Tanga: Serikali yaunda timu kuchunguza madai ya uzembe Hospitali ya Bombo yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kufuatia hoja mbili kuhusu kilichotokea katika Hospitali mbili za Mkoani Tanga, mamlaka zimetoa majibu.

Hoja zenyewe ni hizi hapa:
= Hospitali ya Bombo kuna uzembe mkubwa. Inaumiza sana watu kutothamini uhai wa wengine
= Uzembe wa Wauguzi wadaiwa kusababisha mtoto mchanga kuvunjika mkono wakati mama mtu akijifungua Hospitali ya Magunga - Tanga

Majibu ya Serikali kuhusu hoja hizo...
IMG-20240120-WA0019.jpg

TAARIFA KWA UMMA​
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kifo cha kuhuzunisha cha mwanafunzi mmoja kilichotokea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo), na katika tukio jingine kuvunjika kwa mkono wa mtoto mchanga wakati mama mjamzito alipokuwa anasaidiwa kujifungua katika Hospitali ya Mji-Korogwe (Magunga).

Matukio yote haya mawili yanahusishwa na dhana ya uzembe na watoa huduma za afya katika maeneo hayo.

Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa haraka tayari imeshatuma timu za uchunguzi na Mganga Mkuu wa Mkoa kwenye maeneo hayo ili kubaini ukweli wa kina na hatua zinazostahili kuchukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi huo, na hatutasita kuchukua hatua za adhabu kitaaluma au jinai pale itakapobidi kufanya hivo.

Tunawaomba wananchi waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linafanyiwa kazi kwa uzito unaostahiki.
 
Hii nchi sasa hivi hakuna uwajibikaji. Ni bora liende tu. Kila mahali ni uozo juu ya uozo. Inasikitisha sana.
 
Watumishi wa afya wanaonewa sana

Mazingira ya kazi ni magumu na stress za kisiasa ndo usiseme.
 
Internal Bleeding, huemda Magumga ni kituo kidogo kilichoanza upasuaji karibuni, timu ya RAS/RMO ikajifunze vhangamoto kilichopo pale. Kama ni uzembe au compentency ya madakatri
 
Kufuatia hoja mbili kuhusu kilichotokea katika Hospitali mbili za Mkoani Tanga, mamlaka zimetoa majibu.

Hoja zenyewe ni hizi hapa:
= Hospitali ya Bombo kuna uzembe mkubwa. Inaumiza sana watu kutothamini uhai wa wengine
= Uzembe wa Wauguzi wadaiwa kusababisha mtoto mchanga kuvunjika mkono wakati mama mtu akijifungua Hospitali ya Magunga - Tanga

Majibu ya Serikali kuhusu hoja hizo...
View attachment 2877178
TAARIFA KWA UMMA​
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kifo cha kuhuzunisha cha mwanafunzi mmoja kilichotokea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo), na katika tukio jingine kuvunjika kwa mkono wa mtoto mchanga wakati mama mjamzito alipokuwa anasaidiwa kujifungua katika Hospitali ya Mji-Korogwe (Magunga).

Matukio yote haya mawili yanahusishwa na dhana ya uzembe na watoa huduma za afya katika maeneo hayo.

Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa haraka tayari imeshatuma timu za uchunguzi na Mganga Mkuu wa Mkoa kwenye maeneo hayo ili kubaini ukweli wa kina na hatua zinazostahili kuchukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi huo, na hatutasita kuchukua hatua za adhabu kitaaluma au jinai pale itakapobidi kufanya hivo.

Tunawaomba wananchi waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linafanyiwa kazi kwa uzito unaostahiki.
Tatizo la uzembe katika utoaji huduma sio Tanga Tu hata huku kwetu ni vilevile hivyo Kama uchunguzi unafanyika ufanyike nchi nzima.
 
Back
Top Bottom