Mama Zitto Kabwe amkampenia JK

Status
Not open for further replies.
Simply clueless.
Lakini ni kipi cha kutegemea kutoka kwa watu wasiojua dunia ilipo?? Yaani ni kama kusema mtu aliyezaliwa na kukua huko kwa wahadzabe, upeo wake lazima uendane na mazingira yake.
Haijalishi kuwa mama wa mwana siasa machachari, kama ni mtu asiyejua dunia hii iliko na mambo yake; bado kauli kama hizi hazitakuwa za kushangaza. Yeye, anafikiri Rais kazi yake inaishia tu kutetea walemavu, lakini sera safi na matumizi bora ya rasilimali zilizopo siyo sifa sahihi Rais apaswazo kuwa nazo. Mangapi maswala ya kitaifa yaliyohitaji msimamo/tamko la mkuu huyo wa nchi, yalibaki kunung'unikiwa na wananchi? (EPA, KAGODA, RICHMOND, TANGOLD, CHENGE NA FEDHA NJE YA NCHI, MGODI WA MAKAA YA MAWE KULE MBEYA, MEREMETA, MRADI WA KADI ZA URAIA NCHINI KUCHELEWESHWA NA MASHA n.k.). Labda kama mama huyu ana maana kwamba hakuna mwenye uwezo kiuongozi kumpita kikwete kutoka viongozi waandamizi wa vyama, nitakubali kwamba ni mawazo yake. Lakini siyo kwamba mkuu huyu wa nchi tuliye naye ni hitaji letu mbadala wananchi katika karne hii ya ushindani ndani ya Utandawazi. Tunahitaji mtu mwelewa na tabia ya dunia ma mambo yake kijamii, kiuchumi, kiutamaduni n.k. Lakini pia asiishie kuelewa tu, awe mchambuzi mzuri wa kutambua dira ipi inafaa katika kuiongoza nchi kwa kuzingatia yaliyopo duniani na yale Tanzania iliyo nayo na isiyo nayo.
 
Waooo, nimekubali " In politic there is neither permanent rival nor permanent friend, always there is permanent individual interest"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom