Madaktari waache kutumia uhai wa watanzania kudai maslahi yao!

Ufupi wa akili yako umepelekea ww kuandika pumba hizi, au na ww unaendaga india au sa au uk?
 
mkweche binafsi nimekuelewa.......kwa sisi walimu.....mwalimu aliwahi kusema..
"WALE WALIOPATA FURSA YA KUPATA ELIMU KATIKA JMT, NI SAWA NA KIJIJI CHENYE NJAA AMBACHO KINAAMUA KUTOA AKIBA YA CHAKULA KUWAPA VIJANA WENYE NGUVU ILI WAKAHEMEE MBALI.....VIJANA WALE WANATAKIWA KUHEMEA NA KULETA CHAKULA NYUMBANI........WASIPOFANYA HIVYO NI WASALITI"
Nakama vijana hao wakileta chakula nyumbani halafu wazee wachache walafi wakakila chakula hicho chote bila kuwapatia watoto, je walihemea chakula hicho wafanye nini?
 
Unfortunately Tanzania ya leo siyo ile ya Nyerere. Wakati wa Nyerere tulikuwa tunajua mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali, na hata mshahara wa Nyerere mwenyewe ulikuwa unajulikana. Kuna wakati mshahara wa Nyerere ulikuwa ni Sh 2,500 wakati ule wa kima cha chini ukiwa ni Sh 380, halafu madakatri wakiwa wanalipwa Shs 1800, na medical assistants wakilipwa Sh 1300. Engineering graduates wakiwa wanalipwa Sh 1650.

Kwa statistics hizi, je wanacholipwa madaktari kwa sasa kuna uwiano? Kama hakuna uwiano, ilikuwaje wakaachwa nyuma?
 
Mie Mkweche naishangaa serikali kwanini mpaka dakika hii Haijafukuza Kazi Madaktari wote waliogoma!Kuwafutia vyeti na Usajili,Kuwa fungia Utumishi mahala popote ndani na nje,kuwatoa kwenye nyumba za Umma na kuwafungulia Mashtaka!Mambo ya kubebelezana yanarudisha nchi nyuma!Kama wamefikia hatua ya kuacha wagonjwa wafe ni watu wabaya sana hata Wakoloni hawakufikia ukatili kama huu!Kwa Utamaduni wa Kiafrika Mgonjwa anatakiwa abembelezwe atunzwe na kuhudumiwa vizuri ili apone,Sasa imekuwa kinyume!Mgonjwa Anaachwa Afe tena akiwa Hospitalini, wakifa wagojwa wengi na Madaktari Walipwa Mahela mengi watafaidije heala za DAMU!Mkweche nawashangaa wanaowashabikia Madaktari na Kuwaacha WAGONJWA BILA MTETEZI!
Madaktari walio wengi watulii kazini kwao kazi kuzunguka kwenye mahospitali binafsi kufanya kazi za ziada na kufanya serilini ni kwa kuchukulia mishahara!Serikali iamke na Kutimua Wagomaji wote!
Pelekeni Ruzuku Kwenye Mahospitali Binafsi ili yapokee ndugu zetu watanzania wanaoteseka!
Kwanza Serikali isifanye makosa ya kuongeza Mishahara ya Madaktari kabla ya sekta nyingine!Kada za Afya zinapedelewa sana kwenye mishahara wakati sote ni wafanyakazi na tunatakiwa kulijenga taifa kila mmoja wetu anaumuhimu kwa nafasi yake!
 
POLE!Kama Umeona Madai ya Madaktari ni Makubwa Kuliko Uhai Wa Ndugu yako Sikuwezi!Na siku zote Ujinga wa Watanzani ndio Mtaji wa Wajanja!

Jua kusoma post za watu na kuzielewa bila kukurupuka na conclusion za uwongo. Soma tena post yangu kama inazungumuza hayo uliyoandika hapo juu.


Kama una akili sahihi, utagundua kuwa hata kama madaktari wakiacha mgomo wao huo katika mazingira ya kutoridhishwa na mazingira ya kazi, kumpeleka ndugu yako akatibiwe na daktari ambaye hana moyo wa kazi ni hatari sana kuliko kutompeleka kabisa ndugu yako huyo. Kinachotakiwa ni kwa serikali kuhakikisha kuwa inaondoa manung'uniko miongoni mwa madakatri badala ya kuwalazimisha kutibu watu kwa nguvu. Je daktari akiamua kukuandikia dawa zinazokuharibu mwili zaidi utasemaje, si ni adhadhali ukae nyumbani ukiomba Mungu labda mwili wako utapona kwa natural processes zake kuliko kupewa dawa inayoharakisha kukuua.
 
Ujamaa ni siasa aliyoianzisha Nyerere 1967 kabla ya hapo nchi hii haikuwa ya kijamaa.

Tanganyika ilikuwa nchi ya machifu, mipaka ya machifu hao ipo na inajulikana mpaka leo hii.
Koo za machifu zipo na bado kimila zinaheshimika.

Kwa hiyo ujamaa si asili yetu, wanao lazimisha historia ya nchi hii wangependa iwe hivyo.

Kuishi pamoja vijijini si ujamaa ila ni hulka ya binadamu wa level moja kuishi pamoja na hata kushirikiana.
Hata mabepari huishi pamoja na hushirikiana katika ubepari wao.

Ndiyo maana EU pamoja ngawira zao za nguvu walizo nazo kama nchi moja moja bado wanaulilia sana umoja wa ulaya na sisi Afrika kila nchi inapenda kwenda kivyake na kupinga kwa nguvu zote aina yeyote ile ya umoja. Hata sisi wenye muungano Tz na Zbr tunauona nuksi hata ukifa leo ni sawa tu.
Umasini na umoja si vitu vinavyo changamana vyema. Utajiri na umoja siku zote umekuwa ukifanikiwa.
Ndiyo maana 1884 ,kama sikosei, kule ujerumani ulifanyika mkutano wa wenye fedha kugawana bara la afrika ili walinyonye na ulifanikiwa sana.

Yako mazuri katika ujamaa hata hivyo kuna mabaya.
jambo baya katika ujamaa ni watu kubwetekaa na kusubiri serikali ifanye kila kitu.
jambo jingine baya katika ujamaa ni unafiki. Viongozi wa kitaifa katika ujamaa huishi maisha ya anasa na kujijengea wigo huku wakiwalazimisha wananchi kujifunga mikanda. I have experienced that in my life.

Ubepari nao una ubaya yake lakini uzuri wake ni kwamba watu wanajituma hakuna Free lunch.
Ukikopa ukishindwa kulipa unafirisiwa bia huruma.
Ubaya wa ubepari ni ile hali ya kujali faida kuliko kitu chochote kile. Msingi mkuu wa ubepari ni mtaji( Michuzi) Siyo Kilaza na mchovu Muhidin Michuzi I mean Ngawira.

Labda tatizo letu kubwa sana ni kushindwa kujua tafsiri ya halisi ya mambo yote tunayo yaongelea.
Je tukinena jambo lolote lina huwa tunafanya uyakinifu wa kina??

Tukisema tunajitoshereza kwa chakula kama nchi maana yake nini?
kila mtu Tanzania ana chakula yaani watu wote zaidi ya 45,000,000 au wale wenye uwezo wa kulalamika njaa wakasika ndiyo wenye chakula??
Tukisema hakuna tatizo la umeme na mgao umekwisha, je tuna maanisha tatizo limeisha kwa nchi nzima au kwenye mitaa yetu Dar wa kule Biharamulo wajiju??
Daktari wa muhimbili akisema hana vifaa ana maana gani?
hana gloves, syrynge, gauze, aspirin au X Ray??

Je Muhimbili is another hospital in the next block???

Madaktari wa muhimbili wakisema hawana vifaa wana maanisha kukosekana kwa vifaa kama vile vinavyo kosekana Amana Mwnanyamala Temeke + Vifaa vya nguvu vinavyofanya wawe Hospitali ya Rufaa.

Kuna lugha gongana hapa kiasi kwamba wakati mwingine huwa nasoma hoja ya mtu mpaka mwili unasisimka kwa mshangao. Kuna hoja hapa inasema si haki Madaktari kushindwa kumtibu Dr Ulimboka kwa kufanya hivyo wanamaanisha kusoma kwao ni bure.

Naamini kuna watu hapa wanadhani tunawaongelea Ma medical Assistant kwenye zahanati za ushwazi. MA wana kazi yao muhimu sana katika taifa hili na wasingekuwepo nongwa ingekuwa kubwa.
Tukisema Madaktari tuna maanisha madaktari yaani shule ni POMENI MPAKA BUSHEE

Suala la Ada Dunia nzima.
Si dhani kama kuna mwenye uwezo wa kulipia Full tuition ya Chuo kwa sababu hata hizo 25M hazitoshi hata kidogo wa std ya Bongo. Tuliosoma vyuo vya wenyewe huku ughaibhuni ambavyo ni mali ya State wenyewe huvilipia kwa kodi ukimaliza chuo hawakufuati na kukuambia eti mshiko ulio lipia pale ulikuwa 40% sasa ni lazima ufanye kazi kama sisi tutakavyo kwani 60% tulikulipia.

Faida ya nchi kujenga vyuo kuweka vifaa vyote na kusomesha watu wake si kuja kesho na kuanza kudai kila mtu arudishe fedha aliyolipiwa na serikali. Faida ya kusomesha watu katika taifa ni ile Tija yao katika kufanya kazi popote pale walipo. Ni ule mwamko mzima wa nchi kuwa na kiwango cha wenye uelewa kiachoongezeka kila siku. Ni kujenga tabaka la watu watakao leta changamoto ya maendleao ya nchi yao kwa kuapandisha standard of living. Siku uelewa wetu pale dar ukikuwa tutaandama kudai serikali ijenge mifereji mikubwa ya chini kwa chini ya sewage ili kuondoa usumbufu wa kila nyumba kuwa na shimo lake na maji taka na mafuriko ya mashimo hayo kila msimu wa mvua. Kwa vile kiwango chetu cha STD of living kwa wastani wake kiko chini leo hii hatuoni sababu ya kuandaman kudai mifereji hiyo. Taifa hufaidika kwa namna zote kusomesha watu wake jambo hili halina itikadi ya ujamaa wala ubepari.

Kwanza kabisa tukubali kwamba hata hiyo kodi serikali ya CCM imeshindwa kukusanya kwa udhaifu wake. Pili kwa udhaifu pia inashindwa kujenga mazingira ya kuanzisha vyanzo vingine vya kodi mfano.

Serikali ya CCM kushindwa kujua Nishati ni Muhimu kuliko Bendera na Mashati ya kijani.


Kuna Maamuma hapa JF wanasema heri Edward Lowassa ni mtu wa vitendo kuliko Pinda, kwangu wote ni vilaza wa kutupwa. Mimi kila siku nasema Edward Lowassa ni Nuksi kwa sababu kichwa chake hakifanyi kazi vizuri. Ukiona mtu anahujumu sekta ya Nishati katika nchi yeyote ile ujue mtu huyo ni Adui wa Taifa na mpinga maendeleo namba moja. Mishati ni sekta muhimu katika taifa, sawa sawa kabisa na Mishipa ya Fahamu au misuli ya mwili.
Edward Lowassa alihujumu kwa akili zake zote na nguvu zake zote sekta hii muhimu ili aweze kutunisha pochi ya familia yake ambayo sasa bila haya anapita kuwarubuni kondoo wa bwana na waja wake kila kona ya nchi hii. Edward Lowassa ni mtu hatari sana na ni mtu wa kuogopwa kama Gonjwa Sugu.

Nchi isiyo kuwa na Nishati ya Uhakika ni nchi isiyowekezeka. Hakuna muwekezaji yeyote wa maana atawekeza katika nchi yenye mgao wa umeme na nchi ambayo mikataba ya uwekezaji katika sekta ya nishati hujadiliwa katika vikao vya chama kama NEC ya CCM wakati Nishati ni suala la serikali kuu. Sekta ya umeme ni namba moja maji namba mbili kisha mawasiliano. Hata tungekuwa hatuna mto hata mmoja ili kujenga Hydro eletric power bado kama nchi tunatakiwa tujitegemee katika Nisati ya umeme wa uhakika siku zote. Tun gas ya kutosha tuna makaa yamawe ya kutosha hizi resources mbili tu zinatosha kuzalisha umeme wa kutosha wananchi wote wa Tanganyika na Zanzibar bila kuwa na mgao wowote ule. Kampuni ya GE ina mashine za kila uwezo za kuzarisha umeme kwa kutumia gesi na makaa ya mawe, sis serikali yetu chini ya Edward Lowassa ilikubali kuvuruga taratibu zote za manunuzi ya kiserikali na kuagiza mitambo used isiyokuwa na uwezo wa kutumia gesi yetu.
Mtu mwenye upofu wa vipaumbele vya kitaifa hata awe na mvi kiasi gani hata sura yake iwe na mvuto vipi ni JANGA kwa taifa kumkumbatia

Tukiwa na nishati ya umeme ya uhakika mpaka vijijini tutaweza kubadili hata kilimo chetu ambacho hutegemea misimu na hali ya hewa ya mwaka ule kuliko urithi wa asili wa eneo hilo. Umeme ukipatika mpaka vijini Pampu za maji za kutumia umeme zikifungwa huko vijijini maeneo makavu ya maelfu ya kilomita za mraba yatageuzwa mashamba ya misimu yote.
Tutakuwa na uzarishaji wa mara dufu wa mimea na mifugo.
Kwa kuwa na nishati ya umeme ya uhakika tutaweza pia kujenga mfumo wa Mabasi yatumiayo umeme, siongelei train naongelea mabai ya kawaida kabisa yasiyo tumia diesel bali umeme.
Umeme wa uhakika pia huweza kuzuia kukua kwa uwingi wa watu katika miji kutoka na uhamiaji utokanao na kukimbia karaha za huko kusiko na umeme

Hicho tunacho kiita kodi inayotumika kusomesha watu ni kama bakshish peremende au biskuti.
Shughuli ya kusomesha kijana bado ni ya mama na baba.





POLE SANA!Tatizo Mlio wengi Mnaelewa Mambo juu!Kusomesha "Dokita"moja si chini ya 25Million!Vyuo Vya Ngazi zote, Mahospitali nk Wananchi wanachangia tu hawalipi!Katika Budget za Taasisi nilizotaja Mapato kutokana na Ada au Malipo mbalimbali hayafiki 10% wanachi tunaendesha vyuo vile kwa njia ya KODI!
Ulafiwa Wa fedha na kupenda Ufahari wa wanasiasa,wasomi na watanzania ni Matokeo ya KUUBEZA UJAMAA!Asili ya Watanzania ni Ujamaa!Ubepari Tumechemsha
Narudia tena Pole
 
Badili fan usome dk ili ujitolee jinga ww

Mie ni Mkweche Tayari!Kwa Fani yangu inanitosha!Kwa Taarifa yako mie Matatizo ya madaktari na sekta ya afya nayajua kulilo wewe Zumbu kuku!Na kwa nafasi yangu Hospitali ninayofanyia nimeshiriki kuyatatua
ILA HAKUNA TATIZO KUBWA KAMA KUACHA WAGONJWA WAFE TENA WAKIWA HOSPITALI!
Kinyesi wewe
 
Ufupi wa akili yako umepelekea ww kuandika pumba hizi, au na ww unaendaga india au sa au uk?
Tatizo wengine Hamjui kinachoendelea mahospitalini!Ungekuwa na Akili ndefu Ungepigania Uhai Kwanza na si Posho!
UHAI Wa watanzania ni Mkubwa kuliko posho na mishahara
 
Safi sana hii!
Wanaolaani madaktari wote hawana akili.
Hakuna mtu mwenye mkataba na daktari, ya kwamba atamtibu ht km anapunjwa malipo.
Wananchi wana mkataba na serikali, ndo inapaswa kuwapa hizo huduma za afya.
Km hazipo, iulizeni serikali, madaktari ni waajiriwa tu, wenye haki ya kugoma na kupigania maslahi na hadhi yao.
Ilazimisheni serikali iwatimizie madai yao.
Km mnaona serikali haitaweza fanya hayo kwa madaktari pungufu ya 2000 waliopo serikalini, lkn inaweza kuongeza posho maradufu na kukopesha magari kwa madiwani zaid ya 4000, basi nanyi ni sehemu ya tatizo, mnapaswa kukaa kimya na kufa taratibu tu, bila kelele.
kama hoja zako ndio hizi hapana shaka wewe ndio huna akili majinuni bin hayawani bin taahira. inaonekana hata hujui kuwa madr ni sehemu ya serikali. kumbafu kabisa.
 
....Katika hotuba ya Hayati Mwl.Nyerere kule University of Liberia,Monrovia,29,feb,1969"The Intellectual Needs Society"
Kibwagizo cha Kukikumbuka ni"Without the Society to be served,Intellectualism is meaningless and hollow.Intellectuals should put SERVICE FIRST and SELF SECOND,and be Modest and Practical"
Inapotokea madaktari wanagoma kuiweka mbele na kuihudumia jamii iliowahangaikia na kujiweka mbele wao,majibu yatapatikana hapa hapa duniani!...

Ujumbe huu unamaana kwa madaktari. Ni kweli kwamba hospitali ambazo madaktari wamegoma hakuna kigogo anayetibiwa hapo, hata Ulimboka naye imebidi asitibiwe hapo. Ni ukweli kwamba maslahi wanayodai madaktari hayataweza kupooza roho za wajane. Lakini katika harakati zozote za kudai haki na usawa lazima matatizo yatokee, na madaktari wanajua hilo. Maslahi bora kwa madaktari, huduma bora za afya. Naungana na madaktari kudai haki zao, na pia namwomba Mungu awasaidie wagonjwa katika kipindi hiki kusitokee maafa yatakayotokana na migomo.
 
MKWECHE
Senti Great Thinker,
kama ni mchezo wa karata basi tungesema ni turufu, basi kama ingekuwa draft tungeita kingi..hawa madr wanatumia uhai wa wanyonge kama turufu / kingi kukidhi malengo yao ya kibinafsi. ni bahati mbaya tu serikali yetu tukufu imekosa mipango bora ya kumitigate hii kadhia kutotokea tena tangu ule mgomo wa kwanza enzi za akina Zakhia Meghji. Kwa hili mi nailaumu sana tena sana. Kama alivyosema thinker Ogah, dhulma dhidi ya wanyonge ina mikono mingi. Hakuna substitute ya uhai wa mwanadamu na kama wengine wanavopinga, basi mi nasema kama misingi ni ubinafsi basi kila mtu adai chake tuone kama tutabakiwa na taifa. Lazima kuwe na compromise, ndio jinsi ya ku-co-exist hamna mwene haki kuliko mwenginewe.
 
Last edited by a moderator:
POLE SANA!Tatizo Mlio wengi Mnaelewa Mambo juu!Kusomesha "Dokita"moja si chini ya 25Million!Vyuo Vya Ngazi zote, Mahospitali nk Wananchi wanachangia tu hawalipi!Katika Budget za Taasisi nilizotaja Mapato kutokana na Ada au Malipo mbalimbali hayafiki 10% wanachi tunaendesha vyuo vile kwa njia ya KODI!
Ulafiwa Wa fedha na kupenda Ufahari wa wanasiasa,wasomi na watanzania ni Matokeo ya KUUBEZA UJAMAA!Asili ya Watanzania ni Ujamaa!Ubepari Tumechemsha
Narudia tena Pole

Acha kudanganya watu weye!! Mwaka juzi serikali ya marekani ilitoa misaada ili madaktari walipiwe ada wasijisomeshe, serikali ya Tanzania ikaichukua hiyo hela ikapelekwa kwenye Uchaguzi mdogo, matokeo yake madaktari wanaona wananyanyasika na ndio matokeo haya. Kuna misaada toka nje ya nchi kwa ajili ya kununua ultrasound na x-ray mashines, Blandina aliwemwa pale hizo hela azikusanye ziende kwenye mauchaguzi, madaktari wakigundua hilo na sasa serikali imemuweka Mwinyi afanye alichokuwa anakifanya Blandina ( yeye si ndie rais ajaye, lazima atafute hela ya kampeni).

BTW hao madaktari hawajisikii salama ndani ya nchi yao na hawajisikii usalama kuendelea na kazi mpaka serikali itakapowahakikishia usalama wao na kuwa wakina ACP Msangi hawataendeleza mpango wao wa kuua baadhi kuwatia uchungu na kuwakomoa.
 
Wewe utakuwa Mwigulu au Profesa maji marefu ndiyo wenye maakili ya kipuuzi, hujui hata nani ana wajibu wa kutibu wananchi. Siyo lazima serikali itumie madaktari wa Tanzania inaweza kuleta kutoka nje ya nchi ilimradi watu wake wapate huduma ya afya. Sasa wewe kwa ufupi wa fikra zako unabwatuka tu au unaishi kwa posho za MAGAMBA kuwa na fikra pevu nyinyi ndiyo mnasababisha nchi haiendelei kwa sababu hujui serikali inayochukua kodi ya mwananchi ina wajibika kufanya nini kwa mwananchi wake kama ukusoma shule mbona kuna elimu ya gumbaru nenda kasome.
Mie ni Mkweche Tayari!Kwa Fani yangu inanitosha!Kwa Taarifa yako mie Matatizo ya madaktari na sekta ya afya nayajua kulilo wewe Zumbu kuku!Na kwa nafasi yangu Hospitali ninayofanyia nimeshiriki kuyatatua
ILA HAKUNA TATIZO KUBWA KAMA KUACHA WAGONJWA WAFE TENA WAKIWA HOSPITALI!
Kinyesi wewe
 
Mie Mkweche kwa upande wangu .......Mie ni Mkweche jamani
Mkuu sijui unaongelea nini. Dai kuu la madaktari ni kuwezeshwa kuwasaidia wagonjwa vizuri zaidi, mishahara ni moja ya tu ya hilo, si dai kuu. Ukiangalia utaona kuwa viongozi wetu ni wabinafsi zaidi kuliko madaktari, wao wakiumwa macho, mafua, tumbo wanakwenda kutibiwa Ulaya, lakini Muhimbili hata CT Scan mgogoro, dawa ndio kabisa. Kwa hiyo tunapozungumzia uzalendo tuanze na hawa wa juu, sio wa chini. And the fact is huwezi kuwa mkatoliki kuliko Papa, au huwezi kuwa mwislamu kuliko yule wa Mecca na Medina.

Viongozi wanatutumia sisi kutuibia, wanatuibia kwa kisingizio cha 'kwa ajili ya wananchi'.
 
Katika kudai haki pasipo haki, watu kufa hakukwepeki. Katika kudai uhuru palipo utumwa, kufa hakukwepeki. Katika kupinga udhalimu palipo ukandamizaji, kufa hakukwepuki. Watu huenda vitani wakijua kabisa kifo kinawachungulia lakini inabidi wapambane na adui. Historia dunia nzima kuna watu ilibidi wafe ili haki ipatikane, kuna watu walipoteza maisha ili wengine waweze kuwa huru, kuna watu walijitolea mhanga ili amani ipatikane na dunia iweze kusonga mbele.

Humu kuna watu wanaona uchungu kwa ndugu zao kufa Muhimbili kwa kukosa huduma, wanasahau wapo wengine wengi maradufu wanakufa bila hata kufika Muhimbili, hawana uwezo, hawana namna. Wako wanaokufa kila siku mikononi mwa madaktari kwa dawa kukosekana. Wako madaktari ambao kila wanaporudi nyumbani hata usingizi hawaupati kwa sababu ya mgonjwa moja ambaye wana hakika angeweza kuokolewa lakini haikuwa hivyo kwa ukosefu wa vifaa.

Uhai wa Mtanzania umewekwa rehani, si na madaktari bali haya manyang'au yanayokomba hadi uji wa mtoto. Tungekuwa kweli tuna uchungu na ndugu zetu kupoteza maisha, vidole tungewanyooshea watawala ambao hawaoni umuhimu wa kuboresha huduma ya afya kwani wao wakipata hata mafua, haooo mpaka hospitali ya Apollo, India au Afrika Kusini au Ujerumani. Ujinga wetu ndio unatugharimu.
 
mie naona drs wana genuine demands,ila chonde chonde nawaomba drs muwasihi wafamasia waache kuzifisadi na kupeleka kwenye pharmacies zao dawa chache zinazotoka msd
 
Wewe utakuwa Mwigulu au Profesa maji marefu ndiyo wenye maakili ya kipuuzi, hujui hata nani ana wajibu wa kutibu wananchi. Siyo lazima serikali itumie madaktari wa Tanzania inaweza kuleta kutoka nje ya nchi ilimradi watu wake wapate huduma ya afya. Sasa wewe kwa ufupi wa fikra zako unabwatuka tu au unaishi kwa posho za MAGAMBA kuwa na fikra pevu nyinyi ndiyo mnasababisha nchi haiendelei kwa sababu hujui serikali inayochukua kodi ya mwananchi ina wajibika kufanya nini kwa mwananchi wake kama ukusoma shule mbona kuna elimu ya gumbaru nenda kasome.
Hakuna serikali duniani inayoeza kukidhi whimsical madai ya kila employee, it is common sense. Sasa kama haiezi kuwalipa locals madai yao it is also logical haiezi kuwalipa experts, achilia mbali suala la availability yao. Sasa kama unaona wanachelewa kulipa walipe wewe basi.
 
Mkuu sijui unaongelea nini. Dai kuu la madaktari ni kuwezeshwa kuwasaidia wagonjwa vizuri zaidi, mishahara ni moja ya tu ya hilo, si dai kuu. Ukiangalia utaona kuwa viongozi wetu ni wabinafsi zaidi kuliko madaktari, wao wakiumwa macho, mafua, tumbo wanakwenda kutibiwa Ulaya, lakini Muhimbili hata CT Scan mgogoro, dawa ndio kabisa. Kwa hiyo tunapozungumzia uzalendo tuanze na hawa wa juu, sio wa chini. And the fact is huwezi kuwa mkatoliki kuliko Papa, au huwezi kuwa mwislamu kuliko yule wa Mecca na Medina.

Viongozi wanatutumia sisi kutuibia, wanatuibia kwa kisingizio cha 'kwa ajili ya wananchi'.
Mbinu ni ileile tu ya kutumia turufu ya wananchi / wagonjwa / uhai.
 
POLE SANA!Tatizo Mlio wengi Mnaelewa Mambo juu!Kusomesha "Dokita"moja si chini ya 25Million!Vyuo Vya Ngazi zote, Mahospitali nk Wananchi wanachangia tu hawalipi!Katika Budget za Taasisi nilizotaja Mapato kutokana na Ada au Malipo mbalimbali hayafiki 10% wanachi tunaendesha vyuo vile kwa njia ya KODI!
Ulafiwa Wa fedha na kupenda Ufahari wa wanasiasa,wasomi na watanzania ni Matokeo ya KUUBEZA UJAMAA!Asili ya Watanzania ni Ujamaa!Ubepari Tumechemsha
Narudia tena Pole
Kusomea udakitari siyo sawa na kwenda kenye choo cha public ambako kila mtu anaweza kuingia. Iwako kazi inayofanywa hata na akina Lusinde inalipwa shilingi milioni 10 au iwapo serikali yetu iko tayari kuita madakatari kutoka nje kwa kuwalipa hela nyingi lakini haitaki kuwalipa madakatari wetu ipsavayo basi ni lazima tujue kuwa serikali yetu haijui vipaumbele vyake. Kuwasomesha madakatri hao siyo kuwa walifanyiwa feva, bali wao ndio waliokuwa wanaweza kusomea kozi hiyo.
 
Back
Top Bottom