Sisi tanaangalia mzigo ufike panapohusika na sio hali ya punda! Tunakuomba sana mheshimiwa Freeman Mbowe kama unawapenda watanzania na CHADEMA usifanye kosa la kuachia uongozi wa chama kabla ya angalau 2030.
CHADEMA sio chama cha kuchukuliwa kiepesi epesi, CHADEMA ndio upinzani nchi hii na upinzani wa nchi hii ni CHADEMA. Siku CHADEMA ikifa ndio upinzani umekufa hivyo! Ikumbukwe kuwa kujenga chama imara kama CHADEMA huchukua si chini ya miaka 30.
Tafadhali sana mheshimiwa Mbowe, hatma ya upinzani na demokrasia ya nchi hii vipo mikononi mwako kuliko watu wengi wanavyojua. Hakuna kiongozi mwingine wa upinzani amebaki hai leo hii wote akina Lipumba, Mrema, Zitto, Cheyo, Shibuda, Mbatia na wengine, hao wote ni kundi moja, hawapo tena na hawana ushawishi kwa watanzania, umebaki wewe peke yako na unaangaliwa na watanzania kwa matumaini makubwa.
Siku utakapofanya kosa la kuachia uongozi wa CHADEMA kabla ya 2030, basi siasa za vyama vingi zitarudi zilipoanzia, 1995.
Usiangalie mashinikizo ya watu, kwanza wengi wa hao ni CCM wala si CHADEMA. Kumbuka wewe umetumwa kwa ajili ya Watanzania na wala hujajituma mwenyewe! Tafadhali subiri hadi 2030 na sio vinginevyo!