Mgombea UDIWANI kata ya mwawaza ni mwizi - BABA YAKE mzazi

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
987
Baba amwumbua mtoto wake anayegombea udiwani

Jumatatu, Octoba 15, 2012 06:27 Na Sam Bahari, Shinyanga

*Amtangaza hadharani kuwa ni mwizi, hana sifa
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, Anthony Peter (CHADEMA), juzi aliumbuka baada ya baba yake mzazi kumtangaza katika mkutano wa hadhara, kuwa hana sifa za kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mwizi.

Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika uchaguzi mdogo, ambao umeitishwa baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo Charles Magina, kufariki dunia kwa ajali ya pikipiki.

Katika mkutano huo, mzazi wa mgombea huyo mzee Peter Molla (62), aliwaacha hoi wananchi waliohudhuria mkutano huo pale alipomshambulia kijana wake akisema kuwa, hafai kuwa kiongozi.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Molla alisema pamoja na kuwa mwanaye huyo hapendi kufanyakazi, licha ya kuwa na umri mkubwa na kwamba muda mwingi amekuwa akizurura kwa ndugu zake kijijini bila ya mafanikio.

Molla alisema, hivi karibuni aliuza ng'ombe zake kwa ajili ya kwenda kumuokoa mgombea huyo, baada ya kukamatwa na polisi usiku kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.

"Mimi sikujua nilidhani nimezaa mtoto wa kiume ambaye atakuja kunilea na kunitunza uzeeni, kumbe hakuna kitu, amenitelekeza hapa mnaniona na umri huu nimebaki napata shida.

"Siyo siri mwanangu amekuwa mwizi, hawezi kukaa sehemu moja anatangatanga ovyo na makundi ya vijana wenzake anaozunguka nao huku wakimshauri mambo machafu, hao jamaa zake nao ni wezi," alisema.

source wavuti na magazeti ya jana (mtanzania).

MY TAKE; IMEKUWAJE CHAMA KINASIMAMISHA MGOMBEA WA NAMNA HII BILA KUMCHUNGUZA KWANZA???
 
Waandishi wa habari bana? ukiisoma hiyo habari kituko tupo!
 
Ukweli ukidhihiri ubaya hujitenga..hongera baba yake mana umesema ukweli haya wana CDM munasemajeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Sasa mwizi anafanya nini uraiani? Police wafanye kazi yao sasa, na huyo mzee ni kituko, yeye kaishasema jamaa mwizi alikamatwa na bunduki alafu hapo hapo , kauza ng'ombe ili akamtoe mwizi police.Inamaana alitoa rushwa ili amtoe police.
 
Kwani hujui au unajifanya kama hujui kma haujui basi......................Wizi haoooooooooooooooooooooooo Chademaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hoiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kwa wizi kumbe chama cha wafadhili wa wizi................
 
Ukweli ukidhihiri ubaya hujitenga..hongera baba yake mana umesema ukweli haya wana CDM munasemajeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

vitu vingine jaribu kujiongeza hakuna baba wa aina hiyo babako hata uweje hawezi kukuchafua hadharani wakati akijua lolote likikupata yeye ndie anaeuza ng'ombe akutoe!!
kwanini asifurahi kuwa mwanae anaenda kuwa diwani?
ili ng'ombe wake wasalimike!!?
mzee katumika kisiasa na ametumika vibaya.
ccm walikuwa kwenye ufunguzi wao.
haya ya mgombea wa CDM yakatoka wapi!?
na yule mzee alipewa nafas kama nani ndani ya huo mkutano!!?
siasa bhana sihasa!!!.
 
Mambo mengine bwana, this may be possible lakini there is something very wrong na huyo mzazi??? Hata evolution principles zinakataa, wapi huko umeona baba akimuharibia mwanae nafasi ya mafanikio, kama alikuwa mwizi huu si ndio muda wa kushukuru kwamba amebadilika..
 
Hivi Chadomo mbona huwa hamtaki kukubaliana na ukweli? Baba yake anasema mwanae mwizi nyie mnapinga ebooo.!
 
Molla alisema, hivi karibuni aliuza ng'ombe zake kwa ajili ya kwenda kumuokoa mgombea huyo, baada ya kukamatwa na polisi usiku kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.
Huyu mzee anapaswa kuisaidia takukuru kwakutoa rushwa ili mwanae aachiwe kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.

Namshukuru kwa taarifa hizo maana hatutaki kiongozi mwizi, lakini naye anapaswa kujibu mbele ya vyombo husika alimkomboa kwa shilingi ngapi, na nani aliyelipwa malipo hayo ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom