Mbinu 10 za kumdhibiti mke/GF jeuri.......(FOR REAL MEN ONLY)

Nampikia ananipikia, namfulia ananifulia, ananipa moyo nampa moyo, ananipenda nampenda, ananipa raha nampa raha n.k
Hatuishi kama washindani sie!!

Umesahau anakununulia unamnunulia, anakulipia unamlipia. Hii muhimu sana.
 
Umesahau anakununulia unamnunulia, anakulipia unamlipia. Hii muhimu sana.

Sure!! Nikiwa kwenye mizunguko nikaona kitu kizuri kinachomfaa namnunulia, sirudi baadae kumwambia "naomba unirudishie kiasi fulani cha pesa" though wapo wanaoishi hivyo. Yani he is mine and i'm his, kwakua kila mmoja anampenda na kumjali mwenzake hatuoni tabu kusaidiana majukumu yetu kila inapowezekana.
 
definiton ni ya Mungu siyo mimi..................tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.............akianza kutokosa maharagwe huyo tayari umemtawala hana sifa ya to be a real man.....................

Nikisema bado tunayo kazi ya kumuelewa mungu vizuri watu hanielewi.
Sasa angalia, kwenye kitabu hicho hicho ulicho quote kuna mahali Ibrahimu alitembelewa na wageni nyumbani kwakwe na yeye ndiye aliyewaandalia chakula na alisimama pembeni akisubiri kuondoa vyombo.
Kwa hiyo na yeye alikuwa hajui sheria za mungu au alikuwa kaolewa?
 
Mke wako ana bahati sana. Ni wanaume wachache wako proud kuwasaidia wake zao kama wewe. Nakupa tano

Wanangu ntawalea kwa misingi kama ilokulea wewe; umekula osha vyombo sio kutupa kwenye sinki uje uoshewe; hivi vitu vidogo dogo ndio vinatengeneza wanaume mizigo baadae.

Hiyo title tu "Mbinu za kumdhibiti...." nilijua kuwa hapa nitapingana nawe. Kwa nini umdhibiti. Ikiwa unampenda, anakupenda - mnapendana - tena kudhibitiana kuna haja gani?

Kwanza hapa waombe samahani dada wanaosaidia kazi za nyumbani. Hilo jina lilishaacha kutumiak enzi za utumwa

Napinga hiyo red kwani kwa mawaz yangu ni kuwa "furaha ya ndoa ni kutegemeana". Ahadi zenu zilikuwa "kukaa naye kwa raha na shida, uzima na ugonjwa...mpaka kifo kitakapowatenganisha". Ikiwa mwanamme "must" kutomtegemea mwanamke hata ikiwa wakati wa shida na ugonjwa, hiyo ahadi ingesomeka vyema kama ingekuwa "kukaa naye kwa raha na uzima...mpaka shida na ugonjwa utakapowatenganisha."

Kwenye familia yangu tangu wadogo, wanaume na wanawake tulifunzwa kufanyakzi na kusaidiana katika mtindo wa hukutwanga huli, haikuwekwa kutafuta na kuchanja kuni, kutwanga na kukosha vyombo ni jukumu la msichana. Hata msichana alipoumwa au kutokuwepo, wavulana tuliingia jikoni. Leo niko mkubwa, kamwe sitokka na njaa au kula nje kwa kusubiri mke aje kunipikia.

Aidha, tulipokuwa JKT, wasichana na wavulana tulishirikiana kwa kila kitu, iweje leo nibadilike kwa sababu nimeoa. Kwanza huu msamiati wa kuoa/kuolewa haupo kwangu, ni KUOANA kwa maana ya kukubaliana.

Nambari 9 tayari imeshapata msemaji. Kama ni kweli ulivyoitetea baadaye, isahihshe, ondoa neno hadharani kwani linakupa ruhusa ya kumpiga na kumnyanyasa faraghani.

Mimi wangu nitamsaidia kwa yote uliyosema nisitie mkono. Na hata hilo la ujauzito ambalo kweli ndio nature (mengine yote tunajipangia hakupanga Muumba), akijifungua ninamsaidia malezi ikiwemo kuadilisha mtoto nepi, kufua mikojo na mavi. Kamwe sitomwamsha dada wa kazi amshughulikie mtoto usiku, na mkewangu ndio kabisaaaaa, alishachukua jukumu nilisiloweza kulibeba mimi wakati wa ujauzito, kwa hivyo kumbebesha mengine nikiwa na mikono miwili...hapo nitakubali majirani waseme. I'll do it for the sake of my kids, for the sake of my lifemate.
 
Sure!! Nikiwa kwenye mizunguko nikaona kitu kizuri kinachomfaa namnunulia, sirudi baadae kumwambia "naomba unirudishie kiasi fulani cha pesa" though wapo wanaoishi hivyo. Yani he is mine and i'm his, kwakua kila mmoja anampenda na kumjali mwenzake hatuoni tabu kusaidiana majukumu yetu kila inapowezekana.

he is mine and I'm his.......................what a joke just show it through division of labour....................and we will know that he is truly yours badala ya hizi
 
Nikisema bado tunayo kazi ya kumuelewa mungu vizuri watu hanielewi.
Sasa angalia, kwenye kitabu hicho hicho ulicho quote kuna mahali Ibrahimu alitembelewa na wageni nyumbani kwakwe na yeye ndiye aliyewaandalia chakula na alisimama pembeni akisubiri kuondoa vyombo.
Kwa hiyo na yeye alikuwa hajui sheria za mungu au alikuwa kaolewa?

Tiger hao wageni unajua walikuwa akina nani.............hao ni mkewe sarah? be serious next time bro............[MENTION]@Tiger[/MENTION]
 
Ni rahisi kuona pointi anazoongea Ruta hazifai kwa sasa,well na mimi naafiki kwa kiwango fulani maisha ya leo haipaswi kuishi na mke kwa staili hii,ieleweke bibi zetu walilelewa wakiwaona mama zao wanavyoishi na waume zao hivyo ilikuwa rahisi nao wakiolewa kuendeleza yale waliyoyaona yanafaa kwa mume.Maisha ya leo,wake zetu wamelelewa tofauti sana,ukitaka kuishi naye kwa masharti yote haya ndoa inavunjika siku ya kwanza utakayo implement..ILA na nyie wake zetu tatizo lenu kubwa mwanamume akishirikiana na wewe sana,mnakuwa mnaleta aina fulani ya dharau na kutokuheshimiana na pia mnasahau yapi haswa ni majukumu yenu. pengine ndio maana Ruta ana insist hizi rules..Mfano utakuta mke anamfokea mume kama mtoto,hata hivyo naelewa si wote ila wengi wanasahau majukumu yao
 
Hebu jiulize unamsaidiaje Mmeo kwenye kazi zake?

Kama majukumu yako anakusaidia
 
Hizi mbinu ni muarobaini wa wake/ma-GF korofi na utawashikisha adabu...............nimeifupisha kutoka kwenye hii makala ya
Don’ts for husbands

1) Usifue nguo zako hata siku moja hakikisha anakufulia kwa mikono yake na hakuna mwanya wa kumwachia mtoto wa kazi. Yeye mwenyewe aliapa atakuhudumia na wala siyo kukasimu madaraka tajwa............

2) Usipike hata siku moja hakikisha ni mikono yake ndiyo inabeba haya majukumu na hakuna fursa ya kukasimu haya majukumu nyeti kabisa..............

3) Maji ya kuoga nalo ni jukumu lake kuyainjika na kukupelekea bafuni kwa mikono yake aache soooooooooooooooo.

4) Asiendeshe gari na wewe ukiwepo.

5)Akuchagulie nguo za kuvaa.

6) Lipa bili zote asilipe bili hata moja.......vijisenti vyake atajua nini ya kuvifanyia ili asije kudhani mpo sawa...

7) Hakikisha una ajira na kamwe usimtegemee kwa lolote lile

8) Usifilisike hata siku moja vinginevyo atakutawala tena kwa masimango kibao.........

9) Usimpige au kumnyanyasa au kumdhalilisha mkeo mbele ya kadamnasi ya watu............mpende kama kiapo chako kilivyokuwa.........

10) Usiwe mtu wa matumizi mabaya ya fedha hasa pati na marafiki na hivyo kumpa picha ya kuwa wewe ni mfujaji

Haya ni masharti ya kukwepa mwanandni wako kufikiri naye ni kidume ndani ya mahusiano yenu..........ukishindwa haya au kama ukijipima ukaona hupati maksi 80 au maswali nane kati ya kumi basi wewe unatawaliwa na mwanamke na mahusiano yenu yapo hatarini kuvunjika au wewe kuwa huna furaha maisha yako yote na utakufa kwa shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo...................

amka jikomboe kutoka kwenye utumwa wa mwanamke..............

HIZO MBINU NI SUITABLE FOR THE CATEGORY IN RED APO BUT A SERIOUS MARRIED MAN CA NOT TAKE SUCH A BUNCH OF LOOSE RULES,mapenzi si marathon..thats why a lot of men fail to get married..sababu ya mawazo ya mashindano shindano kama hayo...WOMEN FEEL VERY COMFORTABLE AND RESPECTED ONCE THEY ARE APPROACHED BY THEIR HUSBAND FOR A BIT OF CONTRIBUTION IN A FAMILY BILL...ni sheria nzuri kwa SENIOR BACHELORS
 
Sure!! Nikiwa kwenye mizunguko nikaona kitu kizuri kinachomfaa namnunulia, sirudi baadae kumwambia "naomba unirudishie kiasi fulani cha pesa" though wapo wanaoishi hivyo. Yani he is mine and i'm his, kwakua kila mmoja anampenda na kumjali mwenzake hatuoni tabu kusaidiana majukumu yetu kila inapowezekana.

Hayo ndo mapenzi ya kweli, na kupendana kwa dhati. Sbb naamini sisi ni binadamu, tunategemeana sana, ukisema lazima ufanye haya na mm nifanye haya, kuna kuumwa, kuna kusafiri, kuna bahati mbaya za maisha kuna kukosa. Kwa hiyo siku mume akikosa pesa mm mwanamke namute na pesa zangu na kwamba maisha hayaendi siku hiyo sbb siwezi kuingilia majukumu ya mume.

Maisha ya sasa ni magumu, hatuna budi kubadilika na hatuna budi kusaidiana. Kusaidiana majukumu yanayotukabili km mke na mume. Swala la kusema eti usifanye haya, ukifanya mkeo hatakueshimu yamepitwa na wakati. Km ataamua kutokukukuhesimu anaweza akafanya tu hata km umbane kiasi gani.

Heshima, upendo, mapenzi haupimwi kwa majukumu au kazi. Ni vitu natural toka moyoni mwa mtu.
 
The Boss usisahau na namba 8 zinahusiana moja kwa moja. The Boss

Hivi kufilisika na kukosa kazi ni chaguo la mtu vile eeeh?!

By the way, real men are always straight. Huna haja ya kuwa mbabe kuwa real man. Msaidie mkeo kupika na kufanya shughuli za nyumbani na ndio atakuheshimu.

Haya unayoyasema wewe yatamfanya akuogope na si kukuheshimu. Kwa mfano; kama mke wangu hajisikii kunipelekea maji na taulo bafuni basi hakuna haja ya kumlazimisha. Raha ya kufanyiwa hivyo ni hiari ya mwenzi na si kwamba wewe huna mikono ya kufanya hivyo.

Mimi nilikuwa na demu jeuri kuliko mwanamke wa kihaya lkn sasa tunavyoongea ni mke na ananiheshimu kuliko wazazi wake. Amekuwa inspired, ameridhia kujinyenyekeza kwangu na ananipenda kweli. Sababu ni kwamba sikushindana naye, nilimuacha aone ujinga wake na kabadilika mwenyewe.

Heshima weka kwenye 6" x 6"
 
Last edited by a moderator:
ndoa haifundishwi, kama ambavyo hukwenda darasa la kutongoza au kuingiza au kuingiziwa shipa (msulu) au sponge tissue ndivyo utakavyo ishi. "Enyi waume ishini na wake zenu kwa akili", ndivyo biblia inavyosema, kwahiyo usijaribu kuishi naye kwa imani, hapana, ishi naye kwa akili
 
Kugongelea Misumari kwenye hizi Tactics

Hizi mbinu ni muarobaini wa wake/ma-GF korofi na utawashikisha adabu...............nimeifupisha kutoka kwenye hii makala ya
Don’ts for husbands

1) Usifue nguo zako hata siku moja hakikisha anakufulia kwa mikono yake na hakuna mwanya wa kumwachia mtoto wa kazi. Yeye mwenyewe aliapa atakuhudumia na wala siyo kukasimu madaraka tajwa............

2) Usipike hata siku moja hakikisha ni mikono yake ndiyo inabeba haya majukumu na hakuna fursa ya kukasimu haya majukumu nyeti kabisa..............

3) Maji ya kuoga nalo ni jukumu lake kuyainjika na kukupelekea bafuni kwa mikono yake aache soooooooooooooooo.

Zibaki Kama zilivyo

(4) Asiendeshe gari na wewe ukiwepo.
Asiendeshe kabisaaaa hata kama ukiwepo akitaka anunue lake

(5)Akuchagulie nguo za kuvaa.

6) Lipa bili zote asilipe bili hata moja.......vijisenti vyake atajua nini ya kuvifanyia ili asije kudhani mpo sawa...

7) Hakikisha una ajira na kamwe usimtegemee kwa lolote lile

8) Usifilisike hata siku moja vinginevyo atakutawala tena kwa masimango kibao.........

9) Usimpige au kumnyanyasa au kumdhalilisha mkeo mbele ya kadamnasi ya watu............mpende kama kiapo chako kilivyokuwa.........

10) Usiwe mtu wa matumizi mabaya ya fedha hasa pati na marafiki na hivyo kumpa picha ya kuwa wewe ni mfujaji

Yabaki kama yalivyo

Ruta nimeelewa vizuri hizi rules zako lakini hiyo ya 4 (asiendeshe gari na wewe ukiwepo) bado siielewi ina maana gani? yani akiendesha na wewe ukiwepo inaleta picha gani?
 
Back
Top Bottom