Mgombea UDIWANI kata ya mwawaza ni mwizi - BABA YAKE mzazi

Juzi kati nilisoma uzi humu jamvini kuwa yule baba alinunuliwa na MAGAMBA na kumpa pombe ili amkashifu mwanaye.

Ila hizo njama za kumchafua hazitafanikiwa na ushindi ataupata.
 
Kama mwizi hafai kua kiongozi wa chama makini kama Chadema.

Hizo ni propaganda tu za kutaka kumuharibia kisiasa.
Mbona hata G.Lema alishawahi kukashifiwa kuwa ni muizi wa magari ila kashfa hiyo haikumdhoofisha kisiasa bali ndo alishinda kwa kishindo na mpaka sasa ni JEMBE na mwiba mkali kwa MAGAMBA.
 

Baba amwumbua mtoto wake anayegombea udiwani


Jumatatu, Octoba 15, 2012 06:27
Na Sam Bahari, Shinyanga


*Amtangaza hadharani kuwa ni mwizi, hana sifa
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Mwawaza Manispaa ya
Shinyanga, Anthony Peter (CHADEMA), juzi aliumbuka baada ya baba yake
mzazi kumtangaza katika mkutano wa hadhara, kuwa hana sifa za kuwania
nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mwizi.


Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika
uchaguzi mdogo, ambao umeitishwa baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo
Charles Magina, kufariki dunia kwa ajali ya pikipiki.

Katika mkutano huo, mzazi wa mgombea huyo mzee Peter Molla (62),
aliwaacha hoi wananchi waliohudhuria mkutano huo pale
alipomshambulia kijana wake akisema kuwa, hafai kuwa
kiongozi.


Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Molla alisema pamoja na kuwa
mwanaye huyo hapendi kufanyakazi, licha ya kuwa
na umri mkubwa na kwamba muda mwingi amekuwa akizurura
kwa ndugu zake kijijini
bila ya mafanikio.

Molla alisema, hivi karibuni aliuza ng’ombe zake kwa
ajili ya kwenda kumuokoa mgombea huyo, baada ya kukamatwa na polisi
usiku kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.


“Mimi sikujua nilidhani nimezaa mtoto wa kiume ambaye atakuja kunilea
na kunitunza uzeeni, kumbe hakuna kitu, amenitelekeza
hapa mnaniona na umri huu nimebaki napata shida.


“Siyo siri mwanangu amekuwa mwizi, hawezi kukaa
sehemu moja anatangatanga ovyo na makundi ya vijana wenzake anaozunguka
nao huku wakimshauri mambo machafu, hao jamaa zake nao ni
wezi,”
alisema.

source wavuti na magazeti ya jana (mtanzania).

MY TAKE; IMEKUWAJE CHAMA KINASIMAMISHA MGOMBEA WA NAMNA HII BILA
KUMCHUNGUZA KWANZA???

Mkuu usipate nao shida hao! CDM haina history ya kuwa na viongozi wasafi! wengi ndio hivyo hivyo! he he he he!
 
Juzi kati nilisoma uzi
humu jamvini kuwa yule baba alinunuliwa na
MAGAMBA na kumpa pombe ili amkashifu
mwanaye.

Ila hizo njama za kumchafua hazitafanikiwa na ushindi ataupata.

Apate ushindi akawaibieni vizuri!
 
dingi kwa NASSARI walishindwa hoja hiyo haina mashiko LOWASA CHENGE KARAMAGI niaje njooni A TOWN tuwafundishe mbinu za masisiem
 
Pia nassary walisema kuwa baba yake kasema ni mkorofi na ni muhuni.
MY TAKE: INAWEZEKANA BABA NI GAMBA HIVYO AMEAMUA KUMCHAFUA MTOTO WAKE KWA KUWA KAGOMBEA KWA TIKETI YA CDM.

Umesema kweli, kule vijijini viongozi wa magamba wamekuwa na tabia ya kuwataka watoto wao wawe wakereketwa wa CCM, lakini vijana huwa wanakataa kabisa na kuna mkakati maalumu wa magamba kutumia wazee kuwakatisha tamaa vijana kujiunga na CHADEMA, tena wazee hawa wanapewa na viongozi wa CCM vifaa kama pikipiki, mabati, kofia,, T-Shirt, mashati ya Yanga, mashuka, viroba vya unga, na hata mitumba kwa wale ambao hali ya kivazi ni mbaya zaidi( ili mradi tuu huyo mzee awe mjanja )basi wanapewa hata mialiko kwenye mikutano ya viongozi wa kiserikali ama wa kichama ili wajione wanathaminiwa. wanaloambiwa ni kuwadhibiti vijana wao wasijiunge ama wasishabikie vyama vya upinzani.
My take:
kwa hiyo mzee kwa kuona aibu mbele ya wazee wenzake wa kimagamba, na labda yale mabati aliyopewa yanamsuta ili asionekane kuwa amewasaliti ameamua kuja kihivyo.

Mhalifu hawezi kuwa mtaani na akamjua yeye tu kuwa mhalifu, mtaa mzima na vyombo vya dola vingejua, na wananchi wasingempendekeza agombee kama anayo tabia hiyo. hiyo ni propaganda za magamba kama walivyozoeleka, huyo jamaa inaelekea ni tishio hapo mtaani kwa hiyo wameamua kumtumia baba yake ili ammalize.
lakini mimi naamini kwamba wananchi wanaelewa sana wanachokifanya na watamchagua huyohuyo kwa kuwa wanamjua sana na ndiyo maana akapitishwa kwenye mchujo.
Mbona propaganda za magamba zinazidi kwisha, muda si mrefu watabaki kupigana wao kwa wao.
 
Sitaki kabisa kuamini hizi habari za huyu baba, kwa sababu ya maswali yafuatayo;

1/Inawezekana vipi Baba mzazi aje hadharani kumvua nguo kiasi hicho mwanae wa kumzaa?

2/Kwa nini hakumwekea pingamizi la kutogombea kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha Sheria?

3/Nini kilimsukuma kuuza ng'ombe wake ili amtoe polisi halafu nini kinamsukuma sasa kudai mwizi hadharani ili asichaguliwe?

4/Kwa nini apewe nafasi kuyasema haya kwenye jukwaa la kisiasa tena la CCM?

5/Kwanini Wakati anazurura mtaani bila kazi hukumzuia sasa ameamua kufanya kazi ya siasa unamfitini?

**Kama ni kweli huyo baba alitamka maneno hayo, basi huyo baba atakuwa ni mchawi mkubwa.
 
mi nadahni huyo mdingi anataka tu kuharibia, sia jabu baba ni kula kulala so anataka vya dezo, kanyimwa sasa noma
 
Mwizi aseme kaiba nini?mbona CHENGE,LOWASSA,NGELEJA,MKULO wapo bungeni na ni wizi wanaotambulika na dunia nzima.
kwa hiyo unataka CHADEMA nayo iwe na kina CHENGE,LOWASSA,NGELEJA na MKULO wao ili iweje? Fikiria huyo mgombea angekuwa ni wa CCM ungeandika sentensi hii uliyoandika? Hivi jambo baya ni lile linalotendwa na CCM tu. Mimi kwa ushauri wangu ni kama kweli si Propaganda za kisiasa, ikithibitika kwamba kweli jamaa ni mwizi basi CHADEMA ifute udhamini wake kwani ni bora kutokuwa na mgombea kwa kulinda heshima ya chama kuliko kuwa na mgombea anayechafua heshima ya chama.Halafu kama pia ikithibitika hao viongozi waliomweka huyo jamaa nayo pia waadhibiwe.

UKWELI HAUNA CHONGO WALA KENGEZA!!
 
Huyo baba pia ni mwizi na anafaidika na wizi wa mwanae ndio maana akikamatwa anadiriki kuuza mifugo yake ili akamtoe mwanae na aendelee na wizi ili wafaidike wote, toto halikusaidii kwanini utoe mali zako? Au posho za nyinyiem zinafanya jizi limsaliti jizi toto, tungekuwa na takukukuru hapa leo wote mpo ndani pamoja na hao polisi mliowahonga, SHEENZI TYEP!
 
Huyo baba pia ni mwizi na anafaidika na wizi wa mwanae ndio maana akikamatwa anadiriki kuuza mifugo yake ili akamtoe mwanae na aendelee na wizi ili wafaidike wote, toto halikusaidii kwanini utoe mali zako? Au posho za nyinyiem zinafanya jizi limsaliti jizi toto, tungekuwa na takukukuru hapa leo wote mpo ndani pamoja na hao polisi mliowahonga, SHEENZI TYEP!

Lakini tuache ya baba na mwanae, Hichi CDM mpaka wanapitia mchakato na kumpata huyo mwizi hawakujua? makusudi au kawaida yao?
 
Ni baba anaetakiwa kuwa Milembe anaweza kumtamkia maneno haya mtoto wake mbele ya hadhara, lazima kuna ugomvi baina yao au baba karushiwa maalibino kwenye rubber band sio rahisi kuamini, na watu wa humu ndani wana akili timamu hawadanganywi na wajinga kirahisi hivyo, stay tuned for a story behind the scene
 
Back
Top Bottom