Madaktari waache kutumia uhai wa watanzania kudai maslahi yao!

MKWECHE

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
299
64
Mie Mkweche kwa upande wangu siungagi Mkono Migomo ya Madaktari na watu wengine wa Sekta ya Afya.Migomo nisiyoipenda ni ile ya kukataa kuhudumia wagonjwa ili WAFE kwa kukosa tiba!Kama kunamtu anaeunga mkono wa namna hii ya kuacha wagonjwa wafe wakiwa Tayari ndani ya Hospitali basi,siyo bure huyo mtu atakuwa na lake Jambo!
Mie Mkweche utaniambia nini juu ya Hospitali za TZ!Nna miaka 7 sasa nafanya kazi kwenye hospitali!Hakuna wanachokidai wa wachozungumzia Madaktari kama mapungufu ktk sekta ya afya nisichokijua!
Katika madai yao Yote Hakuna kitu KIKUUBWA Unatakachokifananisha na UHAI wa Binadamu!
Sie wasomi(Kah!Mkweche nae msomi si ana Masterz)Madaktari na Mkweche,Tumesomeshwa na Kodi na Jasho la Watu Mafukara wa watanzania,Kwa Lengo la Kwamba turudishae fadhila za Kuwapa huduma bora za Afya na kubadilisha hali zao za maisha ili siku moja mafurahie matunda ya uhuru!
Katika hotuba ya Hayati Mwl.Nyerere kule University of Liberia,Monrovia,29,feb,1969"The Intellectual Needs Society"
Kibwagizo cha Kukikumbuka ni"Without the Society to be served,Intellectualism is meaningless and hollow.Intellectuals should put SERVICE FIRST and SELF SECOND,and be Modest and Practical"
Inapotokea madaktari wanagoma kuiweka mbele na kuihudumia jamii iliowahangaikia na kujiweka mbele wao,majibu yatapatikana hapa hapa duniani!
Madaktari Hawajaigomea SERIKALI BALI WAMEGOMA Kutibu wagojwa!Hospitali zote wanazofanyia madaktari waliogama ni nadra sana kukuta Kigogo anitibiwa wateja wao ni jamii ya watanzania!Aibu yao waliogoma
Dr.Ulimboka hakutendewa haki hata kidogo kwa kupigwa na kutekwa kwake!Ila nae hakufanya Busara kuongoza Mgomo ambao,Majibu ya Madai yake Yanategemea Roho za wanajamii!
Asiejali MAISHA NA UHAI WA MWENZAKE si Mzalendo na Kamwe hatekelezi mapango wa Mungu!
Mkweche nakiri Madawa,vifaa Tiba,Vitendanishi ni Tatizo kubwa sana mahospitali,Laukama Madokita na wahudumu wengine wa Afya wanamiliki maduka na ma-hospitali ambayo yananeemeka na Uzembe wa Serikali katika kukabiliana na tatizo la dawa na Mahitaji mbalimbali!Sipendi Mgomo kwa Sababu Mwisho wa Siku Anaekufa ni Mnyonge wa Tz!Hata mukiongezewa Ma Call na mazagazaga mengine Je Machungu ya Wajane na Mayatima Mtayapooza!
Mie ni Mkweche jamani
 
Mie Mkweche utaniambia nini juu ya Hospitali za TZ!Nna miaka 7 sasa nafanya kazi kwenye hospitali!Hakuna wanachokidai wa wachozungumzia Madaktari kama mapungufu ktk sekta ya afya nisichokijua!
Katika madai yao Yote Hakuna kitu KIKUUBWA Unatakachokifananisha na UHAI wa Binadamu!
Sie wasomi(Kah!Mkweche nae msomi si ana Masterz)

Naona huna tofauti na nchemba...tena hata kuandika kwa computer tu haujui! Hii Masterez(??) yako ni chuo gani cha kata?
 
Unfortunately, tangu Tanzania tulipojenga msingi wa kila mtu atashibia kwenye meza yake basi hatima yetu ni kwa madakatari kushibia kwenye uhai wetu. Si jambo jema lakini ndiyo hali halisi tunaotakiwa kukabiliana nayo. Iwapo afisa wa ushuru hata wa dxarasa la kumi na mbili atapokea mamilioni ya pesa kutoka kwenye deski lake, na katibu wa siasa naye vivyo hivyo atapokea mamilioni kwa kuzunguka nchi nzima, na mbunge naye atapokea mamilioni kwa kulala bungeni basi ama dakatri naye apokee mamilioni kwa kututibu au atuache tujifie wenyewe. Ninaandika wakati nina mtu wangu wa karibu sana amekosa matibabu aliyokuwa anahitaji kwa sababu ya mgomo huu. Hospitali za binafsi zilizoko karibu hazina uwezo wa kutoa matibabu kwa ndugu yangu huyo isipokuwa ile ya rufaa ambayo madakatari wake wamegoma. Kwa roho nyepesi ya kuona ndugu yangu anavyoumia, ningewalaumu madaktari lakini siwalaumu kabisa; ninajua kuwa ndiyo system tuliyojijengea, itabidi tudumu nayo. Wanasiasa wanapowadanganya wanachi kuwa watafukuza madakatari halafu wataleta madakatari wengine, sijui watawatoa wapi madakatari wa kulipa kiduchu namna hiyo.
 
Nina ujumbe wako kutoka kwa Nepi, anasema usisahau kwenda kuchukua posho yako, kwani unafanya vizuri kazi aliyokutuma....
 
mkweche binafsi nimekuelewa.......kwa sisi walimu.....mwalimu aliwahi kusema..
"WALE WALIOPATA FURSA YA KUPATA ELIMU KATIKA JMT, NI SAWA NA KIJIJI CHENYE NJAA AMBACHO KINAAMUA KUTOA AKIBA YA CHAKULA KUWAPA VIJANA WENYE NGUVU ILI WAKAHEMEE MBALI.....VIJANA WALE WANATAKIWA KUHEMEA NA KULETA CHAKULA NYUMBANI........WASIPOFANYA HIVYO NI WASALITI"
 
..........Wote (Madakitari na Viongozi Serikalini) ni Wauaji ikiwemo sisi wenyewe wananchi kwani tumeshindwa kuiwajibisha serikali pale inapobidi kufanya hivyo.........

Hakuna mwenye unafuu katika dhambi hii...........nina amini kila mtu atajifunza kutokana na kadhia hii..........Kama alivyosema Mkweche...madaktari wasitumie mgongo wa wananchi kutafuta/kuboresha maslahi yao..........by any means IT IS WRONG!........

........Natamani ingekuwepo kura ya wanajimbo (within five years at least kuwepo na nafasi moja) husika kumuondoa mbunge wao anaeonekana ha-perfom..........ili wasiendelee kusinzia huko bungeni.........hii ndio ndio ya Majambazi CCM inatupeleka kusiko kabisa...na mwananchi anaonekana hana nguvu tena hadi miaka mitano ijayo......its too long kwa mbunge asiye-perfom kumsubiria amalize miaka mitano....eti ndiyo mumpige chini........
 
mkweche binafsi nimekuelewa.......kwa sisi walimu.....mwalimu aliwahi kusema..
"WALE WALIOPATA FURSA YA KUPATA ELIMU KATIKA JMT, NI SAWA NA KIJIJI CHENYE NJAA AMBACHO KINAAMUA KUTOA AKIBA YA CHAKULA KUWAPA VIJANA WENYE NGUVU ILI WAKAHEMEE MBALI.....VIJANA WALE WANATAKIWA KUHEMEA NA KULETA CHAKULA NYUMBANI........WASIPOFANYA HIVYO NI WASALITI"

Unfortunately Tanzania ya leo siyo ile ya Nyerere. Wakati wa Nyerere tulikuwa tunajua mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali, na hata mshahara wa Nyerere mwenyewe ulikuwa unajulikana. Kuna wakati mshahara wa Nyerere ulikuwa ni Sh 2,500 wakati ule wa kima cha chini ukiwa ni Sh 380, halafu madakatri wakiwa wanalipwa Shs 1800, na medical assistants wakilipwa Sh 1300. Engineering graduates wakiwa wanalipwa Sh 1650.
 
Naona watu tumeganda katika natharia ya Ujamaa na kujitegemea.
sijui kijiji kina njaa mtu katumwa kwenda kubeba msosi???

Kijana akiwa darasa la kwanza mpaka 7 ni juu ya baba na mama yake kuhakikisha ansoma.
Form I - VI bado ni juu ya baba na mama yake kuhakikisha anasoma.
akienda chuo pia baba yake huhangaika sana kuhakikisha ansoma, kwa taabu sana serikali hutoa hela kupunguza makali.
( hizi hela kidogo za kupunguza makali ndizo wananchi tunadai kasomeshwa kwa kodi zetu)
Jiulize kwa nini wewe hukusoma?
Kwa nini more than 90% ya waTanzania hawama elimu ya University?
Hujiulizi kwa nini elimu imedolola kiasi cha kufanya shule kuwa mahali pa kupoteza muda ukisubiri ukue??

Akimaliza na kuanza kazi, eti kasomeshwa kwa kodi zetu ni lazima alipe. upuuzi
Baba asingejitahidi tangu huko mwanzo mtu huyu asingesoma.
Kuna wengi leo hii ambao walitakiwa kusoma hadi PhD za Udaktari ni madereva, wafagizi, wachuuzi wa mchicha kwa sababu tu wazazi walishindwa kulipa ada sekondari miaka hiyo ya 80 wakiwa form ada yenyewe kwamwaka ilikuwa Tshs 1500.00 tu.
Kwa sababu tunazo jua wenyewe tunajikomba kwa mtu Msomi huyu ambaye historia yake hata hatuijui na wala hatuna anything in common nayo.

Tukiwa na matatizo tunanukuu Itikadi ya ujamaa kwani tunatamani umoja wake.
Tukiwa katika maraha huko kwenye club
Utasikia mimi sitaki mtoto wangu awe Daktari ni kazi ya kimasikin haina mshiko lawama kibao.
Akifanya kazi TRA hivi huko swanu, au awe lawyer atawallamba watu mshiko.
Mi mtoto wangu hawezi kuwa nesi.
Afadhari afanye ile ya kugawa vidonge anaweza fungua duka. Nesi atafungua duka la vidonda?? Hiiiiii! Hiiii!

Huu utetezi kwamba sijui wamesomeshwa kwa kodi ni lazima walipe ni utetezi wa kipuuzi na hauna nafasi leo hii nchini Tanzania.
Nilitegemea kwamba Rais Kikwete aliyesoma Bure bila kulipa hata senti Tano UDSM na ni Rais wa kwanza nchini Tanzana aliyesoma UDSM; kwamba angekuwa mstari wa mbele kulipa fadhira hizo na hata kukipendelea UDSM na kuboresha kila kitu. Wapi Rais wetu yupo yupo tu utadhani baba yake aliuza mchunga kumsomesha UDSM. Kifupi kama kuna mtu anabwetekaa somewhere akidhani wengine wansoma kwa niaba yake kuanzia juzi ajiju.

Namuunga mkono kichuguu juu ya hoja ya kila tu kula mezani kwake.

Watu wa TRA kila siku wanaondoka na mifuko kadhaa ya maburungutu ya NOTI
Sijasikia mtu akitia neno hapo.

Ukiona mtu kachaguliwa kuw Minister in less than a year anajenga nyumba ya $ 1Million ujue anakula mezani kwake.

Tuko Fragmented na tunajenga individualism kwa kasi kubwa mno.

Kama Hekima haitatumika Mwisho wa mgomo huu wa madakitari tutakuwa na aina mpya ya matatizo ambayo sasa hivi hata kuota hatuoti.
 
Safi sana hii!
Wanaolaani madaktari wote hawana akili.
Hakuna mtu mwenye mkataba na daktari, ya kwamba atamtibu ht km anapunjwa malipo.
Wananchi wana mkataba na serikali, ndo inapaswa kuwapa hizo huduma za afya.
Km hazipo, iulizeni serikali, madaktari ni waajiriwa tu, wenye haki ya kugoma na kupigania maslahi na hadhi yao.
Ilazimisheni serikali iwatimizie madai yao.
Km mnaona serikali haitaweza fanya hayo kwa madaktari pungufu ya 2000 waliopo serikalini, lkn inaweza kuongeza posho maradufu na kukopesha magari kwa madiwani zaid ya 4000, basi nanyi ni sehemu ya tatizo, mnapaswa kukaa kimya na kufa taratibu tu, bila kelele.
 
Naona huna tofauti na nchemba...tena hata kuandika kwa computer tu haujui! Hii Masterez(??) yako ni chuo gani cha kata?

Ungekuwa Utumii masaburi KUfikiri Ungenielewa!Kuandika "Masterz" ni Madoido ya Mkweche!Ungejua Mkweche haishi kwa Posho!Mie sio kama hao mnaowasifu wanapiganaji wa wananchi wakati upande wa pili ni waponda raha!
Kwa kuwa wewe ni hamnazo wala Sijitikisi kukujibu!
 
Unfortunately, tangu Tanzania tulipojenga msingi wa kila mtu atashibia kwenye meza yake basi hatima yetu ni kwa madakatari kushibia kwenye uhai wetu. Si jambo jema lakini ndiyo hali halisi tunaotakiwa kukabiliana nayo. Iwapo afisa wa ushuru hata wa dxarasa la kumi na mbili atapokea mamilioni ya pesa kutoka kwenye deski lake, na katibu wa siasa naye vivyo hivyo atapokea mamilioni kwa kuzunguka nchi nzima, na mbunge naye atapokea mamilioni kwa kulala bungeni basi ama dakatri naye apokee mamilioni kwa kututibu au atuache tujifie wenyewe. Ninaandika wakati nina mtu wangu wa karibu sana amekosa matibabu aliyokuwa anahitaji kwa sababu ya mgomo huu. Hospitali za binafsi zilizoko karibu hazina uwezo wa kutoa matibabu kwa ndugu yangu huyo isipokuwa ile ya rufaa ambayo madakatari wake wamegoma. Kwa roho nyepesi ya kuona ndugu yangu anavyoumia, ningewalaumu madaktari lakini siwalaumu kabisa; ninajua kuwa ndiyo system tuliyojijengea, itabidi tudumu nayo. Wanasiasa wanapowadanganya wanachi kuwa watafukuza madakatari halafu wataleta madakatari wengine, sijui watawatoa wapi madakatari wa kulipa kiduchu namna hiyo.
POLE!Kama Umeona Madai ya Madaktari ni Makubwa Kuliko Uhai Wa Ndugu yako Sikuwezi!Na siku zote Ujinga wa Watanzani ndio Mtaji wa Wajanja!
 
Kwanza nikusahihishe kuwa siyo madai yao pekee bali na hata wagonjwa na wewe unaona wangetumia njia gani kwa serikali hii ambayo si sikivu iloko chini ya mr. dhaifu?
 
Naona watu tumeganda katika natharia ya Ujamaa na kujitegemea.
sijui kijiji kina njaa mtu katumwa kwenda kubeba msosi???

Kijana akiwa darasa la kwanza mpaka 7 ni juu ya baba na mama yake kuhakikisha ansoma.
Form I - VI bado ni juu ya baba na mama yake kuhakikisha anasoma.
akienda chuo pia baba yake huhangaika sana kuhakikisha ansoma, kwa taabu sana serikali hutoa hela kupunguza makali.
( hizi hela kidogo za kupunguza makali ndizo wananchi tunadai kasomeshwa kwa kodi zetu)
Jiulize kwa nini wewe hukusoma?
Kwa nini more than 90% ya waTanzania hawama elimu ya University?
Hujiulizi kwa nini elimu imedolola kiasi cha kufanya shule kuwa mahali pa kupoteza muda ukisubiri ukue??

Akimaliza na kuanza kazi, eti kasomeshwa kwa kodi zetu ni lazima alipe. upuuzi
Baba asingejitahidi tangu huko mwanzo mtu huyu asingesoma.
Kuna wengi leo hii ambao walitakiwa kusoma hadi PhD za Udaktari ni madereva, wafagizi, wachuuzi wa mchicha kwa sababu tu wazazi walishindwa kulipa ada sekondari miaka hiyo ya 80 wakiwa form ada yenyewe kwamwaka ilikuwa Tshs 1500.00 tu.
Kwa sababu tunazo jua wenyewe tunajikomba kwa mtu Msomi huyu ambaye historia yake hata hatuijui na wala hatuna anything in common nayo.

Tukiwa na matatizo tunanukuu Itikadi ya ujamaa kwani tunatamani umoja wake.
Tukiwa katika maraha huko kwenye club
Utasikia mimi sitaki mtoto wangu awe Daktari ni kazi ya kimasikin haina mshiko lawama kibao.
Akifanya kazi TRA hivi huko swanu, au awe lawyer atawallamba watu mshiko.
Mi mtoto wangu hawezi kuwa nesi.
Afadhari afanye ile ya kugawa vidonge anaweza fungua duka. Nesi atafungua duka la vidonda?? Hiiiiii! Hiiii!

Huu utetezi kwamba sijui wamesomeshwa kwa kodi ni lazima walipe ni utetezi wa kipuuzi na hauna nafasi leo hii nchini Tanzania.
Nilitegemea kwamba Rais Kikwete aliyesoma Bure bila kulipa hata senti Tano UDSM na ni Rais wa kwanza nchini Tanzana aliyesoma UDSM; kwamba angekuwa mstari wa mbele kulipa fadhira hizo na hata kukipendelea UDSM na kuboresha kila kitu. Wapi Rais wetu yupo yupo tu utadhani baba yake aliuza mchunga kumsomesha UDSM. Kifupi kama kuna mtu anabwetekaa somewhere akidhani wengine wansoma kwa niaba yake kuanzia juzi ajiju.

Namuunga mkono kichuguu juu ya hoja ya kila tu kula mezani kwake.

Watu wa TRA kila siku wanaondoka na mifuko kadhaa ya maburungutu ya NOTI
Sijasikia mtu akitia neno hapo.

Ukiona mtu kachaguliwa kuw Minister in less than a year anajenga nyumba ya $ 1Million ujue anakula mezani kwake.

Tuko Fragmented na tunajenga individualism kwa kasi kubwa mno.

Kama Hekima haitatumika Mwisho wa mgomo huu wa madakitari tutakuwa na aina mpya ya matatizo ambayo sasa hivi hata kuota hatuoti.

POLE SANA!Tatizo Mlio wengi Mnaelewa Mambo juu!Kusomesha "Dokita"moja si chini ya 25Million!Vyuo Vya Ngazi zote, Mahospitali nk Wananchi wanachangia tu hawalipi!Katika Budget za Taasisi nilizotaja Mapato kutokana na Ada au Malipo mbalimbali hayafiki 10% wanachi tunaendesha vyuo vile kwa njia ya KODI!
Ulafiwa Wa fedha na kupenda Ufahari wa wanasiasa,wasomi na watanzania ni Matokeo ya KUUBEZA UJAMAA!Asili ya Watanzania ni Ujamaa!Ubepari Tumechemsha
Narudia tena Pole
 
Hivi madaktari ndio wanatakiwa kuwa wazalendo tu? Tatizo letu kubwa huwa ni kuangalia matokeo badala ya chanzo. Daktari ni mfanyakazi na ana mgogoro na mwajiri wake ambayo ni serikali. Wametofautiana wao na makubaliano yao. Msiwaumize madaktari maana wananchi wanatumika kama sababu ya kuwalazimisha wakubaliane na maamuzi ya serikali hata kama ni mabaya kwao.

Wanaopinga madaktari kugoma naomba wapinge migomo yote hapa nchini maaana mgomo ni mgomo tu. Hivi TUCTA walipo tangazaga mgomo wao nchi nzima wangeumiza serikali au wananchi? Kama madai ya madaktari ni ya upuuzi na wao ni wakorofi si wafukuzwe? Si tunasema madaktari ni sawa na watu wengine? Sasa kwa kuwa mtu ayemgomea mwajiri, kwa mfano mhindi, hufukuzwa kazi basi madaktari wafukuzwe?

La kama sio lahisi kuwafukuzwa kwa sababu ya umuhimu wao then tuache unafiki tuwasikilize. By the way wanasema wamechoka kushuhudia wagonjwa wakifia mikononi mwao kwa magonjwa yanayotibika kwa kuwa hakuna dawa wala vifaa tiba. Kama hiyo nikweli, basi lazima tuwaelewe madaktari kuwa wapo kwenye moral dilemma. Kukubali kufanya kazi ambayo haifanyiki na unajua haiwezi kufanyika nao ni usaliti wa taaluma na kiapo.
 
Safi sana hii!
Wanaolaani madaktari wote hawana akili.
Hakuna mtu mwenye mkataba na daktari, ya kwamba atamtibu ht km anapunjwa malipo.
Wananchi wana mkataba na serikali, ndo inapaswa kuwapa hizo huduma za afya.
Km hazipo, iulizeni serikali, madaktari ni waajiriwa tu, wenye haki ya kugoma na kupigania maslahi na hadhi yao.
Ilazimisheni serikali iwatimizie madai yao.
Km mnaona serikali haitaweza fanya hayo kwa madaktari pungufu ya 2000 waliopo serikalini, lkn inaweza kuongeza posho maradufu na kukopesha magari kwa madiwani zaid ya 4000, basi nanyi ni sehemu ya tatizo, mnapaswa kukaa kimya na kufa taratibu tu, bila kelele.

......semeni tu moja kuwa mnataka muongezewe maslahi na sio kutumia mgongo wa wananchi kuleta tafrani........
 
[QUOTE=Msendekwa;
Km hazipo, iulizeni serikali, madaktari ni waajiriwa tu, wenye haki ya kugoma na kupigania maslahi na hadhi yao.
Kisheria madaktari hawaruhusiwi kugoma na Kama ikilazimu kugoma upo utaratibu wa kufuata.
Siungi mkono mgomo wao kwa sababu una madhara makubwa ya moja kwa moja kwa sisi walalahoi
 
Unadhani hao walipoacha kupeleka vitendea, kazi, Dawa na mambo mengine muhimu katika hospitals zetu kwa ajili ya maslahi yao walikuwa wanatumia uhai wa nani?
Doctors wanapigania hayo ili watanzania waweze kupata matibabu ya uhakika, Posho na mishara ni mambo mawili kati ya kumi wanayodai, mbona hayo mengine hayatajwi watu wanabaki kukomalia posho tu...ebo.
 
[@Madela Wa- Madilu yes,great thinker.critical thinking and great analysis.wacha mkweche abaki na ukweche wake.tulojitambua tunaendeleza mapambano.ukombozi u karibu.
 
......semeni tu moja kuwa mnataka muongezewe maslahi na sio kutumia mgongo wa wananchi kuleta tafrani........
Usisahau kwamba daktari naye ni mwananchi. Wewe ulijitolea lini kuwatetea madaktari wetu ili wito wao uonekane na kuvutia wengine? Mmekalia tu kuchonga midomo pasipo kufikiri ila kwa roho mbaya kwa madaktari kama vile madaktari muwasemao wanaishi mbinguni. Tunapigana vikumbo nao kwenye madaladala wanapowahi kuhudumia wagonjwa hospitali, unajua wanaishije wanakokaa? Waangalie wanavaaje, hata masista na wito wao wanpata support kimaisha. ACHENI UNAFIKI, mara ngapi hujampa hata lift daktari kwenye gari yako ambaye anakaa kituoni kusubiri daldala ili awahu kupunguza msururu wa wagonjwa lakini ingawa nawe waenda kupanga mstari huohuo unamwacha kituoni ama kwa kutambu au pasi kujua kwa sababu madaktari wetu HOHEHAHE????? Nani kakuroga ufikiri kuwa daktari ndiyo tiketi ya umasikini? Mwachie Nyoni abaki na kauli choo kama hizo kwamba madaktari wamejitakia. Huo wito kwa nini wewe usiitikie? Wewe ndio mbaya na muuaji zaidi kw sababu hukutaka kuitikia wito usome namna ya kuhangaikia wagonjwa, kama uliweza kwa nini ulikwepa shule ngumu kama za madaktari ukasarandia The history of Monomotapa? ndiyo inaganga wagonjwa hiyo????? Watu wengine mnaboa kufikiri kwa kutumia masaburi yenu. Amkeni tuwaangalie madaktari wnachosema ni kweli huduma ni mbovu hata serikali inajua, ndio maana watu wa serikali wanakiugua hata mafua wanaenda Apollo, Uingereza na Kwa Madiba. Wanasahau kwamba hata wanakokimbilia waliweka vipaumbele na afya waliiona ni muhimu maana mgonjwa hawezi kuleta maendeleo, mwalimu hafundishi ila kama kashiba na anao usalama anapoishi, anaweza kushant kirahisi kuhamasisha watu waelimike.

Tusijifanye mbumbumbu kwa matatizo ya wenzetu kwa sababu tu sisi tumeshindwa kuwa kama wao, Kawe daktari au mwalimu na wewe ufaidi kama unawaonea wivu. Sasa wanapojieleza kwa ustaarabu wanaambiwa siasa tu na watu wa serikali, kama ungekuwa wewe ungefurahia hayo? Madaktari ni wanasayansi na sio wanasheria au wanasiasa hata waambiwe wakubali kwamba 6 ni sawa na 9 ila inategemea na mkao. Wanajua maumivu wapatayo watanzania na ndio hao wanawapigania. Mnageuza dhana ya madaktari kwa ufisadi wa asili yenu. Midomo inatoka povu kwa dharau juu yao kwa vile mna siha nzuri, subiri siku unaharibu sura kama vile umekula ndimu au mwarobaini, unapomwona daktari kama mungu mdogo. Tuwaheshimu madaktari. Lugha zetu za hovyo zinawavimbisha vichwa wanasiasa waongeze viburi kuwachezea madaktari na sie hohehahe tunaendelea kufa. Ulimboka mmesikia kilichompata, unabishia nini kama ilishatangazwa kuwa LOLOTE NA LIWE na ikawa? Ungekuwa wewe uhasiwe na kung'olewa meno na kunyofolewa makucha kwa sababu tu unajaribu kushawishi serikali ichukue hatu nzuri ungefurahia??? Come on, be serious angalau kidogo tu.

Chukieni mtakavyo juu ya madai ya madaktari lakini ndio ukweli ambao hamtaki kuusikia, sasa tunaendelea kufa sababu ya hila zenu. Kama watanzania kwa sauti moja tungewaambia watu wa serikali wasikilize na kuamua haraka, leo hii kusingekuwapo watu wa kukimbilia India kutibiwa. Hata Burundi, Rwanda, Musumbiji pamoja na vita vyao wanatuzidi???? Tanzania ni kisiwa cha ukandamizaji, ni Roben island ya taaluma ya madaktari na walimu. Nimesema mimi, kwa uhuru wangu kuwatetea wasiopenda kusema sana, masikini madaktari wangu. Unayechonga sana bila shaka hujakutana na upole wa madaktari ukiugua. Great risk but cool!!!
 
Back
Top Bottom