msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 838
- 1,167
Na Nulphin Charles Heche
Wakati vijana Kaskazini Magharibi mwa Bara la Afrika wakifanya mapinduzi kuwaondoa madikteta waliodumu kwa muda mrefu kwa msingi wa kuvunja Demokrasia hali ni sawa na ilivyo kwa chama cha Upinzani nchini Tanzania, Chadema.
Licha ya kuhubiri Demokrasia chama hicho kimegeuzwa mali ya watu wachache ambao hugawana ruzuku na michango ya chama hicho mithili ya kupe wanyonyavyo damu ya Ng'ombe aliyenona bila hofu ya uwajibikaji wala kuhojiwa, au kuulizwa lolote.
Freeman Mbowe amesimika uongozi wa kisultani katika chama kinachosijinasibu kuwa cha kidemokrasia jambo linaloacha maswali mengi kuliko majibu. Tangu Freeman Mbowe ahodhi nafasi ya Uenyekiti wa Chadema, mtoto aliyezaliwa tayari ni mtu mzima mwenye familia. Jambo hili linaondoa sifa ya Chadema kuhubiri Demokrasia wala misingi bora ya uongozi.
Waliowahi kuthubutu kujaribu kugombea ama kuandaa mipango ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Taifa walifukuzwa chama kwa mizengwe au kupotea katika mazingira tata. Zitto Zuberi Kabwe na Chacha Wangwe ni mifano dhahiri ya nadharia hii ya kidikteta isiyofaa kwa ustawi wa Demokrasia.