Dar: Wananchi Mikocheni wagomea Kituo cha Mafuta kujengwa kwenye makazi yao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Wananchi wakazi wa Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi, Kata ya Mikocheni wilayani Kinondoni Dar es Salaam wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao.

Kituo hicho kinajengwa katika Barabara ya Senga, Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi Kata ya Mikocheni.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa huo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema sheria ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi haikufuatwa kabla ya ujenzi huo.

Mwananchi huyo ambaye amejitambulisha kuwa yeye ni mtaafu serikalini, alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo, sheria inamtaka mtu anayetaka kubadilisha matumizi ya ardhi kushirikisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka matangazo eneo la wazi kwa muda wa siku 21 ili kama kuna pingamizi litolewe.
Mojaa.jpg

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (mwenye suti) kushoto akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mikocheni kuhusu madai ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika makazi ya watu.

“Haya mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika eneo hili haikutushirikisha, matangazo hayakuwekwa. Tumekuja kushtuka ujenzi umeanza.”amesema mwananchi huyo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Profesa Anna Tibaijuka amesema kituo hicho cha mafuta kinajengwa kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

“Kwanza barabara hii si barabara kuu, hii ni access road (barabara ndogo ya mtaani), huyu anajenga kituo cha mafuta, yatakuja magari maroli makubwa hapa hakuna hata nafasi, barabara hii ni finyu sana, na si eneo zuri kwa usalama na afya za wananchi ” alisema Profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka ambaye amepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kuwa suala hilo tayari wamelifikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye analishughulikia.

“Tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya ameanza kulishughulikia kwa kufika eneo kinapojengwa kituo hiki cha mafuta, tunaamini suala hili litapata ufumbuzi.”aliongeza Profesa Tibaijuka.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amekiri kupokea malalamiko hayo na wananchi wa Mikocheni.

“Kweli nilipokea malalamiko ya wananchi hao, jana nilikwenda kujionea mazingira ya kituo hicho kinachojengwa, nilichokigundua kampuni inayojenga kituo hicho inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha Baraza la Mazingira (NEMC).
Mbili.jpg

“Ni kweli nilipokea malalamiko ya kituo cha mafuta kujengwa katika makazi ya watu, jana nilikwenda (Novemba 14,2023) kujionea mwenyewe.

“Nilichokigundua ni kwamba hiyo kampuni inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha NEMC (Baraza la Mazingira), hatua inayofuata sasa ni kuangalia kama zile hatua za utoaji wa vibali hivyo ulifuatwa au kuna kilichokosewa. Baadaye nitakwenda kuwaeleeza wananchi tulikofikia”alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni.

Mmoja wa makandarasi wanaosimamia ujenzi wa Kituo hicho (jina tunalo), alipopigiwa simu kuzungumzia suala hilo, aliahidi kupiga simu baadaye. “Nitakupigia, subiri”ulisomeka ujumbe wa simu kutoka kwa mkandarasi huyo.
 
Huo ndiyo unaitwa ushirikishwaji wananchi katika mipango miji. Inatakiwa mradi au jengo tofauti na yaliyopo ktk eneo husika kukubaliwa na wakaazi.

Siyo kwa kuwa umenunua eneo basi unaweza kufanya lolote bila kujali wakaazi wa eneo hilo wanalikubali au kukataa madhumini ya matumizi ya eneo lako.
 
Ahsante Anna Tibaijuka.

Hivi ndivyo watu wenye akili ambao hawakujenga legacy nzuri wakati wa uongozi wao wanavyojisafisha na kuji redeem. Wanapostaafu wanatumia influence yao kutoa moral clarity kwenye matatizo ya kitaifa.

Ulipaza sauti uuzwaji Bandari na hapa unasimamia suala la kijamii ambalo labda wala halikuhusu saaaana kwa saab tunajua una mijengo ya kutosha kupumzikia kuanzia Bukoba mpanga Makongo, mbali na hiyo sheli. Pamoja na Sinde Warioba, Anna Tibaijuka anaingia kwenye orodha fupi ya useful elder statesman wa nchi hii.
 
Licha ya kuwa ni idea nzuri ila sioni point zao,
At the end hicho kituo kitajengwa tu,
Huwezi sema kisa ni Access road hivyo haistahili uwepo wa kituo cha mafuta, + kuhusu eneo kwani hiyo sheli itakuwa inakaa na magari all the time?

Mimi binafsi sioni kama wana point,
 
Kuna sheli ngapi zimejengwa mitaani tena ni karibu na makazi ya watu. Hao wananchi watakuwa na nongwa sio siri waache wivu wa kujinga. Kwanza maroli ya mafuta hayaji kila siku muacheni mwekezaji afanye biashara maana eneo ni lake, na nyinyi fanyeni yenu
 
Kuna sheli ngapi zimejengwa mitaani tena ni karibu na makazi ya watu. Hao wananchi watukuwa na nongwa sio siri waache wivu wa kujinga. Kwanza maroli ya mafuta hayaji kila siku muacheni mwekezaji afanye biashara maana eneo ni lake, na nyinyi fanyeni yenu
Mnazungumza utumbo. Hao wananchi Wana hoja za msingi kabisa. Kujenga kituo karibu na Makazi ni hatari Kwa wananchi na mali zao. Ni bahati mbaya hao wenye kituo wapita njia za rushwa hadi wamepewa vibali.

Sisi tuliopo Kimara hivi sasa tunapata shida sana na Malori ya Asas pale Korogwe kwa kuziba njia ya service Road na kusababisha foleni. Iwapo sisi tunapata kadhia hiyo na ni barabara kuu, vipi kuhusu hao wa mtaani?.
 
Wananchi wakazi wa Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi, Kata ya Mikocheni wilayani Kinondoni Dar es Salaam wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao.

Kituo hicho kinajengwa katika Barabara ya Senga, Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi Kata ya Mikocheni.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa huo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema sheria ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi haikufuatwa kabla ya ujenzi huo.

Mwananchi huyo ambaye amejitambulisha kuwa yeye ni mtaafu serikalini, alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo, sheria inamtaka mtu anayetaka kubadilisha matumizi ya ardhi kushirikisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka matangazo eneo la wazi kwa muda wa siku 21 ili kama kuna pingamizi litolewe.
View attachment 2814581
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (mwenye suti) kushoto akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mikocheni kuhusu madai ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika makazi ya watu.

“Haya mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika eneo hili haikutushirikisha, matangazo hayakuwekwa. Tumekuja kushtuka ujenzi umeanza.”amesema mwananchi huyo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Profesa Anna Tibaijuka amesema kituo hicho cha mafuta kinajengwa kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

“Kwanza barabara hii si barabara kuu, hii ni access road (barabara ndogo ya mtaani), huyu anajenga kituo cha mafuta, yatakuja magari maroli makubwa hapa hakuna hata nafasi, barabara hii ni finyu sana, na si eneo zuri kwa usalama na afya za wananchi ” alisema Profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka ambaye amepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kuwa suala hilo tayari wamelifikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye analishughulikia.

“Tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya ameanza kulishughulikia kwa kufika eneo kinapojengwa kituo hiki cha mafuta, tunaamini suala hili litapata ufumbuzi.”aliongeza Profesa Tibaijuka.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amekiri kupokea malalamiko hayo na wananchi wa Mikocheni.

“Kweli nilipokea malalamiko ya wananchi hao, jana nilikwenda kujionea mazingira ya kituo hicho kinachojengwa, nilichokigundua kampuni inayojenga kituo hicho inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha Baraza la Mazingira (NEMC).
View attachment 2814583
“Ni kweli nilipokea malalamiko ya kituo cha mafuta kujengwa katika makazi ya watu, jana nilikwenda (Novemba 14,2023) kujionea mwenyewe.

“Nilichokigundua ni kwamba hiyo kampuni inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha NEMC (Baraza la Mazingira), hatua inayofuata sasa ni kuangalia kama zile hatua za utoaji wa vibali hivyo ulifuatwa au kuna kilichokosewa. Baadaye nitakwenda kuwaeleeza wananchi tulikofikia”alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni.

Mmoja wa makandarasi wanaosimamia ujenzi wa Kituo hicho (jina tunalo), alipopigiwa simu kuzungumzia suala hilo, aliahidi kupiga simu baadaye. “Nitakupigia, subiri”ulisomeka ujumbe wa simu kutoka kwa mkandarasi huyo.

Chanzo: MATUKIODAIMA
Huko mwingine huwa zinajengwa kwenye makazi ya wanyama pori kio kinahudumia magari na wao ndo wenye magari au wanataka zikawekwe. Hifadhini
 
Mnazungumza utumbo.Hao wananchi Wana hoja za msingi kabisa.Kujenga kituo karibu na Makazi ni hatari Kwa wananchi na mali zao.Ni bahati mbaya hao wenye kituo wapita njia za rushwa hadi wamepewa vibali.Sisi tuliopo Kimara hivi sasa tunapata shida sana na Malori ya Asas pale korogwe,Kwa kuziba njia ya service Road na kusababisha foleni.Iwapo sisi tunapata kadhia hiyo na ni barabara kuu,vipi kuhusu hao wa mtaani?.
Sasa kama ni eneo la mtu unampangia cha kufanya? Hizo kero za malori ya mafuta unazungumzia maeneo gani?. Nilipo mimi kuna sheri kama mbili na zote zina utaratibu mzuri wa kuyaingiza maroli ya mafuta na kuyashusha. Kila kituo kina mifumo ya usalama. NEMC sio wajinga Kuwapa kibali cha ujenzi wawekezaji wa mafuta. Acheni watu wafanye biashara.
 
Hizo ni kick za kisiasa za Tibaijuka,
Waache mtu ajenge kituo chake hapo
 
Hizo ni kick za kisiasa za Tibaijuka,
Waache mtu ajenge kituo chake hapo
Nashangaa mbona mitaa kibao kuna Sheri nyingi zimejaa na watu tupo peace hatuna shida nazo. Sijui hao wanajiona hawako Tanzania ni nini,?? Au kiki za kishamba??
Wamuache mwenye eneo afanye anachotaka kufanya eneo ni lake
 
Licha ya kuwa ni idea nzuri ila sioni point zao,
At the end hicho kituo kitajengwa tu,
Huwezi sema kisa ni Access road hivyo haistahili uwepo wa kituo cha mafuta, + kuhusu eneo kwani hiyo sheli itakuwa inakaa na magari all the time?

Mimi binafsi sioni kama wana point,
Akili finyu! Hujui athari za kituo cha mafuta?
 
Back
Top Bottom