Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,650
Wakuu amani kwenu.

Kumekuwa na maswali mengi sana kutaka kujua kama kweli mwanamie/mwanamume fulani anafaa kufunga ndoa naye ama la. Wengi hutaka kujua ni sifa zipi hasa mwenza anapaswa kuwa nazo kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kudumu. Leo nitazungumzia sifa chache muhimu zaidi ambazo wengi hawazioni bali hukimbilia sifa za nje zisizo na uzito.

Kwa wanawake

1. Upendo wa kweli
Sifa kuu na muhimu kabisa anayopaswa kuwa nayo mwanamume ni upendo wa kweli. Mwanamume ameagizwa na kupewa uwezo wa kupenda, hivyo hilo halina majuto kwake, ni sehemu ya maamuzi yake. Kupenda sio sifa ya nje ya mwili (physical) bali ni sifa ya ndani (spiritual). Kama kweli anakupenda hawezi kukulazimisha ulale naye kabla ya ndoa. Tena atakulinda daima dhidi ya mambo yote yanayoweza kuharibu sifa yako njema kama kwenda club, vilevi, marafuki wa hovyo nk. Anapaswa akupende kwa Agape love na sio eros pekee. Usiruhusu akufanye chombo cha kutimizia tamaa zake za kingono kwa ahadi kwamba atakuoa. Kama baba yako mzazi akulindavyo dhidi ya tamaa mbaya, huyu pia anakusudiwa kuja kuchukua jukumu la baba kukulinda, hivyo haipaswi yeye ndiye awe wa kwanza kukushawishi mtende uovu. Kama kweli anakupenda atakulinda.

Mwanamume ajapo kukuposa mbele ya wazazi wako, anaweka ahadi ya kukulinda kwa gharama yoyote ile. Ahadi hii kwa wazazi hufungwa kwa kutoa mahari, kwa mwanamke hufungwa kwa kukuonyesha upendo wa kweli, sio kukutamani kulala na wewe tu.

2. Mahari

Katika zama hizi ukizungumzia mahari utaonekana mwendawazimu. Tumefikia hatua hata baadhi ya wazazi wetu waliokatishwa tamaa na mienendo mibovu ya binti zao kutamani waolewe hata bila mahari. Hili haliji kwa kupenda, bali wanalazimika kuchukua maamuzi hayo. Lakini leo nataka nikuonyeshe umuhimu wa mahari kama msingi mkuu wa ndoa.

Ziko sababu kadhaa kwa nini mwanamume anapaswa kutoa mahari kabla ya kumtwaa mkewe:

a. Muunganiko wa koo
Katika mila za dunia hii, baba ndiye mpokeaji wa mahari, na kama hayupo hai, jukumu hilo hutekelezwa na ndugu wa kiume wa baba. Mama hana nafasi katika hili kwa sababu yeye ameolewa kujenga ukoo wa mumewe, amekuwa familia ya mume, lakini hata hivyo kupokea mahari ni sawa na kuruhusu wakwe wapokee mahari ya ukoo mwingine. Posa inapopokelewa na baba aliye kiongozi wa familia, maana yake ni kuwa amekubali malipo kujiunga na ukoo wa mwanamume. Koo haziungani kwenye sherehe ya harusi, hili haliwezekani kabisa, bali koo huunganishwa na mahari pekee.

b. Shukurani kwa malezi bora
Mahari itolewapo ni namna ya nje kukiri kwamba wazazi wa binti wamemlea katika maadili mema binti yao. Hivyo hutolewa kama namna ya kuonyesha shukrani kwa wazazi kwa juhudi kubwa waliyofanya mpaka kufikia hatua ya binti yao kuolewa. Haya mambo ya kimila kama kununua kitenge cha mama, koti la baba nk ni alama ya ushindi katika malezi kwa wazazi hawa. Ni vitu vidogo lakini vyenye maana kubwa sana. Hiyo mali inayotolewa ni kama fidia kwa gharama alizoingia baba katika kumlea binti yake. Hii haiwezi kamwe kurudusha gharama zote zilizotumika, bali ni ishara tu (symbolic) kwamba sasa binti anatolewa kutoka mamlaka moja kwenda mamlaka nyingine.

c. Ishara ya kupokea jukumu la baba
Kijana anapotoa mahari anamwambia baba wa mzazi kuwa yupo tayari kupokea jukumu la kumlea na kumtunza binti yake. Kabla ya kuolewa, binti alikuwa chini ya mamlaka ya baba, akipewa mahitaji yote muhimu na baba, huku akifuata na kutekeleza kikamilifu maagizo yote kama yalivyotolewa. Sasa kijana anapotoa mahari anamhakikishia baba kuwa naye keshakuwa mtu mzima na sasa yuko tayari kupokea jukumu la malezi ya binti kama baba yake. Kwa lugha nyepesi binti anatoka kwenye uangalizi wa baba yake mzazi anakuwa chini ya uangalizi wa baba mpya ambaye ni mumewe.

d. Nia njema na heshima kwa wazazi
Kijana anapotoa mahari ni ishara ya wazi kuwa moyo wake una kusudi jema juu ya binti huyu. Hii inajenga uaminifu kwa wazazi wa binti kuwa binti yao anaingia kwenye mikono salama kwa kuwa kijana ametambua nafasi yao kwenye mahusiano. Jambo hili pia huwajengea heshima kubwa wazazi wa binti mbele ya jamii na pia humjengea heshima kijana muoaji mbele ya ukoo wa mke na jamii kwa ujumla. Ni ishara ya tabia njema na maadili bora kwa kijana.

∆∆ Sasa kabla hamjanirarua natambua pia kuwa hasa katika zama hizi, kumekuwa na matapeli wa mapenzi, wanaweza hata kutoa mamilioni ya mahari ili tu wamtumie binti watakavyo. Ndio maana ni muhimu wazazi washiriki hatua zote, wao ndio wafanye upembuzi yakinifuyakinifu.

KWA WANAUME

Yako mambo mengi ya nje ambayo mwanamume aweza kuyatazama kwa mwanamke na kuvutiwa nayo, lakini haya mawili ni ya msingi sana katika ustawi wa ndoa na familia:

1. Utii wa kweli
Mwanamke ambaye ana dalili za kuwa mke bora atakuwa na utii utokao moyoni. Amini usiamini hii ndiyo sifa kuu na ya muhimu kabisa. Sasa utaupimaje huo utii? Usidanganyike na jinsi anavyokuchekea, au kujidekeza ukadhani kujionyesha anakupenda ni utii. Haya hufanywa pia na makahaba watakapo kumnasa mwanamume mjinga. Mwanamke hakuwahi kupewa kupenda, ndio maana anabadilika badilika, mke wa ndoa NI LAZIMA awe na utii kama ilivyokuwa kwa baba yake.

Utii unaanzia kwa baba yake mwenyewe, kwani kama binti hawezi kuwaheshimu wazazi, basi hawezi kumheshimu mume, haipo!! Nikisema kumheshimu baba yake ni kwamba binti awe amezingatia taratibu zote za malezi kama alivyoelekezwa na baba yake. Hapo kale na hata sasa kipimo kikuu kwa mwanamke kwamba ana utii ni bikira, kubali au kataa. Haiwezekani binti anayemtii baba yake awe analala na wanaume hovyo kabla ya ndoa. Ukomo wa heshima ya binti kwa wazazi ni kufanya mapenzi na mwanamume kabla ya ndoa. Hapo anahesabiwa kuwa mtu mzima na si mwali tena. Mahari hutolewa kwa mwanamwali, si kila mwanamke, kwani ndilo kusudi la kuwekwa bikira kwa nwanamke. Kwamba mwanamume wa kwanza kuingia atafanya hivyo kwa kumwaga damu kama ishara ya agano la ndoa.

Sasa utaona vijana wengi wanaoa wanawake wasio na bikira huku wakijigamba kuwa ni watulivu, hii ni nadra sana, kwani siku mkipishana kauli, silaha yake ni kutoka nje ya ndoa. Hii ndio njia rahisi kwake kumkomoa na kumuumiza mumewe. Lakini kama hana hayo mazoea kwa vile anamjua mumewe tu, ana nafasi ya kuwa na utii hata nyakati ngumu na linapotokea tatizo atakimbilia kwa wazazi, sio kuvuta hisia za wapenzi wa zamani. Mwanamke kutokuwa na bikira siku ya kuolewa ni ishara ya wazi kuwa hana utii bali hutii anapotaka yeye. Hakuna mwanamume awezaye kumbadili mwanamke kuacha tabia ambayo wazazi wake hawakuweza kumdhibiti. Kama alileta kiburi kwa baba mzazi, basi mume atarajie hayo hayo, huo ndio ukweli.

2. Kumiliki nyumba
Kimsingi mume hujenga jengo kisha mke huligeuza kuwa nyumba. A husband builds a house, a wife turns it into a home. Sifa nyingine ya mchumba bora ni uwezo wake wa kuhimili majukumu ya familia, mapishi, usafi, malezi nk. Kama mwanamke hawezi kutekeleza hayo kikamilifu, basi upendo wa mume utapoa kwake. Kumbuka mchumba ndiye atakuwa mama wa watoto wako, usioe kwa sababu ana matako makubwa kwa sababu matako hayatalea watoto. Tafuta sifa za ndani ambazo zitakuletea kizazi bora.

Mwanamke haolewi kwa sifa ya kipato, ama elimu, bali huolewa kwa uwezo wake wa kutunza familia. Hilo ndilo jukumu lake la msingi na ndilo eneo awezalo kulitawala vema. Kuoa mwanamke kwa kusudi la kusaidiana kutafuta fedha ni sawa tu na kuishi kwenye danguro kwani watoto wenu wataishia kuwa na tabia mbovu. Huu mfumo wa watoto kulelewa na visichana vya kazi ni wa kishetani na ndio chanzo kikuu cha mmomonyoko wa maadili kwenye jamii. Usikubali kunasa kwenye mtego huu, mwanamume kutaka kuoa ni kwamba umejipima ukaona unao uwezo wa kumudu majukumu ya kuwa baba wa familia, sio partner wa familia. Simama kwenye nafasi yako nawe utaheshimiwa.

Baba bora hutafakari kesho ya kizazi chake, sio burudani ya wakati uliopo.

Kwa leo naweka ukomo hapo.

Asanteni.
 
Wakuu amani kwenu.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutaka kujua kama kweli mwanamie/mwanamume fulani anafaa kufunga ndoa naye ama la. Wengi hutaka kujua ni sifa zipi hasa mwenza anapaswa kuwa nazo kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kudumu. Leo nitazungumzia sifa chache muhimu zaidi ambazo wengi hawazioni bali hukimbilia sifa za nje zisizo na uzito.

Kwa wanawake

Asanteeeee
 
Wakuu amani kwenu.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutaka kujua kama kweli mwanamie/mwanamume fulani anafaa kufunga ndoa naye ama la. Wengi hutaka kujua ni sifa zipi hasa mwenza anapaswa kuwa nazo kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kudumu. Leo nitazungumzia sifa chache muhimu zaidi ambazo wengi hawazioni bali hukimbilia sifa za nje zisizo na uzito.

Kwa wanawake

1. Upendo wa kweli
Sifa kuu na muhimu kabisa anayopaswa kuwa nayo mwanamume ni upendo wa kweli. Mwanamume ameagizwa na kupewa uwezo wa kupenda, hivyo hilo halina majuto kwake, ni sehemu ya maamuzi yake. Kupenda sio sifa ya nje ya mwili (physical) bali ni sifa ya ndani (spiritual). Kama kweli anakupenda hawezi kukulazimisha ulale naye kabla ya ndoa. Tena atakulinda daima dhidi ya mambo yote yanayoweza kuharibu sifa yako njema kama kwenda club, vilevi, marafuki wa hovyo nk. Anapaswa akupende kwa Agape love na sio eros pekee. Usiruhusu akufanye chombo cha kutimizia tamaa zake za kingono kwa ahadi kwamba atakuoa. Kama baba yako mzazi akulindavyo dhidi ya tamaa mbaya, huyu pia anakusudiwa kuja kuchukua jukumu la baba kukulinda, hivyo haipaswi yeye ndiye awe wa kwanza kukushawishi mtende uovu. Kama kweli anakupenda atakulinda.

Mwanamume ajapo kukuposa mbele ya wazazi wako, anaweka ahadi ya kukulinda kwa gharama yoyote ile. Ahadi hii kwa wazazi hufungwa kwa kutoa mahari, kwa mwanamke hufungwa kwa kukuonyesha upendo wa kweli, sio kukutamani kulala na wewe tu.

2. Mahari

Katika zama hizi ukizungumzia mahari utaonekana mwendawazimu. Tumefikia hatua hata baadhi ya wazazi wetu waliokatishwa tamaa na mienendo mibovu ya binti zao kutamani waolewe hata bila mahari. Hili haliji kwa kupenda, bali wanalazimika kuchukua maamuzi hayo. Lakini leo nataka nikuonyeshe umuhimu wa mahari kama msingi mkuu wa ndoa.

Ziko sababu kadhaa kwa nini mwanamume anapaswa kutoa mahari kabla ya kumtwaa mkewe:

a. Muunganiko wa koo
Katika mila za dunia hii, baba ndiye mpokeaji wa mahari, na kama hayupo hai, jukumu hilo hutekelezwa na ndugu wa kiume wa baba. Mama hana nafasi katika hili kwa sababu yeye ameolewa kujenga ukoo wa mumewe, amekuwa familia ya mume, lakini hata hivyo kupokea mahari ni sawa na kuruhusu wakwe wapokee mahari ya ukoo mwingine. Posa inapopokelewa na baba aliye kiongozi wa familia, maana yake ni kuwa amekubali malipo kujiunga na ukoo wa mwanamume. Koo haziungani kwenye sherehe ya harusi, hili haliwezekani kabisa, bali koo huunganishwa na mahari pekee.

b. Shukurani kwa malezi bora
Mahari itolewapo ni namna ya nje kukiri kwamba wazazi wa binti wamemlea katika maadili mema binti yao. Hivyo hutolewa kama namna ya kuonyesha shukrani kwa wazazi kwa juhudi kubwa waliyofanya mpaka kufikia hatua ya binti yao kuolewa. Haya mambo ya kimila kama kununua kitenge cha mama, koti la baba nk ni alama ya ushindi katika malezi kwa wazazi hawa. Ni vitu vidogo lakini vyenye maana kubwa sana. Hiyo mali inayotolewa ni kama fidia kwa gharama alizoingia baba katika kumlea binti yake. Hii haiwezi kamwe kurudusha gharama zote zilizotumika, bali ni ishara tu (symbolic) kwamba sasa binti anatolewa kutoka mamlaka moja kwenda mamlaka nyingine.

c. Ishara ya kupokea jukumu la baba
Kijana anapotoa mahari anamwambia baba wa mzazi kuwa yupo tayari kupokea jukumu la kumlea na kumtunza binti yake. Kabla ya kuolewa, binti alikuwa chini ya mamlaka ya baba, akipewa mahitaji yote muhimu na baba, huku akifuata na kutekeleza kikamilifu maagizo yote kama yalivyotolewa. Sasa kijana anapotoa mahari anamhakikishia baba kuwa naye keshakuwa mtu mzima na sasa yuko tayari kupokea jukumu la malezi ya binti kama baba yake. Kwa lugha nyepesi binti anatoka kwenye uangalizi wa baba yake mzazi anakuwa chini ya uangalizi wa baba mpya ambaye ni mumewe.

d. Nia njema na heshima kwa wazazi
Kijana anapotoa mahari ni ishara ya wazi kuwa moyo wake una kusudi jema juu ya binti huyu. Hii inajenga uaminifu kwa wazazi wa binti kuwa binti yao anaingia kwenye mikono salama kwa kuwa kijana ametambua nafasi yao kwenye mahusiano. Jambo hili pia huwajengea heshima kubwa wazazi wa binti mbele ya jamii na pia humjengea heshima kijana muoaji mbele ya ukoo wa mke na jamii kwa ujumla. Ni ishara ya tabia njema na maadili bora kwa kijana.

∆∆ Sasa kabla hamjanirarua natambua pia kuwa hasa katika zama hizi, kumekuwa na matapeli wa mapenzi, wanaweza hata kutoa mamilioni ya mahari ili tu wamtumie binti watakavyo. Ndio maana ni muhimu wazazi washiriki hatua zote, wao ndio wafanye upembuzi yakinifu\. [/B]

KWA WANAUME

Yako mambo mengi ya nje ambayo mwanamume aweza kuyatazama kwa mwanamke na kuvutiwa nayo, lakini haya mawili ni ya msingi sana katika ustawi wa ndoa na familia:

1. Utii wa kweli
Mwanamke ambaye ana dalili za kuwa mke bora atakuwa na utii utokao moyoni. Amini usiamini hii ndiyo sifa kuu na ya muhimu kabisa. Sasa utaupimaje huo utii? Usidanganyike na jinsi anavyokuchekea, au kujidekeza ukadhani kujionyesha anakupenda ni utii. Haya hufanywa pia na makahaba watakapo kumnasa mwanamume mjinga. Mwanamke hakuwahi kupewa kupenda, ndio maana anabadilika badilika, mke wa ndoa NI LAZIMA awe na utii kama ilivyokuwa kwa baba yake.

Utii unaanzia kwa baba yake mwenyewe, kwani kama binti hawezi kuwaheshimu wazazi, basi hawezi kumheshimu mume, haipo!! Nikisema kumheshimu baba yake ni kwamba binti awe amezingatia taratibu zote za malezi kama alivyoelekezwa na baba yake. Hapo kale na hata sasa kipimo kikuu kwa mwanamke kwamba ana utii ni bikira, kubali au kataa. Haiwezekani binti anayemtii baba yake awe analala na wanaume hovyo kabla ya ndoa. Ukomo wa heshima ya binti kwa wazazi ni kufanya mapenzi na mwanamume kabla ya ndoa. Hapo anahesabiwa kuwa mtu mzima na si mwali tena. Mahari hutolewa kwa mwanamwali, si kila mwanamke, kwani ndilo kusudi la kuwekwa bikira kwa nwanamke. Kwamba mwanamume wa kwanza kuingia atafanya hivyo kwa kumwaga damu kama ishara ya agano la ndoa.

Sasa utaona vijana wengi wanaoa wanawake wasio na bikira huku wakijigamba kuwa ni watulivu, hii ni nadra sana, kwani siku mkipishana kauli, silaha yake ni kutoka nje ya ndoa. Hii ndio njia rahisi kwake kumkomoa na kumuumiza mumewe. Lakini kama hana hayo mazoea kwa vile anamjua mumewe tu, ana nafasi ya kuwa na utii hata nyakati ngumu na linapotokea tatizo atakimbilia kwa wazazi, sio kuvuta hisia za wapenzi wa zamani. Mwanamke kutokuwa na bikira siku ya kuolewa ni ishara ya wazi kuwa hana utii bali hutii anapotaka yeye. Hakuna mwanamume awezaye kumbadili mwanamke kuacha tabia ambayo wazazi wake hawakuweza kumdhibiti. Kama alileta kiburi kwa baba mzazi, basi mume atarajie hayo hayo, huo ndio ukweli.

2. Kumiliki nyumba
Kimsingi mume hujenga jengo kisha mke huligeuza kuwa nyumba. A husband builds a house, a wife turns it into a home. Sifa nyingine ya mchumba bora ni uwezo wake wa kuhimili majukumu ya familia, mapishi, usafi, malezi nk. Kama mwanamke hawezi kutekeleza hayo kikamilifu, basi upendo wa mume utapoa kwake. Kumbuka mchumba ndiye atakuwa mama wa watoto wako, usioe kwa sababu ana matako makubwa kwa sababu matako hayatalea watoto. Tafuta sifa za ndani ambazo zitakuletea kizazi bora.

Mwanamke haolewi kwa sifa ya kipato, ama elimu, bali huolewa kwa uwezo wake wa kutunza familia. Hilo ndilo jukumu lake la msingi na ndilo eneo awezalo kulitawala vema. Kuoa mwanamke kwa kusudi la kusaidiana kutafuta fedha ni sawa tu na kuishi kwenye danguro kwani watoto wenu wataishia kuwa na tabia mbovu. Huu mfumo wa watoto kukelewa na visichana vya kazi ni wa kishetani na ndio chanzo kikuu cha mmomonyoko wa maadili kwenye jamii. Usikubali kunasa kwenye mtego huu, mwanamume kutaka kuoa ni kwamba umejipima ukaona unao uwezo wa kumudu majukumu ya kuwa baba wa familia, sio partner wa familia. Simama kwenye nafasi yako nawe utaheshimiwa.

Umeandika vizuri,ila hapo kwenye bikra kwa zama hizi mazingira yamebadilika.

Imagine mtoto amesoma elimu ya juu (advanced level) na baadaye chuo ,hiyo ni miaka zaidi ya sita bila kuwa na uangalizi wa wazazi!!! Vishawishi ni vingi sana zama hizi,
Zama za zamani binti anakua,anavunja ungo, anasubiri mchumba mapema kabisa!!!
 
Mkuu umeandija vizuri sana na nimekuelewa kwa % zote. Next year nampango wa kuoa bikra mmoja mahali sitaki kuoa ma x wa watu,nataka nimwage damu kwenye shuka jeupe.
Ma-ex na wake za watu walioolewa kwa ndoa bubu huko vyuoni kwa miaka mitatu mizima wanakuja na baggage kibao yaani....

Oa huyo bikra hata akikushinda akushinde mwenyewe tu....
 
Umeandika vizuri,ila hapo kwenye bikra kwa zama hizi mazingira yamebadilika.

Imagine mtoto amesoma elimu ya juu (advanced level) na baadaye chuo ,hiyo ni miaka zaidi ya sita bila kuwa na uangalizi wa wazazi!!! Vishawishi ni vingi sana zama hizi,
Zama za zamani binti anakua,anavunja ungo, anasubiri mchumba mapema kabisa!!!
Ni kweli mazingira yamebadilika na ndio maana hata maisha ya ndoa yamebadilika pia. Ndoa zinasambaratika mchana na usiku, malezi ya watoto yamebadilika kabisa. Kitu kimoja tu hakitobadilika kamwe, mke bora kabisa lazima ajifunze kujizuia toka ujanani. Pia ukweli mchungu ni kuwa ndoa na elimu ya mke havihusiani kabisa. Ndio maana wanawake wengi wasomi wanapata taabu sana kukaa kwenye ndoa, mafundisho ya vyuoni na misingi ya ndoa vimetofautiana kabisa. Chunguza leo!! Uchaguzi ni wako, uoe elimu, pesa au mke wa kukuletea na kukulelea watoto.
 
Vipi wanawake waliobakwa utotoni ,unawaambia nini???
Huu ni utetezi unaojitokeza kila mara. Mkuu, ndoa sio rehab centre, kwamba unaoa au kuolewa kwa sababu ya kumwonea huruma mtu. Ni wajibu wa wazazi na jamii kuhakikisha binti hawi kwenye mazingira ya kubakwa. Wasichana wanalindwa, ila ikitokea hivyo, basi ni kuomba rehema za Mungu.
 
Ni kweli mazingira yamebadilika na ndio maana hata maisha ya ndoa yamebadilika pia. Ndoa zinasambaratika mchana na usiku, malezi ya watoto yamebadilika kabisa. Kitu kimoja tu hakitobadilika kamwe, mke bora kabisa lazima ajifunze kujizuia toka ujanani. Pia ukweli mchungu mi kuwa ndoa na elimu ya mke hazihusiani kabisa. Ndio maana wanawake wengi wasomi wanapata taabu sana kukaa kwenye ndoa, mafundisho ya vyuoni na misingi ya ndoa vimetofautiana kabisa. Chunguza leo!! Uchaguzi ni wako, uoe elimu, pesa au mke wa kukuletea na kukulelea watoto.
Kama suala ni maadili tujiulize,je ni sahihi kwa mwanaume "kudate" na wanawake wengine ,halafu akitaka kuoa atafute "bikra" kwa kigezo cha mke mwema??
Unazungumziaje watoto wa kike wanaobakwa,hawawezi kuwa wake bora huko mbeleni??
 
Huu ni utetezi unaojitokeza kila mara. Mkuu, ndoa sio rehab centre, kwamba unaoa au kuolewa kwa sababu ya kumwonea huruma mtu. Ni wajibu wa wazazi na jamii kuhakikisha binti hawi kwenye mazingira ya kubakwa. Wasichana wanalindwa, ila ikitokea hivyo, basi ni kuomba rehema za Mungu.
Mkuu kwa mujibu wa Waziri Dorothy Gwajima,mwaka 2021 kuanzia ,January hadi December kuliripotiwa matukio 5900 ya ubakaji!!
Hawa ni wanawake 5900 wanaotarajia kuanzisha familia,idadi hii ni ya mwaka mmoja tu,unaona ni sahihi kuwa'judge',kana kwamba walipenda kufanyiwa hivyo??
 
Wakuu amani kwenu.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutaka kujua kama kweli mwanamie/mwanamume fulani anafaa kufunga ndoa naye ama la. Wengi hutaka kujua ni sifa zipi hasa mwenza anapaswa kuwa nazo kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kudumu. Leo nitazungumzia sifa chache muhimu zaidi ambazo wengi hawazioni bali hukimbilia sifa za nje zisizo na uzito.

Kwa wanawake

1. Upendo wa kweli
Sifa kuu na muhimu kabisa anayopaswa kuwa nayo mwanamume ni upendo wa kweli. Mwanamume ameagizwa na kupewa uwezo wa kupenda, hivyo hilo halina majuto kwake, ni sehemu ya maamuzi yake. Kupenda sio sifa ya nje ya mwili (physical) bali ni sifa ya ndani (spiritual). Kama kweli anakupenda hawezi kukulazimisha ulale naye kabla ya ndoa. Tena atakulinda daima dhidi ya mambo yote yanayoweza kuharibu sifa yako njema kama kwenda club, vilevi, marafuki wa hovyo nk. Anapaswa akupende kwa Agape love na sio eros pekee. Usiruhusu akufanye chombo cha kutimizia tamaa zake za kingono kwa ahadi kwamba atakuoa. Kama baba yako mzazi akulindavyo dhidi ya tamaa mbaya, huyu pia anakusudiwa kuja kuchukua jukumu la baba kukulinda, hivyo haipaswi yeye ndiye awe wa kwanza kukushawishi mtende uovu. Kama kweli anakupenda atakulinda.

Mwanamume ajapo kukuposa mbele ya wazazi wako, anaweka ahadi ya kukulinda kwa gharama yoyote ile. Ahadi hii kwa wazazi hufungwa kwa kutoa mahari, kwa mwanamke hufungwa kwa kukuonyesha upendo wa kweli, sio kukutamani kulala na wewe tu.

2. Mahari

Katika zama hizi ukizungumzia mahari utaonekana mwendawazimu. Tumefikia hatua hata baadhi ya wazazi wetu waliokatishwa tamaa na mienendo mibovu ya binti zao kutamani waolewe hata bila mahari. Hili haliji kwa kupenda, bali wanalazimika kuchukua maamuzi hayo. Lakini leo nataka nikuonyeshe umuhimu wa mahari kama msingi mkuu wa ndoa.

Ziko sababu kadhaa kwa nini mwanamume anapaswa kutoa mahari kabla ya kumtwaa mkewe:

a. Muunganiko wa koo
Katika mila za dunia hii, baba ndiye mpokeaji wa mahari, na kama hayupo hai, jukumu hilo hutekelezwa na ndugu wa kiume wa baba. Mama hana nafasi katika hili kwa sababu yeye ameolewa kujenga ukoo wa mumewe, amekuwa familia ya mume, lakini hata hivyo kupokea mahari ni sawa na kuruhusu wakwe wapokee mahari ya ukoo mwingine. Posa inapopokelewa na baba aliye kiongozi wa familia, maana yake ni kuwa amekubali malipo kujiunga na ukoo wa mwanamume. Koo haziungani kwenye sherehe ya harusi, hili haliwezekani kabisa, bali koo huunganishwa na mahari pekee.

b. Shukurani kwa malezi bora
Mahari itolewapo ni namna ya nje kukiri kwamba wazazi wa binti wamemlea katika maadili mema binti yao. Hivyo hutolewa kama namna ya kuonyesha shukrani kwa wazazi kwa juhudi kubwa waliyofanya mpaka kufikia hatua ya binti yao kuolewa. Haya mambo ya kimila kama kununua kitenge cha mama, koti la baba nk ni alama ya ushindi katika malezi kwa wazazi hawa. Ni vitu vidogo lakini vyenye maana kubwa sana. Hiyo mali inayotolewa ni kama fidia kwa gharama alizoingia baba katika kumlea binti yake. Hii haiwezi kamwe kurudusha gharama zote zilizotumika, bali ni ishara tu (symbolic) kwamba sasa binti anatolewa kutoka mamlaka moja kwenda mamlaka nyingine.

c. Ishara ya kupokea jukumu la baba
Kijana anapotoa mahari anamwambia baba wa mzazi kuwa yupo tayari kupokea jukumu la kumlea na kumtunza binti yake. Kabla ya kuolewa, binti alikuwa chini ya mamlaka ya baba, akipewa mahitaji yote muhimu na baba, huku akifuata na kutekeleza kikamilifu maagizo yote kama yalivyotolewa. Sasa kijana anapotoa mahari anamhakikishia baba kuwa naye keshakuwa mtu mzima na sasa yuko tayari kupokea jukumu la malezi ya binti kama baba yake. Kwa lugha nyepesi binti anatoka kwenye uangalizi wa baba yake mzazi anakuwa chini ya uangalizi wa baba mpya ambaye ni mumewe.

d. Nia njema na heshima kwa wazazi
Kijana anapotoa mahari ni ishara ya wazi kuwa moyo wake una kusudi jema juu ya binti huyu. Hii inajenga uaminifu kwa wazazi wa binti kuwa binti yao anaingia kwenye mikono salama kwa kuwa kijana ametambua nafasi yao kwenye mahusiano. Jambo hili pia huwajengea heshima kubwa wazazi wa binti mbele ya jamii na pia humjengea heshima kijana muoaji mbele ya ukoo wa mke na jamii kwa ujumla. Ni ishara ya tabia njema na maadili bora kwa kijana.

∆∆ Sasa kabla hamjanirarua natambua pia kuwa hasa katika zama hizi, kumekuwa na matapeli wa mapenzi, wanaweza hata kutoa mamilioni ya mahari ili tu wamtumie binti watakavyo. Ndio maana ni muhimu wazazi washiriki hatua zote, wao ndio wafanye upembuzi yakinifu\. [/B]

KWA WANAUME

Yako mambo mengi ya nje ambayo mwanamume aweza kuyatazama kwa mwanamke na kuvutiwa nayo, lakini haya mawili ni ya msingi sana katika ustawi wa ndoa na familia:

1. Utii wa kweli
Mwanamke ambaye ana dalili za kuwa mke bora atakuwa na utii utokao moyoni. Amini usiamini hii ndiyo sifa kuu na ya muhimu kabisa. Sasa utaupimaje huo utii? Usidanganyike na jinsi anavyokuchekea, au kujidekeza ukadhani kujionyesha anakupenda ni utii. Haya hufanywa pia na makahaba watakapo kumnasa mwanamume mjinga. Mwanamke hakuwahi kupewa kupenda, ndio maana anabadilika badilika, mke wa ndoa NI LAZIMA awe na utii kama ilivyokuwa kwa baba yake.

Utii unaanzia kwa baba yake mwenyewe, kwani kama binti hawezi kuwaheshimu wazazi, basi hawezi kumheshimu mume, haipo!! Nikisema kumheshimu baba yake ni kwamba binti awe amezingatia taratibu zote za malezi kama alivyoelekezwa na baba yake. Hapo kale na hata sasa kipimo kikuu kwa mwanamke kwamba ana utii ni bikira, kubali au kataa. Haiwezekani binti anayemtii baba yake awe analala na wanaume hovyo kabla ya ndoa. Ukomo wa heshima ya binti kwa wazazi ni kufanya mapenzi na mwanamume kabla ya ndoa. Hapo anahesabiwa kuwa mtu mzima na si mwali tena. Mahari hutolewa kwa mwanamwali, si kila mwanamke, kwani ndilo kusudi la kuwekwa bikira kwa nwanamke. Kwamba mwanamume wa kwanza kuingia atafanya hivyo kwa kumwaga damu kama ishara ya agano la ndoa.

Sasa utaona vijana wengi wanaoa wanawake wasio na bikira huku wakijigamba kuwa ni watulivu, hii ni nadra sana, kwani siku mkipishana kauli, silaha yake ni kutoka nje ya ndoa. Hii ndio njia rahisi kwake kumkomoa na kumuumiza mumewe. Lakini kama hana hayo mazoea kwa vile anamjua mumewe tu, ana nafasi ya kuwa na utii hata nyakati ngumu na linapotokea tatizo atakimbilia kwa wazazi, sio kuvuta hisia za wapenzi wa zamani. Mwanamke kutokuwa na bikira siku ya kuolewa ni ishara ya wazi kuwa hana utii bali hutii anapotaka yeye. Hakuna mwanamume awezaye kumbadili mwanamke kuacha tabia ambayo wazazi wake hawakuweza kumdhibiti. Kama alileta kiburi kwa baba mzazi, basi mume atarajie hayo hayo, huo ndio ukweli.

2. Kumiliki nyumba
Kimsingi mume hujenga jengo kisha mke huligeuza kuwa nyumba. A husband builds a house, a wife turns it into a home. Sifa nyingine ya mchumba bora ni uwezo wake wa kuhimili majukumu ya familia, mapishi, usafi, malezi nk. Kama mwanamke hawezi kutekeleza hayo kikamilifu, basi upendo wa mume utapoa kwake. Kumbuka mchumba ndiye atakuwa mama wa watoto wako, usioe kwa sababu ana matako makubwa kwa sababu matako hayatalea watoto. Tafuta sifa za ndani ambazo zitakuletea kizazi bora.

Mwanamke haolewi kwa sifa ya kipato, ama elimu, bali huolewa kwa uwezo wake wa kutunza familia. Hilo ndilo jukumu lake la msingi na ndilo eneo awezalo kulitawala vema. Kuoa mwanamke kwa kusudi la kusaidiana kutafuta fedha ni sawa tu na kuishi kwenye danguro kwani watoto wenu wataishia kuwa na tabia mbovu. Huu mfumo wa watoto kukelewa na visichana vya kazi ni wa kishetani na ndio chanzo kikuu cha mmomonyoko wa maadili kwenye jamii. Usikubali kunasa kwenye mtego huu, mwanamume kutaka kuoa ni kwamba umejipima ukaona unao uwezo wa kumudu majukumu ya kuwa baba wa familia, sio partner wa familia. Simama kwenye nafasi yako nawe utaheshimiwa.

Baba bora hutafakari kesho ya kizazi chake, sio burudani ya wakati uliopo.

Kwa leo naweka ukomo hapo.

Asanteni.

Andiko zuri sana ILA nasikitika kukwambia haya

mambo yote hayapo kwa Tanzania hii ya sasa
 
Kama suala ni maadili tujiulize,je ni sahihi kwa mwanaume "kudate" na wanawake wengine ,halafu akitaka kuoa atafute "bikra" kwa kigezo cha mke mwema??
Unazungumziaje watoto wa kike wanaobakwa,hawawezi kuwa wake bora huko mbeleni??
1. Kwanza elewa huu utamaduni wa ku date hata Ulaya umeanza majuzi tu, hakuna kitu kama hicho!! Mwanamume akiwa karibu na mwanamke wataishia kitandani tu, tusipende kuiga mambo mradi tu yametoka Ulaya.

Ukiona kijana anatoka na wanawake mbalimbali ni ukosefu wa maadili na sio tabia njema kabisa. Lakini tofauti ipo kimaumbile, hili lazima tukubali, ndio maana hata maandiko yanamlinda sana mwanamke ingawa siku hizi inatafsiriwa kuwa unyanyasaji. Jiulize hivi, mwanamume aliyelala na wanawake 50,halafu mwanamke aliyelala na wanaume 50, yupi kati ya hao ataathirika kimwili na kiroho? Mfano wote wameamua kuachana na maisha hayo watafute wenza, unadhani nani kati yao atapata taabu kupata mwenza wa maisha?

Haya yamekuwa hivyo ili kumlinda mtoto wa kike dhidi ya uharibifu.

2. Mara nyingi kubakwa kwa watoto kunatokea kutokana na wazazi kukimbia majukumu yao, huo ndio ukweli. Umepata kujiuliza kwa nini haya mambo yameshamiri katika zama hizi? Mke ndio mlinzi wa watoto, lakini yeye pia amekimbia jukumu kwa jina la ujasiriamali. Zamani zetu hata mtoto wa kike akibainika kuingiliwa na mwanamume ilikuwa skendo kubwa na kesi ambayo ilikutanisha familia mbili. Mara nyingi zililipwa fidia kwa wazazi kisha harusi iliandaliwa. Kama baba akigundua binti yake ana mahusiano na kijana, zamani hizo mama angekula mkong'oto wa maana kweli kweli kwa kuficha siri za binti yake.

Mtoto akibakwa ni pigo kubwa kwake, anatakiwa kuomba rehema za Mungu na ajizuie asizoelee mchezo huo.
 
Andiko zuri sana ILA nasikitika kukwambia haya

mambo yote hayapo kwa Tanzania hii ya sasa
Kweli kabisa, ila ukweli ndio huo. Sasa hivi tunaiga kila kitu bila kuchuja. Hakuna utaratibu wa malezi ya watoto, wazazi wanajua fika binti zao wanatafunwa, msisitizo wao umekuwa "sitaki mimba". Kwamba wacha wampende binti vile watakavyo mradi asipate mimba tu. Matatizo ya uzazi na kutoshika mimba ni ishara kuwa njia zilifunguliwa kabla hazijakomaa. Ndio baada ya ndoa watu wanabadili makanisa kutafuta mchawi aliyewafunga kizazi
 
Umesema kweli mkuu, kwa binti anayemheshimu na kumtii babaye ni ngumu sana kusex kabla ya ndoa huwa kuna sauti Fulani hivi inakuja, yani unamuona kabisa mzee huyu hapa afu sasa ndo unafanya mbele yake du. Ngumu sana
Kina mama wambieni watoto wenu wakiwa wadogo kuwa bikra INA thamani mkiwaaminisha hivyo watajitunza.

Kuna watu wansema eti siku hizi hakuna bikra, acheni kuharibu akili za washana wadogo wenye nia ya kujitunza. Mabikra wapo tena hats huko vyuoni kuliko jaa ufuska mabikra wapo.
 
Back
Top Bottom