Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
- Thread starter
- #101
Udhamini wa gofu kuboreshwa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 4th December 2010 @ 20:00 Imesomwa na watu: 30
KAMPUNI ya Zantel imepanga kuimarisha udhamini wake kwenye michuano ya gofu ya kila mwezi ‘Monthly Mug' inayofanyika kwenye Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.
Nahodha wa gofu klabuni hapo, Joseph Tango alisema hayo jijini Desemba 3 na kuhamasisha wachezaji zaidi kujitokeza.
Tango alisema Zantel ambao kwa mara ya kwanza wamedhamini michuano ya Mug ya Novemba wameahidi kuendelea kuboresha zaidi udhamini wao na washindi kuondoka na zawadi nono.
"Napenda kuwahamasisha wachezaji kujitokeza kwa wingi kwenye michuano ya mwezi Desemba ili kuongeza msisimko.
"Tunashukuru kwamba hata wadhamini wetu Zantel wameahidi kuboresha zawadi, hivyo ni vema kuwaunga mkono," alisema.
Tango alisema mashindano ya Mug mwezi huu yamepangwa kufanyika Desemba 18 kwenye viwanja hivyo.
Katika mashindano yaliyopita Tango mwenyewe alikuwa mmoja wa washindi na kuondoka na simu aina ya Blackberry.
Mbali na Tango washindi wengine kama chipukizi Vailet Peter pia waliondoka na simu akiwa bingwa kwa upande wa wanawake kwenye mashindano hayo ya siku moja yanayoshirikisha wanaume na wanawake.
Mashindano hayo ya Desemba pia yatakuwa yanafunga msimu wa Mug mwaka 2010.