OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
Mgomo wayeyuka
wakati mgomo huo ukifanikiwa Muhimbili, huduma katika hospitali nyingine kubwa nchini zikiwamo Temeke, Ilala, Mwananyamala na Hospitali za mikoa ya Tanga, Dodoma, Iringa, Shinyanga, Arusha, Mara na Kilimanjaro ziliendelea kama kawaida.
Madaktari katika Hospitali za Mount Meru, Bugando, Bombo, Hospitali Teule ya Muheza, Korogwe na Bunda waliendelea na kazi. Madaktari katika Hospitali za Magunga na Bombo mkoani Tanga walisema wanasubiri kwa hamu maagizo kutoka kwa viongozi wao ili nao wagome kuishinikiza Serikali ili isikilize kero zao.
Katibu Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda, Billy Kinyaha alisema hakuna mgomo wowote kauli iliyothibitishwa pia na baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Samson Winani alisema hakuna mgomo wowote uliofanyika: "Sisi huku hatujagoma. Wanaogoma ni wa huko Dar es Salaam."
Katika Hospitali ya Mount Meru, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha, Dk Omar Chande amesema madaktari wote jana walikuwa wakichapa kazi. Hata hivyo, hakuna daktari aliyekuwa tayari kueleza ni kwa nini hawakutekeleza maagizo ya kugoma kuanzia jana.
SOURCE: Mwananchi