Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere

Makongoro aelimishwe ya kuwa ndani ya kanisani NDOA haivunjwi na mwanadamu. Kiroho Madaraka na Letisia ni wanandoa na kama wanatembea nje kati yao basi huyo ni mzinifu tu.

Mimi sikujua ya kuwa Makongoro anaupeo finyu hivyo yaani mambo ya ndoa yanatoka wapi na sifa za kuwa mbungeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Jamani mimi nina kondoo wawili sijui niwafanyeje lakini ningependa kumtumia Makongoro awachunge maana sioni kazi nyingine awezayo kufanyaaaaaaaaaa LETICIA TUNAMWOMBEA ASHINDE HICHO KITI CHA UBUNGE HALAFU AWAALIKE MASHEMEJI ZAKE KWENYE KARAMUUUUUU
 
Watu mnafurahisha kweli
Kwa hiyo ya slaa na mchumba wake ni special case , sio?? mhh uwalakini mkubwa sana ninyi mkipewa nchi kuongoza, tena sanaa
 
MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.

Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.

Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

Alisema serikali imeshughulikia jambo hilo, kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa.

"Ufisadi ni sawa na kibaka, fisadi anaweza kuwa upande wowote, mbona hata kwao wana mafisadi kibao,ufisadi ni tabia ya mtu,CCM iko safi na ndio maana tumekuwa tukiendesha kampeni zetu kwa ustaarabu bila kutumia matusi. Wnanchi msidanganywe na hoja ya ufisadi mwacheni Dk Slaa aendelee kupiga kelele kuhusu ufisadi,",alisema.

Kwa upande wake, Mansoor alisema akichaguliwa kuwa mbunge, atamaliza matatizo ya maji, huduma za afya na upungufu wa walimu katika shule za jimbo hilo.

markooooo%!?????
 
Yaliyofanywa na Makongoro ni unyanyasaji mkubwa kijinsia. Leticia anazo haki zote za kutumia jina la Nyerere kwa sababu alifunga ndoa takatifu katika kanisa Katoliki. Kuingiza mambo ya ndoa ya mtu kwenye mambo ya siasa ni dalili za kufilisika. Mwacheni Leticia ahukumiwe na achaguliwe na wananchi kwa uwezo wake binafsi. Naamini kabisa Mzee Kambarage Nyerere angelikuwa hai wala Makongoro asingethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumchafua shemejiye. Makongoro amejiaibisha sana!

Ndio mtia nia wa CCM huyo.
 
makongoro nyerere naye analaana kutoka kwa baba wa taifa amekuwa anaropoka Hovyo kila siku mara lowasa mara leticia nyerere
 
Makongoro huyu ndie anataka kua Rais. Busara kidogo . Leticia ana wtt na madaraka leo hii unamkashifu mama wa watoto wenu. Wajukuu wa baba wa Taifa aibu
 
Kwa hiyo yeye kaingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais akitegemea kubebwa na jina la Nyerere siyo?

Makongoro miongoni mwa watia nia wa CCM ndiye niliyekuwa namwona ana nafuu kidogo, lakini kwa hili nimeshamwondoa kwenye orodha yangu.

Na very funny kwamba anajaribu kutetea ufisadi ndani ya CCM na serikalini kwa kumnanga Dr W.P. Slaa kwa kigezo cha eti serikali ya awamu ya nne chini ya Kikwete imeushughulikia, na wakati huohuo anawatukana wenzake hadharani kina Lowassa!

Kiukweli, CCM hakuna kitu......wote ni wezi tu na wasanii wa kutupwa.....hawatufai tena!!!
 
[QUOTE=mikela;1086606]MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba...

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu. …

Kwa upande wake, Mansoor alisema akichaguliwa kuwa mbunge, atamaliza matatizo ya maji, huduma za afya na upungufu wa walimu katika shule za jimbo hilo.

MAONI YANGU:
Mbunge aliyemaliza muda wake, Mh B Sakira, aliwahi kulalamikia mchakato wa kura za maoni kuwa rushwa ilitumika na ya kwamba TAKUKURU haikujihusisha na kufuatilia sakata hilo japokuwa ushahidi ulikuwepo wazi. Na aliyeshinda katika kura hizo ni Shanif ambaye ni mtanzania mwenye asili ya india. Shanif Mansoor anaishi jijini Mwanza na ni mfanya biashara.

Mimi nashindwa kuelewa kilichopelekea Mh Makongoro kwenda kumpa support Mansoor…je ni chuki dhidi ya shemeji yake ? au ni pesa (ambazo nadhani anazo za kutosha) au ni shinikizo la chama kumsaidia huyo mfanya biashara aweze kukabiliana na upepo wa upinzani? Sina jibu sahihi, lakiniMakongoro atakuwa ame-miss step kama wasemaji wengine hapo juu walivyosema. Hili jambo linaanza kuibua hoja za uhalali wa baba wa taifa kutumia jina la Nyerere na vilevile yeye mwenyewe (Makongoro) kujiita ni motto wa baba wa taifa. Haya yanamdhalilisha yeye na mama na ukoo mzima.

Siasa ni mchezo mchafu na sasa hivi ukijiingiza kichwakichwa kwenye siasa hakikisha umejikagua vizuri na kunawa uso wako sawasawa, vinginevo unaweza kujichafua sana. Makongoro arudi Mara akatulie. Watu wana hasira na CCM na umasikini katika nchi tajiri.

Hata hivyo kwa maoni yangu sasa hivi wamempa umaarufu zaidi, kwasababu wengine tulikuwa tunadhani ni motto wa Nyerere mwingine kwasababu jina hilo sasa hivi linatumiwa na wengi tu wasio na ukoo na baba wa taifa. Lakini Makongoro ndio ametujulisha kuwa ni shemeji yake na amezaa wajukuu 3 wa nyerere. Ningekuwa mimi ni mwenyeji wa huko ndio ningempa kura yangu huyo mama ikiwa ni pamoja na kumpigia kampeini ya nguvu zzanhu zote. [/QUOTE]

LA ziada tume ya uchaguzi wako wapi CCM wanazindua campaign za ubunge?
 
Sasa alichokosea nini hapo na wote ni wanasiasa? tatizo humu ndani hamuijui siasa ya vyama, matamko ya kisiasa hujibiwa kisiasa na umalizwa kisiasa ..hayo mengine ni mbwembwe tu za nyinyi mliosoma sanaa alafu leo mnajifanya kuijua siasa, Political Science ni fani jamani kama hauiwezi iache ikiwa safi.
 
mtu mzima anajikojolea tena mbele za watu... huyu chizi kweli kweli...!!!!

Akili za gongo, mbaya sana... !!!!
 
huyo shanif yukoje jamani ? hebu tumuone , je huwa anahudhuria vikao vya bunge au yuko kama mohamed dewji ?
 
Duh kwa uwezo wake huu wa kufikiri alafu anataka kuvaa buti za baba ake anataka akakae pale Magogoni kama baba ake.
 
Makongoro hayupo vizuri upstairs maskini... Ni jambo la kawaida katika familia ya watoto wengi
 
Kumbe na Makongoro naye anashriki kugawa pesa za mhindi kwa wanakwimba ili achaguliwe teenaaaa! Alafu anajiita msafi!!
 
Aiseee kwa kweli Makongoro ni jembe, kumbe hii tabia ya kutoogopa mtu ni ya asili kabisa!! This was 2010 lakini the guy calls a spade a spade, khaaa!! Safi sana Makongoro. Na kwa Tanzania yetu hii sasa, huyu ndo anayetufaa hasa, mafisadi hakika watakiona jamaa akipitishwa, yaani ni kama baba yake alivyokuwa haogopi makaburu na wazungu wanafiki.

Mimi watu wenye misimamo nawapenda sana, hasa wanaoonyesha msimamo kwa ajili ya kunyoosha jambo lilopinda. Sipendi mtu wa kuuma uma maneno au kulia lia wakati ni wazi jambo limepinda.

Mi naendea kumuomba Mwenyezi Mungu Makongoro awe Prezidaaa halafu PM awe Makongoro, katikati pale kwa maana ya Makamu akaye Jaji Ramadhani, hakina nchi hii itasogea hatua nyingi tu mbele. Wazalendo wananielewa nachomaanisha, ila timu fisadi najua kabisa hawapendi hii combination
 
Back
Top Bottom