Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Tanzanians to rub shoulders with Arsenal fans at Emirates
By DAILY NEWS Reporter, 3rd December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 20

A DAR ES SALAAM resident, Alkarim Shamshodin Habib has secured a rare opportunity to attend the Barclays English Premier League match between Arsenal and Everton after winning the lottery organized by the Barclays Bank Tanzania Limited.

Habib and other two previous winners will rub shoulders with Arsenal supporters at the Emirates Stadium in London, when the Gunners host Everton for the Premier League second leg match on February 1, next year.

"The first three first prize winners will travel in a group, with their companions and will go to witness the Arsenal versus Everton match on the 1st of February 2010-a home game for Arsenal," said Elizabeth Mayengoh, the Barclays Bank Kinondoni Branch Manager.

"We introduced the lottery in order to provide the Tanzanians with an opportunity to watch the Premier League matches after realising the majority are good followers of English football," she added.

It was a day to remember for Habib as he also won a Plasma flat screen. The promotion is targeted at building the Bank's retail customer base and also giving a chance to customers who are football fans the chance to watch live matches in England.

It involves Barclays Bank customers with the account dubbed premier life banking. Barclays Bank has been associated with the English Premier League since the year 2001 with Barclaycard, a business arm or Barclays Bank, sponsoring the League for 3 years.

In September, the bank launched seven products for promoting the English Premier League, in which lucky customers will get various products including DSTv subscription and fully paid trip to Britain to watch a match.
 
Friday December 03, 2010 Sports
Malawi coach complains of Dar humid weather
By DAILY NEWS Reporter, 3rd December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 19

MALAWI coach Kinnah Phiri joined other coaches in complaining about the scorching weather during lunch time kick-off in the ongoing Cecafa Senior Challenge Cup matches in Dar es Salaam.

"We're playing under severe condition, it is too hot. If you keep running all the time you end up collapsing. In Malawi we are in a raining season now," said Phiri at the end of their game against Uganda which kicked of at 2:00pm.

Dar es Salaam, host of the 2010 Challenge Cup, experiences the highest monthly average high temperature in December, 32 ° C.

The same concern was aired by Ethiopia and Uganda coaches at the end of their lunch-time match last Monday.

"It's very hot, the weather condition was scorching, we're used to play quick passing football, but we could not do that because of the conditions out there," lamented Ethiopia tactician Ifem Onoura.

"It was extremely hot, players were tired and exhausted," said Uganda coach Bobby Williamson.

There are two matches played each day, with earlier kick-off at 2:00pm followed by the late kick-off at 4:00pm. This fixture is, however, for the group stage matches.

All matches take place at the 60,000-seater National Stadium in the city. In another development, the Malawi coach saluted the performances of his side, following another gripping display on Thursday's 1-1 draw against defending champions Uganda on Thursday.

Malawi were denied victory after Emmanuel Okwi scored in the 80th minute to cancel Victor Nyirenda's first half goal.

"It is very good results. If you compare my team with Uganda, there is big difference; I have many players who are playing in the national team for the first time.

"These players are armature, I don't expect too much from them. To me, I'm very satisfied with what they have given so far, they are still learning and I'm still teaching them," Phiri observed.

Williamson also commended the Flames, saying "Malawi were very good team, they caused us a lot of problems, but I'm very proud with my players because they fought hard to get back into the game. Hopeful we'll qualify for the next stage."

With Thursday's results, Uganda and Malawi lead Group C on four points each followed by Ethiopia on three and Kenya are pointless.

Despite their poor ranking, Kenya head coach Jacob Mulee still hopes some miracles will help them through.

"We need to play well against Uganda to see if we can make the next round," said the Kenyan trainer.

"It is unfortunate that we did not have good preparation for this tournament and it is clear that we are still struggling to get a team in the middle of a tournament," added Mulee.
 
Zambia, Rwanda into quarters
By ABDALLAHS MSUYA, 3rd December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 37

ZAMBIA cruised into the quarterfinals of the Cecafa Tusker challenge Cup in fashion after defeating Somalia 6-0, as Rwanda's Amavubi also booked their place in the knock-out stage despite a goalless draw with Zanzibar Heroes.

In the late kick-off match at the National Stadium in Dar es Salaam, Zanzibar Heroes looked out of sort for most part of the game and had their head coach Stuart Hall sent off by Uganda's referee Ali Kalyango after 76th minutes.

The draw dented Zanzibar's hopes of reaching the quarterfinal stage as it left them on four points, while the Rwandans reached five points that put them through.

Zanzibar should now wait for the results of Sunday's clash between Ivory Coast and Sudan. Their best hopes, however, will be for the two best-loser slots.

The Amavubi reached five points Rwanda could have taken the lead after just five minutes when Heroes defender Nadir Haroub gifted the ball to Peter Kagabo, but the Yanga defender made quick amend of his mistake with a timely block to deny the Amavubi striker, who had rifled a powerful shot from barely six yards.

The Amavubi had another two attempts in the 6th and 17th through skipper Haruna Niyozima and Dady Birori, before Haroub was forced into a goal-line clearance as Rwanda missed their best opportunity of the half.

Jean Baptiste Mugiraneza drew fine save from goalkeeper Ali Mwadini and moments later Zanzibar came into the scene with Suleiman Kassim sending a decent effort off target.

The Islanders' first attempt on target came in the final minute of the opening half through Kassim's free kick from the edge of the box. That, in fact was the only meaningful attack by Hall's side before the interval.

Zanzibar looked little livelier after the restart and managed several attacks early on but lacked the cutting edge.

Rwanda had a goal disallowed for offside in the 71st minute, while Khamis Mcha Khamis threw away Zanzibar's best chance in the 76th.

Seconds later, Birori went even closer to open the scoring for Rwanda. He saw his shot bounce off the crossbar and wrongly placed his follow up shot.

In the lunch time kick-off, Felix Sunzu bagged a quartet, while Allan Makuka and Venecious Mapande were also on target as Zambia eased to all three points to move to the top of group A, that also comprises Mainland soccer team Kilimanjaro Stars and Burundi.

The two meet today to decide which team will join Zambia from the group.

Sunzu broke the deadlock on 25 minutes with a well taken shot from inside the area. He added the second two minutes later and Zambia were 3 up after 28th with Makuka the goal scorer.

Sunzu bagged his hat-trick from a spot kick and scored his fourth goal and fifth for Zambia after the restart.

It was almost like a training session for Zambia given their possession and Mapande nodded home ten minutes before time to put some gloss on the win.
 
Stars, Burundi nani kutinga Robo Fainali leo?
• Zanzibar Mhh, Somalia yaaga

na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, leo inashuka dimbani kuumana na Burundi mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Stars itashuka dimbani ikiwa na ari kubwa kutokana na ushindi wa mabao 3-0 ilipoiadhibu Somalia Jumatano na ushindi wa leo utaipa tiketi ya kucheza robo fainali.
Chini ya kocha wake Mdenmark, Jan Poulsen, Stars imejiandaa kikamilifu kushinda mechi hiyo baada ya kukifanyia marekebisho kikosi chake ambapo kilianza vibaya michuano hiyo na kupelekea kufungwa bao 1-0 na Zambia.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na kuwa Burundi nayo pia itataka kushinda mechi hiyo ili isonge mbele kwani ina pointi tatu kama Stars ilizozipata kwa Somalia baada ya kuifunga 2-0.
Katika hatua nyingine, Somalia imeaga michuano hiyo baada ya jana kufungwa katika mabao 6-0 na Zambia.
Aidha, Zanzibar ambayo ilitoka sare ya bila kufungana na Rwanda; inasubiri matokeo kati ya Ivory Coast na Sudan ili kujua kama itasonga robo fainali..
Katika mechi kati ya Somalia na Zambia, mshambuliaji wa FC Lupopo ya Congo, Felix Sunzu, ndiye alikuwa kinara wa mabao kwa kupachika mabao manne peke yake na mabao mengine yakifungwa na Alan Makuka pamoja na Venecious Mapande.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Rwanda Silas Teteh akizungumza baada ya mechi yao na Zanzibar, alilia na mwamuzi wa mchezo huo Ali Kalyango wa Uganda kwa kukataa goli lililofungwa katika dakika ya 77 na Dady Birori kwa kichwa.
Naye kocha wa Zanzibar, Hall Stewart, alisema mabadiliko ya kipindi cha pili yalifanikisha timu yake kucheza vizuri katika kipindi cha pili lakini makosa madogomadogo ya washambuliaji wake yaliikosesha ushindi timu hiyo.
Naye mwandishi wetu Tutindaga Mwakalonge anaripoti kuwa, jeshi la polisi limelazimika kuweka ulinzi wa kutosha uwanjani hapo ili kudhibiti idadi ya mashabiki wanaojitokeza kutokana na kuingia bila kulipa.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova alisema wamelazimika kuongeza ulinzi ili kuzuia maafa ambayo yanaweza kujitokeza iwapo mashabiki hao watazidi 60,000 kama inavyotakiwa.
 
Kenya yajitoa Chalenji kisa njaa


na Dina Ismail


amka2.gif
TIMU ya soka ya Kenya ‘Harambee Stars' imejiondoa kushiriki michuano ya Chalenji inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ikishinikiza kulipwa posho toka kampuni inayosimia soka nchini Kenya. Wachezaji na benchi la ufundi wanadai posho zao hizo zinazofikia sh mil. 1.2 za Kenya (karibu sh milioni 18 za Tanzania).
Kocha mkuu wa timu hiyo Jacob ‘Ghost' Mulee aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba hali hiyo ndiyo imechangia kwa kiasi kikubwa timu yao kufanya vibaya kwenye michuano hiyo.
Alisema viongozi hao wamekuwa wakiwapiga kalenda kuhusiana na suala hilo hivyo wachezaji waligoma kufanya mazoezi kuanzia jana asubuhi na msimamo huo utabadilika pindi watakapolipwa posho zao.
Mulee aliongeza kuwa hata mechi yao ya kesho dhidi ya Uganda hawatacheza kama hali hiyo itaendelea kwani wachezaji wake wameathirika kisaikolojia kwa kiasi kikubwa.
"Tuko tayari kwa lolote, timu itafanya vipi vizuri kama ina matatizo? Hata wakitulipa kama wanavyodai tutafikiria kwanza kabla ya kuamua," alisema.
Hata hivyo makamu mwenyekiti wa kampuni hiyo Erastus Okuli aliwataka wachezaji kuacha visingizio visivyo na sababu kwani baada ya kufanya vibaya ndiyo wanatoa sababu hizo.
Okuli alisema timu hiyo inajua itafungwa na Uganda katika mechi yao ya kesho na kama wangefanya vema katika mechi zao za mwanzo wasingetoa visingizio hivyo.
"Tumesikia malalamiko yao lakini mpaka sasa hatujapata fedha za kuwalipa, kama atatokea mtu wa kuwapatia itasaidia sana," alisema Okoli.
Kenya iliyo Kundi B pamoja na Ethiopia, Malawi na Uganda imefanya vibaya katika mechi zake zote mbili ambapo ilianza kwa kufungwa na Malawi mabao 3-1 kabla ya juzi kutandikwa 2-0 na Ethiopia matokeo yanayowatoa moja kwa moja katika michuano hiyo.
 
34 wapya wasajiliwa Ligi Kuu


na Makuburi Ally


amka2.gif
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia dirisha dogo, zoezi lililoanza Novemba mosi hadi 30. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni, alisema klabu 11 za Ligi Kuu ndizo zilizofanya usajili wa kujaza nafasi lakini Polisi Tanzania pekee ndiyo ambayo haijajaza nafasi za wachezaji kipindi hiki.
Kayuni alisema wachezaji 34 ndio waliosajiliwa kwa ajili ya kukipiga katika kipindi cha dirisha dogo.
Aliwataja wachezaji waliosajiliwa na Simba kuwa ni Meshack Abel (African Lyon) na Ali Ahmed Shiboli (KMKM), huku Yanga ikiwasajili Juma Seif Dion (JKT Ruvu) na Davies Mwape (Konkola Blades) na Mtibwa Sugar imewasajili Salum Swed (Azam) na Hussein Omar (Huru).
Aidha, JKT Ruvu imewasajili Erick Majaliwa , Bakari Kondo na Feisal Swai (Huru), huku AFC ikiwasajili David Naftal (Simba kwa mkopo) na Majimaji imewasajili Ulimboka Mwakingwe, Yahaya Shaban na Kassim Kilungo (Huru), Patrick Betwel (Polisi Iringa) na Mohamed Kijuso (Simba).
Azam FC imewasajili Ahmad Chimpele na Ali Chimpele (U-20 Azam), huku African Lyon ikiwasajili Shaban Aboma (Mtibwa Sugar) na John Njama (TMK Utd) wakati Kagera Sugar imewasajili Juma Mwenza na Steven Mazunda (Huru) na toto African imewasajili Kamana Bwiza, Mussa Vologwe, Mathias Wandiba, Malegesi Mwangwa na Said Mwangwa (Huru).
Ruvu Shooting imewasajili Jumanne Ramadhan, Maneno Jasho, Lungwecha Shaibu, Omary Senkobo, Oscar Joshua, Shaban Idd, Hamis Sefu na Yasin Selemani.



h.sep3.gif
 
Taifa Queens yakwea pia Singapore, bila Wazenji
• CHANETA yalia na mgomo wa CHANEZA

na Mwandishi wetu


amka2.gif
TIMU ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens' iliondoka nchini jana kwenda Singapore kushiriki mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha mataifa sita huku ikitakiwa kutowaangusha Watanzania. Rai hiyo ilitolewa katika hafla fupi ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo iliyofanyika juzi kwenye kambi yao iliyoko Shule ya Filbert Bayi, Mkuza Kibaha, na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Iddi Kipingu.
Kipingu alisema, kufanya vizuri kwa timu hiyo katika mashindano hayo, kutawaongezea heshima wachezaji pamoja na nchi kwa ujumla, licha ya kambi yao kutokuwa na posho muda mrefu, lakini watumie uzoefu wa mashindano ya kimataifa waliyoshiriki hivi karibuni.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, alitoa pongezi kwa wadau na taasisi mbalimbali ikiwamo Ikulu, Jeshi la Wananchi na Magereza kwa kuwagharamia wachezaji walioko timu hiyo ambao ni waajiriwa huko, huku akisikitishwa na wenzao wa Zanzibar (CHANEZA), kugoma kushirikiana nao.
"Tatizo lingine kwa timu yetu inayosafiri ni kukosekana kwa wachezaji kutoka Zanzibar. Suala hili limetupa shida na wakati mgumu, hasa kutokana na kuwaita wenzetu tukae kikao Julai 3, mwaka huu, lakini hawakutaka na hata tulipofanya hivyo tena Novemba 20 napo wakagoma," alisema.
Wachezaji wanaoondoka leo ni nahodha Jackline Sikozi, Lilian Sylidion, Irene Elias, Lydia Samwel, Restituta Boniphace, Eva Peter, Veronica Kubiru, Sekela Dominick, Mwanaidi Hassan, Paskalia Kibayasa na Zuhura Twalibu.
Viongozi ni Rose Kisiwa, kocha Simone Mckinns na msaidizi wake, Damian Chonya, ambaye pia ni mwamuzi wa kimataifa anayetambuliwa na IFNA na daktari Richard Yomba.
Hivi karibuni katika salamu zake za pongezi kwa Waziri mpya wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Abdillahi Jihad Hassan, mbali ya kumpongeza Rais Ali Mohammed Sheni kwa uteuzi huo, walimuomba aangalie namna ya kudumisha ushirikiano wa vyama hivyo na kutowapa nafasi watu wachache wanachochea makundi badala ya kutanguliza maslahi ya taifa.
 
Majimaji kujipanga Msumbiji


na Juma Kasesa


amka2.gif
TIMU ya Soka ya Majimaji ya Songea ‘Wanalizombe' inatarajiwa kwenda Maputo nchini Msumbiji Desemba 20 kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki kujinoa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 15 mwakani. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Ahmed Dzumba, ziara hiyo ina lengo la kuwaweka tayari wachezaji kwa kinyang'anyiro cha ligi hiyo, ili kuhakikisha inatwaa nafasi tatu juu.
Alisema, kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuingia kambini Desemba 15 mjini Songea, chini ya kocha wao mpya Sebastian Mkomwa akisaidiwa na Peter Mhina kabla ya ziara hiyo ya Msumbiji, ambapo watarejea Januari 10 mwakani kujiandaa na mchezo dhidi ya ‘Maafande' wa JKT Ruvu.
Dzumba alisema timu hiyo imeishakamilisha zoezi la usajili ambapo imewaongeza katika dirisha dogo wachezaji Ulimboka Mwakingwe, Mohamedi Kijuso, Kassim Kilungo, Yahaya Shaban na Patrick Betwel ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kuongeza ushindani katika Ligi Kuu.
 
Usaili wagombea FRAT leo


na Makuburi Ally


amka2.gif
WAGOMBEA 14 wa nafasi za uongozi wa Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (FRAT), leo wanatarajiwa kusailiwa tayari kwa uchaguzi utakaofanyika Desemba 29. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Eugene Mwasamaki, alisema usaili huo utafanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Karume, jijini Dar es Salaam, chini ya Kamati ya Uchaguzi iliyo chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Muhidin Ndolanga.
Mwasamaki aliwataja waliojitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni pamoja na Omar Abdulkadir, Lucas Agoro na Said Nassor, wakati Makamu Mwenyekiti ni Tito Haule na Juma Mpuya.
Katibu Mkuu ni Leslie Liunda na Victor Mwandike, Katibu Msaidizi Abdallah Mitole ambaye ndiye mgombea pekee huku Mweka Hazina ikiwaniwa na Charles Ndagala na Israel Mwansasu wakati Kamati ya Utendaji wako Chaula, Soud Abdi, Siso Ramadhan na Khagula Ruvu.
 
Manju Msita kushiriki maonyesho Msumbiji


na Dina Ismail


amka2.gif
MBUNIFU wa mavazi nchini, Manji Msita anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika wiki ya mavazi ya Msumbiji ‘Mozambique Fashion Week 2010' itakayofanyika kuanzia Desemba 6 hadi 11 jijini Maputo, Msumbiji. Meneja Habari na Matukio wa Swahili Fashion (SFW), inayompeleka mbunifu huyo huko, Saphia Ngalapi, alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba, huu ni mwaka wa pili kupeleka mwakilishi katika wiki hiyo tangu waanze ushirikiano huo, ambapo mwaka 2009 waliwakilishwa na Jamila Vera Swai.
Alisema, hatua hiyo ya ushirikiano ilifuatiwa na wanamitindo Adelia na Sheila Tique kuiwakilisha Msumbiji hapa nchini katika Swahili Fashion Week mwaka jana na mwaka huu iliwakilishwa na Marinella Rodriguez katika SFW iliyofanyika Novemba 4 hadi 6 viwanja vya Karimjee.
Ngalapi aliongeza kuwa Manju alichaguliwa na muandaaji wa maonyesho ya mavazi wa kimataifa Jan Malan Umzingeli kwa kushirikiana na SFW, kwa kigezo kwamba kazi zake zina kiwango cha juu kulingana na ubora wa ubunifu wa mavazi yake.
Naye Manju alisema, anajisikia furaha kupata nafasi hiyo hivyo anaamini ataipeperusha vema bendera ya Tanzania katika ‘Mozambique Fashion Week' ya mwaka huu.
Katika hatua nyingine, SFW leo inatarajiwa kuadhimisha siku ya ukimwi duniani kwa kufanya hafla maalumu ya kutunisha mfuko wa chama cha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi visiwani Zanzibar (ZAPHA), katika Ukumbi wa Mercury's.
 
Hatimaye Rich One apata meneja mpya


na Shehe Semtawa


amka2.gif
MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la TMK lililoibuka kutoka TMK Wanaume Halisi, Richard Shauri ‘Rich One', baada ya kusota kwa muda sasa amefanikiwa kupata meneja mpya atakayesimamia kazi zake kuanzia sasa. Akizungumza na mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rich One alisema, awali walikuwa na Meneja lakini sasa yuko nje ya nchi, hivyo kuwafanya kushindwa kuendeleza shughuli zao, jambo lililowasukuma kumsaka mtu mwingine sahihi wa kusimamia kazi zao na wanashukuru wamempata.
Msanii huyo alimtaja Meneja huyo mpya kuwa ni Vicent Kolosa ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Stanbic.
Alisema, Meneja huyo ndiye atakayewezesha kukamilisha albamu yake ambayo atapewa sapoti na wakali kama vile Daz P, Mzimu, Juma Jaz, A Man na Kaka Man.
Aidha, aliongeza kuwa wanachosubiri ni uongozi wa studio za Mpo Afrika wapange ratiba za shoo za mikoani hivi karibuni kwa ajili ya kutoa burudani na kujitangaza zaidi.
 
Z'bar Heroes njia panda
Friday, 03 December 2010 19:49 0diggsdigg

Iman Makongoro
ZANZIBAR Heroes imejiweka njia baada ya kukubali kulazimishwa suruhu na Rwanda iliyofuzu kwa robo fainali michuano ya Tusker Chalenji sambasamba na Zambia iliyoichakaza bila ya huruma Somalia kwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Zambia na Rwanda zimefuzu, wakati Zanzibar Heroes wenye watabidi kusubili matokeo ya michezo wa mwisho ya kundi yaliyobaki kuona kama watafuzu.

Zanzibar iliyokuwa imebeba matumaini ya Watanzania wengi baada ya kuanza kwa kishindi michuano hiyo kwa kuichapa Sudan 2-0, ilijikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ivory Coast na kulazimishwa suluhu na Rwanda.

Heroes wamefikisha pointi nne huku Rwanda ikiwa imefuzu kwa pointi tano na Ivory Coast pointi 3 kabla ya mechi ya mwisho hapo kesho dhidi ya Sudan inayoshikiria mkia kwa pointi moja katika Kundi B.

Mapema Mshambuliaji Felix Sunzu alipachika mabao manne peke yake na kuisaidia Zambia kuinyuka Somalia kwa mabao 6-0.

Mshambuliaji huyo wa Chipolopolo alifunga mabao yake mawili katika dakika 24 na 27 kwa mashuti yaliyomshinda kipa wa Somalia kabla ya Allan Mukuka kuipatia Zambia bao la tatu dakika 27.

Sunzu aliendeleza kalamu hiyo kwa kupachika bao la nne kwa mkwaju wa penalti baada ya kufanyiwa faulo kwenye eneo la hatari na Adam Hussen Ibrahimu, aliongeza bao la tano dakika ya 49 kabla ya Venecious Mapande kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Somalia dakika 80 kwa kufunga bao la sita.
 
Musonye awapasha Harambee Stars
Friday, 03 December 2010 19:46 0diggsdigg

Jackson Odoyo
KATIBU mkuu wa Shirikisho la Vyama soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, Nicholaus Musonye ameitaka timu ya taifa ya Kenya, Kenya Harambee Stars kuacha tabia ya kuzungumzia masuala yao ya nyumbani ugenini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msonye alisema timu hiyo imekuwa ikilalamika kuwa haina pesa wakati hilo si suala la Cecafa isipokuwa ni suala la shirikisho la soka la nchi hiyo (KFF).

"Ni tabia mbaya kwa timu kubwa kama ya Kenya kutoa siri zao za ndani ugenini, ninatambua kuwa timu hiyo aina pesa na mimi kama mkenya nimekuwa nikijitahidi kila wakati kutafuta kila namna ya kuisaidia timu"alisema msonye.

Alisema kitendo cha timu hiyo kuanza kulalamika kuwa haina fedha inaleta picha mbaya kwa wadhamini wa mashindano ambayo makao makuu yake yako nchini humo na kwamba kila timu katika mashindano haya ina hali mbaya kifedha lakini hawajalalamika.

"Mbona Somalia hawalalamiki?...mbona Burundi hawalalamiki, iweje wao ndiyo wawe wa kwanza kulalamika, hakuna mwanaume anayeweza kumpeleka mkewe mahakamani kwa kushindwa kumtimizia mahitaji yake ya ndani sasa iweje wao waanze kutoa siri zao za ndani nje," alifafanua Musonye.

Alisema itakapofika wakati timu zinapewa posho kila timu itapata posho yake lakini kwa kipindi hiki bado, hivyo sioni sababu ya wao kuanza kulalamikia suala hiolo.

Musonye alisema kama walipewa ahadi ya kupewa fedha kutoka kwenye shirikisho lao hilo si suala la Cecafa isipokuwa ni suala la shirikisho lao,ikuwa ni jambo bora wakisubiri mpaka watakaporudi nyumbani.

"Hatuwezi kukubaliana na suala kama hilo kwa sababu kila timu ilikuja hapa ikifahamu hali halisi ya mashindano haya na kwamba aya kila timu ilipaswa kujipanga ipasavyo,na si kuanza kulalamikia na kuleta mambo yao ndani katika mashindano haya.
 
Kocha Ivory Coast asifu amani Tanzania Friday, 03 December 2010 19:44 0diggsdigg

Sweetbert Lukonge
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Kouadio Georges ambaye timu yake inashiriki michuano ya Chalenji, ameelezea kufurahishwa na hali ya amani na upendo walionayo wananchi wa Tanzania.

Akizungumza na Mwananchi jana kocha huyo alisema kuwa tangu alipoingia nchi amekuwa akifurahia jinsi Watanzania wanavyoishi kwa upendo na amani bila ya kubagua wageni jambo ambalo ni vigumu kuliona katika nyinchi nyingine za Afrika.
"Tanzania ni nchi nzuri pia watu wake ni wema ambao wanaupendo kwa kila mtu jambo ambalo kwa hakika vigumu kulikuta katika nchi nyingine.

"Nimebahaitika kutembea sehemu mbalimbali za jiji la hili la Dar es Salaam na nimejifunza mengi mbayo hata mgeni yeyote atakayeingia leo hii Tanzania lazima atafuraiya kuyaona lakini kubwa zaidi ikiwa ni upendo na amani uliopo kwa kila mutu," alisema Georges.

Katika hatua nyingine kocha huyo ameutaka uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana Serikali kujitahidi zaidi kutengenza msingi wa kuviendereza vipaji vya soka kama zilivyo nchi za Magaribi mwa Afrika.

Alisema Tanzania inavipaji vingi vya soka lakini vinakosa msingi na endapo kama vikiwezeshwa hakika itakuwa ni moja ya nchi tishio katika soka la Afrika.
 
Fifa yatafakari matukio baada ya mchakato wa 2018, 2022 Friday, 03 December 2010 19:43 0diggsdigg

ZURICH, Uswisi

MATOKEO ya uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 ambayo yamezipa nafasi Russia na Qatar yameiachia makovu Fifa.

Misimamo tofauti kutoka kwa nchi ambazo ziliomba kuandaa fainali hizo na kisha kukosa nafasi hiyo imeiacha Fifa ikilazimika kujiangalia upya endapo iendelee na mfumo wa sasa au ibuni mpya.

Lakini, Fifa ina miaka 10 ya kujiangalia upya ili kuona kama inahitaji mfumo mpya au kung'ang'ania huu wa sasa wakati wa kuteua nchi gani zitaandaa fainali za mwaka 2026.

Kipindi hiki kitaliwezesha shirikisho hilo kubadili au kuendelea na mfumo wa sasa wa kutumia wajumbe 24 wa kamati ya utendaji kuamua jambo hilo.

Mwaka huu, kamati hiyo ilikuwa na wajumbe 22 pekee baada ya wawili kusimamishwa kwa kashfa ya kutaka kuuza kura zao na ukosefu wa uaminifu.

Rais wa Fifa, Sepp Blatter, ambaye alionyesha kufadhaishwa na kashfa hiyo iliyohusisha wajumbe wawili wa kamati ya utendaji kama walivyofichuliwa na gazeti la Sunday Times la Uingereza, alisema shirikisho lake lilihitaji kuwa thabiti katika kukabiliana na kashfa.

"Tunatakiwa kujitazama upya ili kuepuka mambo kama hayo katika siku zijazo. Hiki ni kitu ambacho hakina budi kuangaliwa kwa umakini," alisema. "Tukiwa na uzoefu katika maisha, huwezi kurejea kosa hilo mara mbili."

Aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo, Michel Zen-Ruffinen alieleza kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo, lakini kwa kutumia wakaguzi kutoka nje ya shirikisho hilo.

Lakini, swali la msingi ambalo linaulizwa kwa sasa baada ya matukio hayo, nikuwa Fifa itachukua au la, hasa katika suala hili la kupatikana kwa nchi mwenyeji wa Kombe la Dunia kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, au pengine kama Fifa itakaa kando na kuacha vumbi litue na kusahau.

Blatter amesisitiza kuwa tume ya maadili inayoongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Uswisi, Claudio Sulser, inao uwezo wa kuandaa sera zinazoifaa Fifa.

Ili kukabiliana na upunfugu ambao umejitokeza msimu huu, Serikali ya Uswisi imeeleza waziri wake wa michezo ametakiwa kuandaa kanuni na kipengele kinacohusu rushwa katika michezo.

Endapo sheria hiyo itabadilishwa, Fifa inaweza kulazimika kukubali kuingiliwa na vyombo vya nje itake au isitake.
 
Liverpool yafuzu kucheza 32 Europa League Friday, 03 December 2010 19:42 0diggsdigg

MILAN, Italia

KLABU za Liverpool, Paris St Germain, Besiktas, Dynamo Kiev, Sparta Prague na Villarreal zimekata tiketi ya kucheza 32 bora kwenye michuano ya Europa League juzi.

Huku Ulaya ikikabiliwa na hali mbaya ya hewa, idadi kubwa ya mabao ilishuhudiwa katika mechi hizo.

PSG ilishinda 4-2 nyumbani dhidi ya Sevilla, ambao wanashindana na Borussia Dortmund kusaka nafasi ya pili zitakapokutana Desemba 15 kwenye mchezo wa Kundi J.

Dortmund iliikaribia Sevilla baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Karpaty Lviv. Besiktas ilikata tiketi yake kutoka Kundi L baada ya ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya CSKA Sofia ya Bulgaria wakati Rapid Vienna ilishindwa 3-1 nyumbani na Porto, ambayo tayari imekata tiketi.

Dynamo Kiev ilishinda 4-1 dhidi ya BATE Borisov ambayo ilishavuka na hivyo nayo kufuzu , ikimaanisha kuwa sare ya AZ Alkmaar ya bao 1-1 dhidi ya Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi E haukuwa na maana.

Milan Jovanovic, ambaye ni nadara kutumika katika mechi za Ligi Kuu England aliipa uongozi Liverpool dhidi ya Steaua Bucharest kwa kichwa safi kipindi cha kwanza, ingawa Eder Bonfim alisawazisha, pointi ilitosha kuwakatia tiketi mabingwa hao mara tano wa Ulaya.

"Ilikuwa kazi kubwa kwa wachezaji kuhimili vishindo na aina ya soka iliyochezwa na Steaua," alieleza kocha Roy Hodgson akizungumza na waandishi wa habri baada ya mchezo huo.

"Ni mafanikio kwetu, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba tumekuwa na msimu mgumu, kiasi cha kuwatumia wachezaji wasiozoeleka kucheza Ligi Kuu."

Palermo nje

Mabao lukuki Kundi K ambako mchezaji wa kimataifa wa Uruguay,Edinson Cavani alifunga matatu, hat-trick kwenye sare ya 3-3 ya Napoli dhidi ya Utrecht, ambako mshambuliaji Ricky van Wolfswinkel alifunga mawili lakini hayakusaidia.

Sare hiyo inaamanisha kuwa Napoli ni timu pekee ya Italia ambayo bado inasaka nafasi katika hatua hiyo ikiwa pointi mbili nyuma ya Steaua, mchezo wa mwisho utakuwa nyumbani dhidi ya klabu hiyo ya Romania, Desemba 15.

Palermo ikiwa na wachezaji tisa ilitolewa licha ya mara mbili kuongoza dhidi ya Sparta Prague na kumaliza kwa sare ya 2-2 kisiwani Sicily. Dorin Goian alitolewa kwa kadi nyekundu na Javier Pastore pia alifuata dakika za majeruhi.

CSKA Moscow ambao tayari wamefuzu walishangilia uenyeji wa nchi yao kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Lausanne ambayo imetolewa kwa mabao mawili ya Tomas Necid , kutoka Kundi F.
Stefan Scepovic aliipa sare Club Bruges ya bao 1-1 dhidi PAOK Salonika na kuwasaidia vinara wa Kundi D, Villarreal kusonga mbele kwa 3-0 dhidi ya Dinamo Zagreb nchini Hispania.

Makundi A-C na G-I, mechi zao zilichezwa Jumatano, huku mabingwa mara mbili Ulaya, wakiwa timu kubwa pekee kutupwa nje.
 
Kenya watishia kujitoa
Friday, 03 December 2010 19:48 0diggsdigg

Makoba Hassan
BAADA ya kutolewa kwenye mashindano ya Tusker Chalenji timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars imetishia kujitoa na kugomea mchezo wa dhidi ya maasimu wao wakubwa, Uganda kwa kile wanachodai kutolipwa posho zao kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kocha Jacom Mulee alisema kuwa hatua hiyo imekuja mara baada ya wachezaji wake kulalamikia uongozi wa kutowalipa posho zao kipindi chote cha mashindano.

Alisema kuwa wachezaji wamechukua hatua hiyo kwa kile kilichadaiwa kuwa uvumilivu umewashinda kwani wamekuwa wakiaihidiwa kila siku kuwa watalipwa posho hizo.

"Nimeongea na wachezaji ambapo wamenihakikishia kwamba hawatacheza mchezo huo kwani hawajalipwa fedha zao tangu walipocheza na timu ya Kili Stars huku wakisisitiza kuwa si kwamba wanaiogopa Uganda bali wanachotaka ni haki yao

"Waliahidiwa kuwa wangelipwa juzi mara baada ya mchezo wao dhidi ya Ethiopia, lakini hawakulipwa na kuongeza kuwa hata kama wangeshinda michezo ya nyuma wasingecheza mchezo wao dhidi ya Uganda.

Naye nahodha wa timu hiyo, James Situma alisema kuwa ni kweli wameamua kutocheza mchezo huo na wapo tayari kuondoka hata leo kutokana na kucheleweshewa posho zao ambazo walitakiwa kulipwa tangu Jumanne.

Alisema kuwa walipokuja walikuwa wamejiandaa kucheza kwa moyo wote, lakini kitendo cha kutolipwa posho zao kimewakatisha tamaa na hivyo wameamua kutocheza hata huo mchezo wa Jumapili dhidi ya Uganda.

"Hata jana ilitakiwa tusicheze mchezo wetu dhidi ya Ethiopia lakini tuliamua kuheshimu maneno ya kocha ambaye alitusii kucheza huku akituhakikishia kuwa tungelipwa posho zetu baada ya mechi kitu ambacho hakikufanyika," alisema Situma.

Aliongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya wachezaji chipukizi wanaochipukia sasa katika mchezo wa soka nchini mwao na kuwatengenezea mazingira mazuri hapo baadae ili kuepukana na kitu kama hichi.

"Tumeamua kutocheza si tu kwa ajili ya kudai posho zetu bali ni kwa ajili ya kuwatengenezea mazingira mazuri watu wanaukuja nyuma yetu hasa ukizingatia nchini mwetu kuna vupaji vingi hivyo ni vyema wakakuta kuna utaratibu mzuri wa uendeshaji wa soka nchini mwetu," alisisitiza nahodha huyo kwa uchungu mkubwa.

Kwa upande wake makamu wa tatu wa mwenyekiti wa shirikisho la soka la Kenya (KFF), Erustus Okul amesema kuwa kitendo cha timu hiyo kugomea mchezo wao dhidi ya Uganda kwa madai ya kucheleweshewa posho zao si sahii kabisa.
Alisema kuwa wamekuwa wakiwalipa fedha zao kwa wakati katika michezo mbali mbali ya ndani na nje ya nje hivyo hili lililotokea sasa ni suala la bahati mbaya kwani wameshawaahidi kuwa lazima wangewalipa fedha hizo.

Okul alisema kuwa hawawezi kugoma kucheza kisa hatujawalipa fedha hizo pengine hizo ni dalili za kuwaogopa wapinzani wao Uganda na si vinginevyo kama wanavyodai.

"Suala hili limetokea kwa bahati mbaya kwani kiasi kilichotolewa kwa ajili ya wachezaji hao hakikutosha ndio maana tumewaahidi kuwalipa posho zao kwani ni haki yao kupata na si kugomea mechi

"Kwanza hawajashinda mechi hata moja kitendo ambacho hakijatufurahisha hata kidogo na kama wataendelea kugomea mchezo wao basi wajiandae kufungiwa na Shirikisho la Soka, Cecafa," alisitiza Okul.
 
Stars, Zanzibar zategwa Chalenji
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 4th December 2010 @ 07:26 Imesomwa na watu: 170; Jumla ya maoni: 0


12_10_jcxag6.jpg

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda, Abouba Sibomana (mbele) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa timu ya Zanzibar Heroes, Khamis Mcha Khamis wakati wa mechi ya Kombe la Chalenji iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana. (Picha na Fadhili Akida)



MASHINDANO ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yanayoendelea Uwanja wa Taifa Dar es Salaam sasa yameingia kwenye hatua ngumu zaidi.

Zambia ‘Chipolopolo' jana ilikuwa ya kwanza kutoka Kundi A kufuzu baada ya kuifunga Somalia mabao 6-0, hali ambayo inaifanya Somalia nayo kutupwa nje ya michuano hiyo.

Zambia imecheza mechi tatu, imeshinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' kisha ikatoka sare na Burundi na jana ikaifunga Somalia, hivyo imefikisha pointi saba, ambazo ni Burundi pekee yenye pointi nne inayocheza na Kilimanjaro Stars leo inaweza kuzifikia kama itashinda.

Kilimanjaro Stars leo itabidi ikaze buti ishinde ili ifuzu hatua ya robo fainali, vinginevyo nayo hali itakuwa ngumu, kwani kama itashinda itafikisha pointi sita hivyo itakuwa imeingia kwa kushika nafasi ya pili, lakini ikifungwa itakuwa imejiweka kwenye mazingira magumu baada ya Zanzibar jana kutoka 0-0 na Rwanda katika mchezo wa Kundi B.

Matokeo hayo yameifanya Rwanda ifikishe pointi tano na kufuzu robo fainali, huku Zanzibar ikifikisha pointi nne lakini ikitegemea zaidi matokeo ya mchezo wa mwisho kati ya Ivory Coast na Sudani kwa kundi hilo.

Kama Ivory Coast itashinda itakuwa imefikisha pointi sita na kuungana na Rwanda, hivyo Zanzibar yenye pointi nne itasubiri kufuzu kama timu yenye uwiano mzuri wa pointi kwa vile ina pointi nne na kama Kilimanjaro Stars itafungwa, basi Zanzibar itakuwa tayari imejihakikishia nafasi moja kati ya mbili zinazotakiwa.

Lakini kama ikitokea Ivory Coast ikafungwa na Sudani ambayo ina pointi moja, basi itakuwa imetolewa na badala yake Sudani na Zanzibar moja itafuzu kama timu ya pili kwenye kundi na nyingine itasubiria kapu.

Timu za Kundi C, Malawi na Uganda kila moja ina pointi nne, ambapo Ethiopia ina pointi tatu na Kenya haina pointi, ikitokea michezo yao ya mwisho kama Ethiopia itaifunga Malawi basi Ethiopia itakuwa imefuzu, hivyo Malawi itaangalia matokeo ya Uganda na Kenya, ambapo kama Uganda itashinda basi Malawi nayo itakuwa kwenye kundi la kusubiria kapu la timu zenye uwiano mzuri wa pointi ili zifuzu robo fainali.

Kulingana na taratibu za Baraza la Vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) timu mbili za juu kutoka kila kundi kati ya makundi matatu ya michuano hiyo zitafuzu robo fainali, ambapo timu mbili nyingine zitakuwa zile zenye uwiano mzuri wa pointi, ambazo zitapenya.

Katika mchezo wa Zanzibar Heroes na Rwanda jana ulikuwa wa ushindani wa hali ya juu, ambapo washambuliaji wa timu zote walikosa umakini kila walipokaribia lango.
 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza orodha ya wachezaji walioombewa usajili kwenye dirisha dogo kwa ajili ya duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika orodha hiyo wachezaji waliosajiliwa na Simba ni Ali Ahmed Ali ‘Shiboli' kutoka KMKM ya Zanzibar na Meshack Abel kutoka African Lyon, wakati Yanga ni Juma Seif Dion wa JKT Ruvu na Davies Mwape kutoka Konkola Blades ya Zambia.

Walioombewa usajili na timu ya Ruvu Shooting ni Jumanne Ramadhan, Maneno Jasho, Lungwecha Shaib, Omary Senkobo, Oscar Joshua, Shaaban Idd, Hamis Seif na Yassin Abdallah ambao wote ni huru, huku Kagera Sugar ikiwasajili Juma Seif na Steven Mazanda ambao pia ni huru.

Waliosajiliwa na JKT Ruvu ni Erick Majaliwa, Bakari Kondo na Feisal Swai ambao pia ni huru, Mtibwa Sugar ni Salum Swed kutoka Azam na Hussein Javu ambaye ni huru, huku African Lyon ikiwasajili Shaban Aboma kutoka Mtibwa na John Njama wa TMK United.

Azam yenyewe imesajili wachezaji wawili kutoka timu yake ya watoto ambao ni Ahmed Chimpele na Ali Hamis Chimpele, wakati AFC Arusha imemchukua David Naftali kwa mkopo kutoka Simba na Majimaji imewasajili Ulimboka Mwakingwe, Yahaya Haruna na Kassim Kilungo ambao ni huru.

Wengine waliosajiliwa Majimaji ni Mohammed Kijuso ambaye amechukuliwa kwa mkopo kutoka Simba na Patrick Betwel kutoka Polisi Iringa.
 
Lavingia kuanza mambo Syria leo
Imeandikwa na Mbonile Burton; Tarehe: 3rd December 2010


MCHEZAJI nyota wa snuka nchini, Arjun Lavingia anaanza kutupa karata kwenye michuano ya Dunia ya mchezo huo iliyopangwa kuanza leo mjini Damascus, Syria.

Akizungumza na HABARILEO Dar es Salaam jana nahodha wa snuka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Jay Somani alisema mchezaji huyo aliyeondoka nchini juzi amefika salama na ana ari ya kufanya vizuri.

Somani alisema Kamati yake inaishukuru Kampuni ya Cargostars Ltd ya jijini kugharamia tiketi ya ndege kwenda na kurudi mchezaji huyo na Rupesh Sonny ‘Kugi', kuchangia gharama za kuishi nchini humo muda wote wa michuano.

Alisema michuano hiyo inayoanza leo itadumu kwa wiki mbili ikikutanisha miamba kutoka nchi mbalimbali duniani.

Somani alisema nchi zaidi ya 48 zinatarajia kupambana kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.

"Lavingia amesema yupo tayari kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na tunamtakia kila la heri.

"Amefanya mazoezi makali kabla ya kuondoka na tunaimani na kiwango chake kwamba atatoa upinzani mkali na kufanya vizuri."

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo.

Lavingia mapema mwaka huu pia alikuwa Mtanzania wa kwanza kushiriki mashindano ya snuka ya Afrika yaliyofanyika Cairo, Misri ambako alifika hatua ya robo fainali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom