Kama mwizi hafai kua kiongozi wa chama makini kama Chadema.
Baba amwumbua mtoto wake anayegombea udiwani
Jumatatu, Octoba 15, 2012 06:27
Na Sam Bahari, Shinyanga
*Amtangaza hadharani kuwa ni mwizi, hana sifa
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Mwawaza Manispaa ya
Shinyanga, Anthony Peter (CHADEMA), juzi aliumbuka baada ya baba yake
mzazi kumtangaza katika mkutano wa hadhara, kuwa hana sifa za kuwania
nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mwizi.
Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika
uchaguzi mdogo, ambao umeitishwa baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo
Charles Magina, kufariki dunia kwa ajali ya pikipiki.
Katika mkutano huo, mzazi wa mgombea huyo mzee Peter Molla (62),
aliwaacha hoi wananchi waliohudhuria mkutano huo pale
alipomshambulia kijana wake akisema kuwa, hafai kuwa
kiongozi.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Molla alisema pamoja na kuwa
mwanaye huyo hapendi kufanyakazi, licha ya kuwa
na umri mkubwa na kwamba muda mwingi amekuwa akizurura
kwa ndugu zake kijijini bila ya mafanikio.
Molla alisema, hivi karibuni aliuza ngombe zake kwa
ajili ya kwenda kumuokoa mgombea huyo, baada ya kukamatwa na polisi
usiku kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.
Mimi sikujua nilidhani nimezaa mtoto wa kiume ambaye atakuja kunilea
na kunitunza uzeeni, kumbe hakuna kitu, amenitelekeza
hapa mnaniona na umri huu nimebaki napata shida.
Siyo siri mwanangu amekuwa mwizi, hawezi kukaa
sehemu moja anatangatanga ovyo na makundi ya vijana wenzake anaozunguka
nao huku wakimshauri mambo machafu, hao jamaa zake nao ni
wezi, alisema.
source wavuti na magazeti ya jana (mtanzania).
MY TAKE; IMEKUWAJE CHAMA KINASIMAMISHA MGOMBEA WA NAMNA HII BILA
KUMCHUNGUZA KWANZA???
Njaa mbaya!mzee/baba atakuwa amepewa bahasha.
Juzi kati nilisoma uzi
humu jamvini kuwa yule baba alinunuliwa na
MAGAMBA na kumpa pombe ili amkashifu
mwanaye.
Ila hizo njama za kumchafua hazitafanikiwa na ushindi ataupata.
Pia nassary walisema kuwa baba yake kasema ni mkorofi na ni muhuni.
MY TAKE: INAWEZEKANA BABA NI GAMBA HIVYO AMEAMUA KUMCHAFUA MTOTO WAKE KWA KUWA KAGOMBEA KWA TIKETI YA CDM.
This is what i would call booty licking.......from pumpkin heads!!Hivi Chadomo mbona huwa hamtaki kukubaliana na ukweli? Baba yake anasema mwanae mwizi nyie mnapinga ebooo.!
Apate ushindi akawaibieni vizuri!
kwa hiyo unataka CHADEMA nayo iwe na kina CHENGE,LOWASSA,NGELEJA na MKULO wao ili iweje? Fikiria huyo mgombea angekuwa ni wa CCM ungeandika sentensi hii uliyoandika? Hivi jambo baya ni lile linalotendwa na CCM tu. Mimi kwa ushauri wangu ni kama kweli si Propaganda za kisiasa, ikithibitika kwamba kweli jamaa ni mwizi basi CHADEMA ifute udhamini wake kwani ni bora kutokuwa na mgombea kwa kulinda heshima ya chama kuliko kuwa na mgombea anayechafua heshima ya chama.Halafu kama pia ikithibitika hao viongozi waliomweka huyo jamaa nayo pia waadhibiwe.Mwizi aseme kaiba nini?mbona CHENGE,LOWASSA,NGELEJA,MKULO wapo bungeni na ni wizi wanaotambulika na dunia nzima.
Huyo baba pia ni mwizi na anafaidika na wizi wa mwanae ndio maana akikamatwa anadiriki kuuza mifugo yake ili akamtoe mwanae na aendelee na wizi ili wafaidike wote, toto halikusaidii kwanini utoe mali zako? Au posho za nyinyiem zinafanya jizi limsaliti jizi toto, tungekuwa na takukukuru hapa leo wote mpo ndani pamoja na hao polisi mliowahonga, SHEENZI TYEP!