MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,992
- 10,497
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Septemba 15, 2021 kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.
Mahakama itaanza kupokea ushahidi wa Jamhuri katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa, na Mohamed Abdillahi Ling'wenya.
Serikali inawasilishwa na jopo la mawakili nane wakiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, huku washtakiwa wakitetewa na jopo la mawakili 14, likiongozwa na wakili Peter Kibatala.
Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Yusuph Siyani.
----
Wakili wa serikali anaomba kuendelea kwa upande wa mashahidi.
Jaji anauliza kama Kibatala yupo tayari.
Jaji anauliza Kibatala angependa washtakiwa wakumbushwe mashtaka yao?
Kibatala anasema waendelee tu.
Wakili wa serikali anaulizwa Je, washtakiwa wakumbushwe mashtaka yao.
Upande wa Jamhuri wanasema washtakiwa wasomewe tena mashtaka yao. Jaji anauliza kuna ulazima wa kisheria? Kimyaaaa.
Jaji anasema kuna Kifungu cha Sheria kinalazimisha? Kimyaaa.
Jaji anasema sawa, acha tu washtakiwa wasomewe tena mashtaka yao.
Jaji anasema Kibatala asome hayo mashtaka, anayo mamlaka wa kumteua yeyote asome hayo mashtaka.
Kibatala anaomba kwa Jaji pamaoja na heshima hiyo anaomba asisome yeye mashtaka.
Jaji anauliza washtakiwa, je watahuzunika wakili wao akisoma mashtaka?
Wote wanaitikia Ndiyooooo!
Jaji anawaambia Jamhuri wasome mashtaka.
Jamhuri wanauliza kwa kiswahili au kiingereza?
Jaji anasema kwa sababu ya uharaka wasome tu kwa Kiingereza kama yalivyoandikwa.
Serikali wanasoma upya hati ya mashtaka kabla ya kesi kuendelea.
Mashtaka yote sita yamesomwa kwa sauti.
Washtakiwa wote wamekana mashtaka yote dhidi yao
Mashtaka yote 6 yamesomwa...
Jaji anauliza kuna lolote au tuanze kuita mashahidi?
Wakili serikali anasema twende kuita mashahidi
Wakili Serikali anatoka kumuita shahidi
Jaji anasema shahidi wa 1 Upande wa Jamhuri aitwe apande kizimbani
Sasa shahidi kapanda kizimbani tayari.
SHAHIDI-2
Anaitwa ACP Ramadhani Kingai.
Jaji anauliza huyu ni shahidi namba ngapi?
Wakili wa Serikali anasema, namba 2.
Dini yake.?
Shaidi anasema Muislam.
Jaji anasema thibitisha.
Shahidi Wallah,billah,Subillah nathibitisha ushahidi nitakaotoa utakuwa ni wa Kweli
Jaji anauliza, utetezi mpo tayari?
Wakili wa serikali anasema nitakuuliza maswali na utaenda kwa utaratibu sababu Jaji ataandika
Wakili wa Serikali; umejitambulisha ACP Ramadhani Kingai Unafanya Kazi gani?
Shahidi; ni Afisa wa Polisi Wakili wa Serikali upo kituo gani cha Kazi?
Jaji anauliza, tunamskia wote Shahidi?
Wakili Kibatala anasema aongeze sauti
Wakili wa serikali anamuuliza shahidi, unaweza kusema ukiwa kamanda wa polisi majukumu yako ni nini?
Shahidi anasema nikiwa RPC wa Kinondoni Jukumu langu kulinda watu na mali zao 2. Kuzuia uhalifu
Wakili wa serikali; una amuda gani tangu uwe kamanda wa polisi Kinondoni?
Shahidi; miezi 10 tangu nihamie kutoka Arusha
Jaji; Arusha ulikuwa RPC?
Shahidi; Hapana, Arusha nilikuwa RCO
Wakili wa serikali; ulikuwa RCO muda gani?
Shahidi; tangu 2018 hadi November 2020
Wakili wa Serikali; Elezea Dennis Urio unamfahamu?
Shaidi; Ni Luteni wa JWTZ
Wakili wa Serikali; Ulimfahamu lini?
Shahidi; 2020 nikiwa Oysterbay kikazi nilipigiwa simu na Afande aliyekuwa kamishina wa upepelezi wa makosa ya Jinai, aliyekuwa kamishina wa polisi Robert Boazi
Alinipigia simu akitaka niende ofisini kwamba niende kuna maelekezo ya kazi Nilipoenda ofisini kwake ndipo nilipomkuta Luteni Dennis Urio
Wakili wa Serikali; Ofisi ipo wapi?
Shahidi; Ofisi ipo Mtaa wa Ohio hapa Dar es salaam
Wakili wa Serikali Elezea Baada ya Kufika.
Shahidi; baada ya kufika kwa Afande Boazi, aliniambia kuwa Dennis alikuwa na taarifa ya Kihalifu Alimuomba Dennis Urio ambaye ni Luteni wa JWTZ aanze kutuelezea kwa pamoja mimi na DCI alitueleza kuwa kuna kundi la kihalifu ambalo linaandaliwa na Freeman Mbowe
Shahidi; Kundi hilo lilikuwa na lengo la kudhuru viongozi wa serikali Kundi hilo pia lilikuwa limejipanga kufanya vitendo vya kuchoma vituo vya mafuta kwa kuvlipua na masoko yenye watu wengi Lakini pia kukata miti katika barabara kubwa kuzuia magari yasipite
Shahidi; Lengo lilikuwa kuonyesha Nchi haitawaliki kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Wakili wa Serikali; elezea Dennis Urio aliwaeleza taarifa hizi alipata wapi.
Shahidi; alieleza kaambiwa na Freeman Mbowe Mbowe alikuwa anamueleza kwa vyovyote vile lazima tuchukue mamlaka ya nchi
Shahidi; Freeman Mbowe akamueleza Denis kwa kuwa yeye ni homeboy wake, angempa mamlaka makubwa pale ambapo angekuwa amepata mamlaka ya nchi
Wakili wa Serikali; elezea ni kwa nini Mbowe alimueleza Luteni Dennis na siyo mtu mwingine
Shahidi; Dennis alieleza Mbowe amemuomba amtafutie watu wa kutekeleza mambo hayo, wawe Makomandoo wastaafu au waliofukuzwa kazi
Wakili wa serikali; Makomandoo kutoka wapi?
Shahidi; Makomandoo kutoka Tanzania
Wakili wa Serikali; wawe Wstaafu kutoka wapi?
Shahidi; kutoka JWTZ
Shahidi; Vitendo hivi vilikuwa vimepangwa kufanyika MOSHI, Arusha Mbeya, DSM na Mwanza Lakini vitendo vya kukata miti na kuzia magari yasipite ilikuwa imekusudiwa barabara ya Morogoro kuelekea Iringa
Wakili wa Serikali; baada ya kupewa taarifa hiyo kiliendelea kitu gani?
Shahidi; Afande Boazi alimshauri Dennis Urio, aendelee kutoa ushirikiano na kushirki vitendo hivyo lakini aendelee kuripoti vitendo hivyo polisi
Jaji; Kama nimekuelewa Luteni Dennis alipaswa kuripoti kwako?
Shahidi; Ndiyo Shahidi; nilichukua namba ya Ltn Dennis Urio 0787555200
Shahidi; mimi nilimalizia kazi yangu ilikuwa imenileta DSM, nikarudi kazini kwangu, Arusha.
Wakili wa Serikali; Baada ya Kurudi Arusha, ulifanya nini?
Shahidi; samahani, wakati naelekea Arusha Afande Boazi alinielekeza nifungue Jalada la Uchunguzi, kuhusu njama hizo.
Shahidi; na mimi nikamuelekeza Askari anayeitwa Swila afungue Jalada hilo, na kufuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wakili wa Serikali; ulimulekeza Swila afungue uchunguzi kuhusu suala gani?
Shahidi; Uchunguzi ulikuwa upelelezi mipango iliyokuwa inataka kufanyika
JAJI; huyu Swila ni nani?
Shahidi; Swila ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi
Shahidi; baada ya hapo nilikuwa naendelea kuwasiliana na Ltn Dennis Urio na kwamba ameshatumiwa nauli na katika kipindi i hicho walikuwa wameshapatikana vijana wawili
Wakili wa Serikali; Elezea kama hao vijana wawili walikuwa na sifa hizo alizoelekezwa
Wakili Kibatala anasimama, anasema "Objection your honor, Wakili anamfundisha shahidi cha kusema
JAJI; Rudia swali vizuri au jibu Objection
Wakili wa Serikali anarudia swali vizuri
SHAHIDI; Luteni Dennis alinieleza Mbowe amefamfanya Khalfan Bwire kuwa mlinzi wake, huyu alikuwa komandoo alifukuzwa kazi kutokana wizi wa mafuta wa Standard Gauge. Moses Lijemje alifukuzwa Ukomandoo kwa makosa ya Kinidhamu. Baadae nilimuelekeza Swila afungie jalada la KIJANAI
SHAHIDI; ikafunguliwa kesi ya kula njama ya kutekeleza Matendo ya kigaidi. Wakili wa Serikali; ilifunguliwa wapi?
Shahidi; Police Central Dar es salaam.
JAJI; ulifungua kesi gani?
SHAHIDI; Kula njama ya kutenda vitendo vya kigaidi.
Wakili wa Serikali; ACP Kingai, unasema ulimueleleza Inspector Swila kufungua jalada la kesi ya kula njama ya kutekeleza matendo ya Kigaidi, kwanini?
Shahidi; Nature ya makosa yenyewe, yangeweza kufanywa yangeweza kuleta madhara kwa watanzania haswa katika kipindi tulichokuwepo
Wakili wa Serikali; baadae nini kilifuata?
Shahidi; tarehe 04.8.2020 nilienda kukutana na Ltn Denis Urio, aliniambia kwamba alishapata tena vijana wawili na amewaunganisha na Freeman Mbowe Akanitajia vijana hao ni Adam Kasekwa maarufu Adamoo na Mohammed A. Ng'wenya
JAJI; Endelea
Wakili wa Serikali; baada ya taarifa nini kiliendelea? Shahidi; alinieleza tayari vijana wamefika Moshi
JAJI; eleza ni vijana wapi, wote wanne au wawili wa mwisho
Shahidi; ahsante Mheshimiwa, aliniambia vijana 3 kati ya hao wa 4
Waikili serikali; tarehe ngapi?
Shahidi; tarehe 04.8.2020 Wakili wa Serikali; akina nani hao Luteni Dennis Urio aliokueleza wamefika tayari Moshi? Shahidi; ni Mohammed A. Lingwenya, Adam Kasekwa na Moses Lijenge
Wakili wa Serikali; Eleza walikuwa wamefikia kwa madhumuni gani?
Shahidi; Watu hao walikuwa wamefikia wilaya ya Moshi, na walikuwa wamekusudia kumdhuru Lengai Ole Sabaya, ambaye kwa kipindi kile alikuwa Mkuu wa wilaya ya Hai
Wakili wa Serikali; Baada ya kupokea taarifa hiyo ulichukua hatua gani?
Shahidi; Niliwasiliana na DCI nikamfahamisha na baada ya kumfahamisha alielekeza niunde timu itakayofanya ufuatiliaji na hatimaye kuwakamata watu hao. Kabla awajafanya Madhara yoyote kwa wahusika Nilimtafuta ASP wa Polisi ambaye sasa ni mkuu wa upelelezi Arumeru, Jumanne.
Shahidi; Mwingine Inspector Mahita, Detective koplo Francis, Detective Constable Goodluck na Dereva wangu Constable Azizi. Tulianza Kuweka amiundo Mbinu ya kuwakamata watuhumiwa kabla hawajafanya madhara yoyote.
Wakili wa serikali; Elezea Ulifanya nini baada ya Ufuatiliaji.
Shahidi; Siku ya Jumanne nilieleka Moshi, ambapo hao watuhumiwa walikuwa, na kwamba Jioni ile tulianza ufuatiliaji wa hao watuhumiwa kwa ajili ya kuwakamata. Baada ya mawasiliano na wasoro wetu tulihairisha zoezi na usiku ule tukawa tumelala Moshi.
Shahidi; Asubuhi 05.8.2020 tuliamka na kuweka miundombinu na wasiri wetu kwa ajili ya ya ufuatiliaji. Tulipata taarifa kuwa watuhumiwa wapo maeneo ya RAO, Moshi
Wakili wa Serikali; baada ya kupata taarifa hiyo ulichukua hatua gani?
Shahidi; Tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 2, Adam kasekwa na Mohammed Ling'wenya. Wakati tumewakamata, tumewaweka chini ya ulinzi nilimuelekeza ACP Jumanne awapekue maungoni. Adama kasekwa alivyopekuliwa alipatikana akiwa na Pisto 1 aina ya Ruvern iliyokuwa na namba 53A 5340
Shahidi; Pia alikutwa na risasi 3. Alikuwa na kete 58 za Heroine, madawa ya kulevya. Mohammed Kingwenya alikuwa na Kete 25 za Madawa ya Kulevya.
Wakili wa Serikali; Eleza upekuzi huu ulifanyika mbele ya nani? Shahidi; ulifanyika palepale mbele ya mashahidi.
Shahidi; Mmoja namkumbuka anaitwa Anita na mwingine anaitwa Esther. Baada ya kujaza hati ya kuchukua vitu, tuliwachukua watuhumiwa na wale mashahidi hadi kituo cha Polisi mjini kati, eneo la RAU lilikuwa siyo Rafiki kwa kuandika Maelezo yao Pale, ilikuwa la Fujofujo.
JAJI; Spelling za hilo eneo,
Shahidi; Ni RAO JAJI; Mwanzo tulikuwa tunasikia ni RAU. Kwa hiyo ni RAU au RAO?
Shahidi; ni RAO, Madukani. Baada ya Kufika ofisi ya mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro nilimuachia Jumanne aendelee kufanya Mahojiano
Shahidi; Wakati huo tukawa tunaendelea na watuhumiwa kumtafuta Moses Lijenje hatukuwa tumemkamata na wenzake
Wakili wa Serikali; Elezea ufuatiliaji wa Moses Lijenje ulifanyikaje
Shahidi; Wakati Mchana, tulitoka na watuhumiwa na Moses lakini zoezi lile lilituchukua mpaka usiku
Shahidi; Tulipofika usiku tuliamua kupumzika na kulala tena, na kuendelea kesho yake 06.8.2020.
Wakili wa Serikali; 05/8 milipokuwa mmekamata Adam na Lingwenya ni nani aliyekuwa anawaelekeza kumleta Moses
Shahidi; ni watuhumiwa wenyewe
Wakili wa Serikali; Meneo gani mlipita?
Shahidi; Boma Ng'ombe, Machame na Arusha
Wakili wa Serikali; elezea ikawaje
Shahidi; Mpaka September 2020 tulikuwa hatujafanikiwa kumpata Moses Lijenje
Wakili wa Serikali; ufuatiliaji wa 06/8 ikawaje,
Shahidi; tulishindwa Kumpata baada ya ufuatiliaji na kupita maeneo mengi
Wakili wa Serikali; naomba kukurudisha nyuma. Siku 05/8 watuhumiwa uliwapeleka wapi?
Shahidi; Central Station Moshi Wakili wa Serikali; Saa ngapi?
Shahidi; Sikumbuki...zaidi ya saa 4:30
Wakili wa Serikali; maeneo mliyomtafuta Moses Lijenje Moshi Boma Ng'ombe ni Maeneo gani?
Shahidi; Maeneo waliyokuwa wanamtafuta Lengai Ole Sabaya
Wakili Mtobesya anasimama na kusema "Objection naona kama Wakili anaongea mambo ambayo bado shahidi hajaongea
Jaji anaomba serikali wamjibu Wakili Mtobesya
Wakili wa Serikali anasema, nimemuuliza Shahidi ACP kingai, umemfuatilia Moses Moshi, Boma Ng'ombe na Machame, Maeneo gani haswa?
Jaji anamuuliza Wakili Mtobesya kuna tatizo na hilo swali?
Mtobesya anasema nimefanya Objection kwenye Line wakili wa serikali aliyokuwa anaelekea
JAJI; Shahidi amevuka mipaka kwa shahidi anayoelekeza kuhusu fact, Ukisoma section 6 ya Evidence Act
Jaji anauliza je, kuna msingi ya kuendelea na Objection?
Wakili Mtobesya; tunaondoa Objection baada ya ushauri na wenzangu
JAJI; taja maeneo shahidi
Shahidi: ni Moshi Mjini
Jaji; hayo tumeshayasikia
Shahidi; maeneo mengine ni yale waliyokuwa wamefikia wakati wanatoka Dar es salaam na maeneno mengine waliyokuwa wanamfuatilia Ole Sabaya
JAJI; Wakili wa Serikali, hayo yanatusaidia nini?
Wakili wa Serikali; Unasema ulienda Machame, ulienda eneo gani?
Shahidi; Kuna Hotel inaitwa AISHI ambayo ni mali ya Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali; na Boma Ng'ombe?
Shahidi; ni Hapo hapo Boma Ng'ombe
Wakili wa Serikali; nitaenda kwenye swali lingine Baada ya Tarehe 06 baada ya kurudisha taarifa kwa DCI ni hatua gani iliyokuwa umechukua?
SHAHIDI; tulielekea DSM kwa ajili ya ufuatiliaji na hatua nyingine ya upelelezi, ambapo DSM ndipo Center ya Jalada lilipofunguliwa
Wakili wa Serikali; safari ya DSM ilianzia wapi?
Shahidi; Moshi
Shaidi; 07.8.2020 saa 11 Alfajiri ndiyo tulipofika Central Police Station
Wakili wa Serikali; Elezea Adam kwa wajihi wake
Shahidi; Adam Hassan Kasekwa ni yule pale wa Pili si mrefu sana wala mfupi sana.
Na Mohammed ni mtumuhiwa aliyekaa wa tatu kutoka kushoto kwa Khalifan
Shahidi sasa anaruhusiwa kwenda walipo watuhumiwa akawaonyeshe palepale.
Shahidi anamshika Adam kasekwa
Shahidi anamshika Mohammed Lingwenywa
Shahidi anarejea kizimbani.
Jaji anauliza, walioguswa na shahidi ni sahihi?
Adam anasema, ni Sahihi Mohammed anasema, ni sahihi
Wakili wa Serikali; Mpofika Central police alfajiri, nini kilifanyika?
Shahidi; tuliwaweka mahabusu watuhumiwa, sisi tukaenda kupiga mswaki na kunawa uso
Wakili wa Serikali; nini kiliendelea?
Shaidi; nilimuhoji Adam Kasekwa kwa njia ya ONYO
Wakili wa Serikali; mahojiano hayo uliyafanyia wapi?
Shahidi; Central Police station Dar es salaam
Wakili wa Serikali; kwa sababu ulimkamatia Moshi, ni sababu gani iliyopelekea kuufanya mahojiano DSM?
Shahidi; Dar es salaam ni Sehemu kesi ilipofunguliwa. Pia palikuwa na taarifa watuhumiwa wengine wapo Dar es salaam Na kwamba ndipo sehemu sahihi ya watuhumiwa kuhojiwa.
Wakili wa Serikali; elezea ni taratibu gani ambazo ulizitumia
Shahidi; kwanza nilimfahamisha mtuhumiwa haki zake. Haki hizo ni pamoja na mimi kujitambulisha kwake, Lakini pia kumueleza Kosa lake. Nilimuonya halazimishwi kusema lolote.
Shahidi; Nilimueleza anaweza kuwepo Ndugu, Jamaa na Rafiki au Mwanasheria wakati wa kutoa maelezo yake. Alinijibu kuwa yupo radhi kuandika maelezo pekee yake. Haya yote alikuwa anayaongea nikiwa naandika, na Mwisho akawa tayari kusaini maelezo yake akiwa mbele yangu.
Wakili wa Serikali; ulisema ulimfahamisha kosa lake na Sheria?
Shahidi; Kosa la kula njama na kutenda vitendo vya ugaidi
Wakili wa Serikali; baada ya kumuonya na kuandika maelezo ulifanya nini?
Shahidi; niliyafunga
Wakili wa Serikali; Unasema kasaini, kwa namna gani?
Shahidi; kwa saini ya kalamu na dole gumba
JAJI; aina gani ya kalamu?
Shahidi; kalamu kwa maana ya peni
Wakili wa Serikali; Baada sasa kumaliza kuandika maelezo yake, ulifanya nini?
Shahidi; Nilitengeneza jalada la kesi
Wakili wa Serikali; unayatambuaje Maelezo yako?
Shahidi; nayatambua kwa mwandiko wangu, sahihi ya Adam na sahihi yangu
Wakili wa Serikali; Mheshimiwa Jaji naomba kumkabidhi karatasi hii aione
Shahidi; natambua haya ni maelezo niliyoandika kwa mwandiko wangu, na sahihi yangu au Mtuhumiwa
Wakili wa Serikali; Ungependa statement itumike mahakamani kama ushahidi?
Shahidi; ndiyo itumike kama sehemu ya Ushahidi
Mawakili wa Utetezi wamepewa kupitia Hati ya Maelezo aliyoyatoa Shahidi ACP Kingai
Mawakili wa Utetezi wamesimama Kuielezea Hati ya Maelezo iliyotolewa
Kibatala anasema hati ya maeelezo ina matatizo
1. Maelezo yamechukuliwa nje ya muda wa kisheria. Yamechukuliwa zaidi ya saa 48 tangu mshtakiwa atiwe kizuizini
Huko RAU, Moshi n kifungu husika kimeweka masharti ya lazima, yamechukuliwa nje ya muda hawezi kupokelewa mahakamani
2. Kabla na wakati maelezo ya mtuhumiwa yanachukuliwa, kwa Mshtakiwa Adam Kasekwa aliteswa (Tortured) na zoezi hilo la kumtesa lilisimamiwa na shahidi namba 1 ACP kingai na maafisa wengine wa polisi
Anaendela kueleza Wakili Peter Kibatala.
Sehemu ya kwanza ya pingamizi letu kuhusu ushahidi wetu ni kuhusu jambo la sheria na sehemu ya pili ni namna ushahidi ulivyopatikana Naiomba mahakama ifanye kesi Ndogo katika kesi Kubwa.
Wakili Kibatala anaendelea
Jaji kwa maana hiyo tutoe hukumu sehemu ya 1 Au tufanye hukumu kwa zote mbili?
Kibatala; tutoe hukumu sehemu ya 1 kisha tufanye kesi ndani ya kesi
JAJI; unafikiri inawezekana utaratibu zote na uchukuaji wa ushahidi unaweza kuwa sehemu ya kesi ndogo?
Wakili Kibatala; ndiyo inawezekana kwa sababu sisi tunataka tuzingatie kifungu 169 CPA
Wakili Mtobesya; ukisoma kifungu cha 151 kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushahidi wa shahidi wa 1 waliwakamata tarehe 05 na waliwaweka lockup
Maelezo labda kama pangelikuwa na ushahidi Mbele yako unaonyesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo
Ukisoma hukumu mbalimbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yaliyopeleka msichukue maelezo wakati wanafanya Maelezo
Tarehe 06 walikuwa nao wote na akasafiri kuja DSM na wakafika tarehe 07 Alfajiri
Mheshimiwa Jaji Kuna muda hapa haujaelezewa, Ukisoma ushahidi wa Shahidi wa kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 Usiku, Ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue
JAJI: je unaona unahitaji kesi ndogo Nlndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa Kifungu cha 169 cha CPA?
Wakili Mtobesya: Vifungu vya ushahidi vinamtaka shahidi yeye ndiyo aeleze, tukienda upande wa pili wa kesi ndogo inampa shahidi kuelewa ambayo hajayaleza.
Jaji; Je, Mshtakiwa wa pili alitoa hayo maelezo au hajayatoa? Je, washtakiwa walitoa maelezo au hawajatoa iwe kwa mateso au lah?
Wakili Mtobesya; Maelezo yaliyochukuliwa kinyume na Sheria hayawezi kuwa maelezo halali
Wakili Mtobesya; Mheshimiwa Jaji baada ya kujiridhisha kama walifuatisha vifungu vya sheria ndiyo twende Kwenye kesi ndani ya kesi ya msingi.
Wakili wa Serikali wanasimama na kusema tumesikia mapingamizi yote.
Kwa maoni yetu, Mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Upande wa Utetezi, yanaweza kuteuliwa baada ya mahakama hii kufanya kesi ndogo ndani ya kesi.
Ni baada ya Wakili Kibatala sehemu ya Pili Kulalamikia ukiukwaji wa taratibu za kisheria wakati wa kuchukua maelezo
Jambo lingine hata wakati Wakili Mtobesya alikuwa anaelezea anashindwa kujitenganisha na ushahidi.
Wakili wa pili wa serikali; Mheshimiwa jaji ni msimamo wetu kuwa mapingamizi haya yasikilizwe kupitia kesi ndogo, Baada ya ushahidi kuwa umepokelewa mahakama ituruhusu kuwasilisha
Na hata sehemu ya Kwanza ya maelezo ya kwanza ya wakili Kibatala pia ina uhusiano na kesi kubwa
Sasa sisi tunaona pingamizi la kwanza lina uhusiano na Pingamizi la Pili, Mahakama ijielekeze kwenye kesi ndogo katika Kesi ya msingi
Kibatala alisema shahidi na maafisa wengine wa polisi waliwatesa washtakiwa, atusaidie kuwataja pasipo kutuacha, je ni akina nani?
Wakili Kibatala; tunaomba tupate ruhusa ya mahakama twende kwenye kesi ndogo katika kesi ya Msingi (Trial within a trial)
Ukimya unatawala kidogo
Tunasubiri Maamuzi ya Jaji juu ya mapingamizi 2 ya kupokelewa ushahidi wa ACP kingai ambao Umewekewa mapingamizi mawili na upande wa mawakili wa utetezi
1. Maelezo ya watuhumiwa kuchukuliwa nje ya muda.
2.Maelezo ya watuhumiwa kutolewa kwa mateso kwa watuhumiwa.
Lakini kwa Pingamizi la pili linataka mahakama ihairishe kusikiliza kesi ya msingi, tusikilize Kwanza kesi kuhusu pingamizi la pili kuhusiana na watuhumiwa kama waliteswa au sivyo.
Jaji anasema kama ambavyo mawakili wasomi wamebainisha kuhusu maelezo yanayosadikiwa kuwa ni maelezo ya Onyo, Kimsingi pingamizi la kwanza lilikuwa linaweza kutatuliwa bila kuwa na kesi ndogo katika kesi ya Msingi.
Jaji anasema, nakubaliana na mawakili wasomi kusimamisha kesi kuu ya msingi kwanza na kuanza kusikiliza kesi ndogo, hivyo, nahairisha kesi hii ya msingi hadi saa nane mchana, tuanze kesi kusikiliza kesi ndogo.. Kesi imehairishwa hadi sasa nane mchana. Jaji ameondoka mahakamani
KIBWAGIZO; Shahidi wa Jamhuri, ACP Kingai anasema washtakiwa walikutwa na bastola na Risasi 3. Hati ya mashtaka inasema ni risasi 1 na bastola 1. OK!
Kingai anasema aliwakuta na kete 58+25=83 za dawa za kulevya aina ya Heroine. Lakini vyote hivyo havipo kwenye hati ya mashtaka
TUREJEE NGWE YA PILI
Wakili wa serikali wakiongozwa na Robert Kidando wanajitambulisha. Column yao ni ile ya asubuhi. Upande wa utetezi wakili Peter Kibatala anatambulisha Mawakili wenzake, Anaongeza majina ya John Malya. Aliingia Wakili Pacience Mlowe hatukutumtaja, Jumla Utetezi kuna mawakili 16
Wakili wa Serikali; Mheshimiwa Jaji Katika Shauri hili dogo tunategemea kuwa na Mashaidi 7 na Leo tuna shahidi mmoja.
Jaji; upande wa Utetezi Mpo tayari?
Wakili kibatala; Ndiyo tupo tayari
ACP Kingai anaingia mahakamani anapanada Kizimbani.
Jaji anamtaka arudie kujitambulisha
Shahidi; Naitwa ACP Ramadhani Kingai
Jaji; Utetezi hatujaendelea,palikuwa na concern kuhusu chakula cha washtakiwa, je leo wamekula?
Wakili Kibatala; Leo tutumie diplomasia, tuendelee ingawa hawajapewa chakula magereza wamesema kuna hatua wanachukua Kesho wanaweza kuwa tayari
Jaji; Shahidi Kingai wewe ni Muislamu, thibitisha
Shahidi; Wallah, Wabillah nathibitisha
Wakili wa Serikali Kinagi Umesema wewe ni ACP Unafanya shughuli gani?
Shahidi; ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
Wakili wa Serikali; kabla ya hapo ulikuwa kituo gani cha Kazi?
Shahidi; nilikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha
Jaji; sijasikia vizuri
Kingai anarudia tena...
Wakili wa Serikali; ulifanya kwa Muda gani?
Shahidi; nitalifanya kwa mwaka mmoja na Miezi 4.
Wakili wa serikali; eleza majukumu yako ulipokuwa mkoa wa Arusha.
Shahidi; nilikuwa napelekeza Makosa ya Jinai,,Nasimamia nidhamu ya Askari, ukamataji wa watuhumiwa na kufanya Mahojiano na watuhumiwa
Shahidi; Tarehe 05.8.2020 nilikuwa katika Mji wa Moshi, nilienda kuwakamata wa watuhumiwa wa kesi ya kula njama ya Kutenda vitendo vya Kigaidi
Wakili wa Serikali: hao watu ulienda kwa ajili ya kuwamakata ni akina nani?
Shahidi; Khalfan kasekwa Maarufu Adamoo, Mohammed Ling'wenya na Mose Likenja Kwa Taarifa tulizokuwa tumezipata, tulienda kwa dhumuni la kuwakamata
Wakili wa Serikali; Elezea Ulivyo wakamata
Shahidi; siku ya 06.8+2020 tulipata taarifa kupitia kwa wasiri wetu kuwa watuhumiwa tunaowafuatilia wapo eneo la RAO madukani
Wakili wa Serikali; Baada ya taarifa ulichukua hatua gani?
Shahidi: nikiwa na timu yangu ACP Jumanne, OCCID Arumeru, Detective Goodluck CID Arusha, Detective constable Azizi tulienda kuwafuatilia watuhumiwa ambao tuliwakamat
Shahidi: tulifanikiwa kuwakamata wawili kati ya watatu tuliokuwa tunawafuatilia Tulimkamata Mohammed A Ling'wenya na Adam kasekwa
Wakili wa Serikali: baada ya Kuwakamata nini kilifuata?
Shahidi; tulimuamuru ACP Jumanne awapekue maungoni, ili kujiridhisha Kuna usalama katika kuwapeleka sehemu tulizokuwa tunawapeleka
Jaji; Maungoni unamaanisha nini?
Shahidi: search in person Shahidi; Adamoo alikutwa na bastola aina ya Rivern A53 5340 ikiwa na risasi 3
Shahidi; pia alikuwa na kete 58 za dawa ya kulevya baada ya uthibitisho kuwa yalikuwa ni Heroine Mohamed Ling'wenya alikutwa na kete 25 za dawa ya kulevya na baada ya kuthibitisha kuwa nayo ni heroine Baada ya upekuzi, iliandaliwa hati ya Upekuzi Sorry upekuzi huo ulifanyika Mbele ya mashaidi, mmoja anaitwa Anita mmoja anaitwa Esther
Jaji: Esther na nani?
Kingai anarudia
Shahidi; Baada ya upekuzi huo iliandaliwa Hati ya uchukuaji wa vitu kutoka kwa watuhumiwa Hati hiyo baada ya kujazwa ilisainiwa na watuhumiwa wenyewe pamoja na mashahidi.
Wakili wa Serikali; Baada ya kujaza hati hiyo ni hatua gani ilifuata?
Shahidi; niliwachukua watuhumiwa kuelekea Central Moshi Na kuwapeleka mashahidi walishuhudia upekuzi kwa ajili ya kuandika maelezo yao
Wakili wa Serikali; uliwapeleka pale watuhumiwa na mashahidi kuwachukua Maelezo ni hatua gani ilifuata?
Shahidi: tuliwachukua na gari kuwapeleka Central Moshi
Wakili wa Serikali: hilo ulishalisema
Jaji; koplo Francis mlimuacha anafanya nini?
Shahidi: alikuwa anachukua maelezo ya Mashahidi
Wakili wa Serikali: Ulifanya nini baadae?
Shahidi: Tena pale Rao Madukani kumtafuta Moses Lijenje, watuhumiwa walisema Moses alikuwepo kwenye timu yao lakini muda ule hawakuwa naye, na walitoa uwezekano wa maeneo ambayo tunaweza kumpata. Kwa hiyo tulitembea maeneo mbalimbali ya Moshi kumtafuta huyu Lijenje.
Kwa ushirikiano wa watuhumiwa na ushirikiano wa watuhumiwa wetu Tulipita maeneo mbalimbali ya Moshi na kule Boma Ng'ombe Kumtafuta Moses Lijenje mpaka usiku bila ya mafanikio
Wakili wa Serikali; baada ya kutofanikiwa kumpata Moses Lijenje hadi usiku ulichukua hatua gani?
Shahidi; niliwachukua kuwarudisha watuhumiwa mpaka Moshi muda ule usiku kwa kuwa walikuwa wamechoka na kusinzia
Wakili wa Serikali: Muda gani?
Shahidi: zaidi ya saa nne usiku
Jaji: Endelea
Wakili wa Serikali: baada ya kufika Polisi uliwapeleka wapi watuhumiwa?
Shahidi: niliwaweka mahabusu
Wakili wa Serikali: Kule wakati mnawakamata hawa watuhumiwa 2, ukamataji huu ulikuaje?
Shahidi: Ukamataji haukuwa na shida,Tulitegemea kwakuwa Watuhumiwa ni askari pengine wataleta shida lakini hapakuwa na shida
Shahidi: tuliendelea na kumkamata Moses Lijenje, mpaka asubuhi tulikuwa na nia hiyo Wakili wa Serikali: Muda gani na wapi? Shahidi: tulianzia stendi ya Mabasi, Manispaa ya Moshi Asubuhi ya Tarehe 06.8.2020 tukifikiri anaweza kusafiri Wakili wa serikali: ulikuwa na nani?
Shahidi: Timu yangu ASP Jumanne, inspector Mahita, Detective Constable Goodluck, Detective Constable Azizi tukiwa na watuhumiwa kwa ajili ya utambuzi wa Moses Lijenje. Mchana hadi usiku kwa maeneo mbalimbali kama nilivyosema.
Shahidi: Lakini hatukufanikiwa kumpata Moses Lijenje. Tulipofika majira ya Saa 2 usiku niliwasiliana na DCI Kamishina Boaz kuhusiana na ugumu wa kumpata Lijenje. Akaelekeza tuondoke Moshi kuelekea Dar es salaam ambako Kesi imefunguliwa lakini pia kwa hatua zingine za kiupelelezi.
Wakili wa Serikali: Elezea uliondoka Moshi Tarehe ngapi na saa ngapi. Shahidi: tuliondoka Moshi saa 2 usiku nikiwa na timu yangu. Tulipofika njia panda Himo Gari yetu aina ya Land cruiser ilizima taaa ikabidi tufanye mawasiliano kwa ajili ya kupata gari nyingine.
Baada ya mawasiliano tulipata gari nyingine, tukawasiliana na RPC ikabidi Detective koplo Azizi abaki pale sisi tunaendelea na safari Wakili wa Serikali: Dar es salaam mlifika majira gani? Shahidi: Tarehe 07 Saa 11 Alfajiri Tulienda hadi Central police Dar es salaam
Shahidi; Na muda mfupi tuliwaweka mahabusu kwa ajili ya kupiga mswaki na kunawa Wakili wa Serikali; Baadae nini kiliendelea? Shahidi: Majira kati ya saa 1 na nusu na saa tatu Siku hiyo hiyo tarehe 07 mwezi wa nane nilimhoji mtuhumiwa Adam Kasekwa kwa njia ya ONYO.
Wakili wa Serikali; Elezea sasa shughuli hiyo ulifanyika wapi? Shahidi: Central Police Dar es salaam, kabla ya kuandika maelezo nilimfahamisha haki zake Wakili wa Serikali: tuambie hizo haki unazosema ulimfahamisha. Shahidi; nilijitambulisha kwake, Nilimtaarifu kosa lake
Wakili wa Serikali kosa gani? Shahidi; kula njama ya kufanya vitendo vya Kigaidi SHAHIDI; nilimuonya ni kwa hiari kutoa maelezo yake kwangu, na kwamba chochote atakachonieleza kinaweza kutumika mahakamani kama ushahidi dhidi yake
Shahidi; Haki zingine Nilimueleza iwapo anaweza kutoa pekee yake mwenyewe au kumsaidia Kupata Ndugu, jamaa au rafiki au Mwanasheria Wakili wa Serikali: yeye alijibu nini Shahidi: alisema yupo tayari kutoa maelezo yake akiwa pekee yake Na haya yote nilikuwa nayaandika
Shahidi: Akatoa maelezo yake na kuweka sahihi yake Wakili wa Serikali: aliweka sahihi kwa kutumia njia gani Shahidi: aliweka sahihi kwa kutumia kalamu ya wino na dole gumba Wakili wa Serikali: ulipomuangalia alikuwa katika hali gani? Shahidi: alikuwa katika hali nzuri tu
Shahidi: niliandika maelezo yake kama ambavyo alikuwa anayatoa Wakili wa Serikali: Baada ya kumuandika maelezo ilikuaje? Shahidi: nilimpatia Adamu kwa ajili ya kuyaona ili aone kama kuna nilicho ongeza au Kupunguza. Wakili wa Serikali: yeye alikueleza nini?
Shahidi: aliniambia hakuna kilichopungua, yapo kama alivyo yatoa yeye Shahidi: Maneno ya kwamba hakuna kilicho ongeza wala kupungua aliyathibitisha kwa kuandika kwa mkono wake, na akasaini kwa kalamu ya wino na Baadae akaweka dole gumba
Wakili wa Serikali: baada ya yeye Kuandika Maelezo yake mama alivyoeleza Wakili kibatala anasimama anasema "Objection" Wakili wa Serikali: nina rephrase! Wakili Kibatala Sawa kama anarephrase Wakili wa Serikali: baada ya kuandika kuthibitisha maelezo yake wewe ulifanya nini?
Shahidi: niliandika maelezo hayo kuashiria kumaliza kuandika statement Wakili wa Serikali: uliandika kwa muda gani? Shahidi: saa 1:30 mpaka Saa 3:30 Wakili wa Serikali: Ukiyaona maelezo hayo unaweza kuyatambua? Shahidi: naweza kutambua Wakili wa Serikali: kwa sababu gani?
Shahidi: niliandika kwa mwandiko wangu mwenyewe, saini yangu pia na hata saini ya mtuhumiwa naikumbuka Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kumkabidhi kama anaitambua Shahidi: Mheshimiwa nayatambua kutokana na Mwandiko wangu, sahihi ni ya kwangu, Naukumbuka mwandiko wa
Mtuhumiwa na pia nakumbuka sahihi ya mtuhumiwa pia Wakili wa serikali: maelezo hayo tukisema tuyatumie kama sehemu ya Ushahidi wako tutakuwa tunakosea Shahidi: ndiyo Mheshimiwa naomba tuyatumie kama sehemu ya Ushahidi Jaji: kwa Upande wa Utetezi Kuna OBJECTION?
Wakili Kibatala; Ndiyo mheshimiwa Jaji Jaji: Maelezo yanapolekewa Wakili wa Serikali: Anasimama Kingai elezea ni ukurasa wangapi ulimfahamisha Adam Kasekwa haki zake Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji anachofanya Wakili wa serikali siyo Sahihi, Maelezo yaliyopokelewa ni ID anamuelekeza Shahidi Ku' file tena Content Jaji Fafanua... Wakili Kibatala: Hiyo hati ya maelezo imepokelewa tu kama kielelezo, anachofanya ni kujadili content ya kilichopo kwenye maelezo Wakili wa Serikali: hofu tu Mheshimiwa Jaji, mimi sifanyi anachosema
Jaji; naomba mvumiliane Mahakamani, mniachie Jukumu la kuamua tu Kibatala; anachofanya wakili wa serikali anataka kuingiza maelezo ya ziada kwa mlango wa nyuma, yeye alishakuwa na muda wa kutosha na kueleza Jaji Wakili wa serikali: unachotaka kuuliza unataka kukusudia nini?
Wakili wa Serikali: Sifanyi lolote nataka nitumie alichosema shahidi Jaji anakubaliana na Kibatala, ondoa hilo swali lako, Tumepokea for identification hatuna haja ya kujua kilichopo ndani Wakili wa Serikali: Sawa Mh Wakili wa Serikali: Shahidi wakati anachukua Maelezo ya
Mtuhumiwa Adam Mazingira yalikuwaje? Shahidi: Palikuwa na mazingira mazuri na tulivu na alikuwa vizuri Ki-Afya Wakili wa Serikali: Ulimkamatia Adam Moshi, elezea kwanini ulikuja kumchukua maelezo Dar es salaam Shahidi: Kwanza kesi ilifunguliwa Dar es salaam
Pia palikuwa ni sehemu sahih na DSM palikuwa na hatua zingine za kiupelelezi Wakili wa Serikali: Hatua gani za kiupelelezi zilizokuwa zinaendelea Moshi? Shahidi: Kule Moshi paliendelea na hatua za kumtafuta Moses Lijenje, kwa msaada wa watuhumiwa tuliokuwa tumewakamata
Wakili wa Serikali: Mshtakiwa Adam analalamila kuwa alikuwa anateswa kabla na wakati anachukuliwa maelezo yake, aliteswa na wewe pamoja na Maaskari ambao uliwaelekeza wewe Shahidi: Si kweli, hatukumtesa, kwa Sababu hapakuwa hata na resistance wakati wa ukamataji wao
Wakili wa Serikali: ulichukulia maelezo yake ya onyo Shahidi: Ofisi ya RCO Ilala Jaji: umesema ukiwa Kituo kipi? Shahidi; Central Station,ofisi ya RCO Ilala Wakili wa Serikali: malalamiko ya kuteswa alichukuliwa maelezo, tuelez na Mazingira gani wakati wa ukamataji!
Shahidi: hapakuwa na resistance wakati wa Ukamataji, hata wakati tunasubiri nao hawakutuletea shida ya aina yoyote Lakini hata wakati naandika maelezo hapakuwa na shida ya aina yoyote au kuonekana akiwa na shida ya aina yoyote, Alitoa maelezo akiwa free na kwa kupenda mwenyewe.
Wakili wa Serikali: sababu anasema wakati anateswa palikuwa na Askari wengine uliowaelekeza, Je akina nani ulikuwa nao. Shaidi hapakuwa na Mtu, tulikuwa mimi na yeye Wakili wa Serikali: Kule Moshi wakati unawakamata palikuwa ni eneo gani? Shahidi; lilikuwa eneo la kibiashara
Maduka na Migahawa, Sina hakika Maduka ya Jumla, Grocery ya kuuza pombe na vibandaumiza, moja ya huko kibanda cha supu ndipo tulipo mkuta Lipo bize na kuna watu wengi Wakili wa Serikali: Maeneo mengine mliyopita Moshi na BomaNg'ombe, Machame kumtafuta Moses yenyewe yalikuaje?
Shahidi: kote tulikopita ni maeneo waliyokuwa wanapita kula au kunywa Sakina tuliambiwa kuwa ana ndugu yake, lakini hatukufanikiwa kumpata Wakili wa Serikali: Vipi pale mlipokuwa gari yenu umepata hitilfu, eneo likoje? Shahidi: eneo ambalo lipo Bize na watu wengi, biashara
Wakili wa Serikali: ni ni hayo tu Wakili wa Serikali anaketi Jaji anaita mawakili wa utetezi (Cross examination) Wakili Kibatala: utakasirika nikikuita ni kaka yangu? Shahidi: sahihi sababu nimekuzidi umri Wakili Kibatala; bila Shaka hutokasirika nikiwatetea wateja wangu?
Wakili Peter Kibatala anamkabidhi shahidi kitabu cha PGO Shahidi anasema ndiyo yenyewe.. Jaji anamsisitiza aangalie vizuri, ndani na nje Vizuri ajiridhishe.. Wakili Peter Kibatala nae anasisitiza, kwa kuuliza ni yenyewe kweli PGO? SHAHIDI Kingai anasema NDIYO YENYEWE..
Wakili Peter Kibatala anamuonyesha shahidi ukurasa wa kwanza, kwamba IGP wa wakati huo Saidi Mwema alisema kila mshiriki asome na kusoma, akasema mshiriki ni polisi na awe na maadili na ajue miiko ya Polisi. Shahidi anaitikia kwa kichwa.. Jaji anasema usiitikie kwa kichwa hapa
Ufafanuzi
Police General Orders ndiyo (PGO)...
Tuendelee..
Wakili Peter Kibatala; kila member wa polisi muda wote anatakiwa kuzingatia Misingi ya Haki za binadamu kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na watu wa Zanzibar
Shahidi: sahihi...
Wakili Peter Kibatala; Sasa tuanze Vizuri
Kibatala: unapomkamata mtuhumiwa unatakiwa palepale umueleze kuwa wewe ni nani na Unamkamata kwa makosa gani, Je ni sahihi?
Shahidi: ni sahihi
Kibatala: Je ni sahihi kwa mujibu wa PGO unatakiwa kuandika katika Notebook, na kwa mujibu wa Notebook ni kifaa kazi chako wewe?
Shahidi; ni Sahihi
Kibatala; ni sahihi kufunga safari kutoka Arusha-Moshi mkoa mwingine ukijua mtuhumiwa Adamoo anatuhuma za ugaidi?
Shahidi; nilikuwa nafahamu
Kibatala: Mawakili wa Serikali wameku' Brief kuwa ushahidi wa sasa ni tofauti na ushahidi wa Asubuhi, hilo unafahamu?
Shahidi: ndiyo nafahamu Wakili
Kibatala: Unafahamu bila shaka mahakama haikuwepo wakati hayo yanatokea, Mahakama inatakiwa kuunganisha Vidoti vidogo vidogo kujua nini Kilitokea wakati yenyewe haipo eneo la tukio?
Shahidi: sijaelewa
Kibatala: Unafahamu ushahidi mdogo mdogo ndiyo unaunda ufahamu kwa Mahakama Kufanya Maamuzi? Mwambie Jaji kuwa ulipokuwa eneo la Rao huko Moshi kama ulimwambia mheshimiwa Jaji Ulifuatisha tararibu za kwa mujibu wa PGO.
SHAHIDI: PGO gani inasema hivyo?
Wakili Peter Kibatala: Huko tushatoka jibu ninalokuuliza hapa sasa hivi..
Shahidi: hapo hakuniongoza..
Wakili Peter Kibatala: Ulizungumzia Jijibu la Adamoo kuwa uliliweka kwenye Notebook ambacho ni kifaa chako cha Kazi?
Shahidi: hilo sikulisema
Wakili Kibatala: Infact hiyo Notebook hukuitoa Mahakamani, ambacho tumekubaliana ni Kifaa kazi..
Shahidi. Sikuitoa
Wakili Kibatala: Tutoke RAU Madukani, Twende Police Station Moshi, nilikusikia Vizuri Kuna wadada Mliwachukulia Malezo pale Moshi
SHAHIDI. Ndiyo
Kibatala: tukumbushe kuwa investigation file lipo Dar es salaam.
Shahidi: Ndiyo ilikuwa Dar es salaam
Kibatala: Jaji akiandika sema kwamba hukusema kwanini ulichukua maelezo ya wale wadada pale Moshi wakati Investigation Files lipo Dar es Salaam?
Shahidi: sikuulizwa hilo
Wakili Peter Kibatala: jibu ninachokuuliza
Wakili Peter Kibatala: Kwa USHAHIDI wako Kuna Upekuzi wa Adamoo ulifanyika Mbele ya MASHAHIDI pale RAO Moshi?
[Jaji anaomba tunyamaze kupisha Hadhana kidogo Mahakama kimyaaaaa Tunaendelea]
Kibatala: Kuna Mashahidi 2 walihojiwa Moshi wakati kesi imefunguliwa DSM, sasa mueleze Jaji kuwa kama ulifafanua kuna Mazingira yoyote yaliyosababisha watoe maelezo Moshi na Siyo Dar es salaam
Shaidi: Nilieleza Mazingira hayakuwa rafiki ndiyo maana tukaenda kurekodia pale Polisi
Wakili Peter Kibatala: Maelezo kuwa shahidi anaweza kuhojiwa popote kwa mujibu wa kiapo chako hapa mahakamani utatoa hapa leo?
Shahidi: Hiyo mimi sikusema Wakili
Peter Kibatala: Ndicho nilichokuwa nataka, Muda Mwingine Pay attention tafadhali ndugu Shahidi Tuendelee..
Wakili Kibatala: mueleze Mheshimiwa Jaji ni Kifungu gani cha PGO kuwa IR5 ikifunguliwa Dar es salaam Mshtakiwa anatakiwa asafirishwe kutoka Moshi hadi Dar es salaam
Shahidi: hiyo ni manifesto ya CPA sikumbuki kifungu gani Wakili
Kibatala: Ngoja nikupe CPA unitajie Kifungu gani!
[Wakili Peter Kibatala Utaki tena CPA?]
Shahidi; mimi naona nisisumbue Mahakama, nilisema mazingira gani yaliyosababisha niwalete Dar es salaam.
Wakili Kibatala: Tuambie Kifungu cha sheria chochote
Shahidi; Sikumbuki kifungu cha sheria
Wakili Peter Kibatala: Pale Moshi palikuwa na facility zote za Kukuweza kuwahoji watuhumiwa pale Moshi kweli si kweli
Shahidi: Upelelezi ulikuwa bado unaendelea na kesi ilikuwa Dar es salaam
Wakili Peter Kibatala: Umenisaidia ila Bado hujajibu swali langu la msingi tafadhali
Wakili Kibatala: Jibu Kuwa Moshi palikuwa na Facility zote za kukuwezesha Kumuhoji Adam Kwa mujibu wa Sheria
Shaidi: Ndiyo zilikwepo Wakili
Kibatala: ulisema mlitoka Moshi saa ngapi Vile?
Shahidi: saa mbili Kibatala Afisa wa Polisi Gooldluck alikwepo..
Shahidi: ndiyo
Wakili Peter Kibatala: alikuwa na Silaha Yake wakati Mnatoka Moshi Kuja Dar es salaam?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji nitakuwa nimesahau Kumtaja ila nilitaka timu yangu yote nilikuwa nayo
Wakili Kibatala: Let's assume kuwa maelezo kuwa Adama alichukuliwa na wewe ulikuwa na Goodluck
Wakili Peter Kibatala: iambie Mahakama, na nakukumbusha upo chini ya Kiapo, tangu Umemkamata Adamoo ni saangapi umemwambia Jaji kuwa nj wakati gani umemruhusu anywe maji na Chakula?
Shahidi: suala la Chakula sikulizungumzia.
Wakili Peter Kibatala: Kwa mmakadirio tangu Umkamte Adamoo tangu Tarehe 05 Mpaka unamuhoji tarehe 07 ilikuwa ni Masaa mangapi?
Shahidi: Mpaka nipige Hesabu..
Wakili Peter Kibatala: lakini utakumbuka Kuwa zinapotea siku Mbili?
Shahidi: Ndiyo zinapita
Wakili Peter Kibatala: Ulimuhoji Mtuhumiwa ,Unafahamau au ufahamu kuwa Adam kasekwa Komandoo wa zamani kuwa alikuwa na Ugonjwa wa akili akiwa Jeshini TBD traumatic Battle Disorder?
Shahidi: aliniambia Wakili Peter Kibatala: hapa Uliongea?
Shahidi: Sijaongea
Wakili Peter Kibatala: Unafahamu kuwa Ugonjwa wa Battle Fatic Mental Disorder ni Ugonjwa wa Kawaida kwenye Majeshi?
Shahidi: Hayo Mambo ya Kitaalamu
Wakili Peter Kibatala: wewe si umesema ulimuhoji akiwa mzima wa Afya
Shahidi: Ndiyo
Wakili Peter Kibatala: Je unajua alipata Ugonjwa huo akiwa anatumika Nchi hii
Shahidi: Sikufahamu Wakili
Kibatala: Afya mliyokuwa anaongea na Wakili Msomi haikuwa Pamoja na Afya ya Kichwa
Shahidi: nilikuwa nazungumzia Afya ya Mwonekano
Wakili Peter Kibatala: Sasa Hiyo Afya ya
Jumla inajumuisha Afya ya Kichwa
Shahidi:ndiyo Pamoja na Kichwa
Wakili Peter Kibatala: Unafahamu kuwa watu wanaoumwa Battle Fatic au wewe Umeita Stress kuwa wanatakiwa kubebwa kama Yai+
Shahidi: sifahamu
Kwenye Eneo lolote la Central kwa ku Exclude.?
Shahidi: hakuwepo wakati anachukua Maelezo
Wakili Peter Kibatala: wakati wewe Unaongea Mwanzo hukumtoa?
Shaidi Sikumtoa
Wakili Peter Kibatala: Umefanya kazi ya Upelelezi kwa Muda gani?
Shahidi: Miaka 20 Wakili Peter
Kibatala: Shahidi Unafahamu Mtuhumiwa namba 2 ni Komandoo?
Shahidi: ndiyo ninafahamu Wakili
Kibatala: Mshitakiwa unamuona hapa na Kila akiletwa amefungwa Pingu, na najua na wewe
Unafahamu kwakuwa unakuja Mahakamani hapa kuimarisha Ulinzi?
Shahidi: Nakujaga ila naakaga mbali
Wakili Peter Kibatala: Sijakuuliza Unaishiaga Wapi, sema ndiyo nakujaga wakati wa Kesi hii au Hapana
Shahidi: Ndiyo nakujaga Kwenye kesi hii
Wakili Peter Kibatala: Mpaka Mnakuja naye Dar es salaam Mtuhumiwa alikuwa anamfahamu Kuwa Siku ya Mwisho atashitakiwa kwa Ugaidi..?
Shahidi: Ndiyo alikuwa anafahamu
Wakili Peter Kibatala: Muda wote mlikuwa mnazunguka na Watuhumiwa mkiwa mnatafuta Moses Lijenje mkiwa na Silaha?
Shahidi: ndiyo tulikuwa na SMG 2 na Pistol
Wakili Peter Kibatala: Ulimuambia Jaji hapa Kuwa Kuna Mazingira ya Upekee yaliyosabaisha Kuzunguka na Watuhumiwa Kwenye gari yenu na mkiwa na Silaha?
Shahidi: hapana
Wakili Peter Kibatala: Mwambie Jaji kuwa ni kwanini taarifa walizowaambia Watuhumiwa Msiende wenyewe Kumtafuta Mtuhumiwa wa tatu, Mpaka Mzunguke nao Kwenye Magari... Nini Kiliwazuia kwenda wenyewe?
Shahidi: Issue yenyewe ni Serious!
Wakili Peter Kibatala: asingekwepo Adam Kasekwa mngetumia njia zipi Kumpata Mtuhumiwa wa tatu?
Shahidi: tungetumia njia zozote.
Wakili Peter Kibatala: Safi Ndicho nilichokuwa nahitaji
Wakili Peter Kibatala: Ikumbushe Mahakama kuwa mlipotoka Moshi saa 2 Usiku mlifika Dar es salaam saa ngapi vile?
Shahidi: saa 11 Alfajiri Wakili Peter Kibatala: Kwa Hiyo Mlimuhoji na kuchukua maelezo baada ya Masaa 2 tu? Shahidi: Baada ya Masaa 2 ndiyo.
Kibatala: Umesema alikuwa na Afya Nzuri?
Shahidi: kimya Kibatala: Ulipomkamata Adamoo na Bunduki Moshi kule Rao, Ni saa ngapi Umezungumzia kumuonya Kisheria Kuhusiana Kupatikana na Silaha Kinyume na sheria?
Shahidi: Onyo kuhusiana na Bunduki sikutoa JAJI: hebu Rudia tena
Shahidi: Sikumuonya specifically Kuhusiana na kosa la Kumiliki silaha kinyume na silaha
Wakili Peter Kibatala: Mwambie pia Mheshimiwa Jaji kama ulimuonya kuhusiana na madawa ya kulevya
Shahidi: Mimi Binafsi sikumuonya kisheria
Wakili Peter Kibatala: Unakubaliana na Mimi Bunduki, na Madawa ya Kulevya na Kula Njama, ilikuwa ni Ukamataji mmoja?
Shahidi: ndiyo ukamataji Mmoja Wakili Peter Kibatala: unakubaliana Bunduki na Madawa ya Kulevya ni Makosa Makubwa Yanaweza Kusababisha Mtu afungwe Maisha?
Shahidi: inategemea kiasi cha madawa
Kibatala: Vipi Kuhusu kete 58?
Shahidi: sijui uzito wake
Kibatala: Ulitaja maungo ya Adamoo ulikokuta kete za Madawa ya Kulevya
Shahidi: Sikusema
Wakili Kibatala: Ulisema maungo gani Kuwa Ulikuta Bastola?
Shahidi: sikusema
Wakili Peter Kibatala: Umesema hapa Yale Madawa ya Kulevya ulithibitisha Kutoka Kwa Mkemia, Je unafahamu status ya kesi ya madawa ya kulevya status yake ikoje?
Shahidi: siwezi kulizungumzia
Kibatala: hutaki au hujui? ,kama hutaki nitamuomba Jaji Mahakama ikulazimishe
Shahidi: Status ya Kesi ya Madawa Sifahamu
Kibatala: Unakifahamu Kituo cha Polisi Mbweni?
Shahidi: Nakifahamu
Kibatala: Mara ya mwisho lini Kufika Mbweni?
Shahidi: hata Juzi nilienda
Kibatala: Je Adamoo katika kukamatwa Kwake alifika Mbweni?
Shahidi; alifika
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa Adamoo alifika Mbweni Polisi Kufanya nini?
Shahidi: Hilo sikusema
Kibatala: Unafahamu Kuwa Kutoka Mbweni Mpaka Ufike Mbweni Kuna vituo Vya Polisi zaidi ya 6 mpaka ufike Mbweni ukianzia Salenda Bridge Police station?
Shahidi: ndiyo Vipo Vingi. Wakili
Peter Kibatala: Goodluck uliyekuwa nae alifika Pia Mbweni Polisi?
Shahidi: Ndiyo alifika.. Wakili Peter
Kibatala: Afisa wa JWTZ Komandoo Anaitwa CHUMA alifika pia Mbweni.?
Shahidi: simkumbuki
Kibatala: je Ni Maafisa wangapi wa JWTZ Makomandoo waliofika KITUO cha Polisi Mbweni?
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: hukumbuki au hujui?
Shahidi: Sina Knowledge hiyo.
Kibatala: hujui.?
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: tuachane na hilo
[Kibatala anamfuata usoni kwake shahidi Kwa Kumkazia macho anamuuliza],
Je unafahamau Kuwa mshtakiwa Adamoo anashtakiwa makosa matano na moja la kula njama za ugaidi?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mimi siye ninaye andaa Mashtaka, Wanaoandaa ni Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, mheshimiwa
Kibatala: statement yako wanashitakiwa kwa maelezo uliyowaonya?
Wakili wa Serikali: OBJECTION. Mh. jaji wakili anatoa speech sana Jaji :Jamani tumpatie shahidi hata Dakika 2 Jamani, pale Kizimbani Si Mchezo
Shahidi: Kweli naomba niende HAJA NDOGO
Jaji: uende lakini urudi
[Mahakama yote inacheka]
Jaji: Mawakili mnaweza kunishauri Kama tunaweza Ku' break tuendelee kesho Upande wa Mashitaka Mnasemaje?
Ushauri: Tuendelee Kibatala na Mtobesywa wamalizie hoja zao kwanza Shahidi amerudi.
Kibatala: Mwambie Jaji Adamoo kuwa alishawahi kwa sababu yoyote ile kwenda Kituo cha Polisi Tazara
Shahidi; sifahamu
Kibatala: Gari Mliyoitumia kutoka Himo kufika Dar es salaam Unakumbuka namba zake za Usajili?
Shahidi: Sikumbuki Kibatala anaomba Wakili Mtobesya aendelee
Wakili Mtobesya: Shahidi ieleze Mahakama kama unamfahamu Documents ya Police inaitwa Detection Register..
Shahidi: naifahamu Wakili Mtobesya: Mueeleze Jaji hiyo ni Kitu gani?
Shahidi: ni Usajili wa mahabusu wanapoingoa na Wanapotoka
Wakili Mtobesya: nitakuwa sahihi Kuwa hujatoa Detention Register ya Moshi, Dar Central wala Mbweni ulikosema Mshtakiwa alienda?
Shahidi: Mimi sikutoa watatoa Wenzangu Wakili Mtobesya: Siyo Swali langu, Swali ulitoka hapa Mahakamani au hukutoa?
Shahidi: Sikutoa
Wakili Mtobesya: Nimesikia Unasema Ulimuhoji na Mtuhumiwa akathibitisha Maelezo yake?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Mtobesya: Ni sahihi Kuwa Uthibitisho wa mtu anayejua kusoma na Asiye Jua Kusoma ni tofauti?
Shahidi: inategemea
Wakili Mtobesya: Mwambie sasa Jaji inategemea nini.?
Jaji anasema; nahisi shahidi haelewi anachoulizwa. Naona anajibu tofauti na vitu anavyoulizwa. Wakili Msaidie ajue UTHIBITISHO ni nini tafadhali..
Wakili Mtobesya: Kuna aina Ngapi za Uthibitisho
Shahidi: Uthibitisho wa shahidi na Mtuhumiwa.
JAJI: Ngoja twende pamoja, wewe Shahidi kuthibitisha ni tendo gani?
Shahidi: Kuthibitisha ni Kukubali kuwa Kitendo fulani kimefanyika..
Jaji; Wakili endelea.. Wakili
Mtobesya: huo Uthibitisho unaosema ni wa aina gani unatumika?
Shahidi: Kama unamuhoji mtuhumiwa chini ya Onyo lazima urejee sect 53 Mtobesya: wewe kwa zoezi Ulilofanya Ulitumia Kifumgu Kipi
Shahidi: kifungu cha 57 Wakili Mtobesya: Kifungu Kidogo cha 57 (3) kuna aina ngapi za uthibitisho?
Jaji; tumsaidie tusimuulize maswali ya kisheria
Wakili Mtobesya: Mtuhumiwa alikuwa anajua Kusoma na Kuandika?
Shahidi: alikuwa anajua kusoma na kuandika
Wakili Mtobesya: Mtu anayejua Kusoma na Kuandika anathibitisha Vipi?
Shahidi: kwa sahihi ya kawaida au ya dole gumba.
Wakili Mtobesya: ni sahihi nikisema Mtu asiyejua kusoma ndiye yanayoweza kuandika sahihi na Kuweka dole gumba?
Shahidi: ile ni kuthibitisha tu. Finger print Mtu hawezi kukwepa lakini sahihi Mtu anaweza kusema Siyo yake.
Wakili Mtobesya: Isaidie Mahakama hicho unachosema wewe ni Sheria na kanuni zinavyotaka au ni uzoefu tu?
Shahidi: Ni uzoefu siyo sheria.. Wakili Mtobesya: anakaa chini.. Jaji: Upande wa Mashitaka Wakili wa Serikali wanaomba kesi iharishwe mpaka kesho.
Jaji anauliza, upande wa utetezi mnasemaje?
Wakili Kibatala: hatuna Pingamizi, nafikiri ihairishwe mpaka kesho.. Wakili wa Serikali anajibu Saa tatu asubuhi..
Jaji anauliza leo tumefika saa ngapi na washtakiwa wamefika saa ngapi?
Jaji anauliza kesho tuanze saa 2 au Saa 3
Wakili Kibatala anasema Saa tatu wameshindwa kuleta watuhumiwa tufanye saa 4
Jaji anahairisha kesi mpaka kesho saa 4 asubuhi Kuendelea na shauri Dogo
Askari anapiga keleleeeeee..
Jaji anasimama anatoka....
MWISHO
Kwa hisani ya Martin M M - Twitter
Zaidi soma:
Thread 'Updates: Yanayojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi' Updates: Yanayojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi