Makazi ya Mbowe huko Machame yatufunze kujitegemea siyo kuiba mali za umma kama wafanyavyo wanasiasa wengi nchini

Mbowe huyu wa chadema au kuna mbowe new model tusiemjua?!

Bro, unajua pesa za CHADEMA huwa zinatumikaje?!

Mchagga na udokozi ni kama moto na majivu, haviachani.
Nyumba inaonekana mpya na mbowe ni mfanyabiashara angeshajenha tangu miaka ya ya 90...Hapo watu washapigwa hao wengine wanaforce tabasamu ila ukweli wanaujua jamaa ananipa pension ana miaka kama 61 sasa.😅😅
 
Kitendo cha kujenga kijijini alipozaliwa ni Ishara kwamba tulipozaliwa ni muhimu kuliko tulipokulia au tunapigia mishemishe.

Wote tungejenga makwetu na kupaendeleza leo tusingekuwa na vijiji tungekuwa na mitaa nchi nzima

Wapo viongozi hapa nchini hata nyumba ya kawaida tu kwao hawana. Mawaziri wengi vijijini kwao hakuna nyumba, wabunge ndo usiseme bila kusahau makatibu wakuu na wakurugenzi .


Tungekuwa na sera yakujenga vijijini hata umeme na maji, barabara na huduma za afya isingekuwa shida

Ile nyumba ya Mbowe haikosi umeme, maji yapo, hospital lazima ipo karibu nk

Ila vyote hivyo vimepelekwa kwa sababu watu wamewekeza

Sisi watu wa kanda ya ziwa tutaendelea kulalamika ila ukweli lazima tukubali vijijini tulipotoka.......JPM alifanya kile mwanasiasa anapaswa kufanya kwao......let us think about our home villages
Sasa maendeleo huwa hayaji kwa namna hiyo. Watu kutokujenga vijiji wanapotokea sio sababu ya msingi kwa vijiji hivyo kutoendelea bali hicho ni kisingizio. Watu wanaendelea kwa kuhama eneo moja na kwenda kwingine kupeleka nguvu kazi na kukiwa na Halimashauri imara zenye weledi kiitendaji mbona maendeleo yanatokea bila shida.
 
Nyumbani kwa Mbowe ni reflection ya utajiri na ukwasi usiotegemea fadhila za dola wala uteuzi. Huyu mwamba ameishi maisha yake, amepigania haki usiku na mchana na siku zote za vita hakuna siku tumewahi kumsikia akilia kufilisika au kukosa ukwasi wa kumfanya ajisalimishe kwa watawala.

Tofauti ya Mbowe na viongozi wengi wa chama tawala, Mbowe anasimamia biashara zake mwenyewe, analipa kodi zote muhimu na anajiendesha kwa kuzingatia sheria za nchi.

Wakati huo viongozi wa chama tawala wengi wanachofanya nikuiba na kula ; hawana muda wa nafasi ya kuziendeleza mali zao. Kila siku wanabaki kuwa watumwa wa mtawala wasikamatwe kwa wizi, ubadhirifu na ukwepaji wa kodi.

Vijana mnapotafakari kesho yenu, tangulizeni kwanza fikra na nguvu katika kutafuta utajiri wa haki ndipo mgombee nafasi za kuongoza watu kwa haki.

Mzee Mbowe na familia yake wanatufundisha umuhimu wa kujitegemea. Uteuzi iwe Sehemu tu ratiba ya maisha ila siyo maisha. Usipojifunza kusimama mwenyewe watakuoshiriki kukusimamisha lazima wakupe adhabu ya kulipa fadhila na kuwaabudu

Makazi ya Mbowe, utajiri wake na roho yake ikawe dira ya kutafuta utajiri na madaraka ya haki
Inasemekana 2015 alipewa billion 12 Ili amwachie llowasa agombee urais !!
 
Inasemekana 2015 alipewa billion 12 Ili amwachie llowasa agombee urais !!
Mbowe ndo CHADEMA na CHADEMA ndo Mbowe. Ndani ya CHADEMA Mbowe ni kama sheria. Akishatamka hakuna kima mwingine yeyote atakayebisha. Hii agenda yao ya katiba ni ya kupuuzwa kwasababu wao wenyewe hawafuati katiba yao. Katiba yao ni Mbowe.
 
Kuna watoto wa buku mbili wanamchukulia Freeman Mbowe kama mwenzao.

Hapa ni nyumbani kwake kijijini Machame huko kwenye mashamba ya ndizi, Kilimanjaro.

Mwaka 1991 alifunga ndoa ya kifahari sana huku akiwa mdhamini mkuu wa Yanga.

Freeman Mbowe is a living legend.

IMG_8714.jpeg
 
Back
Top Bottom