Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Mh!wewe ni mwandishi wa habari za michezo!hongera kwa post nyingi ulizozitoa!!
 
BFT kunoa makocha wapya


na Samia Mussa


amka2.gif
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limeandaa kozi ya awali ya ukocha ambayo itashirikisha mabondia wa zamani pamoja na walimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa BFT Eckland Mwaffisi alisema, lengo la kozi hiyo ni kupata walimu wazuri ambao wataibua vipaji vya mabondia ambavyo vimejificha mitaani na shuleni ili viweze kuendelezwa.
Mwaffisi alisema, kozi hiyo itafanyika kuanzia Desemba 14 hadi 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambapo mafunzo hayo yatakuwa ya nadharia na vitendo, ambapo washiriki watajengewa uwezo na walimu waliobobea katika fani hiyo.
Alisema, gharama ya kozi hiyo kwa kila mshiriki ni sh 20,000 na kutoa wito kwa makocha kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo hayo, ili waweze kutimiza malengo ya kuibua vipaji vilivyojificha mitaani na shuleni.
Wakati huo huo, shirikisho hilo limempongeza Emmanuel Nchimbi kwa kuchaguliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Habari, Vijana na Michezo pamoja na Naibu wake Dk. Funella Mukangara.
Alisema, BFT inaamini kuwa, viongozi hao wataleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya michezo, hasa kwa kushirikiana na viongozi wa vyama au mashirikisho yanayosimamia michezo mbalimbali nchini.
"Ushirikiano huo na viongozi husika, utabadilisha historia ya Tanzania kuwa watalii au wasindikizaji katika michezo mbalimbali, kwani changamoto kubwa iliyopo katika vyama husika vya michezo ni maandalizi duni ya wachezaji katika mashindano ya kimataifa," alisema Mwaffisi.
 
Nchunga, Mosha wayamaliza kiaina Yanga


na Samia Mussa


amka2.gif
LICHA ya kutangazwa kumalizika kwa mtafaruku wa viongozi wa juu wa klabu ya Yanga, Mwenyekiti Lloyd Nchunga na Makamu wake Davis Mosha hali bado si shwari. Hali hiyo ilijitokeza jijini Dar es Salaam jana, wakati viongozi hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti.
Kwanza alianza Mosha ambaye alipohojiwa kuhusu mgogoro huo, alisema yuko Yanga kwa muda mrefu kwa ajili ya kutetea maslahi ya klabu hiyo na wanachama wake na si kwa maslahi ya mtu binafsi.
Mosha alikiri kujiengua kwenye uongozi wa klabu hiyo kwa muda, ila kwa sasa amerejea tena baada ya kukaa na kuzungumza na viongozi wenzake wa klabu hiyo.
Mosha aliongeza kuwa pamoja na kuumaliza mgogoro huo bado hatambui kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika hivi karibuni, kwa sababu hakikukidhi matakwa yanayotakiwa.
Alisema kuwa awali mdhamini ambaye ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, alikuwa na mapendekezo yake kwenye uongozi wa klabu hiyo, ambapo kamati hiyo ilikaa na kujadili mapendekezo hayo na kumwandikia barua mdhamini huyo, jambo ambalo ni kinyume.
Hata hivyo Moshi alisema, kwa upande wake hana matatizo tena na mwenyekiti wake wala kiongozi yeyote katika klabu hiyo, hivyo yuko tayari kuungana nao ili kufanyakazi kwa ajili ya kuiletea maendeleo klabu hiyo.
"Ni kweli nilijiweka pembeni na klabu ya Yanga, lakini mwenyekiti wangu aliniita tulikaa tukayazungumza hivi sasa yamekwisha, nimeona nizungumze tu kwa kuwa mmeniuliza," alisema Mosha.
Kwa upande wake, Nchunga alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na kuwa ili klabu iende kwenye maendeleo zaidi inatakiwa wamalize migogoro iliyopo, hivyo walikaa na kuzungumza ili kuwatendea haki wana Yanga.
Alisema kuwa matatizo yaliyotokea ni upepo mbaya tu uliopita, hivyo yamekwisha na makamu wake anastahili kufanya kazi zake kama zilivyoainishwa kwenye katiba ambapo alisisitiza kuwa anastahili kufanya kazi za mwenyekiti kama hayupo.
Katika hatua nyingine, Mosha aliwakabidhi vyeti makocha 20 waliohudhuria mafunzo ya muda mfupi ya ngazi ya cheti yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Makocha hao wapya ni Salvatory Edward, Edibily Lunyamila, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya', Willy Mtendamema, Mohamed Hussein ‘Mmachinga', Edgar Chibura, James Manyika, Anthony Chibasa, Said Msasu, Henry Legenga na Hemed Mangwenya.
Wengine ni Burhani Hemed, Chomba Athumani, Oscar Milambo, Jeremiah Ponela, Tangale Tangale, Jagua Kabadika, Salamata Mohamed, Oscar Milambo, Jeremiah Ponela na Daniel Magiro.



h.sep3.gif
 
Nchunga, Mosha wayamaliza kiaina Yanga


na Samia Mussa


amka2.gif
LICHA ya kutangazwa kumalizika kwa mtafaruku wa viongozi wa juu wa klabu ya Yanga, Mwenyekiti Lloyd Nchunga na Makamu wake Davis Mosha hali bado si shwari. Hali hiyo ilijitokeza jijini Dar es Salaam jana, wakati viongozi hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti.
Kwanza alianza Mosha ambaye alipohojiwa kuhusu mgogoro huo, alisema yuko Yanga kwa muda mrefu kwa ajili ya kutetea maslahi ya klabu hiyo na wanachama wake na si kwa maslahi ya mtu binafsi.
Mosha alikiri kujiengua kwenye uongozi wa klabu hiyo kwa muda, ila kwa sasa amerejea tena baada ya kukaa na kuzungumza na viongozi wenzake wa klabu hiyo.
Mosha aliongeza kuwa pamoja na kuumaliza mgogoro huo bado hatambui kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika hivi karibuni, kwa sababu hakikukidhi matakwa yanayotakiwa.
Alisema kuwa awali mdhamini ambaye ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, alikuwa na mapendekezo yake kwenye uongozi wa klabu hiyo, ambapo kamati hiyo ilikaa na kujadili mapendekezo hayo na kumwandikia barua mdhamini huyo, jambo ambalo ni kinyume.
Hata hivyo Moshi alisema, kwa upande wake hana matatizo tena na mwenyekiti wake wala kiongozi yeyote katika klabu hiyo, hivyo yuko tayari kuungana nao ili kufanyakazi kwa ajili ya kuiletea maendeleo klabu hiyo.
“Ni kweli nilijiweka pembeni na klabu ya Yanga, lakini mwenyekiti wangu aliniita tulikaa tukayazungumza hivi sasa yamekwisha, nimeona nizungumze tu kwa kuwa mmeniuliza,” alisema Mosha.
Kwa upande wake, Nchunga alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na kuwa ili klabu iende kwenye maendeleo zaidi inatakiwa wamalize migogoro iliyopo, hivyo walikaa na kuzungumza ili kuwatendea haki wana Yanga.
Alisema kuwa matatizo yaliyotokea ni upepo mbaya tu uliopita, hivyo yamekwisha na makamu wake anastahili kufanya kazi zake kama zilivyoainishwa kwenye katiba ambapo alisisitiza kuwa anastahili kufanya kazi za mwenyekiti kama hayupo.
Katika hatua nyingine, Mosha aliwakabidhi vyeti makocha 20 waliohudhuria mafunzo ya muda mfupi ya ngazi ya cheti yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Makocha hao wapya ni Salvatory Edward, Edibily Lunyamila, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Willy Mtendamema, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Edgar Chibura, James Manyika, Anthony Chibasa, Said Msasu, Henry Legenga na Hemed Mangwenya.
Wengine ni Burhani Hemed, Chomba Athumani, Oscar Milambo, Jeremiah Ponela, Tangale Tangale, Jagua Kabadika, Salamata Mohamed, Oscar Milambo, Jeremiah Ponela na Daniel Magiro.



h.sep3.gif
 
IOC kumchunguza Hayatou


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KAMATI ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), imesema kuwa inajipanga kuendesha uchunguzi dhidi ya madai ya rushwa yanayomkabili Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Issa Hayatou. Madai ya Hayatou kuhusishwa na rushwa yametolewa na kituo cha utangazaji cha Uingereza (BBC) na sasa IOC imesema inahitadi kutoka kituo hicho ili kumchunguza Hayatou na wajumbe wengine wa IOC.
BBC kupitia kipindi hicho cha Panorama imedai kuwa Hayatou na wajumbe wengine wawili kutoka FIFA walipokea mlungula katika miaka ya 1990 kwa ajili ya kuuza kura zao kwa nchi zilizokuwa zikiwania uenyeji.
IOC imebainisha kuwa italifuatilia suala hili kwa umakini ili kuona kama kuna ukweli wowote na kama itabainika kuwa kuna udanganyifu watawachukulia hatua wahusika.
Taarifa hizo za rushwa zilirushwa hewani na BBC Panorama, Jumatatu wiki hii ikiwataja Hayatou, Nicolas Leoz na Ricardo Teixeira kuwa walichukua mlungula ili kuuza kura zao.
Tayari FIFA imewaadhibu kutopiga kura wajumbe wake wawili kuchagua nchi zitakazoandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022; imewatoza fedha na kuwasimamisha kwa muda.
England inachuana na Urusi, Hispania kwa kushirikiana na Ureno na Uholanzi kwa kushirikiana na Ubelgiji kuomba uenyeji wa 2018.
 
Wushu kuwapongeza waliofanya vema


na Samia Mussa


amka2.gif
CHAMA cha mchezo wa Wushu Tanzania (TWA), kimeandaa tamasha maalumu la kuwapongeza wachezaji walioiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali yaliyofanyika nje ya nchi. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TWA, Mwalami Mitete, alisema tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na Mbagala Tai Shaolin Kung Fu Club, litafanyika Desemba 5 kwenye ukumbi wa Equator Grill, uliopo Mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8:00 mchana.
Mitete alisema, tamasha hilo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa mchezo huo, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.
Aliwataja wachezaji watakaopongezwa katika tamasha hilo kuwa ni Ramadhan Mshana na Zacharia Zora 'Mr Zora', ambao Oktoba mwaka huu, walishiriki mashindano ya Wushu ya Dunia nchini China na kupata medali saba pamoja na tuzo ya ushiriki wa mashindano hayo.
Wengine ni Abdallah Athumani na Uswege Mwaseba ambao walikwenda Libya katika mashindano ya Wushu ya Afrika na kufanikiwa kupata medali moja ya shaba.
Mitete aliwataja wachezaji wengine kuwa ni Said Upinde, Abdallah Mneka na Abdallah Mhina ambao walikwenda Nairobi, Kenya kushiriki tamasha la wiki ya utamaduni na kufanya vizuri.
"Kuna vijana sita ambao walikwenda China kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kupewa mafunzo ya sarakasi kuanzia Novemba 6, 2009 hadi Novemba 20 mwaka huu," alisema Mitete.
Mitete aliwataja vijana hao kuwa ni Omari Upinde na Ramadhan Maneno kutoka TWA, Selemani na Zaidini kutoka Kikundi cha Mama Afrika, Mlingo na Neema kutoka Bagamoyo Sanaa Group ambao wote wataonyesha uwezo wa sanaa hiyo katika tamasha hilo.
 
Kili Stars yafufua matumaini robo fainali


na Makuburi Ally


amka2.gif
WENYEJI wa michuano ya Tusker Challenge Cup 2010, timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' jana ilifufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuishushia kipigo cha mabao 3-0 Somalia katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mechi hiyo ambayo mashabiki walijitokeza lukuki na kuishangilia kwa nguvu timu yao, Kili Stars, ilianza mahesabu dakika ya 42 kwa penalti iliyopigwa na Henry Joseph baada ya beki Mohamed kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Baada ya bao hilo Stars waliendelea kulisakama lango la Somalia kwa washambulia Salum Machaku na Mrisho Ngassa kulisakama lango la wapinzani wao mara kwa mara.
Bao hilo lilidumu hadi mwamuzi wa mchezo huo Bamlak Salomon wa Ethiopia anapuliza filimbi ya mapumziko Stars walitoka uwanjani wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Stars waliendelea kulisakama lango la Somalia katika dakika ya 52, Thomas Ulimwengu alikosa bao la wazi baada ya kazi nzuri ya Mrisho Ngassa sambamba na dakika ya 66, John Bocco alikosa bao la wazi baada ya kupiga kichwa kilichopaa juu ya lango la Somalia.
Stars walifunga bao la pili katika dakika ya 76 lililofungwa na Bocco baada ya kipa wa Somalia Khalid Ali kubabatizana na mfungaji.
Katika dakika ya 89 Nurdin Bakari alifunga bao la tatu kwa kichwa baada ya kazi nzuri ya Mrisho Ngassa.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Somalia Yousuf Adam, alisema kukosekana kwa ligi nchini mwao na kuchelewa kuwasili katika mashindano imekuwa ni sababu iliyosababisha kupoteza michezo miwili ya mashindano hayo.
Naye kocha wa Stars, Jan Poulsen, alisema safu ya ushambuliaji awali haikuwa katika hali nzuri lakini alipofanya mabadiliko timu yake ikapata mabao 3.
Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Shadrack Nsajigwa, Idrissa Rajab, Henry Joseph, Shaban Nditi, Mrisho Ngassa, Mohamed Banka/Jabir Aziz na Thomas Ulimwengu/John Bocco na Salum Machaku/Nurdin Bakari.
Katika mchezo mwingine wa kundi A, Burundi na Zambia zilitoka sare ya bila kufungana hivyo kuzifanya zote kufikisha pointi nne huku Stars kwa ushindi wa jana ikiwa na pointi tatu, hivyo
 
Yanga yawasajili Mwape, beki JKT Ruvu Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:39 0diggsdigg

papic.jpg
Clara Alphonce
UONGOZI wa Yanga umefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zambia, Davies Mwape na kupata hati yake ya uhamisho wa kimataifa (ITC) usiku wa kuamkia juzi ili kuwahi dirisha la usajili.

Mbali na mchezaji huyo , Yanga pia imemsajili Salum Seif kutoka JKT Ruvu ili kuongezwa uhai katika kikosi
hicho cha Yanga.

Awali, mchezaji huyo ambaye alikuja mchini mwishoni mwa mwezi uliopita kwa ajili ya kufanya mazungumzo na klabu hiyo alikuwa hatarini kukosa ITC, ambayo hata hivyo iliwasili klabuni hapo usiku wa juzi.

Habari za uhakika ambazo Mwananchi ilizipata jana kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu ya Yanga aliyefanikisha usajili huo zilieleza kuwa mchezaji huyo alichelewa kusajiliwa kutokana na migogoro iliyokuwepo kati ya viongozi wa klabu hiyo, ambao hata hivyo ilimalizika juzi.
Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya wachezaji chaguo la kocha Kostadin Papic ambaye ndiye aliyefanikisha kutua kwake Yanga baada ya kuwataka uongozi wamsajili wakati yeye akiwa Serbia kwa mapumziko.

Mwape, ambaye alikuwa akiichezea Konkola Blades inayoshiriki ligi kuu ya huko amesajiliwa ili kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kwenye mechi za ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Aidha, inaelezwa kuwa kitu kilichochelewesha usajili huo ni utata wa timu gani ambayo alikuwa akiichezea kwa kuwa Yanga walipata barua tatu tofauti, zote zikieleza kila timukwamba alikuwa mchezaji wao.

Hata hivyo, mpaka juzi dirisha dogo la usajili linafungwa, Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa lilishindwa kwa mara nyingine kutoa kibali cha kumruhusu Kenneth Asamoah kuichezeaYanga.
 
Zanzibar Heroes yatiwa kifungoni Chalenji Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:35 0diggsdigg

Jessca Nangawe

KASI iliyoanza nayo Zanzibar Heroes katika michuano ya Chalenji imepunguzwa jana na Ivory Coast katika mchezo wa Kundi B baada ya kulazwa kwa bao 1-0.

Bao hilo la dakika ya 61 la Kipre Bolou aliyetokea benchi kipindi cha pili liliwazima Zanzibar na mashabiki wao wengi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuzidi kulifanya kundi hilo kuwa gumu baada ya mechi ya awali ya Sudan na Rwanda kumalizika kwa suluhu 0-0.

Kwa matokeo hayo, Rwanda inaongoza ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Zanzibar Heroes na Ivory Coast zenye pointi tatu kila moja na Sudan ikishika mkia kwa pointi moja.

Kikosi hicho cha Ivory Coast, timu mwalikwa ambacho kinaundwa na wachezaji wengi wasio na majina na wanaocheza ligi za nyumbani kilionyesha mchezo wa kasi, kumiliki mpira na kuwapeleka puta mabeki wa Zanzibar, wakiongozwa na Nadir Haroub na Aggrey Morris, ambao pia huichezea Taifa Stars.

Hata hivyo, mbinu za kocha Mwingereza Stewart Hall kumtumia zaidi mshambuliajiAlly Ahmed Shiboli pekee, aliyeng'ara katika mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan alipofunga mabao yote mawili, kuliinyima timu yake nafasi za kulitia msukosuko lango la wapinzani wao kwa kipindi kirefu.

Katika mojawapo ya mashambulizi mengi, Ivory Coast walikosa bao kupitia kwake, Diou Sed ambaye alipiga shuti kali na mpira wake kugonga mwamba.

Kocha Stewart aliwasifu wachezaji, lakini akaeleza kuwa walikosa umakini ikilinganishwa na mchezo dhidi ya Sudan ambao walishinda 2-0.

Alisema macho yao yanaelekezwa kwenye mchezo dhidi ya Rwanda kukamilisha michuano hiyo, Kundi B.

Mwenzake wa Ivory Coast, Koudio Georges aliwasifu wachezaji wake kwa mchezo mzuri ambao umewarejesha katika michuano hiyo.

Katika mchezo huo, vikosi vilipangwa:-

Zanzibar Heroes:

Mwadini Ali Mwadini, Ismail Khamis, Waziri Salum,Suleiman Kassim, Amour Kombo/Khamis Mcha, AliAhmed/ Abdi Kassim, Nadir Haroub, Abdulghan Gulam/Maulid Ibrahim, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud,Sabri Ramadhan,

Ivory Coast:
Sangara Dadra Ali, Goua Mahan Marc,Wawa Serge Pascal, Kouame Desire Magloire, Kouadio Konan Serge/Guy Herve, N'goran Kouasi Nicaise, Coulibaly Tiecoura, Kone Zoumana, Kipre Tcheche, Kouame Koffi Christian/Kipre Bolou, Diou Sed Marc/Bile Georges
 
Banka, Ulimwengu waongoza kwa kukosa mabao Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:33 0diggsdigg

Sweetbert Lukonge
LICHA ya timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Somalia, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mohamed Banka ndiye aliyeongoza kwa kukosa nafasi nyingi za kupachika mabao katika mchezo huo.

Katika mchezo huo, Banka ambaye alicheza kwa dakika alikosa nafasi nane akifuatiwa na chipukizi Thomas Ulimwengu ambaye alikosa nafasi nne.

Kutokana na takwimu ambazo zilichukuliwa na mwandishi wa Mwananchi wakati wa mchezo huo, hali hiyo ilionyesha kuwa washambuliaji hao wa Kili Stars wangekuwa makini na kuzitumia nafasi hizo, timu yao ingeibuka na ushindi mnono.

Pia, hiyo ni changamoto ambayo kocha Jan Poulsen na benchi lake la ufundi wanatakiwa kukabiliana nayo kabla ya Kili Stars kuivaa Intamba ya Burundi, Jumamosi.

Katika kipindi cha kwanza, Banka alipata nafasi tano ambazo alitengenezwa na Mrisho Ngassa pamoja na Henry Joseph, lakini mchezaji huyo alishindwa kuzitumia, jambo ambalo lisababisha baadhi ya mashabiki kuanza kupiga kelele wakitaka atolewe.

Hali hiyo pia iliendelea katika kipindi cha pili kwa kiungo huyo mshambuliaji wa klabu ya Simba alikosa nafasi nyingine tatu na kabla ya kocha Poulsen kufanyia mabadiliko na nafasi yake ikachukuliwa na Nurdin Bakari ambaye aliipatia Kilimanjaro Star bao la tatu.

Katika hatua nyingine, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tanga amewataka wachezaji hao kuhakikisha wanapigana kwa nguvu zo zote katika mchezo wao mwisho dhidi ya Burundi ili kuhakikisha wanasonga mbele katika mashindano hayo.
"Hivi karibuni kabla ya mechi ya jana (juzi) tulikutana na wachezaji na tumewataka kuhakikisha wanajituma zaidi uwanjani na nikawataka wasiwe bubu bali wakumbushane majukumu yao wanapokuwa uwanjani," alisema Tenga.

Kilimanjaro Stars inatakiwa kushinda mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi dhidi ya Burundi ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo.

Katika kundi hilo, Burundi inaongoza ikiwa na pointi nne sawa na Zambia, zikitofautina kwa mabao ya kufunga, zinafuatiwa na Kirimajaro Stars yenye pointi tatu
 
Mashabiki: Kili Stars hamjatupa raha Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:32 0diggsdigg

Calvin Kiwia
LICHA ya kuifunga timu ya taifa ya Somalia kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wake wa pili uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi michuano ya Tusker Chalenji, wadau wa soka nchini wamekiponda kiwango kilichooyeshwa na wachezaji wa Kilimanjaro Stars.

Wakizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam wadau hao walisema kuwa kama wachezaji wa timu hiyo wasipofanya mabadiliko ya uchezaji wao uwanjani kwa kumtegemea Mrisho Ngassa pekee haitafika mbali kwenye michuano hii ya Tusker Chalenji pamoja na kuwa mwenyeji.

"Tumekuwa tukimtegemea Ngassa peke yake na hili ni tatizo kubwa kwa mchezo wa soka kumtegemea mchezaji mmoja kupata ushindi... je ikitokea siku hayupo ina maana timu haitaweza kushinda ni tatizo kubwa kwa kweli," walisema kwa masikitiko.

"Kwa kweli tuna tatizo kubwa kwenye timu yetu hasa nafasi ya ufungaji na ulinzi bado kunahitajika marekebisho ya hali ya juu kama tunataka kufika mbali kwenye mashinadno haya," walisisitiza.

Walisema wao hawawezi kumtupia lawana kocha Poulsen kwa uteuzi wake wa wachezaji wa timu hiyo ila lawama zao wanazitupa kwa wachezaji kushindwa kuonyesha kiwango cha kuridhisha kwenye michuano hiyo licha ya kuwa wenyeji.

Waliongeza kuwa wanawaomba wachezaji wa Kilimanjaro Stars kujituma kikamilifu wawapo uwanjani ili kupata matokeo mazuri na kuwapa raha mashabiki wao na kulibakisha kombe hilo nchini Tanzania.
 
Spector aiangamiza Man United Kombe la Ligi Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:30 0diggsdigg

LONDON, Uingereza

BEKI wa zamani wa Manchester United, Jonathan Spector juzi aligeuka adui namba moja wa klabu hiyo baada ya kuiongoza West Ham kuichapa timu hiyo mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la Ligi.

Spector, raia wa Marekani alitibua sherehe za ushindi wa Jumamosi wa mabao 7-1 ilioupata Man United dhidi ya Blackburn katika mchezo wa Ligi Kuu.
Beki huyo alimthibitishia kocha Alex Ferguson kwamba alifanya makoza kumwacha miaka minne iliyopita kwa kufunga mabao mawili kati ya hayo manne.

Kwa kipigo hicho, Man United imevuliwa taji hilo ambalo ilikuwa ikishikilia tangu mwaka jana.

Mabao mengine yaliongezwa na Carlton Cole kwenye mchezo huo ulifanyika Uwanja wa Upton Park.

Akionekana kuduwaa, Ferguson, ambaye alivaa kofia nyekundu ya manyoya alikiri : "Sikutegemea kitu kama hiki kwa hakika.

"Mabao haya yalikuwa laini mno. Hatustahili kutoa zawadi ya mabao kirahisi namna hii.

Kulikuwa na wachezaj chipukizi na pengine hilo ni somo tosha kwa kila mmoja wetu.

"Lakini, tusisahau ulikuwa mchezo wa robo fainali na tulikuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele na kutwaa taji hilo kwa mara ya pili."

Vinara hao wa Ligi Kuu walishuhudia ubabe wao wa mechi 29 bila kufungwa ukimalizikia kwa West Ham inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi.

Akicheza mchezo wake wa pili msimu huu, Spector alicheza kama kiungo, uamuzi ambao kocha Avram Grant aliutetea kuwa umekuwa wenye mafanikio.

Aliweza kuwatungua Man United mara mbili, kipindi cha kwanza kabla ya Cole kuongeza mengine mawili.

Baada ya mchezo huo Grant alikiri : "Ni matokeo ya kushangaza kila mtu.

"Kucheza vizuri na kuishinda timu kubwa, tena kwa idadi kubwa ya mabao, ni jambo la kujivunia, siwezi kuamini nilichokiona, sijui kama kinaweza kutokea tena .

Ni usiku wa kipekee . Nilikuwa na matumaini ya ushindi, lakini si kwa kiasi hiki."

Spector, ambaye hajawahi kufunga bao katika mechi 128, alisema: "Sina hakika kwanini sikuwahi kufunga huko nyuma.

"Kucheza katika nafasi tofauti na niliyoizoea kumesaidia, nilipata nafasi ya kwenda mbele zaidi.

"Bao la kwanza lilikuwa zuri, limecangiwa na mchezo safi wa Victor Obinna na lile la pili, pia limetoka kwa Victor, hakika amecheza vizuri, ni bahati mbaya hakufunga mwenyewe.

"Tuliamua kukaza msuli na kucheza kwa nguvu tangu mwanzo wa mchezo. Tulidharauliwa, lakini tulifahamu kwamba umoja wetu ungeweza kutupa mafanikio zaidi na hilo ndilo limetokea.

"Msimu huu kwetu umekuwa wenye kukatisha tamaa, lakini wote tumeonyesha kuwa tunaweza."

Cole, ambaye amefunga baa baada ya mechi 18 za ukame, aliongeza : "Ni matokeo mazuri. Nimefunga mabao matatu msimu huu, nina matumaini ya kuongeza mengine mechi zijazo. Ninategemea kiwango changu kitaimarika."
 
Man City, Atletico zakaribia kuingia 32 bora Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:26 0diggsdigg

PARIS, Ufaransa

KLABU za Manchester City na mabingwa watetezi wa michuano ya Europa League, Atletico Madrid zimejiweka katika mazingira mazuri ya kuingia 32 bora.

Timu hizo zilikuwa miongoni mwa zile zilizocheza jana, Jumatano, huku timu tano zikiwa zimejihakikishia nafasi hiyo.

Hizo ni pamoja na Zenit St Petersburg, Stuttgart, CSKA Moscow, BATE Borisov na FC Porto.

Timu mbili kutoka kila kundi zitafuzu na kuungana zile zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kucheza hatua hiyo kuanzia Februari na fainali itachezwa Mei 18 mjini Dublin, Ireland kwenye uwanja uliokarabatiwa wa Lansdowne Road.

Miongoni mwa timu kutoka Ligi ya Mabingwa Ulaya zinaweza kuwa, Rangers, Spartak Moscow na FC Twente kutoka Uholanzi.

Man City imejikusanyia pointi saba kutokana na mechi nne, ikiwa ya pili kwa tofauti ya mabao dhidi ya Lech Poznan, kutoka Poland ambayo iliilaza Man City chini ya Roberto Mancini, mabao 3-1 , mchezo wa Kundi A.

Poznan itaikaribisha Juventus, inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne huku Man City ikiikaribisha jana Salzburg kutoka Austria.

Mshambuliaji raia wa Hispania, David Silva alikuwa mwenye matumaini kwamba City itasonga mbele.

"Tunacheza nyumbani , kwa hiyo ni jukumu letu kushinda mechi hiyo . Tunatakiwa kuwa makini, kwani pointi tatu zina umuhimu mkubwa kwetu, zitatukatia tiketi," alisema kupitia mtandao wa klabu hiyo.

Aliongeza : "Lakini, ninaamini tunakwenda vizuri hadi sasa. Kama isingekuwa bahati mbaya ya kushindwa mchezo wetu wa mwisho, tungekuwa tumefuzu na kuongoza kundi letu. Lakini, hatupo mbali, nafasi hiyo ipo mkononi mwetu ."

Mancini amekuwa mwenye matumaini kuwa jeshi lake linaoundwa na wachezaji wa mabilioni litaweka kando matokeo ya 1-1 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na kusaka ushindi.

Alisema jukumu la kila mmoja ni kuishinda Salzburg, kiasi cha kufuzu kucheza hatua ya 32 bora Ulaya.

Man City ilitarajiwa kufuzu ikiwa na mchezo mwingine mmoja mkononi na endapo Lech ingeilaza Juventus mjini Poznan.
Kwenye Kundi B, Atletico wanashika nafasi ya pili kwa tofauti yua pointi moja nyuma ya Bayer Leverkusen.

Leverkusen ambayo pia ilikuwa ikicheza jana ilitarajiwa kufuzu kwa ushindi na pointi tatu dhidi ya Rosenborg ya Norway hukuAtletico ikihitaji kuilaza Aris ya Ugiriki.

Mechi nyingine za jana usiku, Sporting Lisbon v Lille, Kundi C .
Zenit St Petersburg v Hajduk Split, AEK Athens v Anderlecht. Stuttgart v Young Boys , Getafe v Odense. PSV Eindhoven vSampdoria.
 
BFT waomba ushirikiano kutoka kwa Waziri Nchimbi Send to a friend Wednesday, 01 December 2010 21:24 0diggsdigg

Imani Makongoro

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limemtaka Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa na ushirikiano na vyama vya michezo nchini ili kusaidia kuinua michezo kimataifa.

BFT, pia ilimpongeza waziri huyo kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza wizara hiyo pamoja na naibu wake, Dk Fenella Mukangara na kuwataka kuwa bega kwa bega na vyama vya michezo nchini.

Aidha, waliwashauri wawe tayari ksaidia timu za taifa katika mazoezi yao ya kila siku na hatimaye kuziwezesha kufanya vema katika mashindano yao mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Ofisa habari wa BFT, Eckland Mwaffisi alisema kuwa wao BFT wanaamini kuwa, viongozi hao wataleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya michezo hasa kwa kushirikiana na viongozi wa vyama au mashirikisho yanayosimamia michezo mbalimbali nchini.

Alisema kuwa endapo kutakuwa na Ushirikiano huo na viongozi husika, utaweza kubadilisha historia ya Tanzania ya kuwa watalii au wasindikizaji katika michezo mbalimbali kwani changamoto kubwa iliyopo katika vyama husika vya michezo ni maandalizi duni ya wachezaji katika mashindano ya kimataifa.

Mwaffisi alisema mfano mzuri ni mchezo wa ngumi ambao pamoja na hatari zake, kambi ya mazoezi inakabiliwa na ukata mkubwa wa vifaa ambavyo ndivyo umwezesha kocha kutoa mafunzo ya vitendo ili kufahamu uwezo wa kila bondia na upungufu wake.

Alisema kuwa hivi sasa vifaa vyote vinavyotumiwa na mabondia wa taifa vipo katika hali mbaya na havifai kutumiwa katika mazoezi mbali ya mchezo huu,kuiletea sifa kubwa nchi yetu katika mashindano ya kimataifa.

Wakati huo huo, BFT imeandaa kozi ya awali ya ukocha ambayo itashirikisha mabondia wa zamani pamoja na walimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo.


Lengo la kozi hiyo ni kupata walimu wazuri ambao wataibua vipaji vya mabondia ambavyo vimejificha mitaani na shuleni ili viweze kuendelezwa.

Kozi hiyo itafanyika Desemba 14 hadi 24 mwaka huu, jijini Dar es Salaam ambapo mafunzo hayo yatakuwa ya nadharia na vitendo ambapo makocha hao watajengewa uwezo na walimu waliobobea katika fani hiyo.


Gharama ya kozi hiyo kwa kila mshiriki ni Sh 20,000 ambapo lengo la BFT ni kuibua vipaji ambavyo vimejificha mitaani na shuleni ambapo mchezo huu ni hazina kubwa kwa vijana hao kujipatia ajira kupitia michezo.
 
Karibu Nchimbi, Mukangara, mna kazi kubwa Send to a friend Saturday, 27 November 2010 10:31 0diggsdigg

dk.%20emmanuel%20nchimbi.jpg
WIKI hii, Rais Jakaya Kikwete amewateua Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Fenella Mukangara kusimamia Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana.Kwa uteuzi huo, ni mengi yamesemwa, lakini sisi tunachukua nafasi hii kuwakaribisha madaktari hao wa falsafa katika uongozi wa wizara hii, ambayo sisi ni washirika.

Tunaamini kuwa wawili hao ambao leo wataapishwa rasmi watakuwa wamekabidhiwa hadidu rejea pamoja na mwongozo wa kazi zao ambazo wanatakiwa kuzitimiza.

Miongoni mwake ni kutekeleza kwa vitendo sera ya michezo nchini, ambayo hatuna shaka kwamba watakuwa pia wamekabidhiwa.
Pia, tunapenda kuwatadharisha dhidi ya upendeleo au ushabiki katika baadhi ya michezo, ikiwamo soka kama ambavyo imewahi kutokea kwa watangulizi wao.

Tuna imani kuwa Dk Nchimbi na timu yake wizarani hapo mtatambua wajibu wa kuziandaa timu zetu za michezo mbalimbali, ambazo zimekuwa zikishiriki na kutia aibu kimataifa.

Tuliwahi kusema huko nyuma kwamba waziari tunayemtaka si yule wa kuaga timu, kukabidhi bendera ya taifa kwa timu hizo, kumwaga lawama zinapofanya vibaya.

Badala yake, tunamtaka waziri na msaidizi wake ambao wataongoza dira ya michezo katika Tanzania ya leo, wakitambua mchango wa michezo, utamaduni kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Tunarudia kuwakaribisha wizarani hapo, lakini tunasema kuwa mtaweza kuheshimika zaidi kwa kuubadili mwenendo wa uendeshaji wa michezo, habari na utamaduni na kuwasaidia vijana walio wengi nchini.
 
Chaneta, Chaneza wanaangamiza mipira wa pete Send to a friend Sunday, 28 November 2010 19:51 0diggsdigg

Jessca Nangawe
MOJA ya tatizo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya michezo hapa nchini ni suala zima la migogoro inayoota mizizi ndani vyama husika hadi kupelekea kupoteza mwelekeo na mwisho wa siku mchezo husika kufa au kukosa mwelekeo.
Licha ya kuwa ni jambo la kawaida kuwepo kwa migogoro ndani ya chama ama klabu hapa Tanzania jambo geni, lakini endapo inazidi na kuota mizizi ina athari kubwa sana kwa mchezo husika.

Tumeshudia migogoro mikubwa ikizuka katika klabu za Yanga na Simba, vyama vya michezo kama riadha, ngumi, soka na netibali kutokana na matatizo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya michezo hapa nchini.

Nimesukumwa kusema ivyo kutokana na kuwepo kwa mgogoro ambao kwa sasa unaelekea kuota mizizi baina ya Chama cha mchezo wa Netiboli Tanzania (Chaneta) na wenzao wa visiwani (Chaneza) ambapo kila kukicha tatizo hilo halipatiwi ufumbuzi.

Ni muda mrefu sasa tangu mabaraza ya michezo BMT na BMTZ kuvitaka vyama hivi kuondoa tofauti zao na kujumuika pamoja katika shughuli mbalimbali za kimichezo ikiwemo kushirikiana katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Vyama hivi vimeonekana kuziba masikio kwani licha ya Wizara ya michezo kuinglia kati lakini mpasa sasa hakuna dalili wala kuwepo kwa upatano miongoni mwa vyama hivi.

Kikubwa ambacho vyama hivi vimeonekana kutofautiana ni kuhusiana na utendaji kazi miongoni mwa viongozi ambao mpaka nazungumza hakuna maelewano mazuri hali iliyopelekea hata wenzetu wa visiwani kususia kuleta timu kushiriki mashindano ya kimataifa yaliyomalizika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Hali hii kwa kiasi kikubwa imepelekea kuwepo kwa mgawanyiko ambao haufahamiki hatma yake nini kutokana na kila siku viongozi hawa kupiga kalenda ya kukutana na kuonekana kuwepo kwa kiini macho katika jambo hili.

Viongozi wa vyama hivi wanapaswa kufahamu umuhimu na heshima ambayo wamepewa na Rais Jakaya Kikwete kwa kuwaleta kocha kutoka nje kwa ajili ya kuinua mchezo huo hapa nchini.

Baada ya kuletwa kwa kocha huyo ambae alikuja kwa maslahi ya wote (bara na visiwani) Wizara ya michezo ilisisitizwa atumiwe kwa wote kwani agizo la Rais ni kutaka kuona maendeleo ya mchezo huo yakipatikana kwa wote na kumtumia kocha huyo kufundisha timu ya Taifa kwa ujumla kama ilivyo kwa timu ya Taifa ya wanaume 'Taifa Stars'.

Kikubwa ambacho vyama hivi wanapaswa kuliangalia kwa kina ni jinsi ambayo wamepewa heshima na kutekelezewa ahadi yao lakini sasa kushindwa kuwa na shukrani na matokeo yake kuzidi kupandikiza mizizi ya migogoro badala ya kuiondoa.

Pili viongozi hawa wanapaswa kufahamu mchezo huu umefikia wapi na unahitaji kupewa msukumo zaidi ili uweze kukua na kupanuka zaidi kama ilivyo kwa michezo mingine.

Sitapenda kuingilia majukumu ya viongozi hawa, lakini inawapasa kuheshimu kauli ya viongozi wao wa juu na kufanya kama walivyoagizwa kwa maslahi ya mchezo huu na Taifa kwa ujumla.

Nilijaribu kuzungumza na viongozi wa Zanzibar ambao wao walikua tayari kufikia muafaka endepo Chaneta watahitaji kukaa nao, lakini wakadai mpaka sasa hakuna taarifa yoyote waliyoipata kuhusu kukutana huko hivyo wameomba wasilaumiwe kwa kitu chochote kwani wao wanaheshimu katiba na taratibu za nchi.

Kitu kikubwa ambacho kinaonekana kuwepo kati ya vyama hivi ni ushindani usiokua na maana yoyote na hivyo kupelekea mgogoro huzidi kushika kasi bila kuwepo hitimisho lake.

Kama nilivyotangulia kusema migogro kama hii hujitokeza katika michezo yote lakini imekua ikitafutiwa ufumbuzi na kumalizika,hivyo ni muda na changamoto sasa kwa vyama hivyo kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha wanapata suluhu la mgogoro wao mapema na kulimaliza.

Mfano mzuri ni mgogoro ambao ulitokea kati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF na wenzao ZFA ambao mwisho wa siku walifikia muafaka na kumaliza tofauti zao na mpaka sasa wamekua wakishirikiana katika maswala mbalimbali ya soka.

Nasema hivyo ili kutoa changamoto na msukumo wa vyama hivi kuweza kuiga wenzao kwa kubadilika na kuachana na dhana potofu za kulumbana katika zama hizi za ukweli na uwazi.

Chaneta na Chaneza wakae na kumaliza tofauti zao kabla tatizo hili halijawa kubwa zaidi na kuleta mpasuko ambao mwisho wake ni kuua kabisa maendeleo ya mpira wa pete hapa nchini.

Najua kwamba migogoro hii ya vyama vya michezo ni moja ya matatizo ya muungano hakuna shaka kwamba rais Kikwete na Dk Ally Sheini wataishiwishi wizara inayoshughulikia mambo ya muungano kulijumuisha na hili la michezo ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

Naamini migogoro hii ikitatuliwa kwa haraka na vyama hivi vikiweka nguvu zao nyingi kwenye kutafuta mbinu za kuendeleza michezo basi hakuna shaka na sisi siku moja tutafika mbali zaidi kwenye nyanja hii.

Mungu ibariki Tanzania, Ibariki Afrika.
 
Harambee Stars yaaga Chalenji


*Yachapwa na Ethiopia 2-1
Na Elizabeth Mayemba

TIMU ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' imeondolewa katika michuano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ethiopia jana, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Hii ni mechi ya pili kwa
Kenya kufungwa, ambapo mechi ya kwanza walifungwa na Malawi mabao 3-2, hivyo wamebakiwa na mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Uganda kesho.

Mpira huo ulianza kwa Kenya kufanya mashambulizi, ambapo sekunde ya 38, Bob Mugalia alikosa bao la wazi baada ya kuupiga mpira nje akiwa amebaki na kipa wa Jemel Bushera.

Ethiopia walipata bao la kwanza dakika ya 25, baada ya Shemeles Bekele Godo kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni.

Bao hilo liliwaongezea nguvu Ethiopia na kulishambulia zaidi lango la Kenya, dakika ya 45, Godo aliyekuwa mwiba kwa wapinzani wao, aliifungia timu yake bao la pili.
Kipindi cha pili kila timu ilikianza kwa kasi huku kila moja ikitafuta mabao, lakini Kenya ndiyo waliokuwa na kazi wakisaka mabao ya kusawazisha.Kenya itabidi wajilaumu kwani mara kwa mara wachezaji wake walikuwa wakifika langoni mwa Ethiopia, lakini walishindwa kuukwamisha mpira wavuni.

Dakika 15 za mwisho, Kenya walionekana kuutawala mchezo, ambapo dakika ya 84, walifanikiwa kupata bao lililofungwa na Fred Ajwang.Kwa matokeo hayo, Kenya wanasubiri mechi ya mwisho kukamilisha ratiba wakiungana na Sudan.Katika mechi iliyochezwa mchana, timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', imetoka sare ya bao 1-1 na Malawi.

Malawi ndio walioanza kupata bao dakika ya pili, baada ya nahodha wa Uganda, Andrew Mwesingwa kujifunga bao akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa hatari langoni kwao.

Uganda walisawazisha bao hilo dakika ya 80, kupitia kwa Emmanuel OKwi.Leo, kutakuwa na mechi kati ya Somalia na Zambia, ambayo itachezwa saa nane mchana, na kufuatiwa na mechi kati ya Zanzibar na Rwanda.Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza siku kwa mashabiki wa soka nchini kuingia bure uwanjani, badala ya ofa hiyo kumalizika kesho, sasa itamalizika Jumapili.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga, alisema wameamua kufanya hivyo ili kuongeza hamasa katika michuano hiyo, hivyo kuanzia Jumatatu mashabiki wataanza kulipa kiingilio, ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa sh.2,000 na cha juu sh.10,000.
 
'Shibori alicheza chini ya kiwango'


Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', John Stewart, amesema aliamua kumtoa mshambuliaji wake, Ali Ahmad Shibori kutokana na kucheza chini ya kiwango.Mchezaji huyo amejizolea umaarufu hivi kiribuni kutokana na kuonesha kiwango kizuri katika
mchezo kati ya Dar All Stars na Zanzibar Heroes na hata zilipokutana Sudan na Zanzibar Heroes, alitamba kwa kuifungia mabao mawili timu yake.

Kabla ya kukutana na Sudan, klabu ya Simba kutokana na kiwango alichokionesha dhidi ya Dar All Stars, ilifanya naye mazungumzo na kumsajili kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Ivory Coast, ambapo timu yake ililala bao 1-0, Stewart alisema walikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo, lakini bahati haikuwa yao.

"Tulicheza vizuri takribani dakika 60, lakini baada ya kufungwa bao, presha ikahamia kwetu na kujikuta tunahitaji zaidi kushinda wakati tulikuwa tumeshachelewa," alisema.

Akimzungumzia mchezaji Amour Kombo ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki na kuamua kumtoa na kumwingiza Hamis Mcha, alisema ni mchezaji mzuri mwenye uzoefu, lakini alicheza kwa hofu.

Alisema alishindwa kumwingiza mapema Mcha, licha ya kuwa ni mchezaji mzuri kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mashindano kama hayo, lakini anaamini atafanya vizuri zaidi.Zanzibar Heroes itajitupa tena uwanjani leo kwa kuumana na Rwanda ikitanguliwa na mchezo kati ya Somalia na Zambia.
 
Makocha walia uhaba wa viwanja vya mazoezi Thursday, 02 December 2010 20:48

Sweetbert Lukonge

WAKATI michuano ya Tusker Chalenji ikizidi kushika kasi jijini Dar es Salaam, baadhi ya makocha wa timu zianazoshiriki michuano hiyo wameponda utaratibu wa kutumia kiwanja kimoja kwa ajili ya mazoezi na kudai kuwa hali hiyo inawanyia uhuru wa kufanya kazi yao.

Kalibia timu zote zinazoshiriki michuano hiyo zimekuwa zikitumia Uwanja wa Karume kwa mazoezi jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine limekuwa likisabaisha baadhi ya timu kushindwa kutekereza mikakati yake.

Wakizungumza na Mwanachi kwa nyakati tofauti makocha hao wamesema kuwa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambao ndiyo wenyeji wa mashindano wanatakiwa kuhakikisha wanalipatia ufumbuzi suala hilo.

"Ni aibu kubwa kwa timu zote zinazoshiriki mashindano haya kutumia uwanja mmoja kwa ajili ya mazoezi, hali hii kwa hakika ni doa kubwa ambalo linaweza kuondoa maana yote ya mashindano haya ambayo kwa mwaka huu yanaonekana kuwa bora zaidi ukilinganisha na yaliyopita," alisema Nasir Awad kocha wa timu ya taifa ya Sudan.

Naye kocha mkuu wa Rwanda, Sillas Tetteh alisema kuwa hali ya timu tatu kutumia uwanja mmoja kwa mazoezi unawanyima nafasi makocha ya kufanya kazi yao ipasavyo kwa kuofia mbinu zao kugundulika mapema kwa wapinzania wao.

"Kwa hakika sijapendezwa na hali hii, kwa sababu inatunyima uhuru zaidi wa kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yamejitokeza katika michezo yetu iliyotangulia kwa kuofia wapinzani wetu tunaotumia uwanja huo kuzisoma mbini zetu.

"Tunawaomba Cecafa na TFF kuhakikisha wanalipatia ufmbuzi suala hili ili kuhakikisha hadhi na hamasa ya mashindano haya inaendelea na pia kutupa uhuru makocha wa kufanya kazi yetu bilia ya vizuizi." alisema Tetteh.
 
Nyilawila ajitupa ulingoni Czech
Thursday, 02 December 2010 20:07

Iman Makongoro
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Karama Nyilawila leo anashuka ulingoni kuzichapa na Kreshnik Qato katika pambano la kuwania mkanda wa Shirikisho la ngumi la Dunia (WBF) la uzani wa kati litakalofanyika nchini Czech.

Nyilawila aliondoka nchini Desemba Mosi tayari kwa pambano hilo litakalokuwa la raundi 12.

Akizungumza na Mwananchi kabla ya kuondoka jijini Nyilawila alisema kuwa amejiandaa vema kumkabili mpinzani wake na anamatumaini ya kuibuka na ubingwa huo.
"Hii ni nafasi yangu kuonyesha kiwango changu katika kuwania ubingwa wa ngumi za kulipwa wa Dunia kupitia WBF," alisema Nyilawila.

Nyilawila ana rekodi ya kushinda mpambano 12, sita yakiwa kwa Knock Out (KO), alipoteza mapambano saba ambapo matatu alipigwa kwa KO na kutoka sare mawili.

Bondia huyo amepata baraka kutoka Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST) chini ya rais wake, Emmnauel Mlundwa ambaye alisema kuwa wanamtakia ushindi Nyilawila.

"Tumekwisha maliza majukumu yetu kwa bondia huyo, hivyo tunamtaka bondia huyo kupigana vema na kushinda pambano hilo, tunaimani matokeo yake yatakuwa mazuri," alisema Mlundwa.

Bondia huyo alishawahi kupigana na Anton Novikov wa Russia pambano lililofanyika katika kituo cha michezo cha Palace "Znamya", Noginsk, Russia, pambano lililokuwa la uzani wa kati kwa vijana la chama cha WBC.

Pambano hilo liliandaliwa na promota wa ngumi za kulipwa nchini humo Ulf Steinforth (Sport Events Steinforth) na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Germany Sport1.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom