Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Deogratius Ndejembi wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Daudi Charle's Nyerere mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charle's Makongoro Nyerere wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwao Mtaa wa Haile - Sillas Jijini Arusha Novemba 02, 2023.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mb), Jumanne Sagini ameshiriki mazishi ya Marehemu Daudi Charle’s Nyerere mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charle's Makongoro Nyerere na Mjukuu wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, yaliyofanyika Novemba 02, 2023 nyumbani kwao Mtaa wa Haile - Sillas Jijini Arusha.
Akizungumza katika mazishi hayo, Naibu Waziri Sagini ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kuwaomba wazidi kumuombea aendelee kupumzika kwa amani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini akiwafariji wazazi wa marehemu Daudi Charle's Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere na Mkewe Jaji Mstaafu, Aisha Nyerere wakati wa ibada maalum ya mazishi iliyofanyika Novemba 02, 2023 nyumbani kwao Mtaa wa Haile - Sillas Jijini Arusha.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Deogratius Ndejembi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Majaji pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Vyama vya Kisiasa na Kidini.
Marehemu Daudi, alifariki siku ya Jumapili Oktoba 29, 2023 kwa ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya By-pass Jijini Arusha.