Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
- Thread starter
- #41
Na Francis Godwin, Iringa
HUZUNI na simanzi zimetawala katika Kijiji cha Wenda, Wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa baada ya Bw. Mchina Lugasi (picha kubwa juu) kuuawa Ijumaa iliyopita kwa madai ya kuiba kuku na mbwa.
Kufuatia mauaji hayo, Balozi wa mtaa wa Wenda, Bw. Tobias Mkonda alimuambia mwandishi wetu aliyekwenda eneo la tukio kuwa alipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa mtoto mmoja mkazi wa mtaa huo ambaye alikuwa wa kwanza kuiona maiti hiyo.
Aliongeza kuwa baada ya taarifa hiyo, uongozi wa mtaa uliweza kufika eneo la tukio la kutambua mwili huo ambapo Bw Joshua Mduda (picha ndogo juu) anatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo na alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuua.
Mimi nilivamiwa na watu nisiowafahamu ambao walikuwa na nondo mkononi .... baada ya watu hao kuondoka, nilisikia kuku wakipiga kelele na nilipotoka nje nilimkuta marehemu akikimbia na kuku wangu na mbwa, hapo niliamua kumfukuza na nikafanikiwa kumkamata na kumchoma kisu tumboni, alisema Mduda.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na amesema wanachunguza.