Mfano wa unyama utokeao kama utekelezaji wa lililokuwa agizo la Mh. Pinda (Graphic)

1216705886_wev.jpg


Na Francis Godwin, Iringa
HUZUNI na simanzi zimetawala katika Kijiji cha Wenda, Wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa baada ya Bw. Mchina Lugasi (picha kubwa juu) kuuawa Ijumaa iliyopita kwa madai ya kuiba kuku na mbwa.

Kufuatia mauaji hayo, Balozi wa mtaa wa Wenda, Bw. Tobias Mkonda alimuambia mwandishi wetu aliyekwenda eneo la tukio kuwa alipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa mtoto mmoja mkazi wa mtaa huo ambaye alikuwa wa kwanza kuiona maiti hiyo.

Aliongeza kuwa baada ya taarifa hiyo, uongozi wa mtaa uliweza kufika eneo la tukio la kutambua mwili huo ambapo Bw Joshua Mduda (picha ndogo juu) anatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo na alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuua.

“Mimi nilivamiwa na watu nisiowafahamu ambao walikuwa na nondo mkononi .... baada ya watu hao kuondoka, nilisikia kuku wakipiga kelele na nilipotoka nje nilimkuta marehemu akikimbia na kuku wangu na mbwa, hapo niliamua kumfukuza na nikafanikiwa kumkamata na kumchoma kisu tumboni,” alisema Mduda.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na amesema wanachunguza.
 
Picha ipo. Watu wanaonekana wazi wakishuhudia kuanzia kipigo hadi mauti. Mpiga picha yupo. Eneo la tukio linajulikana. Mwenye gazeti yupo. Kama kweli polisi wanataka kuzuia tabia hii na kuwapata wahusika wanashindwa kweli?

Mimi kitu kingine kinachoniuma ni ukiangalia kwenye picha utaona kuna watoto wadogo wakishuhudia. Hatuoni kuwa kwa namna hii tunawafanya wawe sugu kwa vitendo kama hivi? Nyani Ngabu alishudia watu 5 wakiuawa wakati mdogo na angalia alivyo-turn out! Tuna traumatise watoto wetu.

Amandla.....
 
Picha ipo. Watu wanaonekana wazi wakishuhudia kuanzia kipigo hadi mauti. Mpiga picha yupo. Eneo la tukio linajulikana. Mwenye gazeti yupo. Kama kweli polisi wanataka kuzuia tabia hii na kuwapata wahusika wanashindwa kweli?


point nzuri. Hivi umeguundua kuwa wengi wanaouawa namna hiyo hasa kwenye mambo ya vibaka na wizi inatokea mjini (kwa wasomi na watu walioenda shule) wakati kule vijijini wanauana kwa sababu ya ushirikina?



Mimi kitu kingine kinachoniuma ni ukiangalia kwenye picha utaona kuna watoto wadogo wakishuhudia. Hatuoni kuwa kwa namna hii tunawafanya wawe sugu kwa vitendo kama hivi? Nyani Ngabu alishudia watu 5 wakiuawa wakati mdogo na angalia alivyo-turn out! Tuna traumatise watoto wetu.

Amandla.....

hahahahhahahahahhaa!!!! (((ni hilo nyani how he turned out...)))

on the otherhand, watoto wanafanya kile ambacho watu wazima wanafanya.. they are impressionable. Ndiyo maana hakuna watu wenye roho ngumu kama watoto walioingizwa katika mapigano ya vita kama askari..
 
Picha ipo. Watu wanaonekana wazi wakishuhudia kuanzia kipigo hadi mauti. Mpiga picha yupo. Eneo la tukio linajulikana. Mwenye gazeti yupo. Kama kweli polisi wanataka kuzuia tabia hii na kuwapata wahusika wanashindwa kweli?

Mimi kitu kingine kinachoniuma ni ukiangalia kwenye picha utaona kuna watoto wadogo wakishuhudia. Hatuoni kuwa kwa namna hii tunawafanya wawe sugu kwa vitendo kama hivi? Nyani Ngabu alishudia watu 5 wakiuawa wakati mdogo na angalia alivyo-turn out! Tuna traumatise watoto wetu.

Amandla.....

Yeah man...witnessing those vicious beatdowns left me scarred for life. It's no joke man. Post Traumatic Stress Disorder is real man
 
Mzee Mwanakijiji.

Watoto wako kweli impressionable na ndiyo maana ni wajibu wa sisi watu wazima tuhakikishe hatu wafanyi sugu wa vitendo kama hivi. Kwa wenzetu filamu haziwi censored kwa lugha na vitendo vya ngono tuu bali pia kwa violence. Sisi kama jamii hata siku moja hatuoni athari za violence kwa watoto wetu, tunaogopa zaidi masuala ya ngono. Hapo angepita binti amevaa bikini watu wangeziba macho watoto wao. Lakini mtu anachomwa moto wanamwambia angalia tu!

Amandla.........
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu unajua unanishangaza sana...Hivi kweli wewe unaona picha hii ni jambo la kawaida kwa sababu yanatokea kila siku?...umeshindwa kabisa kujiuliza maswali mengi kama alofanya Fundi Mchundo kutokana na picha hiyo badala yake unazungumzia kuvunja katiba isiyomsaidia mwananchi kitu chochote..
Yaani wewe unakubali watu kama hawa waendelee kuyafanya wanayoyafanya nje ya katiba lakinim sio Waziri mkuu kusema kile mnachozoea kukifanya..ukasahau kwamba yeye ni relfection yako..
Mkuu wangu mimi sifikirii kabisa swala la mchawi kuawa kama huyu bali nafikiria hao Albino na huyu jamaa ambao tayari wamekwisha poteza roho zao kwa vitendo ambavyo ni pinzani na katiba...
Na ule mfano wako wa Mwanza na Tanga hata kama ulifikiria kumwitia mtu yule mwizi, bado ni kitu kidogo sana kulinganisha na hali halisi ya Bongo sasa hivi. Serikali yetu toka wakati wa Mkapa ilishindwa kabisa kuwalinda wananchi wake. Ilifikia hadi vibaka wanaua watu kama hukuwaachia kitu... wazxi wazi kabisa walichukua kitu chako kwa nguvu na kama ukitaka wakurudishie ni lazima ukikomboe kwa bei watakayokupa wewe..
Wananchi wamechoka kuishi ktk maisha ya woga na ndio maana wamechukua sheria mikononi mwao kwa sababu serikali imeshindwa kuwalinda.. Na hao Albino ni matokeo pia ya serikali kushindwa kuwalinda...hawa wote ni victims wa sheria butu na utamaduni mchafu ambao tunaujenga sisi wenyewe... kama alivyosema Fundi Mchundo hapo kuna watoto wadogo kabisa wakiona jinsi huyo mwizi akiuawa, haya picha hiyo nyingine hata Mbwa amekaa na huzuni, binadamu anapita akichukua picha tu.. Hii inadhihirisha wazi sisi ni watu wa aina gani...
Nitashukuiru sana kama utafikisha ujumbe huu kwa waziri wa mambo ya ndani na vyombo vya Usalama nchini, bunge na pengine hata kwa rais ambaye anachukulia maswala haya YOTE kwa uzito mdogo sana..Nitakuomba tena jaribu kujenga ujumbe wapo na kuelekeza nguvu zako ktk kuondoa mauaji kama haya iwe Albino au wezi kwani sheria ni msumeno..unakata pande zote isiwe OK kuuawa kwa Albino lakini watuhumiwa hadi sheria itumike..
Let's stop the kilings za hawa watu kwanza kisha ndio tuta worry kuhusiana na katiba..tuweke nguvu zetu ktk kusisitiza serikali na vyombo vyote vya haki za dunia kutupia jicho mauaji kama haya ili viongozi wetu wapate kuwajibika...
Je, sio sisi tuliokuwa tunaunga mkono Israel inayoyafanya huko Palestina mbona hatuombi sheria itumike!..tunajenga hoja kwamba mchokoizi ni nani na nani mwenye haki ya kujilinda tena tunaipa hata sharia kikatiba leo Pinda kusema tu wauaji nao wauawe imekuwa swala la kukamatia kiasi hiki mkuu wangu.. terrorist wanauawa na viongozi wa nchi zote za magharibi wametuma majeshi yao kuua hawa terrorist iweje tuone haki matendo kama hayo lakini sio usemi wa Waziri wetu mkuu inapofikia swala la wachawi au kwa sababu hawa ni ndugu na jamaa zetu..Mkuu hawa wachawi na watu wote wenye imani za kichawi ni home grown Terrorist, now how to deal with them ni shangamoto nalotaka sana kulisikia badala ya hizi habari za Pinda wakati Albino wanaendelea kufa kila siku...
Samahani mkuu wangu unajua inaniuma sana kuona picha kama hizi kwa sababu ni kitu kinachotokea kweli.. sifikirii kesho itakuwa vipi kutokana na maneno ya Pinda kwani ombi lake yawezekana kabisa isitokee... kwa mazingara yetu sisi wote woga wa wachawi!
 
1233817141_mwizi3.jpg


1233817141_mwizi2.jpg


"Kwa mfano eneo letu vibaka ni wengi sana, watu wanaibiwa kila siku na wahusika wanakamatwa lakini siku mbili wanaonekana tena mitaani, ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mkononi," alisema Hamis Juma.

..safi sana, funzo tosha kwa vibaka wengine na wanaotamani kuuwa albinos, ala! ...angalia mfano huyu kibaka aliyekuwa roasted wakati akijaribu kuiba nyaya za umeme, anastahiki huruma gani huyu?

...angalau basi wangekuwa wanawapa japo nusu-kaputi kabla ya kuwanyofoa viungo hao Albino lakini wapi!... nao wanastahili mob-lynching kama huyo kibaka hapo juu!
 
Kama baadhi ya wabongo wana hasira kweli na kuibiwa basi wangewachoma moto na kuwaua majambazi halisi nchini mwetu ambao ni MAFISADI. Huu ni unyama wa hali ya juu wanaowafanyia raia wengine kisa tu mtu kaiba mbuzi au cell phone. Kama ni wajanja kweli wakawatafute kina Mramba, Yona , Chenge, Mkapa, Liyumba NA MAFISADI wengine wote na kuwachoma moto mpaka kuwaua...

...kuna watu aina tatu;

kuna wale kazi yao kunadia, "mwizi huyooo, mwiziii!"

kundi la pili, wenyewe wanakurupuka na kufukuza mpaka wamkamate

kundi la mwisho, wao wanatoa kipondo, kibano nk...mpaka kieleweke!

UFISADI nchini, waheshimiwa kina Dr. Slaa nk weshanadi "Wezi haoooo..."

JF kama kawaida watu wamekurupuka kufukuza,...

nenda pale kisutu uone kundi la tatu!... hukusikia Mkapa alivyopopolewa mawe mpaka waheshimiwa wakaingilia? tuombe amani, lakini kesi za hao waheshimiwa wote zikifa hivi hivi tu, sidhani kama patakuwa tena na simile!
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu unajua unanishangaza sana...Hivi kweli wewe unaona picha hii ni jambo la kawaida kwa sababu yanatokea kila siku?..

Mzee unaniwekea maneno kinywani; kwenye jibu langu kwako nimesema hivi kuhusu hizo picha:



Sasa sijui wapi umeona nimesema au kuashiria kuwa hili "hii picha ni jambo la kawaida kwa sababu yanatokea kila siku"? Nitakuwa ninajipinga, kwani kama ninaona ni jambo la kawaida, why bother even bringing it to attention of more people? It'll defeat the purpose.

.umeshindwa kabisa kujiuliza maswali mengi kama alofanya Fundi Mchundo kutokana na picha hiyo badala yake unazungumzia kuvunja katiba isiyomsaidia mwananchi kitu chochote..

Sijui kama "nimeshindwa kabisa". Kuna maswali yanayoulizwa kwa maandishi na maswali yanayoashiriwa kwa picha. Tunajadiliana hapa kwa sababu nimefanikiwa watu kuhoji kile wanachokiona. Maswali yangu yanabakia pale pale kuwa hili ambalo tunaona "ni la kila siku" linapopata baraka ya Waziri Mkuu linatisha kuliko watu wanavyofikiria.

Nikisimama na kuangalia picha hiyo na kusikitika haitoshi. Siyo mimi wala wewe anayeweza kumsaidia huyo ndugu yetu aliyeuawa kishenzi hivyo. Hata hivyo tunaweza kuzuia mtu mwingine kuuawa namna hiyo. Hilo ndilo lengo langu katika mjadala huu. Sasa mtu anaweza akasikitika na kujisikia vibaya kuhusu picha hiyo lakini hilo halitoshi isipokuwa kuonesha utayari pia wa kuzuia jambo kama hilo kurudiwa tena.

Kwa kauli ya Pinda uwezekano wa matukio kama haya kutokea tena ni mkubwa kwani serikali imesema wananchi wachukue sheria mikononi wasisubiri mahakama!

Yaani wewe unakubali watu kama hawa waendelee kuyafanya wanayoyafanya nje ya katiba lakinim sio Waziri mkuu kusema kile mnachozoea kukifanya..

Nikikubali hivyo nitakuwa sina sababu ya kumpinga Waziri Mkuu, kwani kama Waziri Mkuu hawezi kuamuru kitu nje ya Katiba iweje tena nikubali Mtanzania kama huyo auawe nje ya Katiba? Ni ile ile contradiction, and I don't like contradiction.

Labda nirudie hapa, mauaji ya mtu huyo hayastahili, hayana sababu, na wale waliofanya vitendo hivi wanastahili kuchukuliwa hatua zote. Lakini zaidi ni watu wote wanaotengeneza mazingira ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao kama alivyofanya Waziri Mkuu. Siungi uvunjaji wa sheria uwe wa Waziri Mkuu au wa mtu mtaani. Hakuna aliyejuu ya sheria.

ukasahau kwamba yeye ni relfection yako..

Huo msemo hauna ukweli kwa sababua ngekuwa reflection yangu angetetea Katiba au kupinga mauaji ya watu nje ya sheria. So, anaweza kureflect Watanzania wengine, lakini hanireflect mimi.
Mkuu wangu mimi sifikirii kabisa swala la mchawi kuawa kama huyu bali nafikiria hao Albino na huyu jamaa ambao tayari wamekwisha poteza roho zao kwa vitendo ambavyo ni pinzani na katiba...

Unaona wewe umesema "mchawi kuuawa" hilo hulifikirii (ina maana akiuawa mtu anayedaiwa ni mchawi haikusumbui)! lakini unasema akiuawa albino au huyu jamaa ndiyo unafikiria. Well, hapo ndiyo ninatofautiana na wewe.

Wakati wameuawa "majambazi" kule Kilimanjaro chini ya mikono ya Polisi nilisimama kama peke yangu kutaka uchunguzi ufanyike kwani taarifa zote zilionesha kuwa waliuawa execution style. Watu wakanipinga kwa sababu waliouawa ni Majambazi!

Hiyo tofauti mimi sina. Kwangu mimi mchawi, albino, mwizi wa kuku, n.k wote kwanza kabisa ni wanadamu. Hivyo napinga kabisa mauaji ya mwanadamu mmoja chini ya mikononi ya mwanadamu mwingine. Kuna exception mbili tu ambapo mauaji naweza kuyakubali. Yamefanywa kama kujikinga (aidha vitani, polisi, n.k kwa mujibu wa sheria za upiganaji) na pili kutekeleza hukumu halali ya mahakama. Nje ya hapo, mtu anayeitwa mchawi, ana haki ya kuishi kama vile kikongwe na albino aliyonayo.
Wananchi wamechoka kuishi ktk maisha ya woga na ndio maana wamechukua sheria mikononi mwao kwa sababu serikali imeshindwa kuwalinda..

Hiyo ndiyo pointi yangu pia, lakini kama wameshindwa maana yake wachukue sheria mikononi? Kama jibu ni ndiyo, kwanini tunajisikia vibaya kuhusu hii picha? Hapana, tatizo la usimamizi wa sheria ni kubwa mno na ni jukumu letu kuhakikisha hilo linafanyika.

Na hao Albino ni matokeo pia ya serikali kushindwa kuwalinda...hawa wote ni victims wa sheria butu na utamaduni mchafu ambao tunaujenga sisi wenyewe... kama alivyosema Fundi Mchundo hapo kuna watoto wadogo kabisa wakiona jinsi huyo mwizi akiuawa, haya picha hiyo nyingine hata Mbwa amekaa na huzuni, binadamu anapita akichukua picha tu.. Hii inadhihirisha wazi sisi ni watu wa aina gani...

Samahani mimi siko kwenye kundi la watu wa aina hiyo. Wapo watu wanaoona ni bora kukaa kimya mbele ya adversity kama hiyo mimi sipo hivyo. Siwezi kukaa na kuona mtu anauawa na mimi napiga picha, naangalia au nashuhudia bila kufanya kitu. Siwezi. WEngine wanaweza.

Nitashukuiru sana kama utafikisha ujumbe huu kwa waziri wa mambo ya ndani na vyombo vya Usalama nchini, bunge na pengine hata kwa rais ambaye anachukulia maswala haya YOTE kwa uzito mdogo sana.
.

Mzee, hili ni jukumu letu wote. Sisi wengine tunaongeza chumvi tu lakini sisi sote tunaweza. Kama Watanzania wakishika simu na kumpigia simu WAziri wa Mambo ya Ndani, Rais, Waziri Mkuu n.k wanaweza kujua nini kinaendelea. Lakini guess what, watu hawatafanya hivyo. Hawatathubutu kufanya hivyo. Sijui ni kwanini?

Nitakuomba tena jaribu kujenga ujumbe wapo na kuelekeza nguvu zako ktk kuondoa mauaji kama haya iwe Albino au wezi kwani sheria ni msumeno..unakata pande zote isiwe OK kuuawa kwa Albino lakini watuhumiwa hadi sheria itumike..
Let's stop the kilings za hawa watu kwanza kisha ndio tuta worry kuhusiana na katiba.
.

Hatuwezi kusimamisha mauaji haya nje ya Katiba, period.

tuweke nguvu zetu ktk kusisitiza serikali na vyombo vyote vya haki za dunia kutupia jicho mauaji kama haya ili viongozi wetu wapate kuwajibika...

Hawawezi kuwajibika nje ya sheria.

Je, sio sisi tuliokuwa tunaunga mkono Israel inayoyafanya huko Palestina mbona hatuombi sheria itumike!..

Sakata la Palestina mimi sikulitolea maoni. Hivyo sijui kwa kweli ni nani aliunga mkono mambo ambayo Israeli ilikuwa inafanya au mambo ambayo Hamas ilikuwa inayafanya.


tunajenga hoja kwamba mchokoizi ni nani na nani mwenye haki ya kujilinda tena tunaipa hata sharia kikatiba leo Pinda kusema tu wauaji nao wauawe imekuwa swala la kukamatia kiasi hiki mkuu wangu..

Sina la kusema kwenye hilo kwani sikutoa hoja yoyote kuhusu suala la Palestina na Israeli. Nitaawacha wengine waliofanya hivyo wajibu.


terrorist wanauawa na viongozi wa nchi zote za magharibi wametuma majeshi yao kuua hawa terrorist iweje tuone haki matendo kama hayo lakini sio usemi wa Waziri wetu mkuu inapofikia swala la wachawi au kwa sababu hawa ni ndugu na jamaa zetu..

Waziri Mkuu wetu ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siyo wa Israeli au Palestina. NInajali yanayotokea Tanzania, haya mengine ya kimataifa nayaweka kwenye maudhui yake. Siwezi kumlalamikia Omert wala Abbas wala kutaka wao wawajibike. Ni jukumu la watu wao kufanya hivyo. Mimi wa kwangu ni Lowassa, Idris, Kikwete, Chenge n.k !
Mkuu hawa wachawi na watu wote wenye imani za kichawi ni home grown Terrorist,

No sir.. mchawi ni terrorist!? That is a leap I'll not dare to attempt. Kwa sababu kuliko Shinyanga wanasema wazee vikongwe wenye macho mekundu ndiyo wachawi, nikikubali hoja yako kuwa wachawi ndiyo homegrown terrorists nitakubali kuwa vikongwe =>Wachawi=>terrorists.. No sir I DO NOT AGREE.

now how to deal with them ni shangamoto nalotaka sana kulisikia badala ya hizi habari za Pinda wakati Albino wanaendelea kufa kila siku...

Nimeshatoa mapendekezo yangu, na jana nimepata confirmation yamefika na yameanza kufanyiwa kazi. Bado nafikiria kushiriki kwa namna nyingine zaidi lakini vyovyote ilivyo siko tayari kuacha sheria au Katiba ipuuzwe au kuchezewa kana kwamba is optional.

Samahani mkuu wangu unajua inaniuma sana kuona picha kama hizi kwa sababu ni kitu kinachotokea kweli.. sifikirii kesho itakuwa vipi kutokana na maneno ya Pinda kwani ombi lake yawezekana kabisa isitokee... kwa mazingara yetu sisi wote woga wa wachawi!

Sidhani kama wote ni woga wa wachawi. Mimi siogopi wachawi, sitetemeki mbele yao na hakuna lolote wanaloweza kufanya kwa kutumia ndumba na tunguri zao kunidhuru mimi. Hivyo wengine wanaogopa mimi siwaogopi kwani sina sababu ya kuwaogopa. And believe me, I know what I'm talking about.
 
[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3499&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3500&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3501&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3502&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3503&stc=1&d=1233899436[/media]
 

Attachments

  • mob violence1.JPG
    mob violence1.JPG
    25.9 KB · Views: 101
  • mob violence2.JPG
    mob violence2.JPG
    17.9 KB · Views: 90
  • mob violence3.JPG
    mob violence3.JPG
    22.8 KB · Views: 98
  • mob violence4.JPG
    mob violence4.JPG
    18.7 KB · Views: 103
  • mob violence5.JPG
    mob violence5.JPG
    21.1 KB · Views: 92
[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3499&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3500&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3501&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3502&stc=1&d=1233899436[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3503&stc=1&d=1233899436[/media]

hiki ndio anataka Pinda
 
NB:
Naamini Waziri Mkuu alimaanisha kitu kama hiki. Ingawa kwenye kesi za wizi wa "mbuzi" adhabu ya kifo namna hii ni kitu cha kulaaniwa, nina uhakika kama jamii tuko tayari kuona wauaji wa albino wakipewa kibano namna hii na kuuawa papo hapo.

Kwa vile serikali imetoa kinga kwa wananchi kuchukua sheria mikononi, tusishangae kuona picha za namna hii zikidai kuwa "x ni muuaji wa albino". Waziri Mkuu ambaye alilia kuona mauaji ya albino sijui anaweza kujisikia vipi watu wakianza kutiwa moto, kupata kipigo namna hii kwa kisingizio cha "kutekeleza agizo la serikali".

Mkjj,
This is a spin!!
Do u actually believe PM meant what you've put here? I heard what he said in the parliament and that was what he meant!! Unless unataka kusema he lied to the Parliament and citizens of Tanzania as whole!!
 
Mkjj,
This is a spin!!
Do u actually believe PM meant what you've put here? I heard what he said in the parliament and that was what he meant!! Unless unataka kusema he lied to the Parliament and citizens of Tanzania as whole!!

I know what you heard, because I heard it too and you can go and hear it again.. but you didn't listen to what he said!
 
Mzee Mwanakijiji,
Serikali yetu toka wakati wa Mkapa ilishindwa kabisa kuwalinda wananchi wake. Ilifikia hadi vibaka wanaua watu kama hukuwaachia kitu... wazxi wazi kabisa walichukua kitu chako na kama ukitaka wakurudishie ni lazima ukikomboe kwa bei watakayokupa wewe..
!
mkuu umenena, vibaka/wezi wanatesa sana TZ

majuzi vibaka walikomba karibu kila kitu ktk gari yangu... Katika kufuatilia watu wakaniambia niwahi 'GEREZANI' kabla havijauzwa!....Nilikwenda na kuvikuta vifaa vyote na kuvinunua tena! cha ajabu polisi wafahamu....
 
Tatizo la wananchi kujichukulia hatua wenyewe haliwezi kuondoka au kuondolewa ,hasa kwa mazingira yetu ya kimasikini,mtu analima kuanzia asubuhi hadi jioni ,anapalilia inakaribia kuvuna ,vibaka wanawahi na kuondoka na mazao,hivi utamshauri kitu gani mkulima ?

Masikini ana mbusi au ngombe,kwa ujumla ana mifugo yake ambayo anaitegemea katika kumpatia kipato cha kumuendeleza katika maisha yake ya kila siku pamoja na familia yake ,anatokea kibaka anakwiba mfugo mmoja mmoja kila siku ,unafikiri mfugaji hasira zake zikoje hapo ?

La mwisho ambalo linazidisha hasira maradufu ni baada ya kibaka kukamatwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ,baada ya mwezi unamkuta kibaka akipita mitaani tena chini ya nyumba yako huku anakuangalia na kuchekelea ,utajihisi vipi ? Yaani amekuibia na umemkamata na kumpleka mbele lakini unamwona bado anapeta mitaani.

La kuongezea mmemkamata kibaka ndani ya nyumba na alikuwa ameingia kwa ama zake ama zenu yaani kibaka yupo tayari kuua ikiwa mtamletea ubishi lakini mmemshinda nguvu japo mmoja wapo amejeruhiwa panga la kichwa na kumpeleka kwenye vyombo vya sheria,siku ya pili mnamuona yupo uraiani ,Unafikiria mara ya pili kutakuwa na uvumilivu wa kumpeleka mahakamani ?

Hivyo kuwashughulikia wezi uraiani na kuwasulubu hadi kuwaua ni jambo nature haliwezi kabisa kukomeshwa ila kukomeshwa kwake ni kwa raia kuachwa kama walivyo bila ya kuungwa mkono na chombo au mtu yeyote wa serikalini ,Serikali iendelee kukemea tu na si vinginevyo.
 
I know what you heard, because I heard it too and you can go and hear it again.. but you didn't listen to what he said!

Then you better of not listen to what he said at first!!! Why are we trying to make issues out of no issue??

I think its time we start talking about food shortage, poor infrastructure and the sort rather than putting photos of the dead to make an issue in a statement made by one leader when he was trying to be symphathetic with the deceased!!!

Damn Mkjj i know you are a good analyst you can do better if you put focus in your way of thinking!! look around and make other peoples lives worth living!!

For now I stick to what PM said at the Bunge and you are in no place to convince me otherwise unless you have a better idea on what you are trying to portray here!!

I now believe the saying that goes like "If you read News you are miss informed and if you dont read the news you are un-informed" I stand neutral to what media writes.
 
Mimi naona mila zetu za kiafrika hasa tanzania bado tunahitaji muamko katika kujua haki ya msingi ya mtu ya kuishi,kutoa roho ya mtu eti kaiba mbuzi is not a logic,isitoshe kama mdau mwenzangu alivyosema inawezekana tu mtu mmoja kakurupuka na kusema mwiziiii..kitendo kinachopelekea kushambuliwa hadi kufa hata kama si kwili, JAMANI TUBADILIKE
 
No they won't! Unafikiri katika mbingu hii ni wewe tu na wengine wanaojua ubaya wa kuibiwa? Kama kuna tatizo la sheria maana yake ni kuwa kuna tatizo la serikali. Na kama ni serikali ni viongozi walioko madarakani. Unabadilisha uongozi madarakani kwa kura na kuchagua watu unaofikiri watasimamia sheria.

Kusema utekelezaji wa sheria ni mbaya halafu kila uchaguzi mnarudi kuwachagua watu wale wale mnatarajia nini? Chenge kaoneshwa kavunja sheria guess what.. kapewa Uwaziri mara mbili!

Fikiria Dr. Idris kavunja sheria akazawadiwa ukurugenzi na hata alipotaja kujiuzulul akabembelezwa abakie! Sasa tatizo siyo kwamba sheria ni mbaya au hazisimamiwi, tatizo ni kuwa watu wamezoea ubovu mno, kwani hao hao wenye kukurupuka na viberiti na mafuta ndiyo hao hao kesho wanaimba CCM nambari wani!

Mwanakijiji,

I guess we now share the same sentiment.

Umekiri kabisa kwamba katika nchi yetu, utawala wa sheria haufanyi kazi. Na kama unafanya kazi, basi ni kwa watu wachache sana, tena wale "vidagaa". "Makambale" wataendelea kupeta milele daima. Hali hii sasa ndio inapelekea wananchi kuona kwamba namna ya kukomesha wizi na ujambazi ni kujichukulia sheria mkononi.

You will agree with me kwamba we are not living in a Utopian world. This is th real world. You get what you see. Na kwa Tanzania, utawala wa sheria hauzingatiwi. Wananchi wana kila haki ya "self defense". Kabla kibaka hajaja kukudhuru na wewe, muwahi kabla. Kama kamuibia jirani yako leo, ataiba na kwako kesho. Ukiona mwenzako ananyolewa, tia maji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom