Madaktari waache kutumia uhai wa watanzania kudai maslahi yao!

Madai ya mishahara hayakufanywa kisyansi Kwani ilitakiwa kiwango wanachotaka kiendane na Hali halisi ya Uchumi aw Nchi na siyo kukurupuka tu na kiasi. Hili linatia mashaka kwa wasomi Kama wao. Hata babu aw loliondo inaonekana kiwango cha bei ya dawa yake kilizingatia utz na utu kuliko hawa ndugu zetu wasomi
 
Unapoweka sheria kuwa daktari asigome, sharti pia uweke njia mbadala ya kudai haki zake, pale negotiation inapogonga mwamba.
Na hapa ieleweke kwamba ili Dr aendelee na kazi huku akiwa na mgogoro na mwajiri, na akishatangaza mgogoro huo, wananch sharti waibane serikali yao na kuiagiza iwasikilize madaktari na kuwatimizia accordingly.
Vingnevyo, kwa jinsi ilivyo hapa kwetu, ambapo ht Bunge ni watetezi wa serikali, ambapo Spika amekuwa akizima mjadala tangu ule mgomo wa feb(na sasa anatumia mahakama kuzima mjadala), ma Dr hawana chaguo, ila kutumia silaha ya mwisho, mgomo.
Na kitaeleweka tu, maana damu imekwishamwagika, na imekuwa chachu ya mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini, kuanzia maslahi ya watumishi wa afya na mazingira bora ya kazi.
LITAKALOKUWA NA LIWE!
 
kama hoja zako ndio hizi hapana shaka wewe ndio huna akili majinuni bin hayawani bin taahira. inaonekana hata hujui kuwa madr ni sehemu ya serikali. kumbafu kabisa.

Km unamaanisha CMO ni kweli yuko serikalini na ni mtetez wa serikali daima japo nae ni daktari(hapa pia ma RMO na DMO wako kundi hilo, ni watawala,hawagomi).
Lkn ujue, ewe maamuma, kuwa madaktari, kwa maana ya wale wanaotibu na kuhudumia wagonjwa, si sehem ya serikali, na ndio waliogoma.

Na kama utakuwa na akili, utaelewa hili.
 
Mkuu,si kwamba madaktari wanatumia uhai wa wagonjwa kudai maslahi yao,bali ukweli ni kwamba madai ya madaktari yatakapotimizwa,huduma mahospitalini zitaboreka!
Idadi ya wagonjwa wanao kufa kipindi kisicho kuwapo ngomo kutokana na uduni wa vifaa ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa wanao kufa kwa ajili ya huu mgomo.
 
"Madaktari waache kutumia uhai wa watanzania kudai maslai yao"

Honestly hoja imekaa vema kabisa! Swali la kujiuliza. Inakuwaje Serekali ishindwe kuwa manage hawa Ma Dr hadi Kufikia mtizamo wa hoja iliyo kwenye mada?

Chukulia Ma Dr kuwa they are deadly wrong ni wabinafsi, hawana mtizamo sahihi, wamekurupuka nk. Kwa nini Kama serekali cant handle them? Why the issue is escalating? Chukulia Tatizo limesha fahamika kuwa kimsingi ma Dr ndio Tatizo ...Serekali haijui na haina namna ya kutatua tatizo hilo? Why the problem is going in vicious circle?

Hapa Msingi wa Tatizo linaloendela sio ubovu wa ma DR. Tatizo ni serekali DHAIFU. THE GOVERNMENT IS SIMPLY WEAK AND WIMPY!!! ...AND...

The only way it knows how to solve the basic problems is abduct, intimidate, terrorize,toucher and before death EXTRACT TEETH AND NAILS!!This is insanity!!!

Kama UNYAMA umekuwa kuwa ndio njia ya kutatulia matatizo na UTU kutupiliwa mbali ...What Government is that??

Tatizo la Ma Dr is a Baby problem to be solved like salt dissolving n hot water, simple and effortless. BUT what is happening in our GOVERNMENT? Why can not handle such a tiny problem completely and effectively? HAINA UWEZO HUO!!!

Udhaifu ilipofikia serekali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mkubwa na hautibiki. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko kwenye terminal stage Cancer!!! Dalili za kansa hiyo angalia huko mali asili, angalia, ufisadi, angalia vichekesho bungeni, mipaka ya nchi inaigilika kama maliwatoni, rasilimali kila mtu kujichukulia, Bendera ya Nchi inatumika isivyo kwenye meli za mataifa mengine... angalia ..angalia ... angalia ..etc Im telling you The patient is in convulsion, gasping, kicking, throwing hands, legs ..etc must be real watched and taken care ... ataumiza na wasiokuwamo!!

Wanachi wa Tanzania sisi tutatoana macho hapa bureee ...wakati that wont solve any problem!!!!

A dying CA patient must be watched with care. Kama kutatua tatizo la mgomo wa Ma Dr .. ni sawa na kumtoa mtu meno mawili, kucha ishirini ..and if it works .... then kwa mgomo wa waalimu ... watongeza dose ..kamata walimu wawili then toa meno kumi, kata vidole vyote ... Kama wakitokea wengine just improve the drill ... Hii ina maana KIFO sasa kitatutumika kama TOOL BOX ya kutatulia matatizo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ... muda si mrefu we have SYRIA in Tanzania!!

Fungueni macho Watanzania issue sio WAHANDISI, MARUBANI, MADAKTARI, WAALIMU, WAISLAM , WAKRISTO , WANAMUZIKI, UKABILA, JINSIA, ITIKADI ZA VYAMA , USALAMA WA TAIFA, POLISI, JWTZ ETC!!

TATIZO LA MSINGI LIKISHAONEKANA LISHUGHULIKIWE ...Period!!!!!!!


.
 
mi naona mkweche huo wako ni uganga,na sio wote wanaofanya kazi hospitali wanayajua mapungufu hata yao wenyewe,inawezekana ni serikali ya kichwa chako ndio inakutuma useme hivyo!Je unajua nini maana ya uhai ?na nani anastahili kuitwa yuko hai?ukijua hayo baaaaaash!
 
Km unamaanisha CMO ni kweli yuko serikalini na ni mtetez wa serikali daima japo nae ni daktari(hapa pia ma RMO na DMO wako kundi hilo, ni watawala,hawagomi).
Lkn ujue, ewe maamuma, kuwa madaktari, kwa maana ya wale wanaotibu na kuhudumia wagonjwa, si sehem ya serikali, na ndio waliogoma.

Na kama utakuwa na akili, utaelewa hili.
mabreka haya..
hawa ndio madr wanaopasua kichwa badala ya miguu.
civil service ni part of govt.
Civil service - Wikipedia, the free encyclopedia
fyi: nakuzidi elimu na ujuzi hivo ktk levels za umaamuma kama nipo scale ya 10 wewe upo -10.
 
Kweli we kama unafanya kazi hospitali na hujui takwimu za watu wanaokufa tu just kwa kukosekana vitendea kazi au dawa basi utakuwa hujui unachofanya bora ukapumzike kwenu mana we ndo usiyetakiwa na umma. Watu wanakufa kwa kukosa tu aidha dawa fulani ama kipimo fulani cha bei ndogo alafu unaongea pumba gani. Ningekuona wa mana sana kama ungesema watanzania tufanye mandamano ya amani kuishinikiza serikali kufanya manunuzi ya vifaa muhimu na si kulaumu tu bila kujuwa. WATANZANIA TUMEZIDI KUPENDA SHORT CUT SASA BASI.
Hivi na hili la kusema kuwa madaktari tunasomeshwa kwa kodi za watanzania na wale wanaolipa milioni sita ada kwa mwaka wanatumia kodi ya nani?? tuache siasa bana tuseme ukweli
 
Kweli we kama unafanya kazi hospitali na hujui takwimu za watu wanaokufa tu just kwa kukosekana vitendea kazi au dawa basi utakuwa hujui unachofanya bora ukapumzike kwenu mana we ndo usiyetakiwa na umma. Watu wanakufa kwa kukosa tu aidha dawa fulani ama kipimo fulani cha bei ndogo alafu unaongea pumba gani. Ningekuona wa mana sana kama ungesema watanzania tufanye mandamano ya amani kuishinikiza serikali kufanya manunuzi ya vifaa muhimu na si kulaumu tu bila kujuwa. WATANZANIA TUMEZIDI KUPENDA SHORT CUT SASA BASI.
Hivi na hili la kusema kuwa madaktari tunasomeshwa kwa kodi za watanzania na wale wanaolipa milioni sita ada kwa mwaka wanatumia kodi ya nani?? tuache siasa bana tuseme ukweli

Wewe Ni Zumbukuku Huna Unalojua Kuhusu Mahospitali!Kwani hao madaktari waliogoma(Wauaji) walikueleza Takwimu ya Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi vinavyokoseka hadi iwe Sababu ya Kuacha wagonjwa WAFE?Mbona siku zote hao madokita wamekuwa wakiwaelekeza wagonjwa waende kwenye maduka flaniflani kununua Dawa na Mengine ni yao au maswahiba wao?Iweje Leo WAZUGE wanagoma kutibu kwa ajili ya ukosefu Dawa!Mbona wanachama wa Bima ya Afya wana Form Na 2 Ya kwenda kununua Dawa kwenye pharmacy Binafsi kwanini wasiwatibu hata hao wenye uhakika wa Dawa!
Mie Mkweche narudia tena Posho na Mishahara visitumike kuuwa watanzania!Kwa Taarifa yako Hospitali za Serikali ndio kimbilio la Walalahoi ambao hawana uwezo wa kwenda kupata Tiba Hospitali Binafsi!Ukimwacha Mgonjwa Afie Mgojwa afe Akiwa Ndani Hospitali hakuna Tofauti na Wahutu waliokuwa wanawauwa watusi waliokuwa wamekimbilia Makanisani!
 
Acha kudanganya watu weye!! Mwaka juzi serikali ya marekani ilitoa misaada ili madaktari walipiwe ada wasijisomeshe, serikali ya Tanzania ikaichukua hiyo hela ikapelekwa kwenye Uchaguzi mdogo, matokeo yake madaktari wanaona wananyanyasika na ndio matokeo haya. Kuna misaada toka nje ya nchi kwa ajili ya kununua ultrasound na x-ray mashines, Blandina aliwemwa pale hizo hela azikusanye ziende kwenye mauchaguzi, madaktari wakigundua hilo na sasa serikali imemuweka Mwinyi afanye alichokuwa anakifanya Blandina ( yeye si ndie rais ajaye, lazima atafute hela ya kampeni).

BTW hao madaktari hawajisikii salama ndani ya nchi yao na hawajisikii usalama kuendelea na kazi mpaka serikali itakapowahakikishia usalama wao na kuwa wakina ACP Msangi hawataendeleza mpango wao wa kuua baadhi kuwatia uchungu na kuwakomoa.
Tatizo wewe Unaonekana Magazeti Ndio vyanzo vyako vya Taarifa!Mie Mkweche niwadanganye watz kama wanavyofanya Madaktari kwa Lipi!Kwa Taarifa yako Hizo X-ray na Ultrasound zilizoharibika sio Misaada toka nchi nyingi za nje bali Ulikuwa Msaada Toka Nchi Moja tu ya Ulaya Nayo ni Serikali ya Netherlands kupitia Kampuni ya Philips!Baada ya Mkataba kwisha Philips waliondoka wakaiachia kazi ya Kusimamia matengezo kampuni ya MOKASI medical systems na ni kweli hali ya Mashine ni Mbaya kwenye Hospitali nyingi!zimekuwa zikikosa matengezo inavyopasa!kwa kuwa wa TZ si wabunifu wakiwamo Madaktari mashine ikifa wonaitazama na kuanza kulilia badala ya kuhangaika mashine ipone!
Jamani huo msaada wa marekani(kama sio ule wa weil) ni wa Msimu tu!na wao wanachangia tu na wamezuka tu!Kwa huyo mzigo wa Kuandaa madakitari na watu wa kada Zingine wetu wananchi kupitia Kodi na Tozo Mbalimbali!
Ndio mana mie Mkweche napinga na Kulaani Mgomo wowote ambao unagharibu Maisha ya wanyonge!Hospitali za serikali ndio zinatibu masikini ambao hawana pa kwenda!
SEWA HAJI PAROO alianzisha Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya masikini kupata TIBA Leo hii masikini wanaachwa wafie muhimbili kwa ajili ya Mgomo
 
Ndugu yangu MKWECHE nimekusoma na kukuelewa vizuri mno, siku zote ktk huu mgomo mimi webondo (Mtanzania Maskini) nilikuwa nakerwa sana na bado nakerwa sana kwani Watanzania wengi hasa wale maskini ambao kimbilio lao kubwa ni Hospitali za umma wanazidi kupoteza uhai. Sijajua hadi sasa ni watanzania wangapi wameshakufa, vifo ambavyo vimesababishwa na huu mgomo wa hawa ndugu zetu Watanzania.

Walalahoi sisi tunajua kabisa kuna hali mbaya au hakuna madawa na vifaa Tiba kote mahospitalini, lakini kwa hali hiyo angalao walalahoi sisi tulikuwa tunapata ahueni, lakini leo hii Watanzania hawahawa (doctors) wanadanganya uma eti sababu nyingine ya kugoma ni kwa sababu ya "mazingira mabovu na ukosefu wa vitendea kazi" walalahoi sisi tunajua kabisa hii ni gilba kwa wananchi, ili waeleweke kuwa hawajatanguliza pesa.... kuna mbumbumbu asiyejua kuwa hawa ndugu zetu wanaogoma tangu mwanzo wanahitaji PESA!? Watanzania wanakufa kwasababu wao wanataka waongezewe pesa. Suala la vitendea kazi na mazingira mabaya wameleta ili kufunika suala la PESA.

Nimeona mara nyingi humu JF, Social Media zingine au hata marafiki zangu wananiambia "mbona TRA wanalipwa hela nyingi au wabunge" jamani kwani unaingia katika hii fani yako ulilazimishwa na nani?? Why usiwe mbunge au ukaenda TRA?? Mlalahoi mimi naamini katika maisha haya tunayoishi kuna million of choices za kutaka wewe mwenyewe uwe wapi... haitokei tu unazaliwa then wewe ni diwani, au unazaliwa wewe ni lawyer... kuna mlolongo kila mtu anaenda nao na kufikia ulipofika, kwahiyo siyo excuse ya mtu mwingine. Mimi webondo ni mfagiaji (ingawa nina kaelimu kidogo), katika mlolongo wangu wa maisha nilijua nitaangukia kuwa mfagiaji, lakini kama nafikiri sistahili kuwa mfagiaji au nadhani ninacholipwa ni kidogo kwa kazi yangu ya ufaigiaji basi inanilazimu niachane na kazi yangu ya ufagiaji nitafute shughuli nyingine inayolingana na hadhi yangu au ambayo itanipa kipato stahili kwangu. Otherwise nimwombe huyu bosi wangu aniongeze kamshahara kidogo, maana mara nyingine kazi zinazidi.

Jana katika hotuta ya Kikwete akili yangu ilitaka tu kujua ni kitu gani atazungumzia kuhusu huu mgomo wa madaktari -- lakini baada ya kumaliza hotuba yake nikajisemea moyoni kuwa "hakika amechelewa kusema hivyo" kuwa KAMA DAKTARI ANAYEONA KUWA HAWEZI KUFANYA KAZI BILA KULIPWA MSHAHARA HUO (3.5M salary, na posho zote inakuwa 7.7M) AWE HURU KUACHA KAZI NA KWENDA KWA MUAJIRI ANAYEWEZA KULIPA KIASI HICHO. Hiyo sentensi nimeipa bold ili isomeke vizuri. Hii ina maana kuwa kama hapakuwa na resolution stahili kwa pande zote mbili serikali walistahili kutamka hivyo mapema zaidi, then mtu angechagua. Fikra zangu hasa ilikuwa ni kutambua vifo vinavyomtokea mlalahoi mwenzangu ambaye hakika hata Aga Khan Hosp au Tumaini Hosp hapajui.

Kwahiyo nadiriki kusema na mara zote nimekuwa nikisema kuwa I do not support huu mgomo wa hawa ndugu zetu madaktari, naamini wanayo madai ambayo yana msingi lakini siyo kwa kiwango hicho. Ilikuwa muhimu kufanya negotiations kama ambavyo wamekuwa wanafanya, lakini kwa extent ambayo wangefikia wangekuwa wamefikia wangesema "that's fine" sasa turudi kazini tuokoe maisha ya Watanzania. Uhai kamwe thamani yake hailingani pesa wala chochote.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. webondo

 
Last edited by a moderator:
Mkweche nimerudi tena toka kifungoni!Nilikuwa-banned kwajili ya kujibu mashambulizi ya watu waliotumia Lugha ya kuudhi dhidi yangu!Ila ujumbe yliwafikia!
Msimamo wa Kweche ni Ulele Mgomo wa Madaktari hauvuliki,haukubaliki na ni Haramu kuliko haramu zote!Atakae uwa mtanzani kwa risasi hana tofauti na anaye ua kwa Mgomo(Wote wauaji ila mmoja anauwa wagonjwa)
 
Tatizo la madaktari ni kukosa viongozi wanaoona mbali. Viongozi wao wa sasa wanatumia mbinu za uongozi wa shule, wamesahau kuwa wanaongoza jumuiya ya wataalam wenye haki na wajibu pia.
 
Back
Top Bottom