Kuuza lango la uchumi wa nchi ni usaliti mkubwa katika kuvunja katiba ya nchi, Bandari ni mali za Watanzania wote

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139
DUBAI PORT.jpg

KUUZA LANGO LA UCHUMI WA NCHI AU KUTAFUTA WANAHISA NI USALITI MKUBWA KATIKA KUVUNJA KATIBA YA NCHI: BANDARI NI MALI ZA WATANZANIA WOTE HATUNA WANAHISA (SHAREHOLDERS) NA HATUHITAJI WANAHISA.

WARAKA WA WAZI KWA WAHESHIMIWA WABUNGE
NAKALA KWA WAHESHIMIWA VIONGOZI WA DINI
NAKALA KWA TAASISI YA MWALIMU NYERERE CHINI YA MZEE JOSEPH BUTIKU
NAKALA KWA VIONGOZI WA CCM
NAKALA KWA WASOMI WOTE NCHINI
NAKALA KWA UMMA WA WATANZANIA
NAKALA KWA WAPENDA AMANI DUNIANI KOTE

Jumuiya ya Wanazuoni nchini ambao tumekaa pamoja kutoka vyuo vikuu mbali mbali kutimiza wajibu wetu kama katiba ya Nchi inavyotaka pamoja na ya Chama Tawala iliyorisi misingi ya TANU kwamba nitajielimisha kwa uwezo wangu wote kwa manufaa ya nchi yangu na Elimu yangu ni kwa manufaa ya Taifa. Wanazuoni tunaanza kwa kutumia busara na kujenga hoja mahususi kupinga nchi yetu kuuzwa kienyeji kwa kisingizio cha mashirikiano ya Nchi yetu na Nchi za Falme ya Kiarabu. Hoja zetu ni kama ifuatavyo;

Kwanza; Bandari zetu zote ni mali za Watanzania zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuna ubia na mtu yoyote wala Taifa lolote. Wanazuoni baada ya kusoma kwa kina kile kinachoitwa mkataba wa kubadilisha uendeshaji wa Bandari zetu na kwa jinsi tulivyofuatilia hoja mbali mbali za wanaunga mkono na wanaopinga, Wanazuoni tunapenda kutoa tafsiri sahihi ya hicho kinachoitwa mkataba kwa lugha rahisi , Wanazuoni tumetafsiri kuwa ni kitendo cha kuuza Nchi kwa bei rahisi sana na kuingiza mwanahisa mpya kwenye umiliki wa Bandari zetu ambao utakuwa umiliki wa milele au wa muda husiokuwa na kikomo maana hata waziri ameshindwa kusema huo mkataba utakwisha lini? Tafsiri yetu inatokana na jinsi hao wanaoitwa washirika wanavyogawiwa bure Bandari zetu eti kwa kigezo wanajua kuendesha Bandari. Hata kama wanaleta mtaji bado kwa kupewa mkataba tu kwao ni pesa na watapata mikopo midogo na mikubwa huko Duniani kwa kutumia Bandari zetu.

Kwa kuwa Waheshimiwa Wabunge wameamua kulisariti Taifa na kupitisha ridhio la makubaliano hayo wajue kuwa mkataba huo utalindwa na sheria za Kimataifa huwezi kuuvunja na ukifanya hivyo Nchi itaingia kwenye Vita maana kila upande wa umiliki wa Bandari utatumia jeshi kulinda haki zake za kiuchumi (economic interests). Hoja yetu ya msingi hapa kuwa tutapoteza umiliki ambao tulipewa na Mungu “Sovereign ownership of the ports”. Wanazuoni tunasikitika kwani serikali zilizotangulia zote zimewekeza sana kwenye maboresho ya Bandari zetu kwa kiwango cha juu mno kwa viwango vya Afrika. Ni ujinga (ignorance) wa kiwango cha juu sana kujilinganisha na Nchi za Falme za Kiarabu (Emirates au Dubai) ambazo zinamilikiwa na falme au koo(familia). Ni rahisi sana Mabeberu wa Kimarekani kujificha kwenye kivuli cha Falme za Kiarabu au Vivyo hivyo hata Umoja wa Ulaya ambao wanao mkataba mbovu wa EPA uliokataliwa na Afrika nao ni rahisi sana kuwa kwenye kivuli cha Falme za Kiarabu au Dubai.

Kumbuka Umoja wa Ulaya ulitumia pesa nyingi na muda wa miaka mingi kutaka moja ya masharti yao ya EPA ni kutumia Bandari zetu bila malipo yoyote as Free ports for European goods/products. Ukizingatia uchumi wa Marekani na Umoja wa Ulaya upo kwenye kipindi kigumu sana kuliko wakati wowote. Marekani na Umoja wa Ulaya wanaongezeko kubwa la umasikini, ukosefu wa Ajira na wamezidiwa na China katika uzalishaji viwandani (Manufacturing industries). Hivyo basi , sehemu pekee ya wao kupona na kushindana na China ni kupora utajiri wa Tanzania (Afrika) na kuendeleza unyonyaji ili waweze kuwatunza wazungu wenzao kwa kuwapa sera kinga (social Protection policies). Cha ajabu kubwa na ya karne Tanzania ambayo inataka kugawa Bandari zetu Bure kwa madalali wa Dubai ni moja ya Nchi Duniani ambayo haina sera kinga kwa watu wake na hasa makundi maalum (Lack of National Social Protection Policy). Ina viproject kama vile TASAF nayo inategemea pesa za wafadhili na mikopo ya Benki ya Dunia.

Lakini kwa Wazungu wa Ulaya na Wamarekani wanazo sera kinga ambazo zinalipiwa na pesa za Serikali za Walipa kodi wao na nyingine wanapora nje ya Nchi kama vile Ufaransa inavyopora west Afrika. . Na hii inawezekana tu kwa kuendelea kupora rasimali za Afrika na kupora uchumi wa Nchi zetu. Wanajua wakichukua Bandari zote za Tanzania watakuwa wanamiliki uchumi wa Nchi Karibia kumi zinazotegemea Bandari zetu kwa sababu Nchi yetu ipo kijiographia eneo la kimkakati sana na ndiyo moyo wa Nchi zote zinazotuzunguka.

Ukiharibu uchumi wa Tanzania na Amani ya Tanzania umeharibu uchumi wa majirani zetu, Rejea Wosia wa Baba Taifa Mwalimu Nyerere kwenye hotuba aliyotoa SADC mwaka 1984 ikiwa sehemu ya kuaga kama Mkuu wa Nchi. Hivyo Wanazuoni tunawaomba Waheshimiwa Wabunge wetu wakatae kabisa siyo tu kubadili vipengele vya mkataba waachane kabisa kucheza na Taifa letu maana historia itawahukumu vibaya sana. Wajifunze Libya jinsi Mabeberu walivyowatumia wanasiasa na kuharibu Taifa lile. Ukiingiza Mabeberu wa kimarekani na Ulaya kwenye umiliki wa Nchi kama wanahisa wa Bandari zetu kwa mgongo wa Madalali wa Vinchi vya Falme za Kiarabu vinavyomilikiwa na kuendeshwa na familia za Kifalme ujue umeuza Nchi kabisa na Rushwa waliokupa utajuta maana watakutupa mbali na kutafuta serikali ya kulinda masilahi yao ya kiuchumi. Na hiki ndicho kitakuwa kifo cha chama Cha Mapinduzi na laana ya Waasisi na Watangulizi itatutafuna na kuwatafuna wabunge wote pamoja na spika wao. Mungu tuepushe laana hii. Ndiyo maana tunawaomba wazee wa Taifa hili kupitia Mwalimu Nyerere Foundation wajaribu kumshauri Mh. Rais aweze kupata Neema ya kuona hatari tunayoiona. Wazee mkikaa kimya Taifa letu likauzwa basi mjue nanyi historia haiwezi kuwaacha salama nyinyi na vizazi vyenu.

Hoja ya pili ya Wanazuoni ni kwamba Uchumi wa Tanzania tangia awamu zilizopita na kuchagizwa na awamu ya Tano imeweka Miundo Mbinu mikubwa sana ya Matrilioni ya Shilingi. Tumejenga reli ya Kisasa na tunamiliki wenyewe hatuna ubia, tumejenga vyanzo vya umeme ili kuweza kuendesha Treini za umeme. Tumewekeza sana kuboresha Bandari zetu kwa uwekezaji wa matrilioni ya shilingi na hatuna ubia. Tunahitaji kuendesha wenyewe Bandari na kutumia treini ya umeme kufikisha mizigo ndani ya masaa 20 kwenye Nchi zinazotuzunguka na tutaweza kupata pesa nyingi za kulipa madeni ya miundo mbinu. Ukiweka mbia yaani shareholder kwenye Bandari zetu hutaweza kucontrol mapato na matumizi ili uweze kulipa deni.

Hawa Madalali wa mabeberu wa Vinchi vya Falme za Kiarabu watapewa mgao wao yaani dividends na Tanzania itapewa dividends na tutakuwa wajinga kusaini mikataba kama iliyosainiwa na Kar Peter karne za 14 na Chifu Mangungo wa Msovero. Mikataba siyo tu ya kitapeli bali ni ya kinyonyaji maana thamani ya Bandari ni kubwa mno ni Sovereign wealth na hawa madalali wa Mabeberu watatumia bandari zetu kukopa Duniani hawaji na chochote bali pesa za kuwahonga viongozi wetu pamoja na kuwapa ahadi hewa za umiliki sehemu ya shares. Watawatupa nje kama Mobutu wa Congo zamani Zaire. Imperialists have permanent interests not permanent friends. Baada ya miaka ishirini Nchi itakuwa imeuzwa kabisa kwa Mabeberu ambao watajitanua sana na tutajiingiza kwenye mgongoro wa kiuchumi wa Kimtaifa (Geo political conflicts among imperialists powers). Tujifunze kwa Ufaransa na Nchi walizozitawala wanaendelea kuzinyonya kiuchumi. Hivyo basi tunawaomba Waheshimiwa Wabunge tusikubali kupuuza ushauri huu wa wasomi na kukubali mawazo ya kijinga ya wanaojiita darasa la saba ambao hawana uelewa wa uchumi wa Dunia na vita ya kiuchumi Duniani.

Hoja ya tatu ya Wanazuoni kwa Waheshimiwa Wabunge ni kuomba kabisa kukataa kabisa kutumika kuuza Nchi. Tunapinga hoja ya kusema kuwa wenzetu wana mitaji na technolojia hivyo tutaboresha uendeshaji siyo kweli. Hatuwezi kujilinganisha na Vinchi vinavyomilikiwa na familia za Kifalme ambavyo ni madalali wa mabeberu. Tutaboresha kwa viwango vyetu na tunaweza kuajili mtu yoyote kutoka dunia kuboresha uendeshaji. Tunaweza kuajili Mzungu, au Mhindi, au Mwarabu au Mkorea au MwaAfrika yoyote na tunaweza kununua technolojia popote duniani na kuweka mifumo ya Komputer ili kuondoa kero na Rushwa Bandarini. Mkataba wa TICS wa zamani husitumike kama kigezo siyo kweli, hata TICS hatutaki iwepo kabisa tunatakiwa kuimarisha mamlaka ya Bandari Nchni. Ni Ujinga wa kiwango cha Uprofesa au PhD kwa kudhani kuuza Nchi kwa kumpa mtu ubia ili aweze kuendesha Bandari zetu kwa niaba ni jambo zuri. Tutakuwa tumewasaliti watanzania. Waheshimiwa wabunge mkataba huo hata ukimpa GSM au mfanyabiashara mmarufu Mzee Bharesa au Jumuiya ya Wafanya biashara Nchini watafanya maboresho na utajiri utabaki hapa hapa na usalama wa Taifa utabaki pale pale. Huhitaji kuwa Profesa wa Uchumi kuona kuwa mkataba tajwa ni utapeli wa kimataifa na kuuza Nchi kienyeji ni mtu mjinga pekee anayeweza kukubali bila kupovushwa na Rushwa kubwa (grand corruption).

Hoja ya Nne kutoka kwa Wanazuoni, tunakataa Madalali wa Kiarabu wanaotumiwa na Mabeberu na wanaomiliki Vinchi vyao kupitia familia za kifalme zenye idadi ya watu ndogo na wote wananufaika na utajiri wa Nchi zao, mfano Dubai watu milioni mbili tu na wote wanatunzwa na serikali ya kifalme. Hivyo Social anthropology ya WaAfrika na WaTanzania ni tofauti na hao WaArabu kabisa kwa idadi ya watu na mambo mengine mengi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kihistoria. Kugawa Bandari zetu ni sawa na kuuza Nchin yetu, hivyo tusitafute short cut. Lazima tupambane na Rushwa na tuongeze ufanisi katika Bandari zetu ambazo ni nguzo ya Uchumi wa Taifa letu.

Bunge lenye maprofesa wengi wazuri wakiwepo Prof. Kabudi, Prof. Kitila , Prof. Mkenda, Prof. Ndalichako na wengine. Halafu Bunge lenye Madaktari wa kusomea (PhD) nao ni wengi pia. Wapo Madaktari wa Binadamu (MD) nao wengi. Wapo wasomi wa aina mbali mbali wakiwemo wachumi . Hivyo sisi Wanazuoni tunaomba mkataba wa kukodisha Bandari husipitishwe kwani ni kuuza Nchi. Hawa wasomi wakikaa kimya historia itawaukumu huko mbele ya safari.

MAPENDEKEZO
Wanazuoni tunatoa mapendekezo yafuatayo kwa Waheshimiwa Wabunge pamoja na viongozi wote ambao wamepewa nakala ya wakara huu kutoka kwa wasomi wa Taifa. Tunawaomba wazee kama vile Mzee Butiku, Mzee Msekwa, Wastaafu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na viongozi wa Chama Tawala wasikubali huu mkataba hata kama Bunge limepitisha wakatae maana Watanzania waliowengi wanapinga kabisa Nchi yao kuuzwa kwa mgongo wa mashirikiano kati ya Nchi na Nchi.

Kwanza; tunaomba kabisa Bunge lisitishe kabisa mkataba huu siyo kuboresha bali kusitisha mara moja na Kutunga sheria ya kutoweka mbia yoyote kwenye Bandari zetu zote , iwe Bagamoyo au iwe yoyote. Liwepo katazo la kibunge.

Pili, tunaomba wabunge na spika wamshauri vizuri Mh. Rais kwa upole na uzalendo wa hali ya juu. Inawezekana washauri wa uchumi wa Rais hawajaliona jambo hili kwa bahati mbaya hivyo ushauri wetu utawaamusha uzingizini.

Tatu, tunashauri Treini ya Umeme ambayo Mh. JPM aliacha imekamilika kipande cha DSM na kipande chas Dodoma ilikuwa imefikia asilimia 80%. Tunaomba mshauri Rais azindue Treini hiyo na kwenye bajeti ya mwaka huu tuwekeze kujenga reli mpaka Bandari . Tujenge Bandari kavu kubwa Dodoma kwa kutumia SUMA JKT kwa muda mfupi na gharama ndogo ili treini ianze kubeba mizigo na kuongeza ufanisi wa Bandari bila kuweka madalali wa Mabeberu wanaokuja kwa mgogo wa Vinchi vy Falme za Kiarabu wanavyomilikiwa na Familia. Tanzania ni Nchi yenye hadhi kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimtaifa. Tanzania ni Nchi na Taifa ambalo halimilikiwi na Familia ni Nchi solid kabisa yenye kuheshimika Duniani tusipoteza mwerekeo tuungane na tujenge Nchi yetu kwa uzalendo na Umoja na tuache ubinafsi maana utaliangamiza Taifa.

Nne, Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wetu waweze kutafuta busara za wazee wa Taifa , Mzee Joseph Butiku, Mzee Warioba, Mzee Mangula, Wastaafu wa Jeshi, Wastaafu wa Usalama wa Taifa, Marais Wastaafu, Maprofesa Wastaafu , Wasomi wabobezi kama vile Profesa Shivji na wengine wengi. Wabunge aandaa semina huko Dodoma na Waite hawa Watanzania Wazalendo wawepe Busara zao ili mkifia maamuzi mtaweza kuliokoa Taifa.

Tano Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wamuombe Mh. Rais amsimamishe kazi waziri Mbarawa kupisha uchunguzi maana wizara yake ndiyo inataka kuleta majanga ya Taifa.

Tunatanguliza Shukrani
Wenu Katika Ujenzi wa Taifa
Wanazuoni
 
View attachment 2657946

CCM ni ngome ya kujitoa ufahamu tena ukiwa profesa unatakiwa usimame na kuongea kwakutoa mimacho na mapovu kuonyesha msisitizo ili jamii igundue kama ni hoja timilifu kumbe hakuna kitu, (herding behavior),uyumbu. Taifa limefika hapa tulipo kwasabau ya unyumbu,(kujitoa ufahamu). Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending their reasoning because of group objective or fear of their leaders.
 
TUKAJIFUNZE KWA MAJIRANI ZETU KENYA NA KWINGINEKO KWA NINI WALIWAFURUSHA NDIPO NASI TUONE TUNAFANYAJE,AIDHA TUNAINGIA MKATABA WA AINA GANI.
Nature inatueleza waarabu sio watu wa kunyooka. Although network yao ni kubwa na wako well organised.
 
View attachment 2657946

KUUZA LANGO LA UCHUMI WA NCHI AU KUTAFUTA WANAHISA NI USALITI MKUBWA KATIKA KUVUNJA KATIBA YA NCHI: BANDARI NI MALI ZA WATANZANIA WOTE HATUNA WANAHISA (SHAREHOLDERS) NA HATUHITAJI WANAHISA.

Wanazuoni
Msipodai katiba mpya ya kuwajibisha viongozi!

Mkabaki na nyaraka pale ambapo mambo yanapoharibika hamna cha MAANA ni bora mkae kimya!!
 
Waislam tujitokeze kuwapinga wapotoshaji, sasa wanazidi.

Kila Rais akiwa Muislam vituko vya wakristo huzidi.
 
Swali moja tu
Lango la uchumi limeuzwaje? Shilingi ngapi? Malipo yamefanyika wapi? Tupe uthibitisho
 
TUKAJIFUNZE KWA MAJIRANI ZETU KENYA NA KWINGINEKO KWA NINI WALIWAFURUSHA NDIPO NASI TUONE TUNAFANYAJE,AIDHA TUNAINGIA MKATABA WA AINA GANI.
Nature inatueleza waarabu sio watu wa kunyooka. Although network yao ni kubwa na wako well organised.
Kenya kamfurusha nani? Wakati saivi wanabembeleza Dubai wawekeze kwenye bandari zao?
 
Sijaelewa mpaka sasa ina maana Watanzania wanaelewa CHADEMA kuliko CCM?

Maana tukitazama ukweli wa hili sakata ni kuwa huu mkataba umeshakukuwa haufai. Yaani kila Mtanzania anaamini ukweli juu ya ibara mbovu walizochambua CHADEMA. Na mpaka sas ni kuwa watanzania wanaamini CCM ya wachache imeuza rasimali zao.

Leo nimekutana na Mzee mmoja, akaanza kuhoji, sisi kama taifa hatuwezi kupata utalaamu? Cranes za kisasa na mitambo ya kisasa?

Ina maana CHADEMA wamewazidi CCM kueneza ukweli?
 
hakuna mkataba mzuri kama huu,yaani njia zote za ulaji sasa kwisha.
Wanaopiga makelele kuwa mkataba ni mbovu ni sawa na majibwa koko.
Ila walanguaji na wahujumu uchumi tukubali tu wameshikwa pabaya.
 
Waislam tujitokeze kuwapinga wapotoshaji, sasa wanazidi.

Kila Rais akiwa Muislam vituko vya wakristo huzidi.
Acha udini wewe ajuza. Unataka kufanya waopinga mkataba ni wakristo na wanaoukubali ni waislam. Huo ni ujua. Tetea vifungu vilivyopo kwenye mkataba kama wanaopinga kwa kuonyesha vifungu vibovu ktk mkataba.

Mimi ni muislamu na siwezi kutetea uwovu kwa sababu wanaoufanya huo uwovu ni waislamu.
 
TEC ni Waislam, au siyo?

Siyo "wakristo", sema wakatoliki.
 
hakuna mkataba mzuri kama huu,yaani njia zote za ulaji sasa kwisha.
Wanaopiga makelele kuwa mkataba ni mbovu ni sawa na majibwa koko.
Ila walanguaji na wahujumu uchumi tukubali tu wameshikwa pabaya.
Acha ujiga. Unakata njia za ulaji kwa akina nani kwa kumpa nani hizo njia za ulaji??

Urithi wako ni bora mwanao akuibie maana mali itabaki ndani ya familia kuliko kumpa urithi wako unknown people
 
TEC ni Waislam, au siyo?

Siyo "wakristo", sema wakatoliki.
Kwanza ujue bandari sio za wakristo wala waisamu. TEC ni taasisi ya kanisa la wakatoloki. Wamefanya jukumu lao la kulinda rasilimali zetu kwa kuukataa mkataba kwa hoja na kuorodhesha vifungu vilivyopo kwanye mkataba vyenye utata.

Taasisi za kiislamu zijitokeze kujibu hoja na kwa kufafanua vifungu vyenye utata vinavyolalamikiwa. Sio kienyeji enyeji kama waislamu wengi tunavyofanya. Hutujibu hoja wala hatufafanui vifungu vinavyolalamikiwa ktk huo mkataba zaidi ya kutumia udini
 
Back
Top Bottom