DOKEZO Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Bwilingu (Chalinze-round about) Ndugu Abdul Nasa anatumia vibaya cheo cha baba yake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Mwenyekiti wa Vijana CCM (UVCCM), Kata ya Bwilingu (Chalinze-round about) Ndugu Abdul Nasa ameendelea kukitumia vibaya cheo cha baba yake (Diwani Kata ya Bwilingu Jimbo la Chalinze).

Inadaiwa alifanya jaribio la kujeruhi na kushindwa kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu ndani ya chama kutokana na kile kinachodaiwa kuwa baba yake huyo amekiweka mfukoni chama kuanzia ngazi ya kata mpaka wilaya.

Vyombo vya Dola, navyo vimepata kigugumizi kuchukua hatua yoyote kwa kumhofia baba yake mtenda kosa ambaye ni diwani.
Kamati ya siasa ya Kata ya Bwilingu na Wilaya ya Bagamoyo zimeendelea kulifumbia macho jambo hilo licha ya kufikishwa mezani kwao kwa kinachodaiwa na mtenda kosa kuwa baba yake amemshika katibu wa chama wilaya.

Hivyo, jambo hilo halitajadiliwa kwenye kikao chochote kwa kuwa katibu ndio anaepeleka ajenda za vikao kwenye vikao husika. Amekuwa akijitapa kwa maneno hayo akiwa sehemu zake za starehe huku akiwa anapata kilevi chake pendwa (Mirungi) ambacho amekuwa na uraibu nacho.

Pamoja na mambo mengine mwenyekiti huyo wa vijana amekuwa na tuhuma mbalimbali kama vile kujihusisha na biashara haramu za kusafirisha wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia na Somalia na uuzaji wa madawa na utumiaji wa mirungi lakini ameshindwa kuchukuliwa hatua yoyote kwa kutumia nafasi yake na baba yake ambae ni diwani.

Wanatumia pia wanatumia zaidi mahusiano yao na katibu na Mwenyekiti wa Chama ngazi ya Wilaya kujilinda.

"Waulize kwanini mwenezi Taifa ameishia kuongea tu kwenye tuhuma za mwenyekiti ameshindwa kufanya lolote? Sisi ndio wenye chama na nchi nyie wengine tulieni, mi nakula mrungi hapa na hakuna askari anaweza kunisumbua, kula wewe uone.

“Wale watoto nimewakojolea wameenda kusema kwenye chama umeona chama kimenifanya nini? Mzee kawapoza hela kidogo na njaa zao wametulia, waite hapa uone watakwambia nini. Nimewapoza na fwedha wamekua kimya, chezea diwani Nasa wewe" alisikika kijana huyo akijitapa huku akitafuna gomba!
 
Anza kwa kutafuta no za simu za OCD wa eneo husika.no inapatikana kituo cha Polisi
Ukiwa hapo chukua pia no ya IGP ili kujiandaa kwa mwendelezo wa taarifa endapo hakutakuwa na ufuatiliaji
 
Back
Top Bottom