Hospitali binafsi zinapotanguliza maslahi badala ya Afya za Watanzania

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
347
462
Approach walioichukua watoa huduma za afya binafsi inashangaza na kusikitisha.

Naona kabisa maslahi yakiwa na nguvu sana kuliko utu.
---
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amewataka Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzanja (Aphfta) kuhakikisha wanaheshimu leseni zao kwa kutoa huduma wakati majadiliano yakiendelea

Dar/Lindi. Wakati Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzanja (Aphfta) wakisitisha kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Serikali imewaagiza watoa huduma hao kurudi mezani kufanya mazungumzo na kamati iliyoundwa huku wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Serikali imezitaka hospitali binafsi kupokea wagonjwa kulingana na masharti ya leseni na usajili wa hospitali hizo.
Kauli ya Serikali inakuja wakati ambapo leo Machi mosi, 2024 baadhi ya hospitali ikiwamo ya Kairuki, Regency, TMJ, Hospitali ya Ekenywa za jijini Dar es Salaam zikisitisha kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF.

Mgomo huo ni kufuatia tangazo la saa 48 la Aphfta ikiitaka Serikali warudi meza moja ndani ya muda huo kufikia mwafaka kabla ya kuwasitishia huduma wagonjwa wenye kadi za NHIF na kwa wale wanaoendeela kupata huduma wakiwemo wagonjwa wa kulazwa watapelekwa hospitali za umma kuendelea na matibabu.

Kiini cha mgororo mgomo huo ni watoa huduma hao kugomea maboresho ya kitita kipya cha NHIF kwa madai gharama za huduma zilizopangwa na NHIF zitawafanya kushindwa kujiendesha.

Kauli ya Serikali
Leo Ijumaa, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Lindi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma binafsi kuendelea kufanya majadiliano na kamati aliyoiunda wakati wakiendelea kuwahudumia wananchi.

“Nisisitize majadiliano yatafanyika wakati huduma zinaendelea kutolewa, tuongee wakati huduma zikiendelea kutolewa. Natoa rai kwa hospitali zote zilizositisha kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF ziendelee kuwahudumia wanachama hao.

“Toeni huduma, ni wiki moja mbili tatu njooni tukae Serikali tumeweza kutoa huduma kwa kitita kipya changamoto ni moja mbili tatu, uzuri tunakwenda mwaka mpya wa bajeti 2025,2026 bado fursa ipo kwahiyo majadiliano yatafanyika wakati huduma zinaendelea,” amesema.

“Namwelekeza Msajili wa Hospitali Binafsi kutoa notice na kuchukua hatua mara moja kwa watoa huduma wote ambao kwa namna moja watakiuka sheria anazozisimamia,” amesema Ummy.

“Ninavielekeza vituo/hospitali zote binafsi na za umma nchini kuendelea kuwapokea wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwa kuwa hili ni takwa la Sheria namba 151 ya Usajili wa Vituo Binafsi vya kutolea huduma na kanuni yake namba 32. Kutowapokea wagonjwa hao ni kuvunja Sheria husika.”

Pia, ametoa maagizo kwa wakuu wa mikoa wahakikishe wanaendelea kusimamia kwa karibu utoaji wa huduma za afya katika maeneo yao ikiwemo kusimamia maelekezo haya kupitia wataalam wa afya katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuchukua hatua stahiki kulingana na kanuni na Sheria zilizopo kwa kushauriana na Wizara ya Afya.

Waziri Ummy amesema bado milango ya wizara ipo wazi na wanawakaribisha watoa huduma binafsi kuendelea kujadiiliana maeneo ambayo hawajaridhika kwa hoja na si kupinga kwa maneno.

Hoja alizohitaji Ummy zipingwe kwa hoja na Aphfta ni gharama za dawa, uendeshaji pamoja na faida ambayo kamati iliridhishwa nayo akiwataka watoa huduma hao wasikatae vitu kwa ujumla.

“Aphfta watuambie kama vigezo vilivyowekwa na kamati hawakubaliani nazo, hakuna vigezo vingine dawa umenunua kiasi gani, gharama za uendeshaji na faida waje mezani waseme mmetuwekea faida ndogo, waje mezani watuambie dawa haiuzwi bei hii ushahidi tunao sio waseme hatutaki kitita leteni hoja zenu mezani,”amesema.

Kiongozi huyo wa sekta ya afya amesema Serikali imeielekeza NHIF kuendelea na kitita chao lakini wazingatie maoni na mapendekezo ya kamati.

Amesema gharama ya kumuona daktari NHIF wamebadilisha na kurudi kwenye mapendekezo ya kamati, hivyo maboresho yaliyofanyika ni kupata na kukosa huku akisisitiza vipo vitu NHIF imepoteza na Aphfta wakubali kupoteza baadhi ya vitu.

“Tumewaelekeza NHIF kuendelea kupokea maoni ya wadau kuhusu kitita wakati wa utekelezaji,tumewasiliza sana Aphfta mimi na jopo langu tumewa ‘accommodate’ sana tangu mwaka 2022 Agosti ni kuchelewa tu na tumekuwa wavumilivu, wizara inaendelea kusisitiza umuhimu wa majailiano katika suala hili ili kupata suluhu ya jambo hili,” amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema baada ya kupata taarifa ya kamati, aliitisha kikao akiwa na timu ya watalamu wa wizara ya afya, wataalamu wa NHIF, wamiliki wa vituo binafsi, kamati ya afya chini ya Bakwata, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanznaia (Tira), Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na Tume ya Kikirsto ya Huduma za Kijamii na taarifa ya kamati hiyo ikawasilishwa.

Ummy amekiri baada ya kuwasilishwa taarifa hiyo hakuna mdau yeyote aliyepinga badala yake wadau hao walimuomba wao wakafanye hesabu zao kwanza.

“Pia, suala hili tuliwasilisha bungeni kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi kupata maoni na ushauri wao jambo jema hakuna aliyeweza kujenga hoja,” amesema Ummy.
 
Ushaziita binafsi unaleta vya afya ya watanzania ni binafsi? Za serikali ni za wote za binafsi ni biashara wanaruhusiwa uza panado tsh bil 1
 
Approach walioichukua watoa huduma za afya binafsi inashangaza na kusikitisha.

Naona kabisa maslahi yakiwa na nguvu sana kuliko utu.

1. Hivi zile billions walizokopeshana nhif walisharudisha?

2. Kwa mukthadha huo huo, kumbe serikali wametanguliza maslahi ya nani?
 
1. Hivi zile billions walizokopeshana nhif walisharudisha?

2. Kwa mukthadha huo huo, kumbe serikali wametanguliza maslahi ya nani?
Ni kweli NHIF kuna mapungufu mengi. Ila kwa hili wangeendelea kutoa huduma huku wakiwasilisha malalamiko yao.
UTUKWANZA#
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=OQ3Fpfs4GIk

Perspective ya serikali wanaposhindwa kuelewana.

Ni vizuri kusikia pande mbili kabla ya kuhitimisha who’s right or wrong.

Machache niliyookota kwenye kitita kipya.

Serikali imetumia factors zifuatazo kupanga hizo bei:

1. Kwenye dawa wamefanya research ya bei za wholesale na retail. Wakaangalia bei ya kununulia, shipping na overhead costs za kutunza dawa na kupanga bei based on ‘unit cost + markup profit.

2. Kwenye huduma za afya wamefanya bed service costing ya medical intervention kadhaa kupata ‘service costs + profit (by the wat gharama za matibabu ndio zinavyopangwa).

3. Tatu vipimo wameangalia depreciation rate ya vifaa, possible life time usage ya kifaa/machine na kupata charge + profit.

4. Compensation ya consultant imeangaliwa in line na malipo ya hospitali za serikali.

Hospitali binafsi wameshindwa ku counter hizo hesabu za serikali pamoja na kupewa muda. Though hizo hesabu might vary reasonably kwa upande wa private lakini bora tuwasikie wenyewe kuliko kuwasemea.
 
Ni kweli NHIF kuna mapungufu mengi. Ila kwa hili wangeendelea kutoa huduma huku wakiwasilisha malalamiko yao.
UTUKWANZA#

Una maana kama vipi wangeendelea tu, kutoa huduma kwa hasara japo kwa muda huku wakiendelea kukamuliwa kodi na serikali isiyojali biashara za watu?
 
ifike mahali afya ya watanzania isichezewe kwa misuli ya kifedha nadhani hawa sekta binafsi wajitadhimini
 
Ni kweli NHIF kuna mapungufu mengi. Ila kwa hili wangeendelea kutoa huduma huku wakiwasilisha malalamiko yao.
UTUKWANZA#
Unaposema waendelee na huduma, kwa gharama za nani?. Hawa ni wafanya biashara, kungekuwa na uwezekano wa faida hata kidogo wasingegoma. Kumbuka wapaswa kulipa wafanyakazi, kodi na ada mbalimbali, na mwisho ni kwamba waliwekeza mtaji ambao lazima urudi pamoja na faida.
 
Ni kweli NHIF kuna mapungufu mengi. Ila kwa hili wangeendelea kutoa huduma huku wakiwasilisha malalamiko yao.
UTUKWANZA#
Nafikiri wewe hujawahi kuingia negotiation zozote na serekali ndio maana unasema hvyo. Ukiona mpaka taasisi inaamua kuingia kwenye mgomo dhidi ya Serikali ujue negotiations zimefangika Sana ila utekelezaji umekua sifuri
 
Watanzania ujamaa umetulemaza sana akili....yaani mtu kapangisha au kajenga jengo la gharama.....kalirekebisha.......kaajiri wataalamu na kununua vifaa tiba vya gharama.........alafu anatokea mnyonge mmoja anaongelea kuhusu utu.......cha ajabu sasa huyo anayeongelea utu ikifika mwisho mshahara ukichelewa ni kisirani na boss wake....
 
Hii nchi Ujamaa uliisha pale Mzee Mwinyi alipoingia madarakani

Serikali iache kujipendelea bali iwahamasishe wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima, wanachama wakiwa wengi na fedha itapatikana nyingi
 
Back
Top Bottom