Mgomo wa madaktari kama walimu

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Mgomo wayeyuka

wakati mgomo huo ukifanikiwa Muhimbili, huduma katika hospitali nyingine kubwa nchini zikiwamo Temeke, Ilala, Mwananyamala na Hospitali za mikoa ya Tanga, Dodoma, Iringa, Shinyanga, Arusha, Mara na Kilimanjaro ziliendelea kama kawaida.

Madaktari katika Hospitali za Mount Meru, Bugando, Bombo, Hospitali Teule ya Muheza, Korogwe na Bunda waliendelea na kazi. Madaktari katika Hospitali za Magunga na Bombo mkoani Tanga walisema wanasubiri kwa hamu maagizo kutoka kwa viongozi wao ili nao wagome kuishinikiza Serikali ili isikilize kero zao.

Katibu Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda, Billy Kinyaha alisema hakuna mgomo wowote kauli iliyothibitishwa pia na baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Samson Winani alisema hakuna mgomo wowote uliofanyika: "Sisi huku hatujagoma. Wanaogoma ni wa huko Dar es Salaam."

Katika Hospitali ya Mount Meru, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha, Dk Omar Chande amesema madaktari wote jana walikuwa wakichapa kazi. Hata hivyo, hakuna daktari aliyekuwa tayari kueleza ni kwa nini hawakutekeleza maagizo ya kugoma kuanzia jana.

SOURCE: Mwananchi

Hata mbeya,jana kwenye taarifa ya habari mganga mkuu alisema hawana mgomo,wanachapa kazi kama kawaida,hadi wanaboa!bila umoja watakuwa wanaishia kulalamika kwenye vikao vyao tu.
 
Misscommunication, umasikini wa akili uliokithiri, woga, kukata tamaa, ubinadamu wa mshumaa au ni nini? Kama ni kweli am dissapointed.
Mlitaka nini? Manake this time wananchi wako nyuma yenu, mnashindwa au na nyie binafsi, mnafaidi hii hali?
Mi nadhani kuna jinsi individual doctors wanafaidi kuwepo na hali mbaya mahospitalini.
Mfano manunuzi feki, kugawana madawa, facility zao binafsi kuuza pale za serikali zinazowalipa zinaposhindwa kutoa huduma
 
Hata wasomi kama nyie mnaishia kuongea tu kwa maneno pasipo na vitendo? Basi tena tz kwishne kwishne kaabisa
 
Hivi original yao hawa watu ni wapi? Ingekuwa UDSM ningeshangaa wasameheni bure hawa ndo wanajifunza kudai haki sio hulka yao kujitambua huwga wanabipubipu hivihivi
 
Misscommunication, umasikini wa akili uliokithiri, woga, kukata tamaa, ubinadamu wa mshumaa au ni nini? Kama ni kweli am dissapointed.
Mlitaka nini? Manake this time wananchi wako nyuma yenu, mnashindwa au na nyie binafsi, mnafaidi hii hali?
Mi nadhani kuna jinsi individual doctors wanafaidi kuwepo na hali mbaya mahospitalini.
Mfano manunuzi feki, kugawana madawa, facility zao binafsi kuuza pale za serikali zinazowalipa zinaposhindwa kutoa huduma
Wengine wanaofaidi hali hii sindio hao kama kina Dr Ngoma anabeba chemotherapy anakwenda kuuza kwenye hospital yake hawa ni wauaji kabisa mkuu.
 
Kama habari hii ni kweli, basi madaktari ni wababaishaji na wapuuzi sana. Bora muendelee kuwa na maisha magumu kama ya walimu, na mitoto yenu mshindwe kuisomesha shule nzuri. I mean Govt iwa-tit mpaka mkome. Na hizi porojo zenu mkome na muache kutueleza. Mnatia kichefuchefu tu.
 
Watanzania tumelogwa! Hata pale tunapokuwa na haki hatuwezi kudai.kama madaktari mishipa inawatoka kudai haki yao nani wataweza?
 
Watu wanashindwa kuelewa kuwa waganga wa kuu wa mikoa,makatibu wa hospitali hizo na viongozi wengine hawawezi kutetea mgomo kwani wao ndio wanaofaidi sana mahela haya ya miradi kwani pesa nyingi katika idara hii wao ndio wanaozipangia burget kwahiyo msitegemee watasapot mgomo hali hii ilivyo wao ndio utajiri wao ulipo nitashangaa kama chama cha madaktari hakina viongozi wa mikoa na wilaya ambao sasa ndio wangeratibu mgomo kama walivyofanya hapa Dar.
 
mgomo wa madktari sio kama wa makonda wa kupaki magari au wa rubani kusubiri kuona ndege hairuki ndo uone mgomo. Dr kuwepo sehemu ya kazi sio kuwa hajagoma. au mpaka mnataka atembee na sindano mikononi ndo muelewe?mgomo baridi ni mbaya zaidi,subiri muone!
 
Bora hata walimu walikukuruka kidogo! Waganga wakuu wa wilaya na mkoa ni mafisadi wakubwa hawawezi kugoma.mngejipanga hata Dar tu!
 
mgomo wa madktari sio kama wa makonda wa kupaki magari au wa rubani kusubiri kuona ndege hairuki ndo uone mgomo. Dr kuwepo sehemu ya kazi sio kuwa hajagoma. au mpaka mnataka atembee na sindano mikononi ndo muelewe?mgomo baridi ni mbaya zaidi,subiri muone!
Hizi sasa stori! Unajua majuzi madaktari wa Kenya walifanya nini? We are not organised pamoja na shule zetu tunazidiwa hata na watu wa daladala!!
 
Madaktari subirini peremende na maneno matamu muendelee kuishi kwa matumaini!! Mtapewa stori tamu maisha yaendelee! Mmeshindwa kuibana serikali msiwaonee wagonjwa mnapaswa kujipanga!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom