Mama, "Kwani si tunaalika watu kuhalalisha hilo hilo (tendo la Ndowa)"

Nani amekuambia ndoa imeanzishwa na Mungu?Vp kama siamini uwepo wa Mungu?Huwezi kuona unazidisha mkanganyiko unapoihusisha dhana hii?

Hata kama wewe huamini uwepo wa Mungu haibadilishi kitu. Kuamini kwako kuwa kuna Mungu au hakuna Mungu hakubadishi chochote. Ni sawa na mtu anayesema haamini kuwa gari za brand ya Toyota zimetengenezwa Japan. Kutokuamini kwa mtu huyo hakubadili ukweli huo. Wewe umeumbwa na Mungu na kuna vitu Mungu aliyekuumba ameviwekea guidelines. Unaweza kuchagua kuamini au kutoamini lakini huwezi kuchagua madhara ya uamuzi wako
 
Hebu nithibitishie kama Mungu yupo halafu tutajadili suala la ndoa!
 
Hebu nithibitishie kama Mungu yupo halafu tutajadili suala la ndoa!

nithibitishie kwanza kama wewe kweli umezaliwa na mwanamke ndo na mimi nikuthibitishie Mungu yupo. Nithibitishie kuwa miaka michache iliyopita ulikuwa damudamu tu ndani ya tumbo la mwanamke fulani
 
nithibitishie kwanza kama wewe kweli umezaliwa na mwanamke ndo na mimi nikuthibitishie Mungu yupo. Nithibitishie kuwa miaka michache iliyopita ulikuwa damudamu tu ndani ya tumbo la mwanamke fulani

Huku ni kushindwa hoja,unaulizwa swali badala ya kujibu unauliza swali,acha uswahili kijana,jibu swali!
 
Ngekewa,sikubaliani na suala la mwanamke kudai talaka,kwanini adai?Kwani hawezi kutoa?Ndoa ikimuumiza mwanamke hawezi kutoka?Mwanaume akiwa mlevi na mfujaji mwanamke afanye nini?Asubiri mpaka apewe talaka?

Naam anaweza kutowa. Kwani anapoamuwa kuondoka na akafanya taratibu ya kuformalize kutengana si ameshatowa talaka au unataka aiandike hiyo talaka ndio ufahamu uwezo wake wa kutaliki? Mwanamke au mwanammme anapoamuwa kuingia kwenye ndowa anakubali taratibu zilizowekwa hivyo unapotaka kuwa kila mtu afanye anavyotaka tu eti ana uhuru huwezikueleweka kwani binaadamu tunaishi kwa taratibu.
Unaona tatizo mwanamke kutotowa talaka kwa huo mfumo unaoutaka lakini husemi kuwa sasa wanawake wawe wanatowa mahari ili kuowa.
 
nani kasema ndoa (si ndowa) ni kitu kibaya?

Nasisitiza tena, kila mtu ana mipango yake katika maisha kama wewe unavyosema imani yangu si sawa na imani yako.

Kwa hiyo, kuna wengine wanaona ndoa si kitu kibaya, wengine wanaona ndoa ni kitu kibaya, inategemea umesiamamia wapi.Shilingi moja nikiiangalia kutoa sentimeta 15 na mwingine akiiangalia hiyo hiyo kutoka meta kumi, tutaiona tofauti.Maji hayo hayo kutegemea na nyuzijoto yanaweza kuwa maji, barafu aua mvuke. Sasa wewe huwezi kumwambia mtu "haya ni maji kwa sababu yameundwa na H2O, wakati yeye anaona H2O, lakini kwa sababu ya nyuzijoto anaona mvuke, na mwingine anaona kwake barafu.

Ndiyo maana nashangaa wanaotaka kuoa/kuolewa liwe jambo la lazima. Na wanaofikiri mtoto wa kike ni lazima atake kuolewa.

Wanakuwa wamekariri kama yule aliyekariri kwamba H2O ni lazima iwe maji bila kujali nyuzijoto gani tunaongelea.

Hatujasema kuwa kuna ulazima wa kuowa au kuolewa, tunachosema ni kipi jamii kinaona ni bora. Ubora wa kimoja wapo uje kutokana na kuangalia nyanja tofauti za maisha ya jamii tunayoishi.
Concept ya mtu kwa jambo inaweza ikawa nzuri kwa ke ili kujiepusha na mambo fulani lakini mwisho wa siku mtu analazimika kuelewa kuwa anaishi na binaadamu wengine walio na concept tofauti na yake.
 
Ila hili neno ustaarabu silipendi kabisa!Linatukuza watu fulani!Utumwa!

Pengine kama ulivyosema kuwa hii lugha ndiyo tatizo lako, lakini hili la binaadamu kuishi kwa utaratibu unaokubalika na jamii pia linatukuza watu fulani? Hebu ipe hii concept jina jengine ili usizidi kuchukia.
 
Ngekewa,tatizo langu ni mfumo unaomnyima mwanamke kutoa talaka hata kama ndoa inamuumiza.Ataambiwa afuate "taratibu" kuomba talaka,je akinyimwa?Huu uataratibu uko kwenye jamii kwamba anaetoa talaka ni mwanaume tu,kwanini?Tatizo langu ni huo mfumo,ndo napingana nao,hata wakati wa ukoloni mfumo ndo uliokua unamnyima mtu mweusi haki.Kwenye masuala ya mahari nako kuna matatizo yake,kuna wakati niliwahi kutoa wazo mahari ifutwe.Nilisema hayo kwa sababu inakua kama unamnunua mwanamke.Halafu kwanza mahari ni kwaajili ya nini?
 
Hawa watu ni wa hovyo sana,neno linalowakilisha mambo mema wameyapa maneno ya kuwatukuza wao.Kwanini wizi wasingeita usta-Arabu?
 
Hawa watu ni wa hovyo sana,neno linalowakilisha mambo mema wameyapa maneno ya kuwatukuza wao.Kwanini wizi wasingeita usta-Arabu?

Haya ni matokeo ya kutokuwa na nadharia ndani ya jamii. Mbona neno utumwa halikutoka huko kwavile tulikuwa na nadharia ya utumwa. Hatuwezi kuchukia neno eti limetoka pahala fulani pengine tungechukia nadharia mbaya iliyoletwa ndani ya jamii.
 
Ngekewa,tatizo langu ni mfumo unaomnyima mwanamke kutoa talaka hata kama ndoa inamuumiza.Ataambiwa afuate "taratibu" kuomba talaka,je akinyimwa?Huu uataratibu uko kwenye jamii kwamba anaetoa talaka ni mwanaume tu,kwanini?Tatizo langu ni huo mfumo,ndo napingana nao,hata wakati wa ukoloni mfumo ndo uliokua unamnyima mtu mweusi haki.Kwenye masuala ya mahari nako kuna matatizo yake,kuna wakati niliwahi kutoa wazo mahari ifutwe.Nilisema hayo kwa sababu inakua kama unamnunua mwanamke.Halafu kwanza mahari ni kwaajili ya nini?

Binaadamu wanapoweka utaratibu usitegemee kuwa utaratibu huo utatowa nafasi sawa kwa maana ya 1=1 lakini kutakuwa na makubaliano ya give and take ambapo kila mmoja ataridhika kukoseshwa jambo kwa kupata jambo. Siamini, lakini umejidai huamini Mungu, Yeye alieumba aliumba viumbe viwili hivi tofauti lakini vinavyojitegemea. Sasa utawezaje kuzalisha kitu kinachohitaji -na + kwa kutumia muungano wa kimojawapo?
Unajuwa nadharia ni nadharia lakini unapokuja kwenye ukweli basi ukweli ndio utakaokuja juu. Hebu fikiria huko tulikotoka katika dunia yetu kulikuwa na wanadharia chungu nzima waliopingana na ukweli na wamebaki kupigiwa mfano kinadharia lakini hawana lolote la kuionyesha dunia kwa nadharia zao.
 
Ngekewa,binadamu gani anakubaliana na makubaliano ya hovyo namna hii?Walikaa lini na wapi na mwanamke aliwakilishwa na nani?Acha uongo.Suala la Mungu usililete hapa maana umeshindwa kunithibitishia uwepo wake!
 
Haya ni matokeo ya kutokuwa na nadharia ndani ya jamii. Mbona neno utumwa halikutoka huko kwavile tulikuwa na nadharia ya utumwa. Hatuwezi kuchukia neno eti limetoka pahala fulani pengine tungechukia nadharia mbaya iliyoletwa ndani ya jamii.

Unajichanganya changanya tu!
 
Unajichanganya changanya tu!

Nipo wazi kama unataka kunielewa. Walioleta nadharia ( kwa kukunakili wewe, usta-arabu) ndio walioleta hilo neno kwa vile pengine sisi hatukuwa na nadharia hiyo. Na neno utumwa ni neno letu wenyewe kwani tulikuwa na utumwa kabla ya kuja wageni hapa kwetu.
 
Yes,tatizo langu ni hao hao walioleta neno hilo,walileta kwa madhumuni maalum na lengo maalun.Fungua akili yako kijana!
 
Back
Top Bottom