Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,702
Kiranga nimekuelewa,kuhusu neno "kuoa" au "kuolewa" wewe unalitafsiri vipi?Kuhusu mwanamke kutokuacha nafikiri hiyo inatokana na imani fulani,sidhani kama tunaweza lizungumzia hapa.Hayo maneno ya kiswahili bado sijaona ubaya wake,tatizo tunayachukulia kutokana na dhana ya mwanamke kutokutoa talaka ambayo kama nilivyosema ni dhana ya imani fulani tena moja tu.Kwenye mfumo dume hapo napo kuna mkanganyiko.Mwanaume na mambo ya kiume.Mwanamke na mambo ya kike.Tukubali kuwa mwanamke anapoambiwa "acha kufanya mambo ya kiume" ni sifa?Sidhani,pia mwanaume anapoambiwa acha mambo ya kike,sio aibu.Unapoyataja mambo ya kikekike wewe ndie unaamua yawe tusi,kashfa au vinginevyo.Tafsiri iliyoko kichwani mwako.Lakini pia huu mfumo unaoitwa dume una mambo mengi lakini mengi zaidi yapo vichwani mwetu zaidi,sio halisi!