Mfano wa unyama utokeao kama utekelezaji wa lililokuwa agizo la Mh. Pinda (Graphic)

Mzee Mwanakijiji,
Sioni furaha yeyote katika kuangalia picha hiyo bali kitisho ya nini kinawezekana. Hebu fikiria kama huyo mtu hapo angekuwa anadaiwa kuwa ni muuaji wa albino na wananchi wamemkamata na kumpa kibano? Kwa wengine hilo "anastahili" but what if people are wrong!?[/

Mkuu labda bado hujanielewa...
Nachosema mimi kwa nini wewe unafikiria kile kinachowezekana kutokea wakati mambo haya ya kuua albimo na vibaka yanatokea hadi hivi sasa tunapoongea yasipewe umuhimu zaidi!..
Na n8imekwambia huko nyuma wewe fikiria hizo picha ni Albino ambaye anapigwa hivyo na kisha wanamkata viungo vyake,,, fFikiria huyo jamaa anayeuawa kwa sababu kaiba mbuzi iwe somo la kuanziwa ikiwa kweli unaitafuta haki..
Watu wa kwamza kabisa kuwauliza ni Usalama kisha waziri wa mambo ya ndani, waziri mkuu, bunge na hata rais wetu kwa matukioa kama haya kwa nini serikali inashiondwa kuwalinda wananchi wake..
Kama sheria itaweza kusimama ndio mwisho wa yote haya na hata kauli ya Pinda haiwezi kuwa na maana yoyote...Na kutokkana na imani za mazingara yetu huwezi kunambia kitu ikiwa ndugu yangu Albino ameuawa kwa sababu ya imani za kichawi... na siwezi kuona malipo ya haki zaidi ya wewe pia kuawa..
Lets' stop the killings kwanza mkuu wangu haya ya Pinda wakati ni serikali nzima inashindwa kazi... nadhani ndio yanaturudisha sana nyuma... Tuombe vitendo na kuwajibika kwa serikali badala ya kufikiria sana nini kimesemwa..Apology inaweza kupokewa lakini sidhani kama kuna mtu anaweza kuelewa kwa nini Albino wanauawa!
 
Mzee Mwanakijiji,


Mkuu labda bado hujanielewa...
Nachosema mimi kwa nini wewe unafikiria kile kinachowezekana kutokea wakati mambo haya ya kuua albimo na vibaka yanatokea hadi hivi sasa tunapoongea yasipewe umuhimu zaidi!..
Na n8imekwambia huko nyuma wewe fikiria hizo picha ni Albino ambaye anapigwa hivyo na kisha wanamkata viungo vyake,,, fFikiria huyo jamaa anayeuawa kwa sababu kaiba mbuzi iwe somo la kuanziwa ikiwa kweli unaitafuta haki..
Watu wa kwamza kabisa kuwauliza ni Usalama kisha waziri wa mambo ya ndani, waziri mkuu, bunge na hata rais wetu kwa matukioa kama haya kwa nini serikali inashiondwa kuwalinda wananchi wake..
Kama sheria itaweza kusimama ndio mwisho wa yote haya na hata kauli ya Pinda haiwezi kuwa na maana yoyote...Na kutokkana na imani za mazingara yetu huwezi kunambia kitu ikiwa ndugu yangu Albino ameuawa kwa sababu ya imani za kichawi... na siwezi kuona malipo ya haki zaidi ya wewe pia kuawa..
Lets' stop the killings kwanza mkuu wangu haya ya Pinda wakati ni serikali nzima inashindwa kazi... nadhani ndio yanaturudisha sana nyuma... Tuombe vitendo na kuwajibika kwa serikali badala ya kufikiria sana nini kimesemwa..Apology inaweza kupokewa lakini sidhani kama kuna mtu anaweza kuelewa kwa nini Albino wanauawa!


Mkandara, ninachosema mauaji ya Albino hayawezi kuzimwa nje ya sheria. Hiyo ndiyo tofauti yangu na wewe na hata Waziri Mkuu. Kusema kwamba tukomeshe mauaji ya albino ndipo tuangalie sheria haiwezekani ni sawa na kuweka mkokoteni mbele na farasi nyuma.

Maneno yana nguvu kuliko vitendo. NI maneno yaliyochochea vita ya dunia ya pili, ni maneno yaliyochangia sana mauaji ya Rwanda, ni maneno yanayoongeza moto wa ugomvi mashariki ya kati n.k. Bila kujua matumizi ya maneno na nguvu yake tutafanya makosa yale yale. Waziri Mkuu anaposema "wauawe papo hapo" siyo kwamba ni 'maneno madogo tu' na ya kupuuzia. Ni maneno mazito hasa kwenye jamii ambayo tayari is inclined towards mob justices.

Sihitaji apology kutoka kwa Waziri Mkuu nashangaa watu walitaka aombe msamaha! Mimi nilitaka ayafute na aitishe utawala wa sheria na atilie mkazo kuwa sheria zetu zinasimamiwa sawia, kwa haraka na inavyopaswa. Hajafanya hivyo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkandara, ninachosema mauaji ya Albino hayawezi kuzimwa nje ya sheria. Hiyo ndiyo tofauti yangu na wewe na hata Waziri Mkuu. Kusema kwamba tukomeshe mauaji ya albino ndipo tuangalie sheria haiwezekani ni sawa na kuweka mkokoteni mbele na farasi nyuma.
Mkuu nadhani wewe ndiye unaweka mkokoteni mbele ya farasi...
Mauaji ya Rwanda yalitokana na Ubaguzi wa muda mrefu kati ya makabila mawili - Wahutu na Watusi ktk ardhi ndogo, hayo maneno ni kichombezo tu kinachofuata nyuma kama huo mkokoteni..
Mashariki ya kati pia ni ubaguzi kati yao wakipigania ardhi ndogo ambayo kila mmoja wao anadai ni yake.. maneno yanafuata kama sababu tu, ni sawa na sisi hapa tunabishana kwa maneno lakini issue iliyopo ni mauaji ya Albino. Kama haya wauaji hasingekuwepo mimi na wewe tusingechukua muda hapa kuyazungumziawala tusingemsikia Pinda..

Na kutokana na maneno ya uchocheaji ndiyo maana nikauliza kama wewe na Pinda mna kitu kingine nje ya hoja hii kwa sababu sioni kabisa sababu ya uchochezi unaojaribu kuupandikiza ikiwa hakuna sababu iliyotangulia.. Siwezi kukuita wewe ni mchochezi au kujaribu kufikiria nini matokeo ya hoja zako kwa sababu nina hakika kuna kitu kilichotangulia kabla...Hata kama Pinda ataomba samahani bado hutakubali, Na ili kupata uhakika zaidi nilikuuliza kihsa ni kakubali uliposema kwamba Unachukizwa na Pinda kushindwa kuwalinda Albino..Hiyo pekee ilitosha kabisa lakini hoja ulizoendelea kuzijenga zilikuwa nje kabisa ya sababu kubwa!..


Mkuu wangu hizi sheria na sijui katiba ni upuuzi mtupu kwangu mimi kwa sababu ni Katiba hiyo hiyo inayomlinda Mkapa.. Ni katiba hiyo hiyo inayo wanyima haki vyama vya Upinzani na ni katiba hiyo hiyo inayoshindwa kuwa protect Albino kisheria wakati katiba hiyo inaweza kuwa protect Vifaru,Tembo n.k..tena tumeweka askari wenye bunduki na risasi za moto dhidi ya wawindaji wenye pinde na mishale..Mkuu siwezi kabisa kuitazama katiba kwa maneno ya Pinda isipokuwa nitaitazama katiba na sheria zetu kwa nini zimeshindwa kuwalinda Albino..Na Pinda, Masha na Said Mwema wajiuzuru kwa sababu wameshindwa kazi yao kuwalinda raia wao.

Muuaji yeyote wa hawa Albino anatumia silaha - iwe kisu, rungu au mkuki yaani ni it's a premeditated murder isiyo ya kawaida kwani sijui ni psychological feature gani zina arouse desire zao za utajiri...ila nachoweza kusema ni kwamba hawa jamaa wanapotoka kuwinda Albino wako vitani, kama wanyama vile Predators, hivyo nasi tuangalie zaidi ni jinsi gani tunaweza kuwalinda Albino kabla ya sheria.
Majeshi ya marekani yapo huko Iraq na Afghanstan wanapenda sana watumie sheria na katiba lakini wanajua wanapambana na watu wa aina gani hivyo wao pia wanajiandaa na silaha za kuteketeza.Kama adui atasalimu amri au kukamatwa ndio sheria inafuata lakini kabla ya hapo ni vita tu!..

Hivi kweli ktk akili yako unafikiri unaweza kuwakamata hawa watu kirahisi kiasi kwamba uwafikishe mbele ya sheria kama vile kibaka wa mtaani anayeiba simu na kutoka mkuku..Hatuwezi kuzuia wizi nchini wala nchi za nje ni kitu ambacho kitaendelea kila siku ya maisha yetu na ndio maana tunaunda sheria kali na hukumu zake dhidi ya crimes kama hizi, lakini mauaji ya Albino ni beyond vitu vyote hivi -tumevuta mipaka ya Utu na hakika mauaji haya yanaweza kabisa kukomeshwa!..

Nakumbuka JK alipoingia madarakani kitu cha kwanza ilikuwa kukomesha majambazi, na hakika bila kauli wameuawa wengi sana, wenye bahati ndio wameipata sheria, nadhani unakumbuka wale Wakenya na yuile mama mfanyabiashara waliouawa Moshi..Toka siku ile majambazi wameingia mitini..Kwa hiyo maneno sii lazima kuchochea bali inaweza kabisa kuondoa magugu ktk shamba la ngano...

Mkuu wangu tusijidanganye, wanaoua Albino sii wachawi, ni watu wazima wenye akili zao timamu kwa hiyo wanaua sii kwa kutumia mitulinga ya uchawi ila wanatumia silaha na kibaya zaidi hao Albino sasa hivi ni sawa na Endangered spicies - samahani kwa kutumia lugha hiyo. Muhimu nakuomba unielewe kwamba nachosisitiza mimi ni kuweka nguvu zetu ktk kuwalinda watu hawa kabla hatujafikiria nje ya rai ya Mh. Pinda...
Mkuu Pinda kachemsha politically..hakutakiwa kusema aliyosema lakini binafsi vita dhidi ya wauaji wa Albino ni vita ya kufa na kupona..Ama zao ama zetu!
 
Last edited:
Tuliua wenye vipara. Tulichuna ngozi watu. Tuliua watu kwa kuamini kuwa wametunyonya damu. Tuliua vikonge kwa imani kuwa wana macho mekundu kutokana na kunywa damu za watu. Tuliua bibi vizee waliokutwa wakiranda watupu kwa imani kuwa ni wanga. Haya ya albino ni mwendelezo wa mauaji ya aina hii. Tofauti ni kuwa dunia inatusuta na sisi tunajifanya kuona aibu. Hatuwezi kuvunja katiba kutokana na jambo ambalo halitufurahishi. Hivi wangapi ambao wanaweza kuuawa bila hatia kutokana na statement kama hiyo? Kitu gani kitakachomzuia albino (tusisahau kuwa nao ni binadamu) kumsingizia mtu mwenye ubaya nae kuwa anapiga dili ya viungo vyake? Kitu gani kitakachozuia watu kumwadhibu mtu ambae kwa nia nzuri akaonekana yuko karibu na albino? Kitu gani kitamzuia mtu aliyeoa au mwenye uhusiano na albino kumsingizia mshindani wake wa mapenzi kuwa ana nyemelea viungo vya mke au girlfriend wake?

Kwenye hili, niko na Mzee Mwenyekijiji. Tuendeleze elimu na tuhakikishe kuwa sheria na katiba ( pamoja na mapungufu yake) inalindwa kwa wale wote waishio ndani ya mipaka ya nchi yetu!

Amandla...........
 
Last edited:
Fundi Mchundo,
Tuliua wenye vipara. Tulichuna ngozi watu. Tuliua watu kwa kuamini kuwa wametunyonya damu. Tuliua vikonge kwa imani kuwa wana macho mekundu kutokana na kunywa damu za watu. Tuliua bibi vizee waliokutwa wakiranda watupu kwa imani kuwa ni wanga. Haya ya albino ni mwendelezo wa mauaji ya aina hii. Tofauti ni kuwa dunia inatusuta na sisi tunajifanya kuona aibu. Hatuwezi kuvunja katiba kutokana na jambo ambalo halitufurahishi. wangapi ambao wanaweza kuuawa bila hatia Hivi kutokana na statement kama hiyo?
Mkuu nakuomba unambie hao watu wenye vipara waliochunwa ngozi, mumiani, vikonge na wenye macho mekundu waliuawa kwa kosa gani?...Je, hii katiba inasema hawa wanaweza kuuawa lakini sio wale wanaotenda mauaji?...sidhani.
Katiba ni sheria,i lazima ziwe wazi kuwa wenye kuua watu hawa ni lazima wao pia wauawe, kupitia kortini ni ktk utaratibu wa kisheria kuhakikisha haki hiyo inasimama kama watakamatwa...
Nimesema hawa wote wanaoua wako vitani na sisi ni lazima tuingie vitani, wakijisalimisha tutawapa haki ya katiba wakiendelea na matendo yao tutawafuata kwa nguvu zote... Huu ndio msimamo wangu. 9/11 walikufa watu na Marekani ilipeleka majeshi yake kuwasaka wauaji tena kwa shangwe na vifijo dunia nzima mmeshangilia..
Mimi sioni tofauti kabisa kama tunaweza kuwapa kinga Tembo na kweli wapo watu wameuawa kwa makosa vile vile...lakini kinachofahamika kwa wananchi ni kwamba kuwinda Tembo kwa sababu ya ivory ni kutafuta kifo, mauaji ya Tembo yamepungua kabisa...Je, tunashindwa nini kuwalinda binadamu wenzetu.

Leo umefikia kusema Albino wanaweza kumsingizia mtu na kadhalika ukionyesha wazi jinsi unavyoweza kutetea watu wa mfano wako.. leo Albino wamekuwa kundi jingine kabisa ambalo kufa kwao sio deal isipokuwa tetesi tu ya kifo chenu kinawekewa kinga ya katiba..

Unajua mkuu kutokana na mawazo haya, naanza kujiuliza, hivi ni wangapi kati yetu sisi tulijumuika na hao Albino katika maandamano ya kupinga mauaji yao?... kuna viongozi gani wa serikali na vyama tawala na vya Upinzani walikuwa bega kwa bega na Albino ktk maandamano yale!....sikumbuki support kubwa zaidi ya picha na maneno mengi ya huruma ambayo hayakuondoa wala kupunguza wauaji yao. Tulikuwa kama tunawang'ong'a kwa pemmbeni, picha nyingi na kuuza magazeti lakini mioyo yetu haikuwa wakweli.
sidhani kama tuliwapa support wala uzito swala zima la mauaji yao na nduio maana tunajenga hoja za wao wachukuliwe na mataifa mengine kupewa hifadhi kama vile wao hawana haki na nchi hii isipokuwa ni mzigo kwetu..

Kutumia statemnent ya Pinda ni cheap shot kabisa lakini ukweli unajionyesha wazi kuwa we don't give a damn!.. Ndivyo tulivyo!.. swala la kuua Albino, wenye vipara, vizee na imani za uchawi ni mwendelezo ktk evolution yetu lakini kuuawa kwa wenye kuua inatia shaka kikatiba...
 
Last edited:
Mkandara, I support stand yako kwa sababu unataka kuprotect Albino wasiuawe, which I believe watu wote humu ndani tuna stand hiyo hiyo.

Sasa unapogeuka na kusema watu wanaoua Albino wauawe hapo ndio makosa yanapoweza kutokea sababu unahalalisha mauaji ya watu bila kufuata sheria yaani ikisemekana mtu fulani ni muuaji wa Albino bila proof au uhakika mob justice itamuua, Huoni kuwa hapa italeta revenge na mauaji yasiyo na ulazima???

Je mtu unayemfahamu ambaye hana hatia kabisa na mauaji ya Albino wazushi wakisema tu na yeye ni muuaji akiuawa, itakuwa vipi??? Si uadui kati ya ndugu zake na Maalbino utaongezeka??

Dawa ni kufuata sheria kwa ukali wa ajabu, yaani watu wakamatwe, wapelekwe mahakamani na sheria ifuatwe ( tunaweza hata kuunda special Police force na mahakama moja ikatengwa kufast track hii issue) ili mauaji yaishe ASAP.

While we are at it, let us ALL CONDEMN ALL MOB JUSTICE KILLINGS IN TANZANIA PERIOD and anyone who attempts to kill vibaka should go to court where the full wrath of the law should befall them.

May God Bless All of Us and May we protect all Human Life.
 
Mkandara, I support stand yako kwa sababu unataka kuprotect Albino wasiuawe, which I believe watu wote humu ndani tuna stand hiyo hiyo.

Sasa unapogeuka na kusema watu wanaoua Albino wauawe hapo ndio makosa yanapoweza kutokea sababu unahalalisha mauaji ya watu bila kufuata sheria yaani ikisemekana mtu fulani ni muuaji wa Albino bila proof au uhakika mob justice itamuua, Huoni kuwa hapa italeta revenge na mauaji yasiyo na ulazima???

Je mtu unayemfahamu ambaye hana hatia kabisa na mauaji ya Albino wazushi wakisema tu na yeye ni muuaji akiuawa, itakuwa vipi??? Si uadui kati ya ndugu zake na Maalbino utaongezeka??

Dawa ni kufuata sheria kwa ukali wa ajabu, yaani watu wakamatwe, wapelekwe mahakamani na sheria ifuatwe ( tunaweza hata kuunda special Police force na mahakama moja ikatengwa kufast track hii issue) ili mauaji yaishe ASAP.

While we are at it, let us ALL CONDEMN ALL MOB JUSTICE KILLINGS IN TANZANIA PERIOD and anyone who attempts to kill vibaka should go to court where the full wrath of the law should befall them.

May God Bless All of Us and May we protect all Human Life.

Sounds good to me....
 
Moelex23,
Mkuu maneno yangu na ya Pinda yanasimamia lugha ya wazi tu.. Hakuna tofauti na sheria yenyewe kwani inasema kunyongwa, kupigwa risasi na hata kuchomwa sindano yote haya ni kuua vile vile..wapo waliokufa bila hatia kutokana na utekelezaji mbaya wa sheria..
Kinachowapa taabu ni maneno yetu kutangulia sheria lakini tunashindwa kutanguliza kuitazama sheria kuwa imejengwa ili ku PROTECT watu wote..tukianza na hao Albino, hakuna sheria inayowapa haki sawa na sisi na ndio maana maneno yetu yanasema Albino hivi ama vile..THEM - THEY...na kadhalika.

Leo, hii bunge la Italia wanakaa kujadili uhuru wa mtu kujiua kutokana na kesi moja tu ya mwanamke, na wapo watu wanaokubali mgonjwa huyo ajimalize na wengine wanasema sio haki, hivyo maneno yanayotangulia sheria haina maana ndiyo sheria yenyewe. Na usemi huo hakuna mahala nimesoma kuwa Pinda kasema wauawe bila proof isipokuwa wanaoua Albino nao wauawe! na hakuna kifungu cha katiba kinachopinga hukumu ya kifo. Haya mengine mnaongezea wenyewe kutokana na statement yake tu..huwezi kuua Albino kama hakuna proof sasa huyo mtu atakuwa ameua vipi?..

Hakuna mahala Pinda kasema wazushi pia wauawe hizi ni hisia zetu lakini ukweli ni kwamba sheria zote zinatungwa kutokana na experience zetu za maisha.. Tunakataza yale yanayotokea sio fikra za kile kitakachoweza kutokea..Ni ktk utekelezaji wa sheria hizi ndipo tunajaribu kuepuka kuvunja sheria.. Mkuu wewe ukipania kuua kwa maneno ni kosa kubwa sana lakini uzito wake sio sawa na mtu anayetoka nyumbani kwake na kisu premeditated kwenda kuua au niseme kuwinda Albino ukasema mwacheni auwe kwanza kisha sheria itatumika..Tunachosema ni wale wanaoua Albino wauawe, meaning there must be a proof..hii ni hukumu ya maoni yetu tu kama ule usemi wa - Wanted dead or Alive, unaweza jaza kitabu cha sheria kuutafsiri.

Mkuu nakubali tena sii mara moja kwamba Pinda alichemsha kama mwanasiasa na kiongozi kusema alosema..Na kaomba radhi, lakini wananchi bado wamemshikilia ajiuzuru wakati hamna solution yoyote ya kuwasaidia Albino ambao wanazidi kuuawa..wala hampendekizi sheria ya kuwalinda isipokuwa mwaka mzima mnakuja na ya kujiuzuru kwa Pinda baada ya..hawa jamaa zetu wanaendelea kuawa tu.. Politics as usual!
Sote tulitegemea Pinda aseme - Tutawasaka na wafikishwe mahakamani, which sounds good lakini usemi huo usingeweza kuwachukua na wasio kuwa na hatia!..na hata sheria inapotumika ni hukumu gani ambayo wewe unaiona inafaa!... Usiseme wauawe kwa sababu pia wanaweza kuuawa wasiokuwa na hatia vile vile..hivyo nikitaka kubisha tu naweza bisha sana na nikaweka points zangu..hatutafika mahala popote..
Kwa mwenye kuelewa ameeelewa mkuu kuwa wale wote wanaoua Albino nao wauawe!...jino kwa jino inaweza kuwa sheria vile vile.
 
Last edited:
I'm sorry I'm to impose myself into your debate. I do not know much about Pinda, but the issue of Albino killing and mob justice is something I have read about.
This is a serious moral dilemma.
The course of the law is slow and subject to coercion in the form of bribery and cronyism.
This is not only a dilemma in TZ but also in other countries. People have gotten tired of waiting for the police and the whole judicial system to do its job, meanwhile the suspects walk in and out of remand, and continue to rob civilians with impunity and insolence.

What should people do? Mob justice or not is the question! and everyone's argument is right.
..."presumed innocent until proven guilty"...

This mob justice is rampant...in Kenya, especially Nairobi, the suspects actually run towards the police and identify themsevlves "eti afande mimi ni mwizi"...so as to get into police custody and avoid death by stoning or burning.

There are so many incidences thet are reported, but to my knowlegde i have not heard or seen anything done to rectify the notion that mob justice is dangerous and flaunts Human rights.

In this kinds of situations who is right? Do we ensure the rights of the suspects who will "walk" after giving some bribe to the police or get justice for the victim?
It is possible in a very organized system, as for our systems, God Help us.
In the quest for mob justice alot of innocent people have been lynched.
In Nairobi people have gotten so tired, all one has to say is "mwizii huyo", but also your enemy or antagonist can say the same eh?!!!
I have been fortunate enough not to have witnessed one lynching, but i have heard of incidences and they always send a chill down my spine.

but like someone said, if you have been violently robbed or violated what would you wish for the perpetrators?
 
Bantu girl.. hapa umenipa wazo moja .. let me work on that.. utawala wa sheria hauna haraka vinginevyo jamii inaweza ikajikuta inaingia kwenye tatizo jingine kabisa.. kuwa leo mtu kakamatwa, kesho kafikishwa mahakamani, keshokutwa kanyongwa... halafu wiki moja baadaye ushahidi unaonesha kuwa siyo yeye mhusika wa uhalifu..!


Ni kweli mheshimiwa...
Swala la Msingi ni utawala wa sheria na sio uharaka wa sheria. utawala wa Sheria ujali haki za binadamu na hata kama itapita miaka kumi lakini tuone haki imetendeka. Kuchelewesha kwa makusudi kutimiza haki pia ni uvunjaji wa utawala wa sheria
 
Why should we trust your crap? Kwani sisi hatuishi Tanzania kujua the causes of mob justice? Mbona wanachosema ni kile kile tu?

Mzee/Binti Zero... naona umepata kende (balls) za kuita utafiti wa wanataaluma hawa crap... Okay.. wewe kuishi Tanzania hakuondoi ukweli kuwa yaliyoandikwa hapo na hwa wanazuoni ndiyo yasababishayo hayo mauaji
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom