Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
Mrema aliendelea kusema kuwa suala la ufisadi hata Baba wa Taifa alilishindwa kwa sababu baadhi ya viongozi waliokuwa wakifanya naye kazi walipohusishwa na ufisadi aliwahamisha au kuwaongezea majukumu badala ya kuwawajibisha.
Mwingira aliuza ndege ya serikali, mbona Nyerere alimhamisha na kumpa ukuu wa mkoa wa Arusha? Balozi Mustafa Nyanganyi alinunua kivuko kibovu Mwalimu akampa ubalozi wa Marekani; Rais Kikwete amewapeleka watu mahakamani ninyi mnasema mtamtosa! alishangaa Mrema.
....Mrema unapaswa kufahamu kuwa kosa moja halihalalishi jingine...kushindwa kwa Nyerere kupambana na ufisadi si tiketi ya wewe na Kikwete kuhalalisha ufisadi. Hii njaa itakupeleka pabaya........kupeleka watu wachache mahakamani na kusamehe wanaorejesha pesa bila kuchukuliwa hatua si dalili njema hata kidogo. Sasa nimeelewa bora ulivyokosa urais manake inaelekea wewe ni kinyonga na unachohangaikia ni tumbo tu na si masilahi ya taifa kama unavyodai. Shame on you!