hivyo unawaandaa kisaikolojia kuzikwepa hizi athari.

Sory to say, NI TANZANIA PEKEE NDIPO MAMLAKA ZINAKAZANA KUUA BIASHARA BADALA YA KUSIMAMIA UFANISI. NA HII INATOKANA NA MAMLAKA HIZI NYINGI KUPEWA JUKUMU LA KUDHIBITI. MDHIBITI SIKU ZOTE NI MTU WAKUKWAMISHA.
Bila picha ni uzushi
 
Huyo mmiliki wa Kilimanjaro Express na watumishi wake ingekuwa China wangekuwa wanasubiri kunyongwa sasa.
Eti eeehh ameajiri watu walengi, kwahiyo ukiajiri watu wengi nchi inakuwa umeitia mfukoni?
LATRA wana authority ya kumburuza mahakamani na kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi akaozee huko, wana authority ya kumfutia leseni .
Kumfungia leseni ni huruma na busara tu
 
Back
Top Bottom