Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
305
519
MTATIRO ASHUSHA BEI ZA MAJI SHINYANGA VIJIJINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji kwenye kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga Vijijini na kutaka bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini mara moja.

Akiwa katika Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi, DC Mtatiro ameelekeza kuanzia tarehe 04.04.2024 bei za maji zishuke.

Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo kwenye mkutano huo na kuanza kuyatekeleza mara moja.

Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+.

Wananchi wa kata hizi kwa miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika.

Katika mkutano huo, DC Mtatiro amekiri kumpigia simu Waziri wa Maji Juma Awesso ambaye ameunga mkono mapendekezo ya Wakili Mtatiro.

DC Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni wilaya yake ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya tangu Rais Samia amhamishe kutoka Tunduru Mkoani Ruvuma.
 
Kwani bei za maji hazipangwi na mamlaka moja nchi nzima? Kila mkoa una bei zake??

Mm nilidhani bei zinapangwa na EWURA?

Hebu wajuvi wa mambo njooni mnisaidie mm pamoja na Mtatiro.
 
Mzee wa migomo na kunji enzi zile nipo first year udsm huyu mwamba ndio anamaliza mwaka wake wa mwisho.

Anyway ali-influence mabadiliko ya sera za mikopo vyuo vikuu kipindi kile na sasa wengi wanafaidika. Hongera kwake na Jakaya Kikwete kwa mabadiliko yale yaliyowezwsha sasa hivi kila Kijiji na kitongoji kuwa na msomi/wasomi wa digrii (degree holders)
 
Uzalishaji wa maji na kuyatibu unatofautiana sehemu moja na nyingine.

Hapo gharama za uendeshaji lazima zitofautiane, ndipo inaibuka bei tofauti.

Hata mafuta yanatofautiana bei kati ya mkoa na mkoa
 
View attachment 2954245
Kwanini hawa wanamhujumu Samia ?
Serikali haiwezi kujiendesha bila makusanyo.
 
Kwani bei za maji hazipangwi na mamlaka moja nchi nzima? Kila mkoa una bei zake??

Mm nilidhani bei zinapangwa na EWURA?

Hebu wajuvi wa mambo njooni mnisaidie mm pamoja na Mtatiro.
EWURA hawa ndio wenye shida chini ya MUME WA SPIKA ana Kiburi sijawahi ona! Mungu amshushie Rungu sku moja hata akatike mikono tu
 
Mzee wa migomo na kunji enzi zile nipo first year udsm huyu mwamba ndio anamaliza mwaka wake wa mwisho.

Anyway ali-influence mabadiliko ya sera za mikopo vyuo vikuu kipindi kile na sasa wengi wanafaidika. Hongera kwake na Jakaya Kikwete kwa mabadiliko yale yaliyowezwsha sasa hivi kila Kijiji na kitongoji kuwa na msomi/wasomi wa digrii (degree holders)
Mkuu kwahiyo nyie ndio mlikuwa mnatusumbua pale Revo Square. Anyway kizazi chenu pale Jalalani mlileta sana taharuki kwenye Corridor za maofisi makubwa ya wafanya maamuzi.
 
Kwani bei za maji hazipangwi na mamlaka moja nchi nzima? Kila mkoa una bei zake??

Mm nilidhani bei zinapangwa na EWURA?

Hebu wajuvi wa mambo njooni mnisaidie mm pamoja na Mtatiro.
Kila Mamlaka Ina bei yake mfano Mbeya tsh1400/ Iringa tsh2000/ kwa lita

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Mkuu kwahiyo nyie ndio mlikuwa mnatusumbua pale Revo Square. Anyway kizazi chenu pale Jalalani mlileta sana taharuki kwenye Corridor za maofisi makubwa ya wafanya maamuzi.
Geti la Vice Chancellor Professor Mkandala tuliling'oa .......
Sasa hivi hatusikii kabisa mgomo wala kunji mtakuwa kuna mitoto ya hovyo sana hapo!
 
Hongera kwake,

Unit Moja Kwa 2500 ni kubwa mno, matumizi ya familia Moja hutumia Si chini ya unit 10 ambayo ni 20,000 Kwa mwezi.

Hata Hilo punguzo Bado, Inatakiwa unit 1 angalau iwe 1,300/=
 
deblabant,
Utoaji wako wa hoja inaonyesha Kuna changamoto unapitia na hutaki kukubali makosa,, kulikuwa hamna sababu ya kuandika kwa lugha ngumu kiasi hicho,,, jifunze tu Kuna watu wamebarikiwa japo wewe unajua madhaifu Yao na unafikili kwa madhaifu hayo hawapaswi kufika kule,,,ilaa Mungu siyo mwanadamu ,ndio maana vidhaifu machoni mwetu ndio vyenye kupendeza machoni pake,kubari mafanikio ya wenzio utafanikiwa pia
 
MTATIRO ASHUSHA BEI ZA MAJI SHINYANGA VIJIJINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji kwenye kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga Vijijini na kutaka bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini mara moja.

Akiwa katika Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi, DC Mtatiro ameelekeza kuanzia tarehe 04.04.2024 bei za maji zishuke.

Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo kwenye mkutano huo na kuanza kuyatekeleza mara moja.

Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+.

Wananchi wa kata hizi kwa miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika.

Katika mkutano huo, DC Mtatiro amekiri kumpigia simu Waziri wa Maji Juma Awesso ambaye ameunga mkono mapendekezo ya Wakili Mtatiro.

DC Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni wilaya yake ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya tangu Rais Samia amhamishe kutoka Tunduru Mkoani Ruvuma.
View attachment 2954245
Bei za, huduma, ni, swala LA, kiuchumi, bei inapangwa na factors kibao, bei ya, material nk, Sasa kutoa matamko kushusha bei kisiasa ni ungese tu, hapo bei itashuka, lakini kitakachofanyika, itatafutwa pesa kufidia nakisi! Ni kama kuweka subsides,
Hakuna cha kitaalamu kilichofanyika, ni upuuzi tu,
Na mi ccm, haiwezi kusema kupanda kwa bei kumesababishwa na ni ni, na, ni ni kimefsnyika kushusha bei, au miujiza tu kama ya mwamposa?
 
Nimpongeze kwa kuguswa kwake na kujaribu kuwatetea wananchi lakini hana mamlaka hayo ya kupangia wazalishaji wa maji bei. Mwenye mamlaka hayo ni waziri wa maji au EWURA.

Busara ingekuwa kukaa nao kwanza hao SHUWASA wampe sababu zao na kuwaomba washushe bei au aonge na waziri alitazame. Lakini mkuu wa wilaya hana mamlaka hayo.
 
Kwani bei za maji hazipangwi na mamlaka moja nchi nzima? Kila mkoa una bei zake??

Mm nilidhani bei zinapangwa na EWURA?

Hebu wajuvi wa mambo njooni mnisaidie mm pamoja na Mtatiro.
Kila eneo lina bei zake kulingana na gharama za uzalishaji lakini lazima zipate idhini na EWURA.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Nimpongeze kwa kuguswa kwake na kujaribu kuwatetea wananchi lakini hana mamlaka hayo ya kupangia wazalishaji wa maji bei. Mwenye mamlaka hayo ni waziri wa maji au EWURA.

Busara ingekuwa kukaa nao kwanza hao SHUWASA wampe sababu zao na kuwaomba washushe bei au aonge na waziri alitazame. Lakini mkuu wa wilaya hana mamlaka hayo.
Uko sahihi lakini ziwe muafaka na siyo kufidia uzembe wa watendaji!
 
Uzalishaji wa maji na kuyatibu unatofautiana sehemu moja na nyingine.

Hapo gharama za uendeshaji lazima zitofautiane, ndipo inaibuka bei tofauti.

Hata mafuta yanatofautiana bei kati ya mkoa na mkoa
Sawa mkuu. Nafahamu bei ya mafuta ni tofauti kati ya mkoa na mkoa lkn bei zote zinapangwa na EWURA. Sasa Mtatiro kuwataka SHUWASA washushe bei ndiyo ilinipa ukakasi.

Ni sawa na mkuu wa mkoa wa Tabora kwa mfano kuwataka wauzaji wa mafuta kushusha bei ambazo zimeelekezwa na EWURA.
 
EWURA ni wapuuzi wengine mara nyingi hufanya rubber stamping ya bei zilizopendekezwa na mamlaka.

Tofauti na bei za mafuta ambazo bei ya soko la dunia inafahamika,bei za maji zina utapeli mwingi kwa mamlaka kubambika bei zisizo na uhalisia ili kuficha udhaifu wao.

EWURA wanapaswa kuwasaidia wananchi kukokotoa bei halisi ya uzalishaji maji ili kupata bei ya soko.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom